NBC YADHAMINI MAONESHO SABASABA KWA MWAKA WA TATU MFULULIZO

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), akiangalia baadhi ya vifaa vinavyotengenezwa na Kampuni ya Uzalishaji wa fenicha na Uuzaji wa mashine ya Azienda Group Limited, katika banda la wajasiriamali wadogo na wa kati lililodhaminiwa na benki ya NBC wakati wa ufunguzi wa  maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba hivi karibuni. NBC mdhanini mkuu wa maonesho hayo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara za Kibenki, ElvisNdunguru na kushoto ni Mshauri wa Mambo ya Kibiashara wa Azienda Group Limited, Hekala Sigalla.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akitembelea banda la wajasiriamali lililodhaminiwa na Benki ya NBC wakati wa ufunguzi wa  maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba hivi karibuni. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi. NBC ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Ofisa Mahusiano wa Benki ya NBC, Lena Mwakisale (wa pili kulia) akizungumza na baadhi ya watu waliofika katika banda la Kliniki ya biashara lililodhaminiwa na benki hiyo wakati wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba jana. Kulia kwake ni baadhi ya wafanyakazi wenzake. NBC ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC, Upendo Njogolo (kushoto), akitoa maelezo kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na NBC na pia katika banda la benki hiyo wakati wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba, jijini humo jana. NBC ni mdhamini mkuu wa maonesho hayo.
Ofisa Mkuu wa Usimamizi wa Kodi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Justine Katiti (kulia) akizumzumza na Mfanyabiashara Saidi Lugendo, kuhusu masuala ya kodi katika banda la Kliniki ya biashara linalodhaminiwa na benki ya NBC wakati wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salaam jana. NBC ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Mshauri wa Mambo ya Kibiashara wa Kampuni ya Uzalishaji wa fenicha na Uuzaji wa mashine ya Azienda Group Limited, Hekala Sigalla (kushoto), akitoa maelezo kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kulia), kuhusu vifaa vinavyotengenezwa na kampuni yake katika banda la wajasiriamali wadogo na wa kati lililodhaminiwa na benki ya NBC wakati wa ufunguzi wa maonesho ya 44 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba hivi karibuni. NBC mdhamini mkuu wa maonesho hayo. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na Mkurugenzi wa Huduma za Biashara za Kibenki, Elvis Ndunguru.
Baadhi ya watu wanaofika katika maonesho ya Sabasaba wakipata taarifa mbalimbali kuhusu huduma za kibenki za NBC pamoja na masuala mengine ya kibiashara kutoka kwa washirikika wa NBC kama vile TRA, BRELA, TBS na wengineo katika katika banda la Kliniki ya Biashara ya NBC lililodhaminiwa na benki hiyo.

Benki ya Taifa ya Bishara kwa mara nyingine tena imekuwa mdhamini wa maonesho ya 44 ya Biashara ya Kimataifa maarufu kama Sabasaba yanayofanyika Kurasini jijini Dar es Salaam katika viwanja vya maonesho vya Mwalimu Nyerere kuanzia Julai 1 hadi 13 mwaka huu.

Maonesho hayo ambayo yanakutanisha wajasiliamari, Wafanyabiashara, Wazalishaji na Watoa huduma mbalimbali yanafanyika katika kipindi ambacho wananchi wanatakiwa kuchukua tahadhari za kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya mapafu maarufu kama Corona.

Theobald Sabi, Mkurugenzi Mtendaji NBC katika uzinduzi wa maoneesho hayo leo, amewaambia Waandishi wa Habari kuwa lengo kuu la udha mini wa benki hiyo kwa taasisi hizo za fedha ni kuwawezesha wajasiliamari wadogo na wa kati ambao ndiyo walengwa wakuu wa maonesho hayo kujifunza na kutumia fursa zilizopo katika soko la ndani la nje katika kuuza bidhaa na huduma wanazozizalisha na kuzitoa.

Benki ya NBC pia inalenga katika kuwasogezea wateja wake huduma zake karibu zaidi kupitia maonesho hayo.

“Katika benki yetu ya NBC tunayo huduma maalumu ambayo inalenga katika kuwawezesha wajasiliamari, wafanyabiashara wadogo na wa kati kuona na kuchangamikia fursa za masoko ya ndani nay a nje ya bidhaa na huduma wanazozitoa na kuzalisha;

Pia tumekuwa tukitoa mafunzo ya kibishara kwa makundi haya ya wafanyabiashara, kuwafundisha mbinu za uzalishaji bora na ufungashaji wa bidhaa zao ili ziweze kuvutia na kushindana kimataifa” alisema Sabi.

Elvis Ndunguru, Mkurugenzi wa Huduma za Biashara za Kibenki kutoka NBC Alisema kuwa benki ya NBC imewaalika wajasiriamali wadogo na wa kati ambao ni wanufaika wa mafunzo na uwezeshwaji wa NBC.

Aliwataja wajasiliamari hao kuwa ni Miku Investment Company Limited wazalishaji na wauzaji wa vipodozi, Borah Lemmy Rothblets wauzaji wa asali na mafuta ya alizeti, Takecharge International Limited, na Azienda Group Limited wazalishaji wa samani na mashine. Wengine ni kampuni za Chelsea Tyre Tube wauzaji wa vipuri vya magari na kampuni ya Dagen Traders wauzaji wa vitenge.

“Baadhi ya wajasiliamari hao wamealikwa na benki katika maonesho ya biahsra ya mwaka huu watatumia fursa hiyo kudhihirisha ni kwa namna gani NBC imekuwa taasisi muhimu katika kuwawezesha na hivyo kuchangia ukuaji wao. Tumekuwa pia tukiwawezesha wajasiliamari katika sekta ya madini, ufugaji kuku, ng’ombe, mbuzi, sekta ya uzalishaji amzao ya kilimo na uvuvi” aliongeza Ndunguru.

Akifungua maonesho hayo Ijumaa, Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amezisifu beni za biashara nchini kwa mchango wake wa kuiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa kati kabla ya mwaka 2025. Alisema sekta ya fedha ni muhimu katika ukuaji wa uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na hatimaye taifa kwa ujumla.

“Serikali itaendelea kuweka mazingira wezeshi kwa sekta binafsi zikiwemo benki za biashara ili ziendelee kufanya kazi zake vizuri na kwa mafanikio. Serikali inazihimiza benki kuendelea kuto amikopo ya masharti na riba nafuu kwa wafanyabiashara hususani wajasiriamali ili waweze kukuza biashara zao na hivyo kuongeza wigo wa vipato vyao na ajira” alisema Majaliwa.

Kampuni ya Chelsea Tyre Tube inayojishughulisha na uingizaji na uuzaji wa vipuri vya magari na matairi imekuwa mnufaika wa mikopo ya NBC tangu mwaka 2004 na inajivunia ukaribu wake na NBC katika mafanikio ya bishara yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Martin Massawe, alisema kuwa kampuni yake imekuwa mnufaika wa mikopo ya masharti na riba nafuu kwa miaka zaid ya kumi hivi sasa. Alisema kuwa kampuni imekuwa na mtandao mzuri wa kibiashara kutokana na ushirika wake na NBC. Pia mafunzo mbalimbali yametolewa kwa wafanyakazi wa kampuni yake juu ya kujenga mahusiano ya kibiashara na utafutaji soko.

NBC ni benki yenye uzoefu zaidi nchini ambayo imekuwa ikitoa huduma za kifedha kwa miongo mitano sasa ikihudumia wateja binafsi, biashara ndogo, kubwa, makampuni na uwekezaji. Kwasasa benki ina mtandao wa mawakala zaidi ya 3,000 wakitoa huduma katika matawi yake 49 yaliyosambaa kote nchini.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages