NBC yadhamini Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezeji katika Sekta ya Madini

Wakala wa Mauzo katika Kitengo cha Hazina na Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya NBC, Emmanuel Charles Gasirabo akihojiwa na vyombo vya habari wakati wa mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo.
Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa (kushoto), akitembelea mabanda ya maonyesho ya wadau wa sekta ya madini wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo. Anayemuongoza katikati ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Kamishna wa Tume ya Madini, Prof. Abdulkarim Mruma, akishikana mikono na Meneja Mahusiano wa Taasisi za Umma wa Benki ya NBC, Azza Mnzava (wa pili kushoto), mara baada ya kamishna huyo kutembelea banda la NBC wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo. Wengine kushoto ni Wakala wa Mauzo katika Kitengo cha Hazina na Masoko ya Fedha za Kigeni, Emmanuel Gasirabo (kushoto), na Meneja Mahusiano Kitengo cha Wateja Rejerejea Maalumu, Daniel Kaila.
Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, akisalimiana Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mine, Simon Shayo baada ya kutembelea banda la NBC wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo. Kulia ni Ofisa Mahusiano wa NBC kitengo cha Wateja Maalumu, Daniel Kaila.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia), akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mine, Simon Shayo baada ya kutembelea banda la NBC wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano wa Taasisi za Umma wa NBC, Azza Mnzava na Wakala wa Mauzo katika Kitengo cha Hazina na Masoko ya Fedha za Kigeni, Emannuel Gasirabo.
Share:

WATEJA WA NBC WAENDELEA KUIBUKA KIDEDEA KUPITIA NBC MALENGO

Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa droo ya mwezi Januari ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo ambapo jumla ya washindi watano walijishindia pikipiki mpya kila mmoja. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli Masudi, Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye, Meneja Kampeni ya Malengo, Mtenya Chewa na mmoja wa washindi wa bodaboda wa droo ya Disemba, Rosemary Kibodya.
Meneja wa Kampeni ya Malengo wa Benki ya NBC, Mtenya Cheya ( wa pili kulia), akiziungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa droo ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo aliyejishindia bodaboda. Juma ya washindi watano walishinda zawadi hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli Masudi, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye na mshindi wa bodaboda wa mwezi Disemba.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia), akikabidhi zawadi ya bodaboda kwa Bi. Rosemary Kibodya, mmoja wa washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo. Makabidhiano hayo yalifanyika pamoja na droo ya mwezi Januari ambapo jumla ya washindi watano waliojishindia bodaboda walipatikana. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Tawi la Corporate, Mariam Kombo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye.
Meneja wa Tawi la NBC Corporate, Mariam Kombo akikabidhi kadi ya pikipiki kwa Rosemary Kibodya, mmoja wa washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo. Makabidhiano hayo yalifanyika pamoja na droo ya mwezi Januari ambapo jumla ya washindi watano waliojishindia bodaboda walipatikana.

Dar es Salaam Februari 19, 2020. BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), moja ya benki kongwe nchini imeendelea kuboresha maisha ya wateja wake kwa kuendelea kutoa zawadi mbalimbali kupitia kampeni yake inayoendelea ya akaunti ya Malengo iitwayo 'Ibuka Kidedea na NBC Malengo'.

Akizungumza wakati wa droo ya Mwezi Januari katika droo za kila mwezi za kampeni ya Ibuka Kidedea jijni Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo alisema kampeni hiyo imeendelea kufanya vizuri tokea ilipozinduliwa Oktoba mwaka jana, ikishuhudia wateja wa zamani wakiweka amana katika akaunti zao za Malengo huku wateja wapya wakijiunga na NBC Malengo ili kujishindia zawadi na kunufaika na manufaa lukuki yanayopatikana sambamba na akaunti hiyo.

“Tunaposema ‘Ibuka Kidedea' ni kweli tunamaanisha, Kwani mjuavyo hadi sasa jumla ya washindi 10 wamejishindia zawadi za bodaboda huku washindi nane wameshinda safari za mapumziko kwenda sychelles na Serengeti.

“NBC Ibuka Kidedea imekuja kusaidia watanzania kutimiza malengo yao. Watanzania wana malengo mbalimbali kila mmoja ana malengo yake, natoa wito kwa wateja wetu na wasio wateja kujiunga na NBC Malengo ili kutimiza malengo yenu kwa urahisi na uhakika”, alisema Bi. Maria.

Bi Maria aliongeza kuwaNBC inajali maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla na ndio sababu kila mara imekuwa ikiingiza bidhaa na huduma zinazoendana na kukidhi mahitaji halisi ya watanzania.

“NBC ni benki ya kizalendo, tunajua fika mahitaji halisi ya watanzania, tunajua mahitaji ya wateja wetu, akaunti ya Malengo ya NBC ni moja ya fursa iliyoletwa na NBC ili kumuwezesha mteja wetu kujiwekea akiba kidogo kidogo ili kutimiza malengo yake.

“NBC tunataka wateja wetu na watanzania wawe na utamaduni wa kujiwekea akiba hata Kama ni kidogo kidogo kwani mswahili wanasema 'bandu bandu humaliza gogo”, alisema.

Pamoja na hayo meneja huyo anasema wale wote wanaojiunga na NBC Malengo sio tu kupata nafasi ya kuibuka kidedea lakini pia wanashuhudia akaunti zao zikipata faida nono  kila mwezi hivyo kuwasaidia kutimiza malengo yao.

“NBC hatuishii kwenye Malengo tu, tunaposema 'NBC Daima Karibu Nawe' tunamaanisha kuwa NBC ipo karibu na kila mmoja anayehitaji huduma za kibenki, iwe ni akaunti za vikundi, wanawake, mikopo ya aina mbalimbali, huduma za kibenki kwa wajasiriamali, wafanyakazi, katika sekta za kilimo na madini, kila mahali NBC tupo”, aliongeza Bi Maria.

Katika droo ya leo waahindi watano waliibuka kidedea na kujishindia pikipiki mpya aina ya Yamaha kila mmoja huku zawadi kubwa ikipangwa kuwa pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo itakayotolewa katika droo kubwa inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Mbali na droo hiyo pia mshindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana Bi. Rosemary Kibodya wa Dar es Salaam alikabidhiwa pikipiki yake katika tukio lililoshuhudiwa pia na wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
Share:

Nabii Suguye Vijana Mtandaoni Mnatafuta Nini

Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga jijini Dar es Salaam akiwahubiria waumini wa kanisa hilo (hawapo pichani) kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Waumini wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, jijini Dar es Salaam wakifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kanisani hapo wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Mmoja wa waumini wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, jijini Dar es Salaam, Msanii wa Maigizo nchini Jennifer Kyaka maarufu Odma akifuatilia matukio mbalimbali yaliyokuwa yakiendelea kanisani hapo wakati wa maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Mmoja wa wanenaji waliopata nafasi ya kuhubiri kanisani hapo Askofu Mkuu wa kanisa la CAG, Mtume Danstan Haule Maboya akiwahubiria waumini wa kanisa hilo (hawapo pichani) kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)
Nabii Nicolaus Suguye wa Kanisa la WRM lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga jijini Dar es Salaam akiteta jambo na Mkewe Mwinjilisti Mkuu Anna Suguye kwenye maadhimisho ya kutimiza miaka 13 ya huduma hiyo tangu ianzishwe. (Picha na Phineas Godfrey)

Na Mwandishi wetu,

Nabii wa Kanisa la WRM lenye makao yake makuu Kivule Matembele ya Pili, Nicolaus Paul Suguye amewashangaa vijana wengi siku hizi kutumia muda wao mwingi kwenye mitandao ya kijamii kutuma na kutafuta picha zisizofaa na mijadala isiyo tija katika maisha yao.

Nabii Suguye ni mwanzilishi na mbeba maono wa huduma ya upatanisho ya WRM ameyasema hayo kwenye sherehe za maadhimisho ya miaka 13 tangu kuanzishwa kwa huduma hiyo ambayo ilianza rasmi tarehe 14 februari, 2007 hapo hapo Kivule Matembele ya Pili.

“Biblia inasema…..mkumbuke Muumba wako siku za ujana wako, Kabla hazijaja siku zilizo mbaya, Wala haijakaribia miaka utakaposema, Mimi sina furaha katika hiyo….. wa unasema mimi hapa sasa hivi nina nguvu, naweza nikafanya chochote, ndio muda sahihi Mungu anataka ukamtumikie”, alisema Nabii Suguye.

Suguye aliongeza kwa kusema “Wito wangu kwa vijana waache maovu wamkimbilie Mungu, kwake yeye kuna kila kitu, anaweza kuyasamehe makosa yao na kuwabariki badala ya kutumia muda wao mwingi kwenye mitandao na kuchafua watu, kuandika lugha zisizofaa mitandaoni, na kutazama picha zisizofaa zitakazoharibu mustakabali wa maisha yao ya baadaye.”

“Ikumbukwe nguvu kazi ya Taifa iko kwa vijana, hivyo tukiwa na vijana wenye hofu ya Mungu, Mungu atajivunia na taifa pia litajivunia” alimalizia Suguye.
Share:

DCB FURSA MPYA YA ELIMU KWA WATANZANIA HADI CHUO KIKUU KUPITIA AKAUNTI ZA DCB SKONGA NA DCB MINI SKONGA

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB, James Ngaluko (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Godfrey Ndalahwa na Mkurugenzi wa Masoko, Rahma Ngassa (kulia), wakati wa uzinduzi wa DCB Skonga jijini Dar es Salaam hivi karibuni.

Na Mwandishi wetu,

KATIKA kuhakikisha wazazi na walezi wanakuwa na uhakika wa elimu ya watoto wao, Benki ya Biashara ya DCB imeongeza fursa zaidi kupitia akaunti yake DCB SKONGA kwa kuongeza DCB MINI SKONGA Ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika kuboresha sekta ya elimu nchini. 

Akizungumza kuhusu fursa hizo, Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James Ngaluko alisema tofauti na mpango wa DCB Skonga uliokuwepo awali ambapo mzazi alipaswa kuweka akiba kuanzia mwaka mmoja hadi 17, sasa kwa kupitia DCB mini skonga mzazi anaweza kuweka akiba kidogo kidogo kwa kipindi cha miezi 12 na kupata uhakika wa elimu ya mtoto wake kwa muda wa miaka mitatu. 

‘’mpango huu mpya wa DCB MINI SKONGA’’ mzazi au mlezi anakuwa na uhakika wa elimu ya mtoto kupitia akiba yake anayoweka kila mwezi lakini pia pindi anapopata ulemavu wa kudumu au kupoteza maisha, mtoto atasomeshwa kwa kipindi cha miaka mitatu bure. 

Mkurugenzi huyo alisema licha ya DCB kuanzisha mpango huu mpya, bado wazazi wanaweza kuendelea kuweka akiba kupitia mpango wa awali wa ‘’DCB SKONGA’’ ambapo mzazi anapata uhakika wa elimu ya mtoto wake hadi chuo kikuu kutokana na mpango aliouchagua kuanzia mwaka mmoja hadi miaka 17. 

Kuhusu bidh aa hizo za DCB Skonga Bwana Ngaluko alisema watanzania wengi hasa wenye kipato cha wastani hukabiliwa na hofu nyingi mara wawazapo hatima ya elimu ya watoto wao kutokana na changamoto mbalimbali zinazoweza kutokea kiasi cha kupunguza ama kuondoa kabisa uwezo wao wa kulipa gharama za elimu na mahitaji mengineyo. 

“Kwa kupitia DCB Skonga au Mini Skonga mteja anapata fursa ya kuamua kiwango cha kuwekeza kila mwezi kwa ajili ya kutimiza ndoto zake lakini pia kupata uhakika wa elimu ya mtoto wake, DCB tunaondoa hofu ya mzazi kwani endapo kutatokea majanga yatakayosababisha ulemavu wa kudumu ama kifo kabla ya muda kukamilika, mtegemezi atarudishiwa kiasi cha pesa kilichowekwa tokea mwanzo na mtoto atalipiwa gharama zote za elimu pamoja na hela ya matumizi ya shule kwa kipindi chote kilichosalia cha mkataba” 

“Natoa hamasa kwa wateja wetu na watanzania kwa ujumla kuzitumia fursa za akaunti hizi kwani ndio suluhisho bora na lenye uhakika kwenye masuala ya elimu ya watoto wetu. 

DCB tumeweka kipaumbele katika kutekeleza mipango ya serikali ya awamu ya tano kwa kutoa huduma za kibenki kwa Watanzania nchi nzima katika kutoa fursa na bidhaa zenye tija kwa wateja wetu. Elimu ni kitu muhimu sana kwenye maisha yetu hivyo tunaamini watanzania watakimbilia fursa hii ili kuwapa uhakika wa elimu watoto wao’’, aliongeza bwana Ngaluko 

Nae Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano, Bi Rahma Ngassa aliongeza ‘’kupitia bidhaa hii ya DCB Mini Skongana DCB Skonga mteja anakuwa na uhakika wa usalama wa pesa zake, uhakika wa elimu ya mtoto hadi chuo kikuu, gawio nono la kila mwaka, uhakika wa mkopo wa dharura hadi asilimia 50 ya kiwango cha akiba alichowekeza, bima ya mazishi endapo mwenye akaunti/mume/mke au mtoto atakapofariki. 

“Wazazi walindeni watoto wenu, wekeni mazingira bora ya maisha ya baadae, na njia pekee ya kuwezesha hili ni kujiunga na akaunti za DCB Skonga kwani licha ya manufaa ya elimu kwa watoto, endapo ukichangia kwa kipindi chote cha mkataba bila kusitisha kwasababu yoyote, benki itakurudishia amana zako zote ulizowekeza hivyo kukupa fursa ya kujiendeleza zaidi”.
Share:

Absa Tanzania yawahakikishia wateja wake huduma bora zaidi

Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dr. Bernard Kibesse (katikati), akiinua glasi ili kuitakia mafanikio bora benki ya Absa Tanzania akiwa pamoja na, kutoka kushoto; Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya, Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon Mponji na Mjumbe wa Bodi ya Absa Tanzania, DK. Suleiman Mohamed. Naibu Gavana Kibesse alikuwa megni rasmi katika hafla iliyoandaliwa na Absa kwa wateja wake jijini Dar es Salaama jana.  
Benki Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed alipoenda kuwa mgeni rasmi katika  hafla iliyoandaliwa na  benki hiyo kwa ajili ya  wateja wake jijini Dar es Salaam jana  ili kuwapa taarifa mbalimbali za utendaji wa benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya na Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon Mponji.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), akikaribishwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Absa Tanzania, Simon Mponji alipoenda kuwa mgeni rasmi katika  hafla iliyoandaliwa na  benki hiyo kwa wateja wake jijini Dar es Salaam jana  ili kuwapa taarifa mbalimbali za utendaji wa benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania.. Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Absa wa Kanda, Saviour Chibiya na Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse (wa nne kushoto), akigonganisha glasi na wakurugenzi wa Benki ya Absa Tanzania katika hafla waliyowaandalia wateja wao jijini Dar es Salaam jana ili kuwapa taarifa mbalimbali za benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania. Kutoka kushoto ni Mjumbe wa Bodi, Dk. Suleiman Mohamed, Mkurugenzi wa Fedha, Obedi Laiser, Mwenyekiti wa Bodi, Simon Mponji na Mkurugenzi Mtendaji, Abdi Mohamed.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed (wa pili kulia), akiwa na baadhi ya wateja wa benki hiyo waliohudhuria hafla hiyo katika Hoteli ya Serena, Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed (kulia), Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Absa Tanzana, Aron Luhanga (katikati), pamoja na baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa Absa wakigonganisha glasi ili kutakiana afya bora pamoja na mafanikio ya benki hiyo nchini.
Mkurugenzi Mtendaji wa Absa Tanzania, Abdi Mohamed, akigonganisha glasi na mmoja wa wakurugenzi wa benki hiyo, Esther Maruma (kushoto), katika hafla hiyo. Kulia ni Naibu Gavana wa BoT, Dk. Bernard Kibesse na Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda wa Absa, Saviour Chibiya.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Benard Kibesse akizungumza katika hafla iliyoandaliwa na Benki ya Absa Tanzania kwa ajili ya wateja wake na wadau wengine ili kuwajulisha mikakati mbalimbali ya benki hiyo ambayo awali iliitwa Barclays Tanzania.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Absa Tanzania, Oscar Mwamfwagasi (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Selcom Tanzania, Sameer Hirji, mmoja wa waalikwa waliohudhuria katika hafla hiyo katika Hoteli ya Serena, jijini Dar es Salaam jana.
Share:

NBC kuendelea kuwainua wanawake na vijana wajasiriamli kiuchumi

Mkurugenzi wa Bima wa Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kulia) akizungumza na baadhi ya washiriki wa warsha ya wanawake na vijana wajasiriamali kuhusu masuala ya uchumi iliyoandaliwa na kampuni ya GS1 na kudhaminiwa na Benki ya NBC jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu wa Kanisa la Mennonite Tanzania, Askofu Nelson Kisare akisalimiana na Mkurugenzi wa Bima wa Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kushoto), wakati wa warsha ya wanawake na vijana wajasiriamali kuhusu masuala ya uchumi iliyoandaliwa na kampuni ya GS1 na kudhaminiwa na Benki ya NBC jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Mkurugenzi wa Bima wa Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kushoto) akisalimiana na Balozi wa Heshima wa Zanzibar katika Shirikisho la Jamhuri ya Brazil, Abdulsamad Abdulrahim, wakati wa warsha ya wanawake na vijana wajasiriamali kuhusu masuala ya uchumi iliyoandaliwa na kampuni ya GS1 na kudhaminiwa na Benki ya NBC jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kulia ni Mwenyekiti wa Baraza la Maaskofu kanisa la Mennonite Tanzania, Askofu Nelson Kisare.
Mkurugenzi wa Bima wa Benki ya NBC, Benjamin Nkaka (kushoto) akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya GS1, Fatma Kange, wakati wa warsha ya wanawake na vijana wajasiriamali kuhusu masuala ya uchumi iliyoandaliwa na kampuni ya GS1 na kudhaminiwa na Benki ya NBC jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali wakihudhuria warsha hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya GS1 na kudhaminiwa na NBC, jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Baadhi ya washiriki waliohudhuria warsha hiyo iliyoandaliwa na Kampuni ya GS1 na kudhaminiwa na NBC, jijini Dar es Salaam hivi karibuni wakipewa maelezo kuhusu huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa na NBC ikiwemo akaunti ya wanawake ya Hakika na akaunti ya vikundi kutoka kwa maofisa wa NBC katika sehemu maalumu iliyoandaliwa na benki katika warsha hiyo ili kuwahudumia. Washiriki hao pia waliweza kufungua akaunti ya Fasta ya NBC mahali hapo na kupewa kadi ya Visa papo hapo.
Share:

BARCLAYS BENKI TANZANIA SASA YAWA RASMI ABSA BENKI TANZANIA


Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Dkt Bernard  Kibesse (wa pili kushoto), na Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Absa Tanzania, Simon Mponji (kulia), wakikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa Benki ya Absa Tanzania ambayo awali ikiitwa Barclays Benki Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala ya Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Emmanuel Kakwezi, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed na Mkurugenzi wa Chama cha wenye Mabenki (TBA), Tuse Jumbe.
Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya Absa Tanzania, Simon Mponji, akipokea cheti cha kubadilisha jina la kufanyia biashara kama  Benki ya Absa Tanzania kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Emmanuel Kakwezi (wa pili kushoto), katika hafla ya uzinduzi rasmi wa benki ya Absa Tanzania jijini Dar es Salaam jana. Awali iliitwa Benki ya Barclays Tanzania. Wanaoshuhudia kutoka  ni; Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Bernard Kibesse (wa pili kulia) pamoja na washuhudiaji wengine.
Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT),Dkt Bernard  Kibesse akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa Benki ya Absa Tanzania ambayo awali ikiitwa Barclays Benki Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Absa Tanzania, Simon Mponji, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, Mkuu wa Kitengo cha Sheria na udhibiti wa Benki hiyo, Irene Sengati.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Abdi Mohamed, akizungumza wakati wa  hafla ya uzinduzi rasmi wa Benki ya Absa Tanzania ambayo awali ikiitwa Barclays Benki Tanzania.
Wafanyakazi wa Benki ya Absa  Tanzania wakifanya maandamano ya amani kuashiria uzinduzi rasmi wa Benki ya Absa Tanzania ambayo awali ikiitwa Barclays Benki Tanzania.
Share:

NBC yazindua kampeni ya Kijanisha Dodoma kwa kupanda miti 1000


Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu (aliyepiga magoti), akizindua rasmi zoezi la upandaji miti lililopewa jina la Kijanisha Dodoma na kudhaminiwa na Benki ya NBC katika mtaa wa Swaswa Halmashauri ya jiji la Dodoma likiwa na lengo la kutunza mazingira katika mkoa huo.  Nyuma ya mheshimiwa waziri ni Meneja wa Kanda ya kati wa NBC James Ndimbo, Afisa mauzo wa benki hiyo, Zachalia Lema (kushoto),  pamoja na Mkuu wa huduma kwa Wateja,  Anne Mwasaka. Upandaji miti huo umefanyika Dodoma hivi karibuni.
Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya NBC James Ndimbo, akipanda miti huku wafanyakazi wa benki hiyo pamoja na na viongozi wa kata ya Swaswa wakiangalia wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma  uliofanyika mkoani humo kwa udhamini wa Benki ya NBC hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu (kushoto), akishikana mikono na Afisa Mauzo wa Benki ya NBC, Dodoma, Zachalia Lema wakati wa uzinduzi rasmi wa kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma  uliofanyika mkoani humo kwa udhamini wa Benki ya NBC hivi karibuni.
Mkuu wa Idara ya Mazingira na Udhibiti wa taka ngumu Halmashauri ya jiji la Dodoma, Dickson Kimaro akipanda mti mara baada Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Mhe. Mussa Azzan Zungu kuzindua kampeni ya upandaji miti iliyopewa jina la Kijanisha Dodoma na kudhaminiwa na benki ya NBC katika mtaa wa Swaswa Halmashauri ya jiji la Dodoma hivi karibuni.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mussa Azzan Zungu (katikati), akipiga picha ya pamoja na wafanyakazi waa NBC, wakazi wa kitongoji cha Swaswa pamoja na wakai wengine wa Dodoma walishiriki hafla ya upandaji miti lililodhaminiwa na benki hiyo.
Share:

NBC yasaidia waathirika wa mafuriko Lindi

Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (wa pili kushoto), akipokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda vililivyotolewa na benki hiyo kusaidia waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababishwa na mfua kubwa iliyonyesha mkoani humo hivi karibuni. Msaada huo ulijumuisha mashuka 1,000, katoni 1,000 za sabuni, kilo 500 za mchele, kilo 1,500za unga wa mahindi, kilo 750 za maharage na mikate 500. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (wa pili kushoto), akizungumza kabla ya kupokea msaada wa vitu mbalimbali kutoka kwa Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda (wa tatu kushoto), vililivyotolewa na benki hiyo kusaidia waathirika wa maafa ya mafuriko yaliyosababishwa na mfua kubwa iliyonyesha mkoani humo hivi karibuni. Msaada huo ulijumuisha mashuka 1,000, katoni 1,000 za sabuni, kilo 500 za mchele, kilo 1,500 za unga wa mahindi, kilo 750 za maharage na mikate 500. Kushoto ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Lindi, Rehema Madenge.
 
NA MWANDISHI WETU

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa misaada mbalimbali kwa waathirika wa mafuriko ya yaliyotokea mkoani Lindi Januari 27 mwaka huu na kusababisha vifo, uharibifu wa mali, makazi na miundombinu.

Akizungumza wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi, misaada hiyo hivi karibuni, Meneja wa NBC Mkoa wa Lindi,Iovin Mapunda alisema benki hiyo ya kizalendo imeguswa sana na tukio hilo na kuona umuhimu wa kusaidia.

“Tukiwa kama benki ya Kitanzania, tunaamini kuwa ni muhimu kwa watu waliokumbwa na majanga asilia kama haya kusaidiwa ili waweze kurejea katika maisha ya kawaida,” alisema.

Katika hafla hiyo NBC ilitoa msaada wa mashuka 1,000, katoni 1,000 za sabuni, kolo 500 za mchele, kilo 1,500 za unga wa mahindi, kilo 750 za maharage na mikate 500.

“Wafanyakazi wa NBC ma uongozi wake tupo pamoja nanyi katika kipindi hiki cha majonzi yaliyoletwa na tukio lisilotarajiwa linalotokana na hali ya hewa na sasa limechukua maisha ya Watanzania wenzetu.

“Tunaamini kuwa tunawajibika kuchangia chochote na hivyo kuunga mkono juhudi za serikali katika kuwasaidia wenye mahitaji,” alisema Bw.  Mapunda.

Alisema kama ilivyotangazwa, mafuriko haya yaliharibu miundombinu, shule na madaraja, nyumba hivyo kuwaacha wakazi wa maeneo hayo bila makazi jambo linaloweza pia kusababisha kuenea kwa magonjwa ya mlipuko.

“Tunaahidi kuendelea kushirikiana na serikali katika kuwasaidia waathirika wa majanga mbalimbali kwani ni wajibu wetu kutoa sehemu ya faida kwa jamii,” alisema.

Pamoja na hayo, Bw. Mapunda aliongeza kusema: “Kama benki kongwe nchini tukiwa na uzoefu katika kutoa huduma bora za kibenki kwa zaidi ya miaka 53 sasa, NBC tunaweka msisizitizo mkubwa katika kuhudumia jamii, hapa Lindi tumeunga mkono pia juhudi za serikali kwa kutoa msaada wa vifaa vya ujenzi wa majengo ya vituo vya polisi na shule.”
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages