Rais Shein aipongeza Benki ya NBC

Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein (wa pili kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibari hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu,
Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein ameipongeza Benki ya NBC kutokana na kasi yake na juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya rais wa Zanzibar katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika mjini Zanzbar hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema pato la taifa limekuwa likikuwa mwaka hadi mwaka kutokana na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali ikiwemo Benki ya NBC.
Aidha Dk.Shein ameihimiza benki hiyo kuendelea na juhudi zake za kuimarisha mazingira bora na huduma kwa wateja wake ili kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya huduma za kifedha yanayotokea siku hadi siku na kukuza maendeleo bora nchini.
Hata hivyo ameipongeza Benki hiyo kwa kuonesha umuhimu kwa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo ya kufutarisha na kutoa huduma nyengine mbali mbali kwa jamii.
Awali akizungumza katika hafla hiyo ya futari Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC,  Dk. Kassim Hussein amesema kukuwa kwa huduma za kifedha Zanzibar pia kunatokana na huduma bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja wake.
Amesema mazingira salama yaliopo Zanzibar yanayoimarishwa na viongozi wakuu wa nchi imewezasha benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma za kifedha kwa ufanisi na umakini zaidi.
Dk. Kassim amesema  licha ya huduma mbali mbali zinazotolewa na benki hiyo pia imeanzisha huduma za kibenki zinazofuata misingi ya kiislam ambayo inatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa misingi ya sharia ya kiislamu .
Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutumia benki hiyo katika kufanya miamala mbali mbali bila kujali misingi ya dini kwani ni salama katika ukuwaji wa uchumi nchini.
Katika Hafla hiyo ya futari iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein , mawaziri , Jaji mkuu , Mufti Mkuu wa Zanzibar na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wateja wa benki ya NBC.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages