Mkurugenzi mshauri wa USAID afanya ziara kukagua miradi ya USAID Afya Yangu na Kizazi Hodari Kanda ya Kusini

MSHAURI Mkuu wa kiufundi wa watoto yatima na walioko katika mazingira magumu kutoka USAID Sarah Dastur akiwa kwenye picha na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya JJ Mungai iliyopo Manispaa ya Iringa baada ya kuwatembelea walengwa wanaonufaika na miradi ya USAID Afya yangu na Kizazi Hodari, Kanda ya Kusini mwishoni mwa wiki.

Iringa Jumatatu Agosti 5 2024, MSHAURI Mkuu wa kiufundi wa watoto yatima na walioko katika mazingira magumu kutoka USAID Sarah Dastur amefanya ziara ya siku moja ndani ya Mkoa wa Iringa kwa lengo la kuwatembelea walengwa wanaonufaika na miradi ya USAID Afya yangu na Kizazi Hodari, Kanda ya Kusini. Miradi hiyo miwili inatekelezwa na Deloitte Consulting Limited kupitia shirika la Msaada Kutoka Kwa Watu Wa Marekani.

Miradi hiyo inalenga kushughulikia utoaji wa huduma ya afya kwa wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI, kifua kikuu, uzazi wa mpango pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia Nchini Tanzania.

Sarah Dastur alitembelea shule ya Msingi ya JJ Mungai kuona miradi inavyowasaidia wanafunzi hao hasa katika mapambano ya ukatili wa kijinsia dhidi yao, aliwatembea walengwa wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI eneo Isakalilo, pia alitembelea hospital ya Tosamaganga moja ya hospital zinazotoa huduma ya dawa kwa ya kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV).

Moja ya wanaufaika wa mradi wa USAID Afya yangu ambaye ameomba kutotajwa jina lake wala kuchukuliwa picha ameshukuru mradi huo kuwa Mkombozi na Msaada Mkubwa kwa watanzania wengi hasa wale wenye uwezo wa chini kwa kuwarudushia tabasamu.

Aidha alitoa ombi kwa niaba ya wenzake uongezwe usiri kwa vituo/ club ambazo wanakutana vijana wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI kwa lengo la kubadilishana mawazo kwani vingi vipo katikati ya muingiliano wa watu jambo ambalo linaondoa ufalagha wao akieleza linachochea hali ya unyanyapaa kwa watu wenye Elimu hasi.
Dkt Stella Mtera ambaye ni Msimamizi wa kitengo cha CTC hospitali ya Tosamaganga iliyopo manispaa ya Iringa akimsikiliza MSHAURI Mkuu wa kiufundi wa watoto yatima na walioko katika mazingira magumu kutoka USAID Sarah Dastur wakati alipotembelea walengwa wanaonufaika na miradi ya USAID Afya yangu na Kizazi Hodari, Kanda ya Kusini mwishoni mwa wiki.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages