OFISI YA RC SINGIDA, BODI YA KOROSHO WAKUTANA KUMALIZA CHANGAMOTO YA WAKULIMA WA KOROSHO MANYONI

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dk. Binilith Mahenge akiongoza kikao cha kutatua changamoto iliyojitokeza baada ya wakulima waliolipia mashamba kwa ajili ya kilimo cha korosho wilayani Manyoni mkoani hapa kutopatiwa mashamba yao kwa zaidi ya miaka mitatu. Kikao hicho kilichowahusisha viongozi wa juu wa Bodi ya Korosho Tanzania kilifanyika jana wilayani humo.
Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Brigedia Jenerali Mstaafu Aloyce Mwanjile akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu  Bodi ya Korosho Tanzania (CBT), Francis Alfred akizungumza kwenye kikao hicho. 

 Katibu Tawala wa Mkoa wa Singida, Dorothy Mwaluko akichangia jambo kwenye kikao hicho.

Wakulima wakiwa kwenye kikao hicho.
Kikao kikiendelea.
Kikao kikiendelea.
Taswira ya kikao hicho.
Share:

MR & MRS MREMA WAMALIZA 'HONEYMOON TOUR' MBUGA ZA WANYAMA, WASISITIZA JAMBO

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha TLP, Augustino Mrema na mke wake Doreen Kimbi wakiwa katika ziara ya siku sita kwenye hifadhi nne za wanyama kwa ajili ya kukamilisha fungate yao ziara waliyoimaliza juzi.


Na Thobias Mwanakatwe, Moshi


MWENYEKITI wa Taifa wa Chama TLP, Augustino Mrema, ametoa wito kwa watanzania kuendelea kuimarisha ulinzi kwenye hifadhi zilizopo nchini kwa kushirikiana na vikosi vya ulinzi ili kuweza kukabiliana na tatizo la ujangili.

Alitoa wito huo wakati akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari jana baada ya kumaliza ziara yake ya siku sita kwenye hifadhi nne za wanyama akiwa na mke wake Doreen Kimbi kwa ajili ya kukamilisha fungate yao.

Mrema alisema pamoja na kwamba kumeimarishwa kwa vikosi vya ulinzi kwenye hifadhi lakini bado wananchi ambao vijiji vyao vipo karibu na hifadhi wana nafasi ya kusaidia ulinzi ili kumaliza tatizo la ujangili.

Aidha, Mrema aliwataka wananchi kujenga utamaduni wa kutembelea hifadhi za wanyama badala ya kidhani kuwa kazi hiyo ni kwa ajili ya wageni tu kutoka nje.

Alisema Watanzania wanapaswa kumuunga mkono rais Samia Suluhu Hassan ambaye amejipanga vizuri kwa ajili kutangaza vivutio vyetu vya utalii ndani na nje ya nchi kupitia filamu ya Safari Royal Tour kwa kutembelea mbuga  za wanyama.

"Nimekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani y Nchi, nimekuwa Waziri wa Kazi na Maendeleo ya Vijana, nimekuwa Naibu Waziri Mkuu, nimekuwa mbunge Vunjo lakini sikuwahi kutembelea kwenye mbuga za wanyama  lakini kiukweli kuna mambo mazuri ya kujifunza unapopata fursa usikose kutembelea hifadhi zetu," alisema.

Naye mke wake Mrema, Doreen Kimbi, alisema katika mbuga za wanyama kuna vitu vingi vizuri vya kujifunza hivyo wananchi kila mwezi wewe wanapanga ratiba kutembelea hifadhi zetu.

Doreen alisema wazo la kufanya fungate kwenye hifadhi za wanyama alilitoa yeye na mume wake (Mrema) kulikubari haraka kwani hiyo ndio njia mojawapo ya kumuunga mkono rais Samia ambaye amekuwa akisisitiza umuhimu wa wananchi kutembelea hifadhi zetu zilizopo nchini.

Naye Afisa Uhifadhi Utalii wa Hifadhi ya Ziwa Manyara, Renard Twinzi, alisema katika kipindi cha kuanzia Julai 2021 hadi April 2022 hifadhi hiyo imetembelewa na watalii 57,485.

Alisema hifadhi hiyo kwa kushirikiana na wadau wengine wa utalii imeweka mikakati ya kuhamasisha utalii wa ndani ili kuweza kufikia malengo ya hifadhi kutembelewa na 100,000 kwa mwaka.

Mrema na mke wake katika ziara hiyo iliyopewa jins la Mr&Mrs Mrema Honeymoon tour’walitembelea hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Tarangire, Manyara na Ngorongoro 

Share:

Absa Tanzania yakabidhi zawadi kwa mshindi wa kampeni ya Absa Card Assist ya ligi kuu ya Uingereza (EPL)

 
Meneja wa Kitengo cha Wateja Maalumu wa Benki ya Absa Tanzania (Premier Center Manager), Agnes Mushi (wa tatu kulia) akikabidhi zawadi ya smart tv nchi 43 na sound system kwa Catherine Mwakisu akimwakilisha James Samson Babala aliyeibuka kidedea katika kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyokwenda kwa jina la ‘Absa Card Assist’ iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya miamala mingi ya kibenki kwa kutumia kadi. Kampeni hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 4 disemba 2021 hadi 31 januari mwaka huu. Katika makabidhiano hayo Dar es Salaam jana, mshindi pamoja na washirika wake 10 waliandaliwa sherehe fupi huku wakiangalia kupitia luninga moja ya mchezo wa ligi hiyo uliyozikutanisha timu za Arsenal na Manchester United ambapo Arsenal ilishinda kwa mikwaju 3-1.
Mkuu wa Bidhaa na Mipango Mkakati wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Heristraton Genesis (wa tatu kulia) akikabidhi zawadi ya smart tv nchi 43 na sound system kwa Catherine Mwakisu akimwakilisha James Samson Babala aliyeibuka kidedea katika kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyokwenda kwa jina la ‘Absa Card Assist’ iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya miamala mingi ya kibenki kwa kutumia kadi. Kampeni hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 4 disemba 2021 hadi 31 januari mwaka huu. Katika makabidhiano hayo Dar es Salaam jana, mshindi pamoja na washirika wake 10 waliandaliwa sherehe fupi huku wakiangalia kupitia luninga moja ya mchezo wa ligi hiyo uliyozikutanisha timu za Arsenal na Manchester United ambapo Arsenal ilishinda kwa mikwaju 3-1.
Mshindi wa kampeni ya Absa Card Assist, washirika wake na baadhi ya wafanyakazi wa Absa wakishangilia wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza ya ‘Absa Card Assist’ iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya miamala mingi ya kibenki kwa kutumia kadi. Kampeni hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 4 disemba 2021 hadi 31 januari mwaka huu. Katika makabidhiano hayo Dar es Salaam jana, mshindi licha ya kukabidhiwa zawadi mbalimbali yeye pamoja na washirika wake 10 waliandaliwa sherehe fupi huku wakiangalia kupitia luninga moja ya mchezo wa ligi hiyo uliyozikutanisha timu za Arsenal na Manchester United ambapo Arsenal ilishinda kwa mikwaju 3-1.
Mkuu wa Bidhaa na Mipango Mkakati wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Heristraton Genesis (kulia) na Meneja wa Kitengo cha Wateja Maalumu wa benki hiyo, Agnes Mushi (wa pili kulia) wakikabidhi zawadi ya smart tv nchi 43 na sound system kwa Catherine Mwakisu (kushoto), akimwakilisha James Samson Babala aliyeibuka kidedea katika kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyokwenda kwa jina la ‘Absa Card Assist’ iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya miamala mingi ya kibenki kwa kutumia kadi. Kampeni hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 4 disemba 2021 hadi 31 januari mwaka huu. Katika makabidhiano hayo Dar es Salaam jana, mshindi pamoja na washirika wake 10 waliandaliwa sherehe fupi huku wakiangalia kupitia luninga moja ya mchezo wa ligi hiyo uliyozikutanisha timu za Arsenal na Manchester United ambapo Arsenal ilishinda kwa mikwaju 3-1.
Meneja wa Kitengo cha Wateja Maalumu wa Benki ya Absa Tanzania, Agnes Mushi (katikati) akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa mshindi wa kampeni ya Ligi Kuu ya Uingereza iliyokwenda kwa jina la ‘Absa Card Assist’ iliyokuwa na lengo la kuhamasisha wateja wa benki hiyo kufanya miamala mingi ya kibenki kwa kutumia kadi. Kampeni hiyo ilifanyika kuanzia tarehe 4 disemba 2021 hadi 31 januari mwaka huu. Katika makabidhiano hayo Dar es Salaam jana, mshindi licha ya kukabidhiwa zawadi mbalimbali yeye pamoja na washirika wake 10 waliandaliwa sherehe fupi huku wakiangalia kupitia luninga moja ya mchezo wa ligi hiyo uliyozikutanisha timu za Arsenal na Manchester United ambapo Arsenal ilishinda kwa mikwaju 3-1.
Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YAJITOLEA UPIMAJI WA AFYA BURE DAR ES SALAM

 


Meneja wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Tawi la Mbagala Edward Mwoleka (katikakati), akifanyiwa kipimo cha moyo na Mtaalam kutoka Alliance insurance Group Ravi Kumar, wakati Tanzania Commercial Bank waliposhirikiana na Alliance insurance kutoa vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa mbagala na viunga vyake bure anaeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan. Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi za Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam.


Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Edward Mwoleka (wapilikushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan (kulia), wakiangalia mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam, Joeseph John, akipatiwa huduma ya kipimo cha moyo na Mtaalam kutoka Alliance Insurance Group Ravi Kumar, wakati Tanzania Commercial Bank waliposhirikiana na Alliance insurance kutoa vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa mbagala na viunga vyake bure bila malipo


Baadhi ya wananchi waliojitokeza ili kupata vipimo hivyo.


Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala Edward Mwoleka(Kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan na wakati wa hafla maalum ya utoaji vipimo bure uliyodhaminiwa na Tanzania Commecial Bank kwa kushirikiana ikishirikiana na Shirika la Bima Alliance Insurance incorporation kwa wakazi wa Dar es salam.


Mkazi wa Mbagala akifanyiwa kipimo cha shinikizo la damu na Mtaalamu kutoka Shirika la Bima Alliance Insurance incorporation Group Ravi Kumar,kwakushirikiana na Tanzania Commercial Bank walipokuwa wakitoa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake bila malipo.


Meneja wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Tawi la Mbagala Edward Mwoleka (kushoto) akishuhudia mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam akipata kipimo cha sukari kutoka kwa Mtaalamu wa Maabara Husna Hassan (kulia)  wakati Benki ya Tanzania Commercial Bank ilipoungana na kampuni ya bima ya Alliance kutoa vipimo vya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake bila malipo.



Mamia ya wananchi leo wamejitokeza kupima afya zao  bure Tanzania Commercial Bank tawi la Mbagala iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikiwa ni sehemu ya Tanzania Commercial Bank pamoja na shirika la bima la Alliance Insurance Corporation kujali wateja wao na wananchi kwa ujumla.


Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala Edward Mwoleka  “Amesema kuwa kila mtanzania angependa kujua afya yake hivyo Tanzania Commercial Bank imeamua kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan hasa katika sekta ya afya kwa kutoa huduma ya vipimo bure bila malipo yoyote kwa wananchi wa mbagala.na viunga vyake”.


“Benki ya Biashara ya Tanzania tuna kila sababu ya kuwajali watanzania na kuwapa wanachotamani ndio maana leo tumeungana na wenzetu wa Alliance Insurance Corporation kwa kutoa huduma ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali bure”.


Mwoleka  amewataka watanzania na wakazi wa Mbagala kujiunga na Benki ya TCB kwani imekuwa ikitoa huduma bora na rafiki kwa kila mtanzania pamoja na kujali jamii ya wananchi.


 “Tuna mikopo ya kuanzia Mfanya Biashara mdogo, wa kati na hadi mkubwa hivyo niwasihi wateja wetu wajitokeze kuja kupata huduma katika benki yetu pendwa”.


 “Pia tuna mikopo ya wastaafu hivyo amewasihi wastaafu kujitokeza na kujiunga kwenye fursa hizi. Pia Benki inatoa mikopo mingi mbalimbali  yenye masharti nafuu na rafiki”.


Kwa upande wake Msemaji wa Alliance Insurance Justin Erick ameishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kuwaamini na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.


 Ameongeza kuwa kwa huduma zote za bima zinapatikana katika matawi yote ya Tanzania Commercial Bank hivyo amewasihi wananchi wa Mbagala wajivunie uwepo wa Alliance Insurance kwani ni kampuni ya kwanza na ubora Tanzania katika utoaji wa huduma.

 

Share:

Absa Yaahidi Kuimarisha Ubora Wa Huduma Huhakikisha Ukuaji Endelevu

 
Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Shehe Khalid Ali Mfaume akihutubia katika hafla ya futari iliyoandaliwa na Benki ya Absa kwa wateja wake wa visiwani humo jana.
Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Melvin Saprapasen (kulia), akisaidia kuweka mlo wa futari kwenye sahani ya mmoja wa wateja wao katika hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa Zanzibar, visiwani humo jana.
Meneja wa Tawi la Benki ya Absa Mjini Zanzibar, Rabia Abood (kushoto), akisaidia kuweka mlo wa futari kwenye sahani ya mmoja wa wateja wao katika hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa Zanzibar, visiwani humo jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi.Hellen Siria (kushoto), akisaidia kuweka mlo wa futari kwenye sahani ya mmoja wa wateja wao katika hafla waliyoiandaa kwa wateja wao wa Zanzibar, visiwani humo jana.
Meneja wa Tawi la Benki ya Absa Mjini Zanzibar, Rabia Abood (kulia), akiwakaribisha baadhi ya wateja na wadau wa benki hiyo visiwani humo katika hafla ya futari waliyowaandalia mjini Unguja jana.
Mwakilishi wa Mufti Mkuu wa Zanzibar, Shehe Khalid Ali Mfaume (wa pili kushoto), akiagana na Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Absa Tanzania, Melvin Saprapasen (kulia),mara baada ya hafla ya futari iliyoandaliwa na benki huyo kwa wateja wake wa Zanzibar jana. Kushoto ni Shehe Salum Maridhia kutoka ofisi ya Mufti Mkuu wa Zanzibar na Mkurugenzi wa Makampuni Mkubwa na Uwekezaji wa Absa, Hugo Chilufya.

Na Mwandishi Wetu, Zanzibar

Benki ya Absa Tanzania imeahidi kumarisha ubora wa huduma zake kwa wateja ili kuhakikisha kuwa ukuaji wa shughuli zake unakuwa endelevu, imeelezwa mjini Zanzibar Jana.

Akizungumza katika hafla ya mlo wa futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake walio kwenye Mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Absa Tanzania, Melvin Saprapsen, alisema : “Tuna uhakika na uimara wa shughuli zetu kwa siku zijazo, kwa kuwa tunaendelea kubuni na kuzindua bidhaa nyingi na ufumbuzi ambazo zipo kidijitali zaidi na hivyo kuwezesha wateja wetu kufikia huduma zetu kwa urahisi.

Alisema mwaka wa fedha wa 2021 ulikuwa mzuri kibishara kwa benki hiyo, kwa kuangalia utendaji wa shughuli zake, ambapo benki iliweza kuibuka kutoka kwenye hasara ya Tsh 532 mwaka 2020 na kujipatia faida Kabla ya Makato ya Kodi ya Tsh 9.4 bilioni kwa mwaka 2021.

Katika mwaka huo benki ilizindua bidhaa mpya ya huduma ya utoaji mikopo kwa biashara ndogo na za kati, na vilevile kuboresha mfumo mzima wa miamala kwa biashara ndogo na za kati ikiwa ni sehemu ya mkakati wetu wa kupanua bidhaa na huduma na kuongeza huduma za kidijitali” alisema Saprapsen.

Ushiriki wa benki katika kuchangia shughuli za umma ulikua kwa kiasi kikubwa kwa mwaka 2021, ikiashiria kushika kasi kwa mkakati wa benki wa kupanua nafasi yake katika sekta ya umma ili kuchangia maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Bi. Ndabu Lilian Swere, akitoa maoni kuhusiana na mwelekeo chanya wa shughuli za benki hiyo, alisema: “Katika mwaka 2021, benki ilizindua bidhaa kadhaa za kidijitali na kupanua wigo wa aina za bidhaa zake, ikiwa ni pamoja na kuzindua bidhaa ya utoaji wa mikopo kwa wateja binafsi kupitia simu ikishirikiana na kampuni ya mawasiliano ya Tigo Tanzania ambayo imefikia maelfu ya wateja na wasio wateja wao kuwasaidia kufikia huduma za kifedha kwa urahisi zaidi na kuboresha maisha yao.

Ndabu alisema kuwa Benki ya Absa ina utamaduni wa muda mrefu wa kuandaa hafla za futari ikiwa ni hatua ya kuwashukuru wateja wake, na akaongeza kuwa benki hiyo imejikita katika kutoa huduma kwa wateja wadogo, wa kati na wakubwa, ikiwa ni pamoja na kufanya kazi na serikali na mashirika makubwa ya ndani na nje ya nchi

Akimwakilisha Mufti Mkuu wa Zanzibar katika hafla hiyo, Sheikh Khalid Ali Mfaume alitoa pongezi kwa Absa huku akinukuu moja ya hadithi za Mtume Muhammad inayosema "mwenye kumfuturisha aliyefunga anapata malipo ya thawabu zote za aliowafuturisha.

Benki ya Absa imeendeela kuwa na mtaji wa kutosha kuendesha shughuli zake, ikiwa ni juu ya kiwango kinachohitajika kibishara na kima cha chini kilichowekwa kisheria. Uwezo wa benki wa kidijitali umekuwa ukiimarika zaidi na kuongeza wateja wapya na vilevile kuongeza matumizi ya huduma na bidhaa kwa wateja waliopo.

Kwa mwaka wa fedha wa 2021, Benki ya Absa ilishinda Tuzo Mbalimbali za ubora, ikiwa ni pamoja na Benki Bora ya Matumizi ya Kadi Tanzania (inayotolewa na Global Brand Magazine), Benki Yenye Ubunifu Bora wa Huduma za Wateja Binafsi (Inayotolewa na Global Business Outlook), na Benki Iliyotia Fora Kwenye Matumizi ya TEHAMA mwaka 2021 inayotolewa na Tume ya TEHAMA Tanzania.
Share:

COSOTA YAMTUNUKU TUZO YA HESHIMA KATIBU MKUU WA TAMUFO STELLA JOEL

Kaimu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hati Miliki Tanzania (COSOTA) Filemoni Kilaka akimkabidhi Tuzo ya Heshima Katibu Mkuu wa Umoja wa Wanamuziki Tanzania (TAMUFO) Stella Joel kwa kazi kubwa anayoifanya ya kuhamasisha maendeleo ya muziki nchi. Hafla ya kukadhiwa tuzo hiyoilifanyika juzi jijini Dar es Salaam.
Share:

MTENDAJI KATA YA DUNG'UNYI WILAYANI IKUNGI AONGOZA KUKAGUA MRADI WA MAJI SHULE YA SEKONDARI DADU

Afisa  Mtendaji  Kata ya Dung'unyi wilayani Ikungi mkoani Singida Yahaya Njiku akizungumza na Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Dadu baada ya kukagua mradi wa maji wa Kisima Kirefu uliokwisha kamilika katika Shule hiyo jana na kuridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali kwa ajili ya utekelezaji wake.
Afisa Elimu wa Kata ya Dung'unyi Ester Mkoma akizungumza na wanafunzi wa shule hiyo wakati wa ukaguzi wa mradi huo.
Afisa Mtendaji Kata Dung;unyi Yahaya Njiku akiwaongoza Wanafunzi wa shule hiyo kula kiapo cha kutunza miundombinu ya mradi huo.
Wanafunzi wa shule hiyo wakipokea maelekezo baada ya ukaguzi wa mradi huo.
Wanafunzi wakipokea maelekezo.
Wanafunzi wakipokea maelekezo.
Mkuu wa shule hiyo Kassim Gawaza akitoa taarifa ya mradi huo.
Share:

RAIS MWINYI ATOA SADAKA YA FUTARI KWA WAZEE, YATIMA NA WANANCHI WENYE HALI NGUMU WILAYA YA KUSINI UNGUJA

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimkabidhi Sadaka ya Futari mmoja wa Mzee wa Mkoa wa Kusini Unguja Bi.Arabia Ali Kombo, wakati wa kukabidhi sadaka ya futari kwa Wazee, Yatima na Wananchi wenye hali ngumu, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kwa Kibeshi Unguja Ukuu Wilaya ya Kusini Unguja.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akimsikiliza mmoja wa Wazee wa Mkoa wa Kusini Unguja Bw.Mohammed Abdalla, akitowa neno la shukrani, wakati wa kutoa sadaka ya futari kwa Wazee, Yatima na Wananchi wenye hali ngumu, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kwa Kibeshi Unguja Unguja Ukuu Wilaya ya Kusini Unguja, (kulia kwa Rais) Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Mhe.Rashid Hadidi na (kushoto kwa Rais) Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba, Sheria, Utumishi na Utawala Bora Zanzibar.Mhe.Haroun Ali Suleiman.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi akizungumza na kuwasalimia Wananchi wa Mkoa wa Kusini Unguja, baada ya kumaliza kutoa Sadaka ya Futari kwa Wazee, Yatima na Wananchi wenye hali ngumu, hafla hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kwa Kibeshi Unguja Ukuu Wilaya ya Kusini Unguja.(Picha na Ikulu)
Share:

WANANCHI IKUNGI WAHIMIZWA KUTUNZA CHAKULA ILI KUJIKIGA NA BAA LA NJAA

 Mwenyekiti  wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Ikungi Mika Likapakapa akiwahutubia Wananchi wa Kijiji cha Mwisi Kata ya Lighwa katika mkutano wa hadhara wa kuzungumzia maendeleo na kupokea kero za wananchi ili zifanyiwe kazi ulioandaliwa na Diwani wa Kata hiyo Gabriel Mukhandi na kuhudhuriwa na umati wa watu uliofanyika jana mkoani Singida.
Katibu wa CCM Wilaya ya Ikungi, Stamili Dendego akizungumza kwenye mkutano huo.
Diwani wa Kata ya Lighwa Gabriel Mukhandi akijibu maswali ya wananchi katika mkutano huo.
Katibu Mwenezi wa CCM  Wilaya ya IKungi, Pius Sanka akizungumzia Wana CCM wa kijijiji hicho wenye sifa kujitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi.
Share:

BENKI YA ABC YATOA VIFAA VYENYE THAMANI YA ZAIDI YA MILIONI 2 KUSAIDIA UJENZI WA CHOO CHA WAALIMU SHULE YA MSINGI MTAWALA MANISPAA YA MOROGORO.

 


Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga,(katikati), akikabidhi vifaa vya ujenzi wa Choo kwa Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya (wapili kutoka kulia), kulia Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati.

Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akimkabidhi taarifa ya manunuzi ya vifaa vya ujenzi , Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.

Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro, Chausiku masegenya.akizungumza katika hafla hiyo.

Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga akizungumza katika hafla hiyo.

Diwani wa Viti Maalum Mhe. Hadija Kibati akisalimiana na waalimu waliojitokeza katika hafla hiyo.

Waalimu wa shule ya Msingi Mtawala. 

BENKI ya ABC Kanda ya  Morogoro, imekabidhi vitu vyenye thamani ya  zaidi ya milioni 2 katika kusaidia ujenzi wa Choo cha Waalimu katika Shule ya Msingi Mtawalaa Manispaa ya Morogoro ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Serikali kusaidia kuondoa changamoto zilizopo kwenye sekta ya elimu hususani katika upande wa vyoo.

Hafla hiyo fupi ya kukabidhi vifaa hivyo, imefanyika leo Aprili 20/2022 katika shule hiyo huku tukishuhudia Afisa Elimu Msingi Manispaa ya Morogoro , Chausiku masegenya ,akipokea vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi mara baada ya kupokea vifaa hivyo, Masegenya, ameishukuru Benki ya ABC  huku akibainisha kuwa msaada huo utagusa maisha ya Waalimu  wengi kwa miaka mingi ijayo.

“Wadau wetu muhimu na washirika kama Benki ya ABC ndio nguzo muhimu kwa mafanikio yetu. Tunashukuru kwa msaada huu ambao utasaidia katika kuweka mazingira rafiki kwa waalimu ya kupata huduma ya choo , lakini pia kuwaondolea adha ya kutoka nje kwa ajili ya kufuata huduma ya choo" Amesema Masegenya.

Mwisho, Masegenya, ametoa wito kwa taasisi zingine za kifedha na wadau wanaopenda kuunga mkono juhudi za serikali za kuboresha mazingira ya vyoo pamoja na mazingira ya kujifunzia katika shule za umma zilizopo Manispaa ya Morogoro  kujitokeza kwa wingi katika jitihada hizo.

Naye Diwani wa Viti Maalum anayetokana na Kata ya Mwembesongo, Mhe. Hadija Kibati, ameishukuru Benki ya ABC Kwa kuwaunga mkono kwenye sekta ya elimu kwa kuwapa vifaa hivyo  ambayo yatasaidia kuondosha changamoto ya choo cha walimu shuleni hapo.

Kwa upande wa Meneja BANC ABC-Kanda ya Morogoro , Raphael Kalinga, akizungumza wakati wa halfa ya makabidhiano hayo, amesema kwamba  utoaji wa misaada kwa jamii  ni sehemu ya dhamira endelevu ya benki hiyo katika kusaidia sekta za elimu na kuona benki hiyo inachukulia kwa uzito sana suala la uwekezaji kwenye sekta ya elimu.

Kalinga, amesema wametoa msaada huo ili kuunga mkono Serikali na  juhudi za wananchi na kurudisha kwao ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa na hamasa ya kutenegeneza miundombinu ya elimu kwa manufaa ya sasa na kizazi cha baadae.

“Benki yetu inajivunia kuona Taifa linapiga hatua kubwa kwenye sekta ya elimu ambapo kupitia sera ya serikali elimu bure imeongeza idadi ya wanafunzi lakini pia ufaulu ambao maendeleo yake yanaakiisi hadi kiwango chetu cha uchumi ambapo mwaka jana nchi iliingia kwenye uchumi wa kati” Amesema Kalinga.

“Tumejitolea kuhudumia watu, biashara na jamii kwa ujumla. Benki yetu ya ABC, tumeguswa na changamoto ambayo iliwasilishwa kwetu , dhamira yetu kwa jamii ni kuona ni kuona tunaunga mkono na  kusaidia juhudi za kielimu na ustawi wa wanafunzi wetu na shule kote nchini na sio kwa Manispaa hii ya Morogoro pekee,  hivyo ni muhimu zaidi tukiweka jitihada katika kuboresha mazingira ya vyoo shuleni ili sasa Waalimu waweze kuwa na mahala rafiki kwa kutumia na kuacha kutoka eneo lao kwenda mbali  na shule zao,  ABC tutaendelea kushirikiana na Serikali kwa kadri tunavyoweza kuguswa na changamoto katika jamii ” Ameongeza Kalinga.

Mwalimu Mkuu Shule ya Msingi Mtawala, Mwl. Godfrey Binagwa , ameishukuru Benki ya ABC kwa msaada huo ambao wameutoa ambao utasaidia kuondoa changamoto walizokuwa wakikabiliana nazo za uhaba wa choo cha walimu.

Vifaa hivyo vya ujenzi ambayo walikabidhi benki hiyo ni Mifuko 50 ya saruji, mchanga Lori 1, Kokoto Lori 1, Mawe Lori 1, Milango 2 ya mbao, Fremu 2 za milango, Tofali za block 400 pamoja na Mabati 70.

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages