NBC kusaidia wanafunzi wanaoshindwa kumudu gharama za ada chuo kikuu

Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC, David Raymond (kulia), akizungumza na wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Hafla hii iliratibiwa na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO).
04
Baadhi ya wahudhuriaji wakishangilia moja ya onesho lililokuwa likifanywa na mmoja wa wachekeshaji mahiri kutoka Kenya, Erick Omondi katika hafla iliyoandaliwa mwishoni mwa juma lililopita na Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) na kudhaminiwa na Benki ya NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada chuoni hapo. 
01
Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda (katikati) akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Kulia ni Meneja Chapa na Mawasiliano wa NBC Bw. David Raymond.02
Meneja Chapa na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bw. David Raymond (kulia), akisalimiana na Rais wa Serikali ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (DARUSO) Bw. Hamis Mussa katika hafla ya kuchangisha fedha kwa njia ya vichekesho na burudani iitwayo ‘Cheka Nisome’ iliyodhaminiwa na NBC yenye lengo la kuwasaidia wanafunzi wanaoshindwa kuendelea na masomo kutokana na kushindwa kumudu gharama za ada. Hafla hiyo ilifanyika chuoni hapo jijini Dar es Salaam juzi. Katikati ni Meneja wa NBC Tawi la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Bw. Emmanuel Mapunda.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages