WANAWAKE WA KATA YA BONYOKWA WALAMBA DUME

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bonyokwa Malyatabu akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa WOMEN  TAP yenye lengo la kuinua wanawake kiuchumi na uongozi bora.
Muhasisi wa WOMEN TAP ambae pia ni Rais wa Vicoba Tanzania Bi.Devotha Likokola akizungumza na wanawake wa bonyokwa wakati wa hafla ya uzinduzi wa WOMEN  TAP yenye lengo la kuinua wanawake kiuchumi na uongozi bora.
Moja na mshiriki akiuliza swali wakati wa hafla hiyo

Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bonyokwa Malyatabu akiwa katika picha ya pamoja na  washiriki.

Muhasisi wa WOMEN TAP ambae pia ni Rais wa Vicoba Tanzania Bi.Devotha Likokola Amewataka Wanawake wa kata ya Bonyokwa na Mtaa wa Bonyokwa Unaoongozwa na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa Malyatabu  Kutumia Vizuri Fursa Wanazozipata Katika Kujikwamua na Umasikini Katika Kujiunga Kwenye Vikundi Mbali mbali Vya Kijamii na Kiuchumi.


Akizungumza na Mamia ya Wanawake  wa Bonyokwa wakati wa uzinduzi wa WOMEN TAP yenye lengo la ukombozi wa wanawake na kimaendeleo kutaka kila mwanamke aishi maisha bora na ya furaha kuanzia kwenye mafunzo ya kujitambua na uongozi bora.



WOMEN TAP inawakutanisha wanawake wajasiriamali, wafanyabishara,wanaharakati wakurugenzi na viongozi wa serikali  na itakuwa inafanyika kila tarehe 7 ya mwezi ili kuweka maendeleo yakuwakutanisha wanawake kila mahali kuanzia ngazi ya mtaa, kata wilaya mkoa hadi taifa ili kuhakikisha kila mwanamke anapata mafunzo yenye lengo la kila mwanamke kuwa kiongozi bora.



Pamoja na Mambo Mengine Amewaagiza Wanachama Wote Pamoja na Viongozi Wake Kufuata Mfumo Rasmi wa uanzishaji na  Uendeshaji wa vikundi/ Vicoba IIi Kuhakikisha Jamii Inanufaika na vicoba Endelevu.



Katika Hatua Nyingine Amelaani Tabia Za Baadhi ya Watu Wanaojitokeza Mitaani Kuwadanganya Wananchi Kuanzisha Vikundi Visivyoendelevu Vinavyoweza Kusababisha Mifarakano Mikubwa Pindi Fedha Zitakapo Kuwa Zikipotea Bila Utaratibu.



Kwa Upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Bonyokwa Maliyatabu  Amewataka Akina Baba wa Bonyokwa Kuwaruhusu Wake Zao Kujiunga na WOMEN TAP  Ili Waweze Kuacha Kumtegemea Baba Kwa Kila Kitu.



Ameyasemahayo wakati alipoalikwa kuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa WOMEN TAP ameeleza kuwa hivi karibuni Rais wetu mpendwa Dk John Magufuli ametoa taarifa kuwa nchi yetu imetangazwa  kuingia kwenye uchumi wa kati hivyo ni hatua nzuri na tunapaswa kumuunga mkono rais kwa maenndeleo ya taifa letu.



Aidha Amesema Pia anamshukuru sana Muanzirishi wa   Women tap Bi.Devotha Likokola kwa maono yake ya kuwainua wanawake ya kijamii na kiuchumi amemuahidi kumpa ushirikiano wa kila hatua na asisite kupeleka fursa nyengine katika mtaa na kata ya Bonyokwa  alisema Maliyatabu.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages