
Kupungua kwa zaidi ya asilimia 90 kwa muda wa upakuaji wa shehena kunadhihirisha mabadiliko ya kiutendaji yaliyofanyika ndani ya miaka miwili ya mageuzi ya uendeshaji.
DAR ES SALAAM, TANZANIA – 7 July 2026: Bandari ya Dar es Salaam imeshuhudia mapinduzi makubwa kiutendaji baada ya kampuni ya DP World kuweka rekodi mpya ya kasi ya kuhudumia meli na kupunguza muda wa kushusha mizigo kwa zaidi ya asilimia 90. Mafanikio haya ni hatua kubwa katika mageuzi ya bandari hiyo tangu kampuni hiyo ianze uendeshaji wake rasmi mnamo Aprili 2024.
Chini ya mkataba wa uendeshaji wa miaka 30, kampuni ya DP World inaendelea kuwekeza katika ukarabati na upanuzi wa bandari hiyo ili kuunga mkono malengo ya muda mrefu ya nchi kiuchumi na kibiashara.
Kupitia uhamishaji wa mifumo ya kisasa ya uendeshaji wa meli za mizigo ya magari (RoRo) unaowezesha bandari kuhudumia meli kubwa na zenye mahitaji ya hali ya juu kwa usalama zaidi, huku ikipunguza gharama za mnyororo wa ugavi, huku ikiongeza ushindani wa kibiashara na kuchochea ukuaji wa uchumi.
Mageuzi haya yameleta mapinduzi makubwa kwa kupunguza muda wa kushusha mizigo ya aina hiyo kwa zaidi ya asilimia 90—kutoka zaidi ya saa 300 hadi chini ya saa 28. Hatua hii imeweka kiwango kipya kabisa cha ufanisi katika bandari hiyo.
Meli hiyo yenye urefu wa mita 240, ndiyo meli ndefu zaidi kuwahi kutia nanga katika Bandari ya Dar es Salaam, ikiwa na uwezo wa kubeba hadi magari 7,790. Ilitumia muda wa saa 27 tu kukamilisha zoezi la kushusha shehena ya magari 779, ambayo mengi yake yalikuwa ni magari makubwa na mitambo mizito.
Akizungumzia hatua hiyo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa DP World nchini Tanzania, Martin Jacob, alisema: “Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, tumefanya mapinduzi makubwa katika mfumo wa usafirishaji wa shehena kupitia Bandari ya Dar es Salaam. Kasi kubwa ya kuhudumia meli, kuongezeka kwa uwezo wa bandari, na uwezo wa kupokea meli kubwa zaidi zenye mizigo mchanganyiko, kunazidi kuimarisha nafasi ya Tanzania kama lango kuu la biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki, huku kukileta tija kwa wateja, wafanyabiashara na uchumi kwa ujumla.”
Mabadiliko kuelekea matumizi ya meli maalum za kusafirisha magari na malori (PCTC), yaliyofanyika kwa ushirikiano na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), yamewezesha ushushaji wa magari na mitambo mizito kwa kasi, usalama na ufanisi mkubwa zaidi. Hatua hii ya kuacha mifumo ya zamani ya upakuaji mizigo ya kawaida imeleta mafanikio endelevu katika makundi yote ya shehena huku yakiimarisha nafasi ya Dar es Salaam kama kitovu cha biashara chenye ushindani mkubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki.
Muhtasari wa Mageuzi na Matokeo
- Kasi ya kushusha shehena kuongezeka kwa 90% – Muda wa kushusha mizigo ya aina hiyo umepungua kutoka zaidi ya saa 300 hadi chini ya saa 28.
- Uwekaji wa rekodi mpya ya meli – Kufanikiwa kupokelewa na kuhudumiwa kwa meli ndefu zaidi kuwahi kufika bandarini, yenye urefu wa mita 240.
- Upanuzi wa uwezo na ufanisi – Kuanza rasmi kwa uendeshaji wa meli maalum za magari (PCTC) kumeongeza kasi na usalama wa kazi.
- Uchochezi wa ukuaji wa uchumi – Kupungua kwa gharama za usafirishaji kunasaidia kuongeza tija, kukuza Pato la Taifa, na kuleta ushindani wa kibiashara.
- Kuendeleza wataalamu wazalendo – Zaidi ya Watanzania 2,900 wamepata ajira na wanaendelea kupatiwa mafunzo ya kiutendaji na usalama kazini.
Ili kukidhi ongezeko la shehena na ujio wa meli kubwa zaidi, DP World inaendelea kuwekeza katika kuwajengea uwezo wafanyakazi na kuimarisha usalama bandarini hapo. Kituo hicho kimeajiri zaidi ya Watanzania 2,900, ambao wanapatiwa vyeti vinavyotambulika kimataifa pamoja na mafunzo maalum ya kiutendaji na ukabilianaji wa dharura, kwa lengo la kuhakikisha shughuli za bandari zinakuwa salama, za ufanisi na za kuaminika.
Uwekezaji wetu endelevu katika Bandari ya Dar es Salaam unaonyesha dhamira ya muda mrefu ya DP World katika kuchochea ukuaji wa uchumi wa Afrika na kuiunganisha na mifumo ya biashara ya kimataifa. Kupitia ushirikiano wetu na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA), hatuboreshi tu miundombinu hii muhimu, bali pia tunawezesha mtangamano wa kikanda, kupunguza vikwazo vya kibiashara, na kutengeneza fursa endelevu za kiuchumi," anasema Mohammed Akoojee, Ofisa Mtendaji Mkuu na Mkurugenzi Mkuu wa DP World kanda ya Afrika.

Kwa taarifa zaidi kuhusu jinsi DP World inavyoboresha biashara ya kimataifa, tembelea tovuti yetu: www.dpworld.com
Kwa maswali ya vyombo vya habari, tafadhali wasiliana na;
Keitumetse Masike
Mkurugenzi: Mawasiliano ya Biashara na Mikakati Afrika
Keitumetse.masike@dpworld.com
+27 61 831 8490
Kholiswa Hashe
Meneja Mwandamizi, Mawasiliano – Afrika Mashariki
Kholiswa.Hashe@dpworld.com
+27 72 741 0099
Fuatilia DP World kupitia:
X (Twitter): https://twitter.com/DP_World
Kuhusu DP World
DP World inabadilisha mustakabali wa biashara ya kimataifa ili kuboresha maisha ya watu kila mahali. Tukifanya kazi katika mabara sita tukiwa na timu ya wafanyakazi zaidi ya 125,000, tunajumuisha miundombinu ya kimataifa na uzoefu wa maeneo husika ili kutoa huduma jumuishi za ugavi. Kuanzia Bandari na Vituo vya Huduma (Terminals) hadi Huduma za Majini, Lojistiki na Teknolojia, tunatumia ubunifu kutengeneza njia bora zaidi za kufanya biashara—huku tukipunguza changamoto kuanzia kiwandani hadi mlangoni mwa mteja.
Katika kanda ya kusini mwa jangwa la Sahara, DP World imeajiri zaidi ya watu 28,000, ina magari zaidi ya 6,300, na inafanya kazi katika masoko 48.
TUNAFANIKISHA MTIRIRIKO WA BIASHARA







No comments:
Post a Comment