ESRF, Ubalozi wa Sweden na UDSM waandaa Mdahalo wa Uchumi Jumuishi

TANZANIA itahitaji kutengeneza mkakati mpya wa maendeleo na kuachana na falsafa za zamani kama itataka kufikia ustawi na kuwa nchi yenye kipato cha Kati.

Mkakati huo katika; masoko, rasilimali na uwezeshaji unatakiwa kuwezesha sera za maendeleo zilizo endelevu kwa kuangalia zaidi changamoto tofauti za maendeleo na kuzikabili kabla ya kuzitumia kubadili harakati za maendeleo.

Kauli hiyo imo katika mdahalo uliofanyika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na kuongozwa wataalamu wa uchumi.

Walisema katika mdahalo huo kwamba mkakati wa zamani kuhusu maendeleo kwa kutegemea kuzalisha bidhaa na kuziuza nje una vikwazo vingi hasa katika uzalishaji kutokana na masuala ya teknolojia na hivyo mkakati utakaokuwa jumuishi, unaoratibu kilimo, madini na huduma unaweza kuwezesha kukua kwa uchumi kama ilivyokuwa katika mkakati wa zamani wa uzalishaji kwa ajili ya kupeleka nje.

Wamesema katika mkakati huo mpya serikali inatakiwa kufanya wajibu mkubwa kufanya mabadiliko ya kimfumo na kimkakati kuelekea uchumi jumuishi ambapo kila mwananchi atashiriki.

Uchumi huo hautategemea uzalishaji wa viwandani pekee bali uchumi wa kisasa unaozingatia huduma ambao katika awamu ijayo kilimo cha kisasa nchini Tanzania kitakuwa sehemu ya mkakati huo.

Wanazuoni hao wamesema kwamba mafanikio ya kuwa na uchumi jumuishi kwa nadharia za sasa zinategemea mpango mkakati wa maendeleo wenye kuangalia mambo mengi yatakayowezesha kuwa na ukuaji jumuishi, unaoshirikisha na kuzingatia uwiano wa masoko, serikali na jamii.

Walisema taratibu hizo mpya duniani zitasaidia kuwa na uchumi wenye mafanikio unaobadili maisha ya watu kwa kuangalia changamoto mbalimbali ikiwamo vifo na kutengeneza mfumo mpya wenye kuzingatia uwezo na mahitaji.

Prof. Basu alizungumzia misingi ya maendeleo kwa kuzingatia sosholojia na saikolojia ya watu. Katika mazungumzo yake aligusia nadharia za misingi ya uchumi kama zilizvyoonwa na akina Nyerere na Nkurumah  na wengineo, akiangalia Azimio la Arusha na maendeleo ya binadamu nadharia ambazo zinashabihiana na msimamo wa Stockholm.

Aidha katika mada yake alizungumzia uratibu na udhibiti kama kitu muhimu katika soko na kuona mipango inavyotakiwa kuzingatia watu ambao washiriki katika ujenzi wa uchumi badala ya serikali kufanya makosa ya kudhani watu wanatakiwa kufanyiwa kila kitu,

Prof. Stiglitz yeye alizungumzia kutoka uzalishaji unaolenga soko la nje hadi ukuaji uchumi jumuishi wa karne ya 21 kwa taifa la Tanzania.

Katika majadiliano washiriki walisema kwamba hakuna tishio la roboti kuchukua nafasi za kazi na kuzungumzia haja ya kubadili kilimo ili kuwa msaada mkubwa katika uchumi jumuishi.

Katika majibu ya hoja mbalimbali zilizotolewa na washiriki Prof. Basu alisema kwamba utandawazi  si suala la mtu kuudhibiti bali ni namna gani unatumia utandawazi huo kusonga mbele  na kusema sera ni muhimu  katika maendeleo na kwamba elimu inaweza kusaidia kudhibiti soko.

Naye Prof. Stiglitz alisema kwamba uzalishaji kwa mauzo ya nje hakutasaidia kuimarisha uchumi wa wananchi kutokana na ukweli kuwa uzalishai huo kwa sasa unakwenda chini na  njia mpya lazima kuangaliwa ili kuwa na uchumi jumuishi ulioendelevu.

Mdahalo huo uliwezeshwa na ESRF na kushirikisha Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam.

Baada ya mdahalo huo uliokuwa na mafaniko makubwa UDSM, kesho kutakuwa na mkutano wa kitaifa  wa 7 mwaka wa ESRF ambao utakaozungumzia Maendeleo ya Binadamu na Uchumi kwa kuzingatia rasilimali zilizopo.
BASU%2B1

BASU%2B2
Profesa wa Uchumi wa Chuo Kikuu Cornel, Ithaca na aliyekuwa mchumi wa Benki ya Dunia  Prof. Kaushik Basu akiwasilisha mada kuhusu misingi ya maendeleo kwa kuzingatia sosholojia na saikolojia ya watu wakati wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
STIGLITZ
Aliyekuwa mchumi wa zamani wa Benki ya Dunia kutoka Chuo Kikuu cha Columbia, Prof. Joseph Stiglitz akiwasilisha mada kuhusu kutoka uzalishaji unaolenga soko la nje hadi ukuaji uchumi jumuishi wa karne ya 21 kwa taifa la Tanzania wakati wa mdahalo uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam
NDULU
Mwenyekiti  wa mdahalo kutoka kigoda cha Mwl. Julius Nyerere, Prof. Benno Ndulu akiongoza mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
AIKAELI
Mkuu wa Idara ya Uchumi katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Jehovaness Aikaeli akitoa neno la shukrani kwa washiriki wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
KIDA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akizungumza na kituo cha Habari cha ITV kuhusu mdahalo huo na manufaa yake kwa Tanzania na kwa sekta ya uchumi wakati wa mdahalo kuhusu uchumi  jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
CHANGIA%2B1

CHANGIA%2B2
Baadhi ya washiriki wakitoa maoni ya mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
HIGH%2BTABLE
Kutoka kulia ni Mchumi kiongozi wa Ubalozi wa Sweden nchini, True Schedvin, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida pamoja na baadhi ya maafisa kutoka Ubalozi wa Uswidi.
MDAHALO
WASHIRIKI%2B1
WASHIRIKI%2B2
WASHIRIKI%2B3
WASHIRIKI%2B4
WASHIRIKI%2B5
Sehemu ya washiriki wakifuatilia kwa umakini mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa wakati wa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
KIDA%2BSALIMIA
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF), Dkt. Tausi Kida akisalimiana na mmoja wa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
GROUP%2BESRF
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Taasisi ya Utafiti wa Uchumi na Kijamii (ESRF) mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
GROUP%2BPHOTO
Meza kuu katika picha ya pamoja na wadau mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
GROUP%2BWANACHUO
Meza kuu katika picha ya pamoja na baadhi ya wanafunzi wa UDSM mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
GROUP%2BUDSM
Meza kuu katika picha ya pamoja na wafanyakazi na wahadhiri wa UDSM mara baada ya kumalizika kwa mdahalo kuhusu uchumi jumuishi uliowezeshwa na ESRF kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya ufadhili wa Ubalozi wa Sweden uliofanyika katika ukumbi wa Nkurumah Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Share:

TCCIA KWA KUSHIRIKIANA NA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM WAZINDUA TYM


Naibu makamu mkuu wa chuo kikuu Dar es salaam, Pro. Cuthbert Kimambo akiongea na TYM wakati wa kusain makubaliano na TCCIA.

Katika kuhakikisha Taifa letu la Tanzania linakuwa imara kiuchumi na kuwa na nguvu kazi kubwa ya Taifa, Tanzania Chamber of Commerce Industry and Agriculture ‘TCCIA’ imeingia makubaliano maalumu pamoja na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ambapo TCCIA imetiliana saini katika makubaliano hayo ‘Memorundum of Understanding’ .

Makubaliano haya yanatoa nafasi kubwa kwa vijana kupitia TCCIA Youth Members, kitengo maalumu kwa vijana hasa waliopo vyuoni kuweza kutumia rasilmali zilizopo TCCIA kuweza kujijenga zaidi katika kazi zao pindi wanapokuwa bado wapo shule na hata baada ya kumaliza shule.

Akizungumza na TYM Makamu wa Rais wa TCCI Bw. Octavian Mshiu alisema TCCIA imeingia makubaliano haya na chuo kikuu cha Dar es Salaam ili kuhakikisha inatoa fursa kwa vijana wengi kuweza kupata nafasi za kuonesha kazi zao, kupata nafasi ya kuwa na watu ambao watawawezesha kuweza kutimiza ndoto zao ‘Mentorship’, kutoa nafasi ya wenye makampuni na biashara kuwatumia vijana wa ndani ambao sio tu ni wabunifu bali pia wenye uthubutu wa kuleta mabadiliko chanya kwenye nchi yetu, katika kuongeezea hilo prof. Cuthbert Kimambo lisema, makubaliano haya hayataishia tu kwa chuo cha UDSM bali wataendelea na kwenye vyuo vyote nchini.


Makamu WA Rais wa TCCIA Octavian Mshiu, wakibadilishana makubaliano Na naibu makamu Mkuu WA chuo kikuu prof Cuthbert Kimambo baada ya kutia sain kuhusu ushiriki wawezekaji vijana wa Chama hicho TYM.

Mkuu wa Kitengo cha Utafiti UDSM Dr. Amelia Buriyo katika hotuba yake kwenda kwa wanafunzi baada ya uzinduzi huu alionesha kufurahishwa na jambo hili ambapo alitoa shime kwa vijana kuanza kuamka na kuchangamkia fursa hii adhimu kwao kwani sio kwamba itawakutanisha na watu ambao watawafanya ndoto zao katika miradi wanayoibuni kuwa kweli bali pia kuwezesha kupata nyezo za kufanyia kazi hasa upatikanaji wa mikopo.

Moja ya vijana ambao wamefanikiwa kupitia kujiajiri katika sekta ya ubunifu wa mavazi Bw.Jeff Jersey (Speshoz) alikuwepo kwenye halfa hii ambapo pamoja na mambo mengi aliyoyagusia alisisitiza sana kuhusiana na kuongeza thamani kwenye kila kitu ambacho wanakifanya kwani dunia ya sasa ni dunia ya ushindani na ushindani huhitaji sana ubunifu na kuongeza thamni katika kila kitu ambacho tunakifanya. Bw. Speshoz ambaye ni mkurugenzi wa kampuni ya Speshoz aliwahi kuwa mwanafunzi wa chuo kikuu cha Dar es Salaam miaka kadhaa iliyopita.


Jeff Jersey "Speshoz" akizungumza na TYM wakati wa kusaini makubaliano kati ya TCCIA na UDSM.TCCIA Youth Members ‘TYM’ sasa imefunguliwa rasmi ambapo kila kijana anaweza kwenda kujisajili bila malipo yoyote.
Share:

SPIKA NDUGAI ATEMBELEA KIWANDA CHA ASASI KILICHOPO MKOANI IRINGA


MNEC wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Salim Abri akimkaribisha Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa jana.

MNEC wa Chama cha Mapinduzi kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Fuad Abri akisalimiana na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa jana katikati ni MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza na Ahmed Salim Mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha ASAS wakati alipowasili kiwandani hapo na kufanya ziara ya kukagua uzalishaji wa kiwanda hicho mjini Iringa leo katikati ni MNEC wa Chama cha Mapinduzi CCM kutoka Mkoani Iringa na mmoja wa wakurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS Bw.Salim Abri.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akiendelea na ziara yake kiwandani hapo.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimsikiliza Bw. Fuad Abri Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha ASAS wakati akitoa maelezo alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo jana mjini Iringa katikati ni MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri na wa pili kutoka kulia ni Mbunge wa jimbo la Kilolo Mh. Venance Mwamoto.

Fuad Abri Mkurugenzi wa Kiwanda cha maziwa cha Asas akitoa maelezo wa kwa Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo leo Mjini Iringa, Ahmed Salim mmoja wa wakurugenzi wa ASAS na Mbunge wa jimbo la Kilolo Mh. Venance Mwamoto.

Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda hicho wakiendelea na kazi.

Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati akitembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo jana.

Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai wakati akionyeshwa moja ya bidhaa zinazozalishwa na kiwanda cha ASAS wakati alipokembelea kiwanda hicho na kukagua uzalishaji pamoja na shughuli zingine za uzalishaji wa Bidhaa mbalimbali zinazofanyika kiwandani hapo jana, wa pili kutoka kushoto ni MNEC wa CCM Mkoa wa Iringa na anayefuatia ni Ahmed Salim Mmoja wa wakurugenzi wa ASAS.

MNEC wa CCM mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri akizungumza na Spika wa Bunge ofisini kwake wakati Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai alipotembelea kiwanda cha Maziwa cha ASAS jana.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akizungumza jambo huku MNEC wa CCM Mkoa wa Iringa Bw. Salim Abri akimsikiliza wakati alipotembelea kiwanda cha maziwa cha ASAS mkoani Iringa jana.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Job Ndugai akimsikiliza Mkurugenzi wa Kiwanda cha Maziwa cha ASAS Bw. Fuad Abri wakati akitoa ripoti ya kiwanda hicho wakati alipokitembelea na kukagua uzalishaji.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (353) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (132) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages