Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto), aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani Morogoro, akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati akizindua rasmi klabu hiyo mkoani humo jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru.
Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (wa tatu kushoto), aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani humo jana, akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein katika uzinduzi wa klabu hiyo Mkoani Morogoro jana. Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa mkoa huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara NBC, Elvis Ndunguru, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa kati na Wadogo, Evance Luhimbo na Meneja wa Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo.
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto), aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani humo akikaribishwa na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati akiwasili kuzindua rasmi klabu hiyo mkoani humo jana. Katikati ni Meneja wa Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo. Uzinduzi huo ulitanguliwa na semina ya siku moja juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati.
Ofisa Biashara Mwandamizi Taarifa za Biashara na Takwimu kutoka Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), Magdalena Shirima akitoa elimu kuhusu fursa za masoko ya nje ya nchi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa Biashara wa Asasi ya Kusaidia Uwekezaji kwenye Kilimo (PASS), Irene Benedicto akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Julius Mjenga akitoa elimu kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia mada katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyuabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Na mwandishi wetu, Morogoro
JUHUDI binafsi za wafanyabiashara kwa kushirikiana na taasisi za kifedha ni moja ya nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya mpango mkakati wa serikali ya awamu ya tano katika kutoa kipaumbele katika uchumi wa viwanda.
Hayo yalisemwa na Mjumbe Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dkt. Kassim Hussein katika hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC, maarufu kama ‘NBC B-Club’ ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni klabu ya 11 kuzinduliwa katika mikoa mbalimbali nchini.
“Kwenye biashara serikali imefanya mageuzi makubwa mfano katika kuwahamasisha wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki, kurasimishwa kwa biashara, lakini kunahitaji juhudi kubwa katika kuangalia masuala ya masoko, vifungashio, mitaji na viwango vya TFDA ili kufanya biashara hizo zikue”, alisema.
Ni kutokana na hayo alisema NBC B-Club itakuwa faida kubwa kwa wafanyabiashara na nguvu ya kuleta maendeleo kwa taasisi na mtu mmoja mmoja, huku benki NBC ikiongeza mafunzo ya mara kwa mara kwa kuleta wataalam mbalimbali na kutoa punguzo la riba kwa wanachama wa klabu hizo.
Akizungumza zaidi kuhusu klabiu hiyo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara NBC, Elvis Ndunguru, alisema lengo pia ni kuwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali ili kuweza kubadilishana uzoefu, kupata fursa mbalimbali za masoko ndani na nje ya nchi pamoja na kuwaunganisha na wafanyabiashara wa nje.
Ndunguru alisema ni rahisi kutoa nafasi ya elimu kwa wafanyabiashara hao kupitia klabu zao, kwenye maeneo wanayobaini yanayotakiwa elimu baada ya kupata mrejesho toka kwa wateja wao.
“Klabu za Biashara tumeshazianzisha maeneo mbalimbali Tanzania, lakini lengo hasa ni kuwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali ili kuweza kugundua fursa, kuwapa elimu, kuleta wataalam tofauti, pia kuna fursa za kupeleka wafanyabiashara katika nchi mbalimbali” alisema Ndunguru.
Pia alisema wanatarajia kuongeza nchi nyingine ambazo zinafanya vizuri kibiashara ikiwemo Uturuki, Ujerumani na Marekani, na kwamba wana mpango wa kutengeneza dirisha maalum la wafanyabiashara wanawake wadogo na wakati ili kuwahamasisha zaidi kuingia katika biashara.
Awali akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Afisa Uvuvi na Mifugo Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzimu, alisema Klabu hiyo itawawezesha wanachama hao kuwa na uelewa wa biashara wa kisasa, na kwamba mafunzo wanayoyapata yataleta tija na kuongeza weledi katika shughuli zao.
Chamzimu aliwataka wafanyabiashara hao kujitokeza na kujiunga kwa wingi katika klabu hiyo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.
Kwa upande wao Wafanyabiashara hao akiwemo Bupe Kamugisha wameipongeza benki hiyo kwa huduma bora na masharti nafuu ya kuchukua mikopo, na kusema kwamba imekuwa haina vitendo vya kutaifisha mali za wateja wao pindi wanapopata ugumu kwenye marejesho.
Nae mfanyabiashara Lusako Mwakiluma alisema mafunzo waliyoyapata toka kwa taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) yatawasaidia kuboresha biashara zao sambamba na kujua utaratibu unaowapasa kufuata ili kuweza kukidhi viwango vinavyotakiwa.
Uzinduzi wa klabu hiyo ni wa 11 baada ya Klabu nyingine 10 kuzinduliwa katika mikoa mingine ikiwemo Mwanza ambayo imeonyesha mafanikio makubwa.
No comments:
Post a Comment