Wateja watano wajishindia bodaboda na Ibuka Kidedea na NBC Malengo

Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya Malengo ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya bodaboda kila mmoja.  Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo na kulia kabisa ni mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.
Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (mbele kulia), akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya pikipiki aina ya Yamaha kila mmoja.  Washindi wa leo ni; Augustine Hatari kutoka Pwani, Williumu Pendaeli Isack wa Moshi, Scholastica Peter Yamawasa, Honest Christopher Kimaro na Daudi Majani wote kutoka Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,

WATEJA Watano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wameibuka washindi wa bodaboda mpya aina ya Yamaha katika droo ya kwanza ya kampeni ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC” kupitia akaunti ya Malengo ya benki hiyo kongwe hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwenye droo ya kwanza ya kampeni hiyo iliyoanza mwezi wa Oktoba, Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo alisema kwamba akaunti ya malengo inampa mteja njia rahisi ya kuweka akiba kidogo na kupata faida kubwa kila mwezi.

“kwenye akaunti hii ya malengo kila Tsh 100,000 atakayoweka mteja kwenye akaunti hii inampa nafasi ya kushida zawadi kemkem ikiwemo bodaboda ambapo leo droo ya kwanza itashuhudia wateja hawa watano wakipata zawadi zao,” alisema Kimaryo.

Aliongeza kwamba katika kipindi chote cha kampeni bodaboda tano aina ya Yamaha zitatolewa kila mwezi na safari tatu za kwenda kufanya utalii Serengeti na safari tano za kwenda Seychelles mwezi wa Disemba na washindi wanaruhusiwa kwenda na mtu mmoja kwenye safari hizo.

“ukiwa na akaunti ya NBC malengo unapata faida nyingi ikiwemo ya kuhifadhi fedha kwa ajili ya kutimiza malengo na ndoto zako pamoja na mambo mengine ya kupata riba ya hadi asilimia 7 ya pesa uliyoweka kila mwezi,’ alisisitiza Kimaryo.

Washindi kwenye droo ya jana walikuwa ni Augustine Hatari kutoka Pwani, Daudi Majani, Dar es Salaam, Williumu Pendaeli Isack, Moshi Kibololoni, Scholastica Peter Yamawasa, Dar es Salaam, na Honest Christopher Kimaro wa Dar es Salaam.

Katika kampeni hii wateja watakao ongeza salio kwa kiasi Tsh milioni moja kwenye akaunti ya Malengo watapata nafasi ya kushinda zawadi kuu ya TOYO na jumla ya TOYO tatu zitatolewa kwenye kampeni hiyo ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC MALENGO”.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages