WAZIRI MKUU ARIDHISHWA NA MRADI WA UJENZI WA ‘TERMINAL III’


Waziri Mkuu Kassim Majaliwa(wa pili kulia) akikagua maendeleo ya ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) Jijini Dar es Salaam leo March 23, 2018 . Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mkoa Dar es salaam Paul Makonda na kudhoto ni Msimamizi wa Mradi, Eng. Julius Ndyamukama .
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa ametembelea mradi wa ujenzi wa jengo la tatu la abiria katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) na kwamba ameridhishwa na maendeleo yake.

Mradi wa ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 70 na unatarajiwa kukamilika Juni 2019 na utakuwa na uwezo wa kuegesha ndege kubwa 24 kwa wakati mmoja, pamoja na kuhudumia abiria milioni sita kwa mwaka.

Waziri Mkuu ambaye ametembelea mradi huo leo (Ijumaa, Machi 23, 2018) amesema amefarijika na maendeleo ya ujenzi wa mradi huo pamoja na kukuta Watanzania wengi wakishiriki katika kazi za ujenzi.

“Serikali imejiimarisha katika kuboresha usafiri wa anga, ambapo kukamilika kwa jengo hili kutachangia ongezeko la ndege kubwa nyingi kutua nchini. Pia sekta ya utalii nayo itaimarika kwa kuwa watalii wanaoingia nchini wataongezeka.”

Amesema mbali na ujenzi wa jengo hilo, pia Serikali inaendelea kuvikarabati viwanja mbalimbali vya ndege nchini kikiwemo cha Musoma, Iringa, Kilwa Masoko, Lake Manyara, Lindi, Moshi, Njombe, Tanga, Simiyu, Singida na Songea ili kuboresha huduma za usafiri wa anga nchini.

Akisoma taarifa za ujenzi wa mradi Mkurugenzi wa Miradi wa TANROADS, Mhandisi Christianus Ako amesema mradi huo umeajiri wafanyakazi 1,400 kwa sasa na wanatarajia kuongeza watumishi na kufikia 1,800.

Pia wanatarajia kufanya majaribio ya kwanza ya mifumo na vifaa vya umeme kuanzia Julai, 2018 kwa kuwa tayari utekelezaji wa kazi kubwa za ujenzi wa mradi huo zimefanyika.


Share:

KUWAIT KUING'ARISHA DODOMA KWA BARABARA

Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem, akizungumzia uhusiano mzuri ambao umeendelea kuwepo kati ya Tanzania na Kuwait alipomtembelea Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb)(hayupo pichani), ofisini kwake Mjini Dodoma.
Maafisa Waandamizi wa  Wizara ya Fedha na Mipango na Ubalozi wa Kuwait wakifuatilia kwa umakini mazungumzo kati ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani) kuhusu ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma,  katika Makao Makuu ya Wizara ya Fedha na Mipango Mjini Dodoma.
 Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (Kulia) na Afisa mwandamizi kutoka Ubalozi wa Kuwait wakifuatilia mazungumzo ya Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) kuhusu ufadhili wa ujenzi wa barabara za Mkato za kuingia Makao Makuu ya Nchi Mjini Dodoma.
Msaidizi wa Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Bw. Edwin Makamba na Afisa kutoka Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Bw. Hangi Laban, wakifuatilia mazungumzo kati ya Waziri huyo na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hawapo pichani), Mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akimkabidhi zawadi Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea kwa mazungumzo Mjini Dodoma.
Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Mhe. Jassem Al-Najem (kulia) akiagana na mwenyeji wake  Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kushoto) alipomtembelea Mjini Dodoma.
Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb) (kulia) akizungumza jambo na Kamishna wa Fedha za Nje wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw. John Rubuga (katikati) baada ya kuagana na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania Mhe. Jassem Al-Najem (hayupo pichani) alipomtembelea Ofisini kwake Mjini Dodoma.
Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma
Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Kiuchumi wa Kuwait (Kuwait for Arab Economic Development Fund), imeahidi kuipatia Tanzania mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 207.3, sawa na shilingi bilioni 466.4, kwa ajili ya ujenzi wa barabara za mzunguko wa kuingia katikati ya mji wa Dodoma pamoja na mradi wa ujenzi wa barabara kutoka Morogoro hadi Dodoma, yenye urefu wa kilometa 257.
Ahadi hiyo imetolewa mjini Dodoma na Balozi wa Kuwait hapa nchini, Mhe. Jassem Ibrahim Al-Najem, alipokutana na kufanya mazungumzo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Dkt. Philip Mpango.
Balozi Al-Najem amesema kuwa mradi wa ujenzi wa barabara za mzunguko za kuingia na kutoka mjini Dodoma zitasaidia kuondoa msongamano wa magari yanayopita katikati ya mji huo kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu na vyombo vya moto baada ya Makao Makuu ya Serikali kuhamia Dodoma.
Aliahidi kuwa nchi yake kupitia Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait na taasisi washirika (Mifuko ya Waarabu) wa mfuko huo, wataendelea kushirikiana na Tanzania kwa kutoa ufadhili wa ujenzi wa miradi mbalimbali ikiwemo ya miundombinu na kilimo ili iweze kukuza uchumi na maisha ya watu wake.
Katika kipindi cha miaka 40, Serikali ya Kuwait, kupitia Kuwait Fund, imeipatia Tanzania mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni 608 kwa ajili ya kutekeleza miradi 14 ya kiuchumi katika sekta za barabara, kilimo, umeme, Maji na Afya.
Baadhi ya miradi hiyo ambayo imekamilika ni pamoja na barabara ya Dar es Salaam hadi Somanga inayohusisha pia ujenzi wa Daraja la Mkapa, Kiwanda cha Karatasi Mufindi, Mradi wa kuzalisha Umeme unaotokana na nguvu ya maji-Mtera, na gharama za upembuzi yakinifu wa upanuzi wa Bandari ya Zanzibar.
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango, ameishukuru Serikali ya Kuwait kupitia Mfuko wake wa Maendeleo wa Kuwait kwa kuisaidia nchi kutimiza majukumu yake ya kuwaletea wananchi maendeleo kupitia mikopo yenye gharama nafuu inayotolewa na taasisi hiyo.
Dkt. Mpango alisema kuwa mwaka jana, Mfuko wa Maendeleo wa Kuwait uliipatia Tanzania mkopo nafuu wa shiingi bilioni 115 kwa ajili ya kuboresha barabara ya Chaya hadi Nyahua (km 85) kwa kiwango cha lami pamoja na mradi wa maji safi na salama wa miji ya Same na Mwanga mkoani Kilimanjaro na sehemu ya eneo la wilaya ya Korogwe mkoani Tanga wenye thamani ya shilingi bilioni 77.

Mradi mwingine ni ufadhili wa ukarabati wa hospitali ya Mnazi Mmoja-Zanzibar utakaogharimu kiasi cha dola za Marekani milioni 13.6 sawa na shilingi bilioni 31.
Share:

MAGAZETI YA JUMANNE LEO MARCH 19, 2018







Share:

Benki ya NBC yaahidi kuendelea kutoa huduma bora kwa wateja wake

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kushoto), akizungumza katika hafla ya wateja ambapo pia aliwatambulisha baadhi ya wakurugenzi wa benki hiyo (kushoto kwake), jijini Dar es Salaam juzi. Alisema lengo la hafla hiyo ni kukutana na wateja kuzungumza nao na kupata mrejesho kuhusu huduma wanazowapa.
Mkurugenzi wa Huduma kwa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi akizungumza katika hafla hiyo ambapo pamoja na mambo mengine alizungumzia jinsi NBC ilivyojipanga kutoa huduma bora kwa wateja wake katika mwaka 2018. Alisema wamezindua kampeni iitwayo Karibu Nyumbani ikilenga kuwarudisha nyumbani katika Benki ya NBC wateja wao wa zamani ili waweze kufurahi huduma zao.
Mkurugenzi wa Huduma za Biashara wa NBC, Elvis Nduguru akizungumza na wateja wa benki hiyo katika hafla waliyowaandalia jijini Dar es Salaam juzi. Alisema   NBC kitengo cha biashara kimejipanga kuboresha huduma zake hususan huduma za malipo kwa njia ya kadi (POS).
Mmoja wa wateja wa NBC, Sadock Magai, akitoa neno la shukrani kwa niaba ya wateja wenzake katika hafla hiyo.
Mteja wa NBC na mmoja wa wanasiasa wakongwe nchini, Steven Masato Wassira (kulia), akizungumza na baadhi ya wafanyakazi wa NBC katika hafla hiyo.
Baadhi ya wateja wa NBC waliohudhuria katika hafla hiyo ambayo Mkurugenzi Mtendaji wake, Theobald Sabi alisema benki hiyo iliyodumu kwa zaidi ya miaka 50 imejizatiti katika kuhudumia wateja wake kwa ufanisi na weledi mkubwa.
Baadhi ya wateja wa NBC wakimsiiliza Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (hayupo pichani), wakati akizungumza nao. Bwana Sabi alizitaja baadhi ya huduma zao mpya ikiwa na pamoja na Klabu za Biashara (NBC Business Club) kwa ajili ya wafanyabiashara wadogo na wakati kuwasaidia kukuza biashara zao, akaunti ya vikundi na nyingine nyingi.
Baadhi ya wateja na wafanyakazi wa NBC wakiselebuka katika hafla hiyo.
Viongozi mbalimbali wa Idara ya Wateja Binafsi ya NBC wakipozi mbele ya wateja wao katika hafla hiyo. Wa tatu kutka kushoto mstari wa nyuma ni Mkuu wa Idara hiyo, Filbert Mponzi.
Viongozi mbalimbali wa Idara ya Biashara ya NBC wakipozi mbele ya wateja wao katika hafla hiyo. Wa tatu utoka kushoto mstari wa mbele ni Mkuu Idara hiyo, Elvis Ndunguru.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (331) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (129) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages