KLABU YA BIASHARA YA NBC YAINGIA MKOANI RUVUMA

 

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando (wa nne kushoto), pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC,  Elibariki Masuke (wa tatu kulia), akimuwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo,  Theobald Sabi wakifungua bango kuashiria uzinduzi rasmi wa ufunguzi wa Klabu ya Bishara Mkoani Songea wenye lengo la kuwakutanisha wateja wake wafanyabiashara na wenye viwanda na wadau wengine. Kutoka kushoto ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Simon Ntwale,
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakipiga makofi mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea.
Mkuu wa Wilaya ya Songea, Pololet Komando pamoja na maofisa wa Benki ya NBC na wateja wake wakiserebuka mara baada ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara iliyozinduliwa na Benki ya NBC Mkoani Songea.

Benki ya Taifa ya Biashara imezindua NBC Biashara Club, Mkoa wa Ruvuma katika hafla ya uzinduzi ilifanyika katika hoteli ya Heritage Cottage Wilaya ya Songea na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Songea, DC Pololet Komando ambaye pia alikuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, RC John Ibuge.

NBC Biashara Club ni sehemu ya mkakati mpana wa benki hiyo wa kuwainua wajasiriamali kwa kuwajengea uwezo wa kibiashara kupitia semina za mafunzo, kuwasogezea huduma za kibenki, kuwajengea mitandao ya kibiashara pamoja na kuwapa mbinu za kurasimisha biashara zao ili waweze kukopesheka. Jitihada hizi za Benki ya NBC zinaonekana kuzaa matunda kwani benki hiyo ilifanikiwa kuzindua klabu ya biashara kwa Mkoa wa Kigoma miezi michache iliyopita.

Zaidi ya kutoa mafunzo kwa wafanyabiashara, NBC Biashara Club pia inatoa fursa ya kuwakutanisha wanachama wake na watoa huduma mbali mbali katika sekta ya biashara zikiwemo taasisi za serikali kama TRA ili kujadili na kutatua changamoto na kupata mafunzo zaidi kwenye masuala ya kodi, uagizaji malighafi na bidhaa kwenda na kutoka nje.

Uzinduzi wa NBC Biashara Club mkoani Ruvuma unakuja siku chache baada ya benki hiyo kuanzisha huduma ya NBC Wakala Plus wilayani Mbinga. Benki hiyo pia iliendesha semina za mafunzo kwa makundi mbali mbali ya wajasiriamali wilayani humo kwa dhumuni la kuwajengea uwezo katika kuendesha biashara. Pamoja na semina kwa wajasiriamali benki ya NBC kupitia huduma ya NBC Shambani, ilikutana na viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika (AMCOS) Mkoani Ruvuma ili kujadili fursa zinazotokana na kushirikiana kwa sekta za kilimo ya kibenki.

Benki ya NBC kupitia klabu yake ya biashara pia iliandaa semina maalum kwajili ya wajasiriamali wanawake wa Wilaya ya Songea ambapo pia walitoa mafunzo na kupata fursa ya kutambulisha huduma zake za kibenki na kuwaelimisha wajasirimali hao juu ya faida na manufaa ya huduma hizo.

Akizungumza katika hafla hiyo ya uzinduzi, mgeni rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Songea, DC Pololet Komando aliwahikishia wafanyabiashara wa Ruvuma kuwa Benki ya NBC ni benki kongwe nchini ambayo inaelewa changamoto na mahitaji ya wafanyabiashara. DC Sololet pia aliipongeza benki hiyo kwa kutoa elimu kwa wajasiriamali wa mkoa huku akiwasihi kutumia fursa za mikopo inayotolewa na Benki ya NBC kukuza biashara. zao.

“Tunawapongeza kwa kufunga safari kuja kuonana na wananchi wa Ruvuma ambao ni wafanyabiashara na wakulima wa mazao ya chakula na biashara, huu ni uthibitisho kwamba benki yen uinathamini wateja wake.” Alisema DC Pololet

Aidha kwa upande wake, Mkurugenzi wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC,Nd ElibarikiMasuke alisema kamba mafanikio makubwa ya klabu ya biashara ya NBC yametokana na ushikiano kutoka kwa serikali kupitia taasisi zaidi ya 15 zikiwemo TRA, BRELA, SIDOna TABWA. Ushirikiano ambao umesaidia benki hiyo kufikia dhumuni la kuongeza ukaribu baina ya Benki ya NBC na wateja wake kupitia na mafunzo ya ujasiriamali.

“Mpaka sasa tumeweza kufungua NBC Biashara Club katika mikoa ya Dodoma, Arusha, Mbeya, Moshi, Morogoro, Singida Kahama, Lindi, Mtwara, Masasi, Tanga , Kigoma, Dar es Salaam na leo tunazindua hapa Songea. Kupitia jukwaa la NBC Biashara Club, wafanyabiashara zaidi ya 6,300 wamenufaikana mafunzo tunayotoa na safari za kibiashara kwenda nje ya nchi.” Alisema Nd Elibariki.

Aidha Nd Elibariki alisema kwamba pamoja na changamoto ya gonjwa la Uviko-1, benki hiyo ina azma ya kufikia mikoa yote ya Tanzania hivyo benki hiyo inachukua tahadhari zote za kujikinga na gonjwa hilo wanapoendesha makongamano na wajasiriamali.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages