
Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya (kushoto), na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dk. Mfaume Kibwana (Katikati), wakifungua pazia kuashiria makabidhiano rasmi ya Wodi ya Wazazi, iliyofanyiwa ukarabati na Benki ya Absa. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Temeke, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.
Benki ya Absa Bank Tanzania leo imekabidhi rasmi wodi iliyokarabatiwa ya Wazazi katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, ikiwa ni sehemu ya mpango wa kijamii unaoongozwa na wafanyakazi wa benki hiyo, wenye lengo la kuboresha mazingira ya huduma kwa kina mama, watoto pamoja na wahudumu wa afya.
Ukarabati huo umetekelezwa kupitia mpango wa Absa unaojulikana kama “Adopt a Ward”, ambao unaendeshwa na wafanyakazi wenyewe kwa kubaini mahitaji ya jamii, kukusanya rasilimali na kushirikiana na benki katika kuleta mabadiliko chanya yenye tija kwa jamii.
Kazi za ukarabati zilizofanyika katika wodi hiyo ni pamoja na akarabati wa paa na dari, uwekaji wa vigae kwenye kuta za vyoo, ukarabati wa madirisha, kazi za nje za mabomba maalumu ya plastiki (PVC), ukarabati wa mifumo ya umeme, kazi za mabomba ya maji, ufungaji wa milango ya alumini, ufungaji wa viti vya vyoo na sinki pamoja na uchoraji wa majengo.
Akizungumza wakati wa hafla ya makabidhiano, Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya, alisema kuwa mpango huo unaonyesha imani ya muda mrefu ya benki kwamba jamii huimarika pale taasisi na watu binafsi wanapowekeza pamoja katika suluhisho za vitendo zinazoboresha maisha.
“Katika Absa, tunaamini kuwa ‘Stori yako ina Thamani’, na leo tunakumbushwa kuwa hadithi za kina mama, watoto, familia na wahudumu wa afya zina umuhimu mkubwa. Ukarabati huu ni utekelezaji wa dhana yetu ya ‘Kuwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, Hatua Moja baada ya nyingine’. Pia unaonyesha utamaduni tunaoujenga Absa, ambapo watu wetu wanachukua jukumu la kubaini mahitaji ya jamii, kuhamasisha msaada na kushirikiana na benki kuleta mabadiliko endelevu.”
Aliongeza kuwa mradi huo unaakisi ajenda pana ya uwajibikaji wa kijamii na uendelevu ya Absa, kwa kusaidia kuboresha mazingira ya huduma kwa heshima na ustahiki kwa wanawake na watoto, sambamba na kuimarisha mchango wa benki katika ustawi wa jamii.
“Huu ni mfano halisi wa namna Absa inavyokuwa nguvu chanya katika jamii. Kwa kuboresha wodi ya Mama na Mtoto, tunawaunga mkono wahudumu wa afya wanaohudumia jamii kila siku, na pia kuboresha uzoefu wa huduma kwa kina mama na watoto. Tunaamini uwekezaji wa pamoja wa aina hii ni muhimu katika kujenga jamii imara na yenye afya.”
Mpango huo uliwakutanisha wafanyakazi wa Absa kutoka idara mbalimbali, ukiakisi utamaduni wa ndani wa taasisi hiyo unaowahamasisha wafanyakazi kushiriki kikamilifu katika miradi ya maendeleo ya jamii, huku benki ikiongeza nguvu katika jitihada zao ili kuongeza athari chanya.
Mfumo huu wa utoaji unaoongozwa na wafanyakazi pamoja na msaada wa taasisi, umeendelea kuwa sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya Absa Tanzania katika uwajibikaji kwa jamii, unaojikita katika ushirikiano, ujumuishi na uundaji wa thamani ya muda mrefu kwa jamii.
Hatua hiyo ya makabidhiano pia inaendana na lengo la Absa ya “Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, Hatua Moja baada ya nyingine” pamoja na ahadi yake ya chapa ya “Stori yako ina Thamani”, ambayo ni msingi wa namna benki hiyo inavyotoa thamani kwa wateja, jamii na wadau wake.
Kupitia uboreshaji wa mazingira katika sekta muhimu ya afya, Benkiy a Absa Tanzania inalenga kuchangia katika kuboresha huduma za afya ya mama na mtoto, huku ikiimarisha umuhimu wa ushirikiano wa pamoja katika kutatua changamoto za jamii.

Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya (katikati), akikata utepe kuashiria makabidhiano rasmi ya Wodi ya Wazazi ya Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, iliyofanyiwa ukarabati na Benki ya Absa. Hafla hiyo, ilifanyika hospitalini hapo, Temeke, Dar es Salaam leo. Kulia ni na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mfaume Kibwana na kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.

Mkuu wa Udhibiti ya Udhibiti Ubora wa, Bw. Hosptali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Dk. Selemani Kivoja, akisalimiana na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya (kushoto), huku Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dk. Mfaume Kibwana (kushoto), akiangalia, katika hafla ambayo beni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya wazazi lililokarabatiwa na benki hiyo, katika hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Temeke, Dar es Salaam leo. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na Mahusiano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga.

Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania wakiongozwa na Mkurugenzi wa Rasilimali Watu, Bw. Patrick Foya, pamoja na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Temeke, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya kumalizika kwa hafla ya makabidhiano ya Wodi ya Wazazi iliyofanyiwa ukarabati na benki hiyo.







No comments:
Post a Comment