Mbunge
wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) akizungumza na waandishi wa habari
pamoja na wakazi wa Beach Pemba kata ya Mzinga jijini Dar es Salaam jana katika
ziara yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa pamoja na kusiliza kero za wakazi wa kata
hiyo.Moja ya Miundo mbinu inayotengenezwa Beach Pemba ni ujenzi wa mifereji ya
chini kwa chini ambayo inatoa maji ya mvua yanayotuama katika eneo hilo na
kumwaga moja kwa moja katika bonde la mto Mzinga.Wanne kulia ni Diwani wa kata
hiyo Job Isaack.
Diwani
Viti maalumu Manispaa ya Ilala, Sara Katanga akizungumza jambo na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana juu ya kero ya kutuama kwa maji ya mvua katika
eneo la Beach Pemba kata ya Mzinga ambayo imefanyiwa utatuzi kwa kutengenezwa
mifereji ya chini kwa chini itakayo
yaongoza maji hayo moja kwa moja katika Bonge la Mto Mzinga.
Mkazi
wa Beach Pemba, Alhaji Hassani Magogwa akitoa shukrani za dhati kwa Mbunge wa
Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (hayupo pichani) baada ya kutatua kero ya maji
ya mvua yanayotuama katika eneo hilo.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (ailyevaa shati la kaki) akiongozana na wakazi
wa kata ya mzingo baada ya kumaliza kukagua mradi wa Beach Pemba.
Mwenyekiti
wa Kamati ya ujenzi wa kituo Kikubwa cha Polisi kata ya Mzinga, Godfrey Mujungu
(kulia) akizungumza jambo na Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (watatu kushoto) baada ya kuwasili katika kata hiyo kwa aijli ya ukaguzi wa ujenzi wa
Kituo hicho kinachotengezwa kwa nguvu ya wananchi kutoka katika mitaa mitatu
ambayo ni Mwanagati, Mzinga na Magole. Wapili kulia ni Diwani wa kata hiyo, Job
Isaack na Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Mzinga, Mussa Mtani.
Msimamizi
wa ujenzi wa kituo Kikubwa cha Polisi upande wa wakazi wa kata ya Mzinga, Nasir
Suleiman (kushoto) akimuonesha Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara
maendeleo ya ujenzi wa kituo hicho ambacho kipo katika msingi.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa Kituo cha
Kikubwa cha Polisi cha kata ya Mzinga.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akifanya ukaguzi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha
Kitunda, Kivule na Msongola.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara akizungumza
na msimamizi wa ujenzi wa Barabara inayounganisha Kitunda,Kivule na Msongola
baada ya kuwasili maeneo ya Matembele kata ya Kivule katika ziara yake ya
ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa jimboni jijini Dar es Salaam jana.
Mbunge
wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (wapili kulia) akiongozana na Diwani wa kata
ya Kivule, Wilson Molel (watatu kulia) pamoja na viongozi wengine wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kuelekea katika ujenzi wa Daraja la Mto
Mzinga katika hafla yake ya ukaguzi wa miundo mbinu inayotengenezwa jimboni.
Daraja
la Mto Mzinga likimaliziwa kuwekwa kifusi.
Mkazi wa Kata ya Kivule akitoa shukrani kwa
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara (kulia) kwa kutatua kero ya Daraja la
Mto Mzinga ambalo lilikuwa ni kikwazo kikubwa cha shughuli za kiuchumi na
kijamii kuwa ngumu kwa sababu gari zilikuwa hazivuki kutokana na kuvunjika kwa
daraja hilo.Huu ni mwendelezo wa Mbunge kutimiza ahadi ambazo aliziahidi kwa
wakazi wa jimbo la Ukonga.
Mbunge wa Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara
(kulia) akiongozana na Diwani wa kata ya Kivule, Wilson Molel katika ziara ya
ukaguzi wa ujenzi wa Daraja la Mto Mzinga.
Diwani
wa kata ya Kivule, Wilson Molel (kulia) akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar es Salaam katika ziara ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Ujenzi wa Barabara
Mabibo Construction Company Limited, Charles Werongo akizungumza katika ziara
ya Mbunge wa Jimbo la Ukonga.Mkurugenzi alisema baada ya wiki tatu Daraja
litakuwa tayari kwa aijli ya matumizi ya wananchi.
Mkazi
wa kata ya Kivule pia Katibu Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo
(Chadema) wa kata hiyo, Bihimba Mpaya akitoa neno la Shukrani kwa Mbunge wa
Jimbo la Ukonga, Mwita Waitara pamoja na Diwani wa kata hiyo, Wilson Molel
kutoka na juhudi walizozifanya juu ya kupambana na kero ya Daraja la Mto Mzinga ambayo ilikuwa ni
kikwazo kikubwa kwa wakazi wa kata hiyo pamoja na wafanyakazi wa Taasisi za
Kijamii kama Walimu,Madaktari ilikuwa ni ngumu sana kufika maeneo ya kazi
mapema kutokana gari kuishia kati kutokana na kukatika kwa Daraja hIvyo kwa
Juhudi za Mbunge na Diwani wake kero imetatulika kwa muda mfupi.
No comments:
Post a Comment