Washindi wa Ibuka Kidedea na NBC Malengo wakabidhiwa bodaboda zao

Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC  Malengo, Scholastika Peter (kulia), akibonyeza kitufe cha kompyuta ili kumpata mmoja wa washindi wa droo ya pili jijini Dar es Salaam leo. Wanaoangalia kulia kwake ni Meneja Amana za Uwekezaji, Dorothea Mabonye, Meneja Uhusiano Wateja Binafsi, Deogratius Kibodya, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Innocent Shayo na Mkuu wa Bidhaa wa NBC, Japhet Fungo. Katika droo ya pili, washindi watano wamejishindia tiketi za kwenda Ushelisheli, huku watatu wakishinda safari za kwenda Serengeti, kila moja akitunukiwa bakshishi ya kuandamana na mwenza atakayemchagua.
Meneja Masoko wa benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo ( kulia), akikabidhi zawadi ya  pikipiki kwa mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Daudi Majani, katika hafla iliyofanyika pamoja na droo ya pili ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam.
Mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo, Scholastika Peter, akifurahia zawadi yake ya pikipiki mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Bidhaa wa benki hiyo, Japhet Fungo (kulia).
Ofisa wa Benki ya NBC, Hussein Issa ( kulia), akikabidhi zawadi ya  pikipiki kwa mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NCB Malengo, Honest Kimaro, katika hafla iliyofanyika pamoja na droo ya pili ya kampeni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya washindi wa zawadi ya bodaboda wakipozi kwa picha ya kumbukumbu na maofisa wa NBC mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao jijini Dar es Salaam leo. Pikipiki hizo tano zilizokabidhiwa leo zina thamani ya shs milioni 12.3.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages