Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya
Biashara ya DCB, James Ngaluko (wa pili kulia), akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule
jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Balozi wa DCB Skonga, Zamaradi
Mketema, Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkuu wa
Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.
Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa
Benki ya Biashara ya DCB, Fortunata Benedict (kulia), akizungumza na waandishi
wa habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule
jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Masoko na
Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa na Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James
Ngaluko.
Balozi wa bidhaa ya DCB Skonga ya Benki
ya Biashara ya DCB, Zamaradi Mketema (kushoto), akizungumza na waandishi wa
habari wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma ya mkopo maalumu wa ada ya shule
jijini Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Masoko na
Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James
Ngaluko na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi, Fortunata Benedict.
Dar es Salaam 19 Disemba, 2019. BENKI ya Biashara ya DCB imezindua huduma ya
mkopo maalumu wa Ada ya Shule ikiwa ni fursa nyingine tena itakayowawezesha
wateja wa benki hiyo kulipa ada za watoto wao kwa wakati na uhakika.
Mkopo wa ada wa DCB ni mwendelezo wa mkakati wa
benki kubuni huduma na bidhaa bora zinazowanufaisha wateja. Benki imekuja na
bidhaa hii ya mkopo wa ada katika harakati ya kuwaondolea hofu wazazi
linapokuja suala zima la elimu kwa watoto wao hii ni sambamba na akaunti ya DCB
Skonga inayomuwezesha mtoto kusomeshwa pindi mzazi anapopata ulemavu wa kudumu
ama kifo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati wa
uzinduzi rasmi wa mkopo huu, Mkuu wa kitengo cha Masoko na Mawasiliano Bi Rahma
Ngassa alisema ‘’DCB inaendelea kuleta kwenye soko bidhaa zinazo kidhi maisha
ya watanzania, benki hii ni ya watanzania hivo ni lazima kuja na fursa
inayowawezesha wateja wetu kunufaika na benki yao.
Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Bwana James
Ngaluko aliongeza ‘’mkopo huu ni wa dharura na ni suluhisho kubwa kwa wateja
wetu, siku hazilingani na kama Benki tunataka watoto wetu wasome, elimu ndio
ufunguo wa maisha hivyo tunampa mzazi fursa ya kupata mkopo wa dharura ndani ya
masaa 48 kwa ajili ya ada ya mtoto pindi amekwama.
Alisema wakati tunaendelea kusherekea sikukuu za
mwisho wa mwaka na kukaribisha mwaka 2020, Benki tumeona tuwazawadie zawadi ya
kipekee kabisa wateja wetu kwani ni jambo lililo dhahiri kuwa suala la ada ni moja ya changamoto kubwa
inayowakabili wazazi wengi kila ifikapo mwanzoni mwa mwaka. Mkopo wa Ada wa DCB
una riba ya chini sana na utalipwa moja kwa moja kwenye shule ya mtoto. Mkopo
huu unakupa fursa ya kukopa hadi shilingi milioni tano ndani ya masaa 48 na muda wa marejesho unachagua mwenyewe hadi
miezi sita.
Nae Mkuu wa kitengo cha Wateja Binafsi Bi Fortunata
Benedict alisema ‘’Wazazi wengi kwa kutambua umuhimu wa elimu kwa watoto wao
wamejikuta wakihangaika kutafuta fedha za ada kwa njia zozote hivyo kujikuta
kuingia katika matatizo. Mzazi sasa huna haja ya kupata stress za kulipa ada,
acha DCB ikufikirie masuala ya elimu ya mtoto wako hii ni suluhisho la uhakika
la kifedha.
Ikumbukwe kua mwaka wa 2019 DCB imetoa fursa
mbalimbali kwa wateja ikiwemo:
§
DCB imewapa maelfu ya watanzania fursa ya kuwekeza kwa kununua Hisa
na kua wamiliki halali wa benki hii kupitia mfumo wa hisa za upendeleo.
§
DCB kibubu inampa
fursa mteja kuweka akiba mwenyewe kidogo kidogo kupitia simu ya mkononi (DCB
Digital) na kuhakikisha watanzania wengi wanafikiwa na huduma za kibenki.
§
DCB ilizindua DCB
Sokoni inayolenga kumkomboa mkulima na mfanyabiashara wa kilimo katika
mnyororo wa thamani.
§
DCB Lamba kwanza
inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14% papo hapo na kila mwanzo
wa mwezi.
§
DCB Skonga, ikilenga
kuwasaidia wazazi katika suala zima la elimu ya watoto wao pindi watakapopata
majanga ya ulemavu wa kudumu au kifo.
No comments:
Post a Comment