KAMPUNI YA MAFUTA YA PUMA YAFANYA JAMBO KUBWA KWA WATEJA WAKE.

KAMPUNI ya Mafuta ya Puma Tanzania imewakutanisha watanzania na wadau mbalimbali katika futari iliyoandaliwa na Kampuni hiyo huku ikitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuendelea kutumia bidhaa zinazotoka Kampuni hiyo 
Hafla ya futari iliyoandaliwa na Kampuni hiyo ikiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wake Fatma Abdallah imefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa wadau mbalimbali wakiwemo wakuu wa taasisi za umma na binafsi pamoja na wateja wa kutoka maeneo mbalimbali nchini.

Mgeni rasmi katika Iftar hiyo alikuwa Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Alhad Walid aliyewakilishwa na Sheikh wa Wilaya ya Temeke ...

Akizungumza wakati wa Iftar hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni hiyo Dk Selemani Majige ametumia nafasi hiyo kueleza kuwa ni vema kila Mtanzania kwa nafasi yake kuendelea kuliombea Taifa sambamba na kumuunga mkono Rais Dk.Samia Suluhu Hassan.
"Tunafahamu kwa sasa tunaendelea na Mfungo wa Ramadhan pamoja na Kwaresima hivyo wakati tukiendelea na Mfungo ni vema tukaliombea Taifa letu lakini wakati huo huo kudumisha Umoja,amani na mshikamano,"amesema Dk Majige.

Amesisitiza kuendelea kudumisha amani katika nchini Kunafanya uchumi Wetu kuendelea kuimarika  na biashara zetu ziendelee vizuri."Kulinda amani ni jambo kubwa kwani kama hakuna amani basi hata biashara haziwezi kufanyika vizuri.

"Hivyo kupitia mwezi mtukufu wa Ramadhan ni vema kuendelea kumuomba Mungu na kuendelea kumuombea Rais Dkt Samia Suluhu Hassan ili aendelee kutuongoza na kudumisha amani katika taifa letu."
Pia amewaomba Watanzania kuendelea kutumia mafuta  ya Puma Energy Tanzania pamoja na bidhaa zake zote huku akifafanua mafuta ya Kampuni hiyo yana ubora na viwango vya hali ya juu.

"Tunawaomba muendelee kutumia mafuta ya Puma  ili tuongeze faida na tukiongeza faida Serikali inapata gawio na inapotoa gawio zinapatikana fedha ambazo zinakwenda kuhudumia jamii katika maeneo mbalimbali,"
Kwa upande wake Sheikh wa Wilaya ya Temeke Sheikh Zailai Hassan Mkoyogole aliyemwakilishwa  Sheikh wa Mkoa wa Dar es Salaam Walid Alhad Omar  aliyekuwa mgeni rasmi, amesema kipindi hiki cha Mwezi mtukufu wa Ramadhan jambo kubwa ni kuzidisha wema kwa maana wanadamu ni wakosaji mbele za Mwenyezi Mungu.

"Binadamu anamkosea Mwenyezi Mungu kwa vitu vingi hivyo sasa ameleta Mwezi mtukufu wa Ramadhan ili kutubu kwa yale yote ambayo ameyafanya.Hivyo kinachotakiwa katika mwezi huu ni kufanya yale yaliyomema na kurejea  kwake,"
Pia amesema Mwenyezi Mungu anapenda kuombwa ,hivyo ametoa wito kwa watu wote kurejea kwa Muumba  na kuomba msamaha.

Awali Mkurugenzi Mkuu wa Puma Energy Tanzania Fatma Abdallah  amewashukuru wadau  kwakuitikia wito  katika futari hiyo huku akitumia nafasi hiyo kuwaomba Watanzania kuwaunga mkono kwa kununua bidhaa za mafuta ya Kampuni hiyo.

Aidha amesema  kama Puma Energy Tanzania wataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali hasa katika utekelezaji matumizi ya  nishati safi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi kwa lengo la  kuendelea kutunza mazingira .

"Puma  Energy Tanzania tunatambua mwelekeo wa Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dkt Samia Suluhu Hassan na hasa kwenye suala la nishati safi hivyo tutaendelea kua mstari wa mbele kutoa elimu kwa lengo la kuhakikisha   mazingira yanalindwa na matumizi ya nishati  safi kwa watanzania yanakuwa kipaumbele."

Wakati huo huo Mkurugenzi Mkuu UDA- RT  Waziri Kindamba aliyeshiriki futari hiyo amewapongeza kwa kuandaa futari hiyo ni kuwaalika wateja wao ambao wanatumia bidhaa zao ikiwemo vilainishi na mafuta.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages