


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw. Jema Msuya (wa tatu kushoto) akikata keki wakati wa maadhimisho ya wiki ya hudima kwa mteja. Hafla hiyo iliyofanyika katika tawi jipya la benki hiyo lililozinduliwa hivi karibuni Mpwapwa mkoani Dodoma. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo Edmund Mndolwa, Meneja wa Tawi hilo pamoja na wateja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw. Jema Msuya akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo lililozinduliwa hivi karibuni Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Kaimu kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdallah Shaib.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw. Jema Msuya pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo wakifurahia mara baada ya kuzindua tawi jipya la benki hiyo lililozinduliwa hivi karibuni Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Kaimu kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdallah Shaib.
Tanzania Commercial Bank imetoa semina kwa mawakala wake zaidi ya 1300 wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa TCB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.
Akizungumza katika semina hiyo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw, Jema Msuya alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala waTCB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi kuboresha katika kumuhudumia mteja.
Alisema TCB Hadi sasa tumekuwa na mwakalazaidi zaidi ya 5600 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 82 na mashine za ATM zaidi ya 400 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.
Jema alisema huduma ya TCB Wakala iliyoanzishwa ili kusaidia na kuondoa kero mbalimbali kwa wateja wa TCB ikiwemo foleni katika matawi mbalimbali ya benki hiyo huku ikitoa ajira kwa mawakala zaidi ya elfu 5600 ambao nao wameajiri vijana mbalimbali ambao wanajipatia kipato.
Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.
kwa upande wake mmoja ya mawakala Raqeeb Hamidu ameishukuru TCB kwakuandaa semina hizi marakwamara kwasababu wanazidi kunufaika nakuongeza uwezo wakuwahudumia wateja kwa uadilifu mkubwa na wepesi.
Tanzania commercial bank imekuwa Benki ya kwanza kwakutujali sisi mawakala na wateja wake maana hizi semina zinakwenda kumsaidia wakala wa zamani lakini pia wakala wapya
Baadhi ya maofisa wa Tanzania Commercial Bank pamoja na wateja wa benki hiyo wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa benki hiyo wakati wa chakula jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya (katikati) akikata keki pamoja na wateja wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja katika tawi la Mlimani City jijini Da es Salaam. hivi karibuni ambapo ilikuwa na kaulimbiu ya "TEAM SERVICE", Mkurugenzi amesisitiza dhamira ya benki yake kuendelea kutoahuduma bora kwa wateja wake.
Tanzania Commercial Bank jana iliungana na mataifa mbalimbali duniani kote kuadhimisha Wiki ya Huduma kwa mteja kwa mwaka 2023 ilikuwa na kaulimbiu ya “TEAM SERVICE” hiyo huku benki hiyo ikijikita zaidi na dhamira yake ya kuendelea kutoa huduma bora na zinazokidhi mahitaji ya wateja.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wiki wa huduma kwa wateja Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo ambaye ni mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya alisema benki ya TCB inachukulia kwa ukubwa wa hali ya juu sana kutoa huduma kwa wateja ndiyo maana kwa Tanzania commercial bank huduma ni moja ya mikakati na utamaduni wa benki hiyo.
Msuya alisema “kaulimbiu ya mwaka huu inaendana hasa na utekelezaji wa majukumu yetu ya kutoa huduma kwa wateja wetu wa Tanzania Commercial Bank na kuboresha huduma ni hamasa ya biashara na TCB imeweka kipaumbele cha kutoa huduma bora kwa wateja”.
"Hii ndiyo sababu Tanzania Commercial Bank inaendelea kuwekeza mara kwa mara katika jamii na kuwapa wafanyakazi wetu ujuzi na rasilimali zinazohitajika ilikuhakikisha wanawapa wateja wetu huduma za hali ya juu," Msuya alisema.