Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka (kushoto), akizungumza wakati wa Uzinduzi
rasmi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililoandakliwa na Benki ya
Serikali ya Biashara TCB, hafla hiyo imefanyika makaop makuu ya nchi Jijini
Dodoma wengine pichani ni , Afisa
Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi, pamoja na Mkurugenzi Rasilimali
watu na Utawala Diana Myonga.
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka akitembelea babanda ya wanawake
wajasiliamali wakati wa Uzinduzi rasmi wa Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi
lililoandakliwa na Benki ya Serikali ya Biashara TCB, hafla hiyo imefanyika
makaop makuu ya nchi Jijini Dodoma
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka (wapili kulia), akipata maelezo
kutoka kwa mmoja ya wajasiliamali walijitokeza wakati wa Uzinduzi rasmi wa
Jukwaa la kuwawezesha wanawake kiuchumi lililoandakliwa na Benki ya Serikali ya
Biashara TCB, hafla hiyo imefanyika makaop makuu ya nchi Jijini Dodoma kushoto ni Afisa
Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi pamoja na Maofisa wengine wa Benki hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mh Anthony Mtaka akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa benki ya TCB
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imejipanga kuwa taasisi kinara ya kuwahudumia wanawake nchini hili kuwakwamua kiuchumi kupitia suluhisho za kifedha ambazo zinazingatia changamoto zao kama wajasiriamali.
Katika kutimiza hazma hiyo, TCB jana ilizindua Kongamano la Wanawake na Biashara jijini Dodoma ambalo litakuwa jukwaa maalum la kuchochea maendeleo yao binafsi, familia, jamii na taifa kwa ujumla.
Kongamano hilo lilijikita zaidi kujadili nafasi ya akina mama katika kukuza uchumi wa taifa. Na hili kuwa na matokea chanya, Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi, alisema midahalo kama hiyo itafanyika pia Zanzibar, Morogoro, Mwanza, Mbeya, Arusha na Dar es Salaam.
“Katika makongamano hayo, wanawake hasa wajasiriamali, watapata fursa ya kuifahamu vizuri TCB na huduma zake wezeshi huku wakibadirishana mawazo na uzoefu wa mambo mbalimbali,” Bw Moshingi aliwaambia washiriki.
Aidha, aliongeza kuwa jukwaa hilo litazingatia sana nafasi ya wanawake kuwa chachu ya uchumi na maendeleo na jinsi wanavyoweza kutumia fursa za kibiashara zinazopatikana TCB kupitia huduma na suluhisho zake mbalimbali.
Bw Moshingi alisema benki hiyo ina wajibika kuupa kipaumbele uwezeshaji wa wanawake baada ya serikali kuziunganisha shughuli zake na zile za iliyokuwa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB).
“Uongozi wa Benki ya Biashara Tanzania unapenda kuishukuru Serikali kwa kuwa na imani na sisi na kuamua kutuunganisha na benki za TWB, Twiga Bancorp na TIB Corporate,” Bw Moshingi alisema katika wasilisho lake.
Hatua hiyo imeiimarisha TCB sokoni kiushindani na kuifanya iwe na msuli wa kifedha wa kuweza kulihudumia taifa kwa ufanisi.Hilo aliliweka bayana kupitia takwimu za kiutendaji zinazoonyesha mali na amana za TCB kuwa 1.04trn/- na 888bn/- mtawalia kufikia mwishoni mwa mwaka jana.
Wakati faida kabla ya kodi ya TCB iliongezeka kutoka 400m/- mwaka 2007 hadi 21bn/- mwaka 2020, ukopeshaji ndani ya kipindi hicho ulikua hadi 618bn/- kutoka 36bn/-.
Bw Moshingi pia alisema zipo huduma maalum zinazowalenga akina mama kama akaunti ya TABASAMU, dirisha maalum kwa ajili yao kwenye matawi yote ya benki na huduma za bima maisha kwa vikundi ambavyo wanachama wake wengi ni wanawake.
“Mikopo zaidi 120bn/- imetolewa kwa wanawake na tumekusanya amana za 11.9bn/- kupitia akaunti za vikundi zaidi ya laki tatu ambapo asilimia 85 ya wanachama wake ni wanawake,” mtendaji huyo alisema.
Mgeni rasmi kwenye kongamano hilo la ufunguzi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Bw Anthony Mtaka, ambaye aliipongeza Benki ya TCB na viongozi wake kwa kuanzisha utaratibu huo wa kimaendeleo na kiuwezeshaji.
Alisema ubunifu huo wa hali ya juu ni nyenzo mahsusi ya kuwakomboa wanawake kifedha na kuwajengea uwezo kibiashara huku akiitaka benki hiyo kuwaonyesha fursa ilizonazo za kuwasaidia.
Kwa mujibu wa maofisa waandamizi wa TCB, lengo la jukwaa hilo si tu kuwawezesha wanawake wa Kitanzania kiuchumi bali pia kuwaimarisha kifedha na kuwajenga kibiashara ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.
Walisema Jukwaa la Wanawake na Biashara la TCB linaendana na mpango wa Rais Mama Samia Suluhu Hassan wa kuongeza ushiriki wa wanawake katika kusimamia na kumiliki uchumi wa taifa.
“Kwa muktadha huo benki na taasisi nyingine za fedha nchini zinawajibu wa kushiriki kutekeleza ajenda hiyo ya serikali na TCB imeonyesha mfano mzuri wa hilo,” walifafanua.
Jukwaa hilo jipya litaendeleza huduma jumuishi kwa ajili ya wanawake kupitia mikakati mbalimbali itakayowawezesha kufungua uwezo wao wa ujasiriamali na kuchangia mabadiliko kuanzia ngazi ya kaya hadi taifa.
Pia litajikita zaidi kwenye ufumbuzi wa changamoto zinazozikabili biashara zinazomilikiwa na kuongozwa na akina mama.

*****************************
| Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea. |
| Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakiserebuka mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea. |
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Akiba Commercial Bank Webster Kaunga (kulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa benki hiyo ilipozindua huduma za Akiba Wakala katika Tawi la Makao Makuu barabara ya Ohio jijini Dar es Salaam jana wengine pichani n Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Akiba Commercial Benki PLC (ACB), Dora Siria na Mkuu wa Kitengo cha mikopo wa Benki hiyo Charles Kamoto.
Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano Akiba Commercial Bank Dora Saria amesema benki hiyo imeanzisha huduma ya Wakala ijulikanayo kwa jina la Akiba Wakala.
Huduma hii itawasaidia wateja wa benki hiyo kupata huduma kwa urahisi zaidi popote pale walipo kupitia mtandao mpana wa huduma za Wakala unaopatikana nchi nzima.
Dora Saria ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo kwenye tawi la benki hiyo ililopo baeabaea ya Ohio mkabala nahoteli ya Serena jijini Dar es salaam jana.
Amesema Mteja anaweza kupata huduma ya kutoa na kuweka fedha mahali popote penye tangazo la Akiba Wakala Kupitia huduma hii tutawafikia Watanzania wengi popote pale walipo na wataweza kunufaika na huduma zetu.
Pia ameongeza kuwa kwamba, kupitia huduma hii ya Akiba Wakala Benki watakuwa washiriki wazuri katika kuunga mkono harakati za Serikali za kuhakikisha uwepo wa huduma jumuishi za kifedha yaani (Financial inclusion) kwa Watanzania wote.
Tumeingia sokoni na jumla ya Wakala wapatao 200 na lengo letu ni kuendelea kuongeza Wakala wengi kadri iwezekanavyo kwa lengo la kukidhi kiu ya upatikana wa huduma za Akiba nchi nzima, kwa urahisi na ukaribu kwa kumfata mteja popote alipo au kwa urahisi waweza kusema pasipo na ulazima kwa kufika tawini.
Aidha, Benki itaendelea kuboresha huduma hizi za Akiba Wakala kwa kuhakikisha upatikana wa mahitaji mengi ya kibenki kadri iwezekanavyo kwa Wakala wetu kwa lengo la kuleta urahisi na huduma zaidi kwa wananchi kama tulivyoainisha kwenye kauli mbiu ya huduma hii ya Akiba Wakala ambayo inasema Huduma Zaidi.
“Tunategemea kutoa huduma za kufungua akaunti na nyinginezo nyingi hapo mbeleni. Vile vile Benki imeanzisha mkakati rasmi wa kuhakikisha kuingia rasmi katika mfumo wa kidigitali katika mchakato wa kutoa huduma.”. Amesema Dora Saria
Mfumo huu utaendelea kuleta unafuu na kuokoa gharama za upatikananji wa huduma zetu.Pia tunazo huduma za Akiba Mobile, ambazo zinawawezesha wateja wetu kupata mahitaji mbali mbali ya Kibenki na mengineyo mathalani kununua LUKU, ving’amuzi, muda wa maongezi pamoja na malipo yote ya Serikali kupitia simu zao za mikononi.
Ameongeza kuwa wateja wote wa Benki ya Akiba wanaomiliki akaunti binafsi wanakuwa wameunganishwa na huduma hii na wanaweza kufanya miamala popote pale walipo. Huduma ya Akiba Mobile inaptikana kupitia mfumo wa USSD na App kwa wale wanoatumia simu janja.
Pia huduma ya Akiba Mobile inamuwezesha mteja kufanya miamala yake ya kibenki kupitia Akiba Wakala vile vile.Kabla ya hitimisho naomba pia niwadokeze ndugu wnahabari kuwa Benki ya Akiba inatoa huduma nyingine nyingi za Amana, Mikopo, kuuza na kununua float, kutuma na kupokea fedha kupitia Western Union n.k.
Ametoa rai kwa Watanzania wote watembelee matawi yetu yote pamoja na Akiba Wakala kwa ajili ya kuhudumiwa na ufafanuzi.Kwa kumalizia, ikumbukwe kwamba benki yetu imepata mwekezaji wa kimkakati, ambaye ni National Bank of Malawi (NBM).
Ni imani yetu kwamba ubia huu utasaidia kupanua wigo wetu wa kibiashara ikizingatiwa NBM ni moja ya benki kubwa kwenye ukanda wetu wa nchi kusini mwa Afrika.
Vile vile, tutaendelea kuboresha na kuanzisha huduma nyingi zikiwemo za kidijitali na hizi za Akiba Wakala imezinduliwa rasmi na tunawakaribisha Wateja wetu wote watumie huduma hiyo kwa mahitaji yako kibenki na wakumbuke kuwa hawana ulazima wa kufika matawini kwa ajili ya kuweka na kutoa fedha kwenye Akaunti zao, kufanya marejesho ya mikopo
Meneja Mwanadamizi Suruhisho za Biashara wa Benki ya Serikali ya Bishara Leonard Katamba akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa ya TCB Kuunganisha huduma za Kibenki Mtandaoni na mifumo ya malipo, wapili kulia ni Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango na Mlipaji Mkuu wa Serikali, Emmanuel Tutuba ambae ndio alikuwa Mgeni rasmi pamoja na Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki hiyo Bw, Sabasaba Moshingi
Benki ya Biashara Tanzania (TCB) imekuwa benki ya kwanza nchini kuunganisha huduma zake za kibenki mtandaoni na mifumo yote ya kitaifa ya malipo.
Afisa Mtendaji Mkuu wake, Bw, Sabasaba Moshingi, amesema maboresho yaliyofanyiwa mfumo wa soluhisho hiyo ya kidijitali unaifanya huduma ya TCB Internet Banking kuwa ya kipekee na isiyokuwa na mpinzani sokoni.
“Suluhisho hii imebuniwa na kutengenezwa na wataalam wetu wenyewe bila gharama yoyote na ubora wake dhidi ya mifumo mingine ni kuunganishwa kwake na mifumo yote ya kitaifa ya malipo,” Bw Moshingi alitabainisha jana wakati wa unzinduzi wake jijini Dar es Salaam.
“Tungeinunua sokoni ingetugharimu kati ya dola 300,000 na 500,000,” alifafanua akionyesha unafuu wake kwani bei hizo ni sawa na TSh milioni 695.7 na karibu TSh bilioni 1.16 mtawalia.
Kwa mujibu wa Bw. Moshingi, uwekezaji wa kuboresha huduma ni sehemu ya mpango mkakati wa kuimarisha suhuhishi za kibenki za TCB na kuzifanya za kisasa zaidi ili ziendane na mahitaji ya soko.
Alisema maboresho ya TCB Internet Banking pia yanalenga kuiwezesha benki hiyo kujipanga vizuri zaidi kibiashara na kujiimarisha kiushindani sokoni.
Serikali imeipongeza benki hiyo kwa kufanya maboresho hayo na kusema yataongeza thamani kwenye mifumo ya kitaifa ya malipo.
Akizumgumza kabla ya kuizindua rasmi huduma hiyo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango, Bw Emmanuel Tutuba, alisema uwekezaji huo pia unalipa na kuifanya TCB kuwa tishio.
Kiongozi huyo amewahasa wananchi na taasisi zote kujiunga na mfumo huo mpya wa TCB ili waweze kufanya miamala ya kifedha kwa urahisi, usalama na uharaka ili waweze kuongeza ufanisi katika shughuli zao.
“Nimefurahi kusikia kuwa mfumo huu pia umeunganishwa moja kwa moja na mfumo wa MUSE ili kurahisisha taasisi za serikali kufanya malipo pasipo na ulazima wa kutembelea benki,” Bw. Tutuba alisema.
MUSE ni mfumo wa ulipaji serikalini ambao ni sehemu ya mchakato wa serikali mtandao kwa ajili ya kuziwezesha taasisi za umma na makundi mengine kama watumishi, raia, wanafunzi na wafanyabiashara kupata taarifa na huduma kwa njia ya intaneti.
Katibu Mkuu Tutuba ameichagiza TCB kutumia umahiri wake wa ubunifu kusaidia kutafuta ufumbuzi wa maswala mbalimbali na kusaidia kutatau changamoto mbalimbali kama kupunguza gharama za mikopo na riba kubwa.
Akiutambulisha mfumo huo, Meneja Mkuu Suluhishi za Biashara wa TCB, Bw Leonard Katamba, alisema huduma hiyo imebuniwa kwa kuzingatia mahitaji ya sasa na maendeleo ya kidijitali ya siku za usoni.
“Huduma ya TCB Internet Banking itatoa wigo mpana wa huduma za kibenki kwa wateja wetu; taasisi za serikali, makampuni, mashirika ya dini na mengine yasiyo ya kiserikali, wafanyabiashara wakubwa na wadogo, wafanyakazi, vikundi mbalimbali, taasisi za elimu pamoja na mtu mmoja mmoja,” alifafanua.
“Mfumo huu pia unawazesha wateja kufanya miamala ya kibenki ndani na nje ya nchi kupitia mifumo kama TISS, EFT na SWIFT, ukusanyanji mapato ya serikali na tozo kieletroniki (GePG), miamala ya simu, malipo ya mishahara na kupata taarifa zote muhimu za kibenki.”




