Meneja wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Tawi la Mbagala Edward Mwoleka (katikakati), akifanyiwa kipimo cha moyo na Mtaalam kutoka Alliance insurance Group Ravi Kumar, wakati Tanzania Commercial Bank waliposhirikiana na Alliance insurance kutoa vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa mbagala na viunga vyake bure anaeshuhudia ni Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan. Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi za Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala jijini Dar es Salaam.
Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Edward Mwoleka (wapilikushoto), pamoja na Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan (kulia), wakiangalia mmoja ya wakazi wa Dar es Salaam, Joeseph John, akipatiwa huduma ya kipimo cha moyo na Mtaalam kutoka Alliance Insurance Group Ravi Kumar, wakati Tanzania Commercial Bank waliposhirikiana na Alliance insurance kutoa vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa mbagala na viunga vyake bure bila malipo
Baadhi ya wananchi waliojitokeza ili kupata vipimo hivyo.
Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala Edward Mwoleka(Kulia), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Alliance Insurance Group, KVA Krishnan na wakati wa hafla maalum ya utoaji vipimo bure uliyodhaminiwa na Tanzania Commecial Bank kwa kushirikiana ikishirikiana na Shirika la Bima Alliance Insurance incorporation kwa wakazi wa Dar es salam.
Mkazi wa Mbagala akifanyiwa kipimo cha shinikizo la damu na Mtaalamu kutoka Shirika la Bima Alliance Insurance incorporation Group Ravi Kumar,kwakushirikiana na Tanzania Commercial Bank walipokuwa wakitoa huduma ya vipimo vya magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake bila malipo.
Meneja wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Tawi la Mbagala Edward Mwoleka (kushoto) akishuhudia mmoja wa wakazi wa jiji la Dar es Salaam akipata kipimo cha sukari kutoka kwa Mtaalamu wa Maabara Husna Hassan (kulia) wakati Benki ya Tanzania Commercial Bank ilipoungana na kampuni ya bima ya Alliance kutoa vipimo vya uchunguzi wa magonjwa mbalimbali kwa wakazi wa Mbagala na vitongoji vyake bila malipo.
Mamia ya wananchi leo wamejitokeza kupima afya zao bure Tanzania Commercial Bank tawi la Mbagala iliyopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ikiwa ni sehemu ya Tanzania Commercial Bank pamoja na shirika la bima la Alliance Insurance Corporation kujali wateja wao na wananchi kwa ujumla.
Akizungumza katika hafla hiyo Meneja wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Tawi la Mbagala Edward Mwoleka “Amesema kuwa kila mtanzania angependa kujua afya yake hivyo Tanzania Commercial Bank imeamua kuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Mama Samia Suluhu Hassan hasa katika sekta ya afya kwa kutoa huduma ya vipimo bure bila malipo yoyote kwa wananchi wa mbagala.na viunga vyake”.
“Benki ya Biashara ya Tanzania tuna kila sababu ya kuwajali watanzania na kuwapa wanachotamani ndio maana leo tumeungana na wenzetu wa Alliance Insurance Corporation kwa kutoa huduma ya kufanya vipimo vya magonjwa mbalimbali bure”.
Mwoleka amewataka watanzania na wakazi wa Mbagala kujiunga na Benki ya TCB kwani imekuwa ikitoa huduma bora na rafiki kwa kila mtanzania pamoja na kujali jamii ya wananchi.
“Tuna mikopo ya kuanzia Mfanya Biashara mdogo, wa kati na hadi mkubwa hivyo niwasihi wateja wetu wajitokeze kuja kupata huduma katika benki yetu pendwa”.
“Pia tuna mikopo ya wastaafu hivyo amewasihi wastaafu kujitokeza na kujiunga kwenye fursa hizi. Pia Benki inatoa mikopo mingi mbalimbali yenye masharti nafuu na rafiki”.
Kwa upande wake Msemaji wa Alliance Insurance Justin Erick ameishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kuwaamini na kufanya kazi pamoja ili kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi.
Ameongeza kuwa kwa huduma zote za bima zinapatikana katika matawi yote ya Tanzania Commercial Bank hivyo amewasihi wananchi wa Mbagala wajivunie uwepo wa Alliance Insurance kwani ni kampuni ya kwanza na ubora Tanzania katika utoaji wa huduma.
No comments:
Post a Comment