WANANCHI IKUNGI WAHIMIZWA KUTUNZA CHAKULA ILI KUJIKIGA NA BAA LA NJAA
BENKI YA ABC YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 2 KUSAIDIA UJENZI WA CHOO CHA WAALIMU SHULE YA MSINGI MTAWALA MANISPAA YA MOROGORO.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga,(katikati), akikabidhi vifaa vya ujenzi wa Choo kwa Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya (wapili kutoka kulia), kulia Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akimkabidhi taarifa ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi , Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.
Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.akizungumza katika hafla hiyo.
Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga akizungumza katika hafla hiyo.
Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati akisalimiana na waalimu waliojitokeza katika hafla hiyo.
Waalimu wa shule ya Msingi Mtawala.
BENKI ya ABC Kanda ya Morogoro, imekabidhi vitu vyenye thamani ya zaidi ya milioni 2 katika kusaidia ujenzi wa Choo cha Waalimu katika Shule ya Msingi Mtawalaa Manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia kuondoa changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu hususani katika upande wa vyoo.
Hafla hiyo fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, imefanyika leo Aprili 20/2022 katika shule hiyo huku tukishuhudia Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro , Chausiku masegenya ,akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Masegenya, ameishukuru Benki ya ABC huku akibainisha kuwa msaada huo utagusa maisha ya Waalimu wengi kwa miaka mingi ijayo.
“Wadau wetu muhimu na washirika kama Benki ya ABC ndio nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao utasaidia katika kuweka mazingira rafiki kwa waalimu ya kupata huduma ya choo , lakini pia kuwaondolea adha ya kutoka nje kwa ajili ya kufuata huduma ya choo" Amesema Masegenya.
Mwisho, Masegenya, ametoa wito kwa taasisi zingine za kifedha na wadau wanaopenda kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya vyoo pamoja na mazingira ya kujifunzia katika shule za umma zilizopo Manispaa ya Morogoro kujitokeza kwa wingi katika jitihada hizo.
Naye Diwani wa Viti Maalum anayetokana na Kata ya Mwembesongo, Mhe. Hadija Kibati, ameishukuru Benki ya ABC Kwa kuwaunga mkono kwenye sekta ya elimu kwa kuwapa vifaa hivyo ambayo yatasaidia kuondosha changamoto ya choo cha walimu shuleni hapo.
Kwa upande wa Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo, amesema kwamba utoaji wa misaada kwa jamii ni sehemu ya dhamira endelevu ya benki hiyo katika kusaidia sekta za elimu na kuona benki hiyo inachukulia kwa uzito sana suala la uwekezaji kwenye sekta ya elimu.
Kalinga,
amesema wametoa msaada huo ili kuunga mkono Serikali na juhudi za
wananchi na kurudisha kwao ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na hamasa ya
kutenegeneza miundombinu ya elimu kwa manufaa ya sasa na kizazi cha
baadae.
“Benki yetu inajivunia kuona Taifa linapiga hatua kubwa kwenye sekta ya elimu ambapo kupitia sera ya serikali elimu bure imeongeza idadi ya wanafunzi lakini pia ufaulu ambao maendeleo yake yanaakiisi hadi kiwango chetu cha uchumi ambapo mwaka jana nchi iliingia kwenye uchumi wa kati” Amesema Kalinga.
“Tumejitolea kuhudumia watu, biashara na jamii kwa ujumla. Benki yetu ya ABC, tumeguswa na changamoto ambayo iliwasilishwa kwetu , dhamira yetu kwa jamii ni kuona ni kuona tunaunga mkono na kusaidia juhudi za kielimu na ustawi wa wanafunzi wetu na shule kote nchini na sio kwa Manispaa hii ya Morogoro pekee, hivyo ni muhimu zaidi tukiweka jitihada katika kuboresha mazingira ya vyoo shuleni ili sasa Waalimu waweze kuwa na mahala rafiki kwa kutumia na kuacha kutoka eneo lao kwenda mbali na shule zao, ABC tutaendelea kushirikiana na Serikali kwa kadri tunavyoweza kuguswa na changamoto katika jamii ” Ameongeza Kalinga.
Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mtawala, Mwl. Godfrey Binagwa , ameishukuru Benki ya ABC kwa msaada huo ambao wameutoa ambao utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo za uhaba wa choo cha walimu.
Vifaa hivyo vya ujenzi ambayo walikabidhi benki hiyo ni Mifuko 50 ya saruji, mchanga Lori 1, Kokoto Lori 1, Mawe Lori 1, Milango 2 ya mbao, Fremu 2 za milango, Tofali za block 400 pamoja na Mabati 70.
TANZANIA COMMERCIAL BANK WASHIRIKI UZINDUZI WA RELI TABORA
Tanzania Commercial Bank TCB) imesema itaendelea kuwa mdau mkubwa wa maendeleo ili kuboresha uchumi wa Tanzania.
TCB imeshirikia kikamilifu katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kipande cha kutoka Tabora mpaka Makutupora Mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi wakati wa uzinduzi wa mradi wa uwekaji wa jiwe la msingi wa ujenzi wa reli ya Kisasa (SGR) awamu ya tatu leo Mkoani Tabora
“Tanzania commercial Bank ni wadau wakubwa wa maendeleo hapa nchini na kuchangia ujenzi wa Taifa, TRC ni wenzetu hivyo mradi huu wa SGR utaleta mafanikio kwa mkoa wa Tabora,”amesema
“Kufanikiwa kwa mradi huu kutarahisha usafiri wa kutoka Tabora hadi Dar es Salaam kwa masaa sita, na treni ya mizigo kwa masaa kumi pia kutafungua fursa za kiuchumi kwa mikoa ya Tabora, Dodoma, Singida , Shinyanga hadi Mwanza,”amesema
Moshingi amesema, wananchi wa Tabora kwa sasa wataanza kukua kiuchumi, kwa kusafirisha mazao yao kwenda Dar es Salaam ambapo ndio soko kuu la biashara na usafiri utakuwani ni wa uhakika zaidi.
BENKI YA CRDB YATOA MSAADA WA TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI RUANGWA










TANZANIA COMMERCIAL BANK LAUNCHES NEW BRANCH MBAGALA CHARAMBE
Temeke
District Commissioner Jokate Mwegello with Acting Chief Executive
Officer of Tanzania Commercial Bank Moses Manyatta opening the curtain
to mark the official launch of the Bank's new Branch opened at Mbagala
Charambe in Dar es Salaam today.Temeke
District Commissioner Jokate Mwegello addressing various stakeholders
and users of financial services during the Official Launch of the new
Tanzania Commercial Bank Branch opened today in Mbagala Charambe, others
pictured are Acting Chief Executive Officer of Tanzania Commercial Bank
Moses Manyatta, Branch Manager Edward Mwoleka along with other Bank
officials.
Acting Chief Executive Officer Moses Manyatta addressing various stakeholders, customers and users of financial services during the Official Launch of the new Tanzania Commercial Bank Branch opened in Mbagala Charambe.
Temeke District Commissioner Jokate Mwegello receiving a commemorative gift during the Official launch of the new Tanzania Commercial Bank Branch opened in Mbagala Charambe.
Temeke
District Commissioner Jokate Mwegello receiving an ATM card during the
Official Launch of the new Tanzania Commercial Bank Branch opened in
Mbagala Charambe today.TANZANIA COMMERIAL BANK goes live in Mbagala with 12th branch in Dar es Salaam.
By A Special Correspondent
National lender Tanzania Commercial Bank (TCB) has upped presence in Dar es Salaam by opening the 12th branch in the country’s commercial capital and economic hub that went live yesterday in Mbagala.
Temeke DC Jokate Mwegelo graced the ceremony to unveil the newest outlet in the TCB stable that now comprises an extensive network of 85 branches across the country.
Speaking before its inauguration, Chief Executive Officer Sabasaba Moshingi said the TCB Mbagala Branch is the fifth outlet to be launched by the oldest lender in Tanzania so far this year.
He said the financial inclusion investment in one of the most populous suburbs in Dar es Salaam makes the branches the bank has opened in the city this year to be two. The TCB Kigamboni Branch, which opened for business in March, was the first and the lender’s 11th in the region.
Apart from a blossoming population, which no operations expert can ignore, Mbagala also has a thriving and enterprising economy that lured TCB to come up with the mortar and brick presence idea in the area.
The venture is part of the transformation agenda of the bank and a key aspect of its endeavour to become fully fledged universal bank. Before the transformation journey kicked off in 2011, TCB had a limited branch network that mostly comprised dilapidated outlets.
“This is our 12th branch in Dar es Salaam that gives Mbagala residents the opportunity to join mainstream banking and conveniently enjoy our top notch services,” Mr Moshingi said.
He said the new outlet consolidates TCB position of being among the banks that have the widest branch networks in the market.
The ongoing transformation efforts have also made TCB to be among the ten top performing banks in the country. Its latest financials put the assets base at around TZS 1.18 trillion as to the end of 2021 and customers’ deposits, which the new branch will help to mobilise, standing at 729,137.
The lender said another four branches are lined up for opening before this year ends as part of the operational scheme to take its services closer to the people and strategically position itself to better and competitively serve the country.
“The Mbagala branch is the fifth we have launched in 2022. Branches already opened this year are Kigamboni, Mbinga, Usa River and Mpanda. Our plan is to expand our outreach in four new locations this year,” TCB noted in a presser.
DC Jokate lauded the bank for its inclusive finance zeal and championing financial inclusion for all saying it was in line with the government’s grand mission to make life better for all.
According to her, TCB should be emulated for its continued in-roads into the underserved areas like Mbagala and going for un-banked populations in many parts of the country
Absa Tanzania yahamasisha watanzania kuchanja chanjo ya Covid-19
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZINDUA KADI YA MALIPO YA KIMATAIFA YA POPOTE VISA

Makamu wa Rais wa VISA card Africa Mashariki Corine Nana (katikati) pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Sabasaba Moshingi (wapili kushoto) wakionesha mfano wa POPOTE VISA CARD wakati wa uzinduzi rasmi wa kadi hiyo iliyozinduliwa na Tanzania Commercial Bank wengine pichani ni pamoja na Mkurugenzi wa Teknohama wa Tanzania Commercial Bank Jema Mssuya, Mkurugenzi Mtendaji wa UBX Tanzania LTD, Seronga pamoja na Meneja Mwandamizi wa Intanet Banking wa TCB Allen Manzi hafla hiyo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi,
akizungumza wakati wa uzinduzi rasmi wa Popote Visa Card iliyozinduliwa
na Tanzania Commercial Benki kwaajili ya kuwarahisishia wateja wa Benki
hiyo kupata huduma yoyote na wakiwa sehemu yoyote ndani na nje ya nchi
hafla ya uzinduzi huo umefanyika leo jijini Dar es Salaam
Makam wa Rais wa VISA card Africa Mashariki Corine Nana (kulia), akikabidhi
kadi ya POPOTE VISA CARD kwa mmoja ya wateja waliohudhulia uzinduzi
rasmi wa Popote Visa Card iliyozinduliwa na Tanzania Commercial Benki
kwaajili ya kuwarahisishia wateja wa Benki hiyo kupata huduma yoyote na
wakiwa sehemu yoyote ndani na nje ya nchi hafla ya uzinduzi huo
umefanyika leo jijini Dar es Salaam (katikati) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa
Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi.
Mteja wa Tanzania Commercial Bank akionesha kadi ya POPOTE VISA CARD iliyozinduliwa leo na Benki hiyo bara baada ya kukabidhiwa.
Benki
ya Biashara Tanzania (TCB) jana imezindua kadi ya malipo ya kidijitali
ambayo itaisaidia Serikali ya Awamu ya Sita kufanikisha mpango mkakati
wake wa kuifanya Tanzania kuwa uchumi usiotegemea sana fedha taslimu.
Huduma
hiyo ya malipo ya kimataifa inayojulikana kama Kadi ya Popote Visa ni
matokea ya ushirikiano kati ya TCB na Visa International ya Marekani
inayoongoza duniani katika teknolojia bunifu za malipo ya kidijitali.
Akizungumza
wakati wa uzinduzi wake jijini Dar es Salaam, Afisa Mtendaji Mkuu wa
benki hiyo, Bw Sabasaba Moshingi alisema Popote Visa Card ina uwezo wa
hali ya juu kusaidia kutimiza ndoto za taasisi hiyo ya kuendeleza huduma
jumuisha za kifedha nchini.
TCB na mshirika wake wameazimia
kuunga mkono juhudi za kitaifa za kujenda uchumi wenye matumizi madogo
ya fedha taslimu kwa kuwekeza katika suluhisho bunifu za malipo ya
kidijitali ambazo ni rahisi zaidi, salama na zinazozingatia ufanisi wa
usimamizi wa fedha.
“Huduma kama kadi ya malipo ya kimataifa
tuliyozindua leo na ushirikiano wetu na kampuni ya Visa ni muhimu sana
katika juhudi za serikali kujenga uchumi wa kidijitali na kuifanya
Tanzania kuwa taifa lisilotegemea sana malipo yanayofanywa kwa fedha
taslimu,” Bw Moshingi alibainisha.
Aliwaambia waandishi wa habari
kuwa uamuzi wa TCB kushirikiana na Visa unatokana na kampuni hiyo kuwa
kigogo wa teknolojia za malipo duniani ikiwa na mtandao wa
wafanyabiashara milioni 61 wa kimataifa.
Wakizungumza wakati wa
uzindunzi huo, maafisa waandamizi wa Visa Afrika Mashariki, walisema
dhamira ya kampuzi hiyo si tu kuongeza matumizi ya kadi za kidijitali
nchini peke yake bali duniani kote kuwahudumia wananchi, wafanyabiashara
na serikali mbalimbali.
Makamu wa Rais wa Visa na Mkurugenzi
Mtendaji wake wa Afrika Mashariki, Bi Corine Mbiaketcha Nana, alisema
Tanzania ina kila kitu kinachohitajika kuwa uchumi wa kisasa zaidi wa
kidijitali.
“Kama suluhisho zote bunifu za malipo ya kidijitali, matumizi ya Popote Visa Card yana manufaa mengi na faida kubwa kwa watu binafsi, mashirika na serikali,” Bi Nana alifafanua na kusisitiza kuwa mchango wake mkubwa hasa kwa wananchi wa kawaida ni maendeleo ya huduma jumuishi za kifedha.
Uzinduzi wa UCB Popote Visa Card umefanyika wiki mbili bada ya serikali kutangaza mipango na uwekezaji wake kwenye ujenzi wa uchumi usiotegemea sana fedha taslimu kupitia Mpango wa Tanzania ya Kidijitali.
Kwa mujibu wa Waziri wa TEHAMA, Bw Nape Mnauye, hivi karibuni Tanzania ilipata mkpo nafuu kutoka Benki ya Dunia kwa ajili ya utekelezaji wa azma hiyo wenye thamani ya dola za kimarekani milioni 150.
Wakizumgumza kwa nyakati tofauti twakati wa uzunduzi wa bidhaa hiyo mpya sokoni wateja na wandau mbalimbali wa TCB walisema kuzinduliwa kwa kadi hiyo mpya kutasaidai michakato mbalimbali ya kuharakisha maendfeleo ya kidijitali nchini.
“Ushirikiano wa kimkakati kati ya TCB na Visa si tu unazinufaisha taasisi hizo mbili peke yake, bali pia utasaidia kupanua wigo wa malipo ya kidijitali nchini na kuongeza faida za kibiashara katika nyororo wa thamani wa malipo kitaifa,” Meneja Mkuu wa dt card Tanzania, Bw Christiaan Wielengs, alibainisha.





















