Benki ya DCB yaunga mkono jitihada za serikali ujenzi wa Reli ya SGR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, akihutubia mkoani humo jana, katika hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa huo kabla hawajaondoka Kwa treni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na Benki ya Biashara ya DCB kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na utalii kupitia Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.

Katika kuunga mkono juhudi zilizofanywa na serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR pamoja na kukuza utalii kupitia Royal Tour, Benki ya Biashara ya DCB imedhamini safari ya walimu zaidi ya 1000 kutumia treni ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kisha Mikumi ili kukuza utalii wa ndani na kujifunza mambo yatakayowasaidia wanafunzi wao wawapo madarasani.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga walimu hao kutoka Jiji la Dar es Salaam, katika Stesheni ya SGR, jijini humo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema taasisi yao imeshirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kuwapa nafasi walimu hao kutembelea mbuga za wanyama ya Mikumi ili kujionea vivutio vya utalii vitakavyowasaidia kuwafundisha wanafunzi wa mashuleni.

Alisema DCB inamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambalo ndiko wanakotoka walimu hao hivyo akawashauri kutumia huduma zilizoboreshwa za benki hiyo kama vile kuweka amana, bima mbalimbali na mikopo yenye masharti nafuu ili kuboresha maisha yao na kuacha kuangukia katika taasisi zinazotoa mikopo inayowaumiza na yenye masharti magumu.

Naye Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Bw. Ramadhan Mganga alisema DCB ndio mkombozi halisi wa watanzania kwani wanazo huduma na bidhaa tofauti zinazokidhi mahitaji ya kibenki ya watanzania hivyo kutoa hamasa kwa walimu hao na kwa watanzania kwa ujumla kuchangamkia huduma hizo.

Aidha alisema ili kufanikisha safari hiyo wamedhamini mabasi 30 yatakayowasafirisha walimu hao kutoka Morogoro kwenda Mikumi ikiwa pia ni kutambua mchango wa walimu hao katika maendeleo ya benki yao.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila aliipongeza DCB Kwa kufanikisha safari hiyo ya walimu akisema ofisi yake itaendelea kuandaa safari kwa makundi mengine ikiwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuitangaza treni ya SGR.

Ziara hii sio tu itaongeza maarifa kwa walimu kupitia ziara ya Mikumi, bali pia itaongeza chachu ya kampeni inayoendelea ya Royal Tour,”alisema.

Benki ya Biashara ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikitokana na wito wa Rais wa awamu ya tatu, Hayati, William Benjamin Mkapa, kufuatia kilio cha mitaji cha wananchi wenye kipato cha chini na cha kati wa Jiji la Dar es Salaam kukosa mikopo katika benki nyingi za kibiashara kwa kutokidhi vigezo vilivyokuwa vikiweka na benki hizo.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Bw. Ramadhan Mganga akizungumza kuhusu udhamini wa benki hiyo Kwa ziara ya walimu 1000 wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ziara yao kwenda Mikumi kwa kutumia treni ya SGR kutokea mkoani humo jana. Benki ya imedhamini mabasi 30 Ili kusafirisha walimu hao kutoka Morogoro kuelekea Mikumi Ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na utalii kupitia Royal Tour.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (katikati), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshi mkoani humo jana, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa huo kabla hawajaondoka katika stesheni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na DCB kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila, mkoani humo jana, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa wa Dar es Salaam, kabla hawajaondoka kwa treni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na Benki ya Biashara ya DCB ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.
Baadhi ya walimu kutoka jijini Dar es Salaam wakiwasili kwa treni ya SGR mjini Morogoro jana, wakiwa safarini kuelekea katika mbuga za wanyama ya Mikumi. Benki ya Biashara ya DCB ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour imedhamini safari hiyo Kwa kutoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi mbugani huko kutoka Morogoro.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages