Wafanyakazi wa Benki ya NBC wajitolea damu kusaidia wenye mahitaji

Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Waziri Barnabas (katikati), akihojiwa na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, wakati yeye na mwenzake, Fanuel Jenga (kushoto), wakijitolea damu katika zoezi lililoandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake kujitolea damu kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Waziri Barnabas (kulia), pamoja na Mhasibu wa benki hiyo, Fanuel Jenga (kulia kwake) wakichukuliwa vipimo vya damu kabla ya kujitolea damu jijini Dar es Salaam leo, katika zoezi liloandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake pamoja na wakazi wengine wa jiji hilo kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Kushoto ni Evelyn Dielly kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wakijitolea damu katika zoezi liloandaliwa na benki hiyo kwa wafanyakazi wake pamoja na wakazi wengine wa Jiji la Dar es Salaam leo kujitolea damu kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama.
Mkazi wa Chalinze, Joshua Mjuni akijitolea damu katika zoezi liloandaliwa na NBC kwa wafanyakazi wake pamoja na wananchi wengine leo, kujitolea damu kusaidia wenye mahitaji kupitia Mpango wa Taifa wa Damu Salama. Anayemhudumia ni muuguzi kutoka Damu Salama, Peter Chami.
Ofisa Uhamasishaji wa Mpango  wa Taifa wa Damu Salama, Fatuma Mjungu, akihojiwa na waandishi wa habari katika zoezi la uchangiaji damu wa hiari lililkoandaliwa na Benki ya NBC jijini Dar es Salaam leo.

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Watanzania wamehimizwa kushiriki zoezi la kuchangia damu kwa hiari ili kukidhi mahitaji makubwa ya damu na kuokoa maisha ya wenzao pamoja na kusaidia huduma za afya nchini.

Hayo yamesemwa jana jijini Dar es Salaam na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) Waziri Barnabas akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Bbenki hiyo, Theobald  Sabi wakati wa tukio la kuchangia damu kwa hiari lililondaliwa na NBC akisema kwamba huo ni utamaduni wa benki hiyo wa kuchangia damu kwa kujitolea.

Alisisitiza kwamba ni muhimu kwa watanzania kuanza kujitokeza na kujitolea damu kwa hiari ili kuendelea kuokoa maisha ya wenye mahitaji.

"Hii ni mara ya tatu kwa benki hii na wafanyakazi wake kushiriki kwenye kampeni ya uchangiaji damu ili kuokoa maisha ya wakinamama wanaojifungua, waliopata ajali na watu wengine wenye mahitaji ya damu nchini,” aliongeza.

Barnabas aliongeza kwamba kwamba mahitaji ya damu bado yapo juu kwenye mahospitali hasa kwenye upasuaji na bado mwamko upo chini kwa wananchi kama uchangiaji wa damu kwa hiari.

"Ni muhimu sana kwa watanzania wenzetu kuungana nasi katika shughuli ya kujitolea ya kuchangia damu ambayo inatarajiwa kumalizika kesho,” alisema.

Alisema kwamba kwenye shughuli hiyo wanatarajia kukusanya takriban chupa 100 kutoka kwa wafanyakazi wa benki hiyo na watu wengine kutoka maeneo mbalimbali ya jiji ili kupunguza mahitaji makubwa ya damu nchini na alisisitiza kuwa kampeni hiyo inapaswa kuwa endelevu kukidhi matarajio ya nchini.

Kwa upande wake, Kaimu Ofisa Rasilimali watu wa benki hiyo, Grace Mgondah alisema kwamba wanatarajia wafanyakazi 500 kutoka kwenye matawi mbalimbali watashiriki katika zoezi hilo la siku mbili ya kujitolea damu kwa hiari.

"Hii ni sehemu ya huduma kwa jamii ambayo benki yetu ya NBC inasikia fahari kuwahudumia na ninatoa wito kwa watanzania wenzetu kujitokeza kwa wingi kuja kutuunga mkono,” alisisitiza.

Fatuma Mjungu kutoka Kitengo cha Taifa cha Damu Salama (NBTS) alisema kwamba mwaka huu wanatarajia kukusanya chupa 450,000 za damu kutoka kwenye taasisi mbalimbali na watu wanaojitolea kwa hiari.

"Mahitaji ya damu kwa sasa nchini ni chupa 520,000 lakini asilimia moja tu ya watanzania wote wakichangia damu tunaweza kukidhi mahitaji ya damu kwa taifa,” aliongeza

Mjungu pia ametoa wito kwa taasisi na makampuni nchini kuinga mkono benki hiyo ya NBC kwa kuhamasisha wafanyakazi wake na wananchi wengine kwa ujumla kujitolea damu kwa ajili ya watu wenye uhitaji.
Share:

Barclays Bank hosts its Zanzibar customers to a thanks-giving cocktail event

Barclays Bank’s Managing Director, Abdi Mohamed (on the right) in conversation with a client during the cocktail event.
Barclays Bank’s Finance Director, Obedi Solomon Laiser (in the middle) engaging with clients during the cocktail event.
Barclays Bank’s Human Resource Director, Patrick Foya (right) engaging with customers during the cocktail event.
Barclays Bank’s Chairman, Simon Mponji (left) and Dr Suleiman Rashid Mohamed (extreme right) in conversation with clients during the cocktail event.
Barclays Bank’s Corporate Director, Brian Kalero (Right) in conversation with clients during the cocktail event.

Barclays Bank Tanzania Limited (BBT) on Tuesday, 26th of November hosted its Zanzibar customers to a cocktail event. The event was not only a platform to appreciate the continued support of its customers but was also used to provide an opportunity for clients to join BBT in its transition journey and be informed of the expected milestones as the Bank prepares to rebrand into Absa.

Speaking during the event, the bank’s Managing Director, Mr. Abdi Mohamed said, “Our brand and name change to Absa is proceeding as planned. We have taken a sequenced approach and expect some branches to reflect several elements of the new brand in the first half of December, while some branches will retain the current look.  The intention is to take our customers and the public with us through the transformation journey visually.  We will however continue to operate and trade as Barclays Bank Tanzania Limited until our name officially changes, as approved by the Regulator.” 

Speaking on the bank’s commitment to Tanzania, Mr. Mohamed said, “Barclays is committed to serving its customers and we are proud of the momentum we have built over the past 3 years. Our commitment to our clients has been demonstrated in the successful execution of key financing transactions amounting to TZS 529bn, across sectors such as Oil & Gas, Public Sector, Manufacturing and Agriculture. In addition, our non-funded strategy and focus has been reaffirmed by The Asian Banker 2019 recognition of BBT as the best ‘Cash Management Bank in Tanzania’.

Responding to a question on whether customers can have the same confidence in Absa as they had in Barclays, the bank’s Head of Retail Banking, Mr. Oscar Mwamfwagasi said ”Absa Group is committed to building on Barclays' heritage in Africa and the strengths that we already have on the continent. We have a deep history and local knowledge in Tanzania. Our main products and services haven’t changed. Our customers can bank with us as confidently as they always have. 

You can bank with us as safely as you always have. Absa Group is one of the largest banking groups in Africa, with a balance sheet of more than USD 91 billion, as well as new systems with robust security provisions. ”

In conclusion, Mr. Mwamfwagasi; called for clients to remain vigilant, saying “We will not ask any customer for additional information during this time, and all customer account details will remain the same before and after the transition.”

Share:

Wateja watano wajishindia bodaboda na Ibuka Kidedea na NBC Malengo

Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo wakati NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya Malengo ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya bodaboda kila mmoja.  Wengine pichani ni maofisa wa benki hiyo na kulia kabisa ni mwakilishi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha.
Meneja Masoko wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Alina Maria Kimaryo (mbele kulia), akizungumza jijini Dar es Salaam leo wakati NBC ikichezesha droo ya kwanza ya kampeni ya akaunti ya Malengo ya NBC ambapo wateja watano walijishindia zawadi ya pikipiki aina ya Yamaha kila mmoja.  Washindi wa leo ni; Augustine Hatari kutoka Pwani, Williumu Pendaeli Isack wa Moshi, Scholastica Peter Yamawasa, Honest Christopher Kimaro na Daudi Majani wote kutoka Dar es Salaam.

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam,

WATEJA Watano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) wameibuka washindi wa bodaboda mpya aina ya Yamaha katika droo ya kwanza ya kampeni ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC” kupitia akaunti ya Malengo ya benki hiyo kongwe hapa nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kwenye droo ya kwanza ya kampeni hiyo iliyoanza mwezi wa Oktoba, Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo alisema kwamba akaunti ya malengo inampa mteja njia rahisi ya kuweka akiba kidogo na kupata faida kubwa kila mwezi.

“kwenye akaunti hii ya malengo kila Tsh 100,000 atakayoweka mteja kwenye akaunti hii inampa nafasi ya kushida zawadi kemkem ikiwemo bodaboda ambapo leo droo ya kwanza itashuhudia wateja hawa watano wakipata zawadi zao,” alisema Kimaryo.

Aliongeza kwamba katika kipindi chote cha kampeni bodaboda tano aina ya Yamaha zitatolewa kila mwezi na safari tatu za kwenda kufanya utalii Serengeti na safari tano za kwenda Seychelles mwezi wa Disemba na washindi wanaruhusiwa kwenda na mtu mmoja kwenye safari hizo.

“ukiwa na akaunti ya NBC malengo unapata faida nyingi ikiwemo ya kuhifadhi fedha kwa ajili ya kutimiza malengo na ndoto zako pamoja na mambo mengine ya kupata riba ya hadi asilimia 7 ya pesa uliyoweka kila mwezi,’ alisisitiza Kimaryo.

Washindi kwenye droo ya jana walikuwa ni Augustine Hatari kutoka Pwani, Daudi Majani, Dar es Salaam, Williumu Pendaeli Isack, Moshi Kibololoni, Scholastica Peter Yamawasa, Dar es Salaam, na Honest Christopher Kimaro wa Dar es Salaam.

Katika kampeni hii wateja watakao ongeza salio kwa kiasi Tsh milioni moja kwenye akaunti ya Malengo watapata nafasi ya kushinda zawadi kuu ya TOYO na jumla ya TOYO tatu zitatolewa kwenye kampeni hiyo ya “IBUKA KIDEDEA NA NBC MALENGO”.
Share:

Jubilee Insurance yawakumbuka watoto wenye mahitaji maalumu

Daktari kutoka Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, Dk. Romana Malikusema (kushoto) na Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa Wateja wa kanpuni hiyo, Dk. Maria Janja (kulia), wakimpima macho mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha kulea watoto yatima cha Umra Orphange Centre, Kulwa Erasto kituoni hapo Yombo Buza, Temeke, Dar es Salaam jana katikahafla ambayo Jubilee Insurance walipima afya watoto hao wakichukua vipimo kama vile malaria, wingi wa damu, uchunguzi wa meno pamoja na macho ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya  kusaidia jamii.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bima ya Jubilee, Angela Tungaraza (kulia) akimsaidia kupata vipimo vya damu mmoja wa watoto wa kituo cha kulela watoto yatima cha Umra Orphange Centre, Hassani Hijja katikahafla ambayo Jubilee Insurance walipima afya watoto hao wakichukua vipimo kama vile malaria, wingi wa damu, uchunguzi wa meno pamoja na macho ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya kusaidia jamii. Kushoto ni Mhudumu wa Afya wa Kampuni hiyo, Salha Mtinge.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa Kampuni hiyo, Dk. Maria Janja (kulia), akimsaidia kupata vipimo vya macho mmoja wa watoto wa kituo cha Kulea watoto yatima cha Umra Orphange Centre, Hassani katikahafla ambayo Jubilee Insurance walipima afya watoto hao wakichukua vipimo kama vile malaria, wingi wa damu, uchunguzi wa meno pamoja na macho ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya kusaidia jamii.. Kushoto ni daktari wa kampuni hiyo, Dk. Romana Malikusema.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bima ya Jubilee, Angela Tungaraza (katikati) akimsaidia kupata vipimo vya damu mmoja wa watoto wa kituo cha Kulea watoto yatima cha Valentine Childrens Home, Christina Lucas katika hafla ambayo Jubilee Insurance walipima afya watoto hao wakichukua vipimo kama vile malaria, wingi wa damu, uchunguzi wa meno pamoja na macho ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya  kusaidia jamii. Kushoto ni Muhudumu wa Afya wa Kampuni hiyo, Salha Mtinge.
Mkuu wa Kitengo cha Huduma kwa wateja wa Kampuni ya Bima ya Jubilee, Dk. Maria Janja (Kulia), akimsaidia kupata vipimo vya macho mmoja wa watoto wa kituo cha Kulea watoto yatima cha Valentine Childrens Home, Maria Mateo katikahafla ambayo Jubilee Insurance walipima afya watoto hao wakichukua vipimo kama vile malaria, wingi wa damu, uchunguzi wa meno pamoja na macho ikiwa ni sehemu ya majukumu yao ya kusaidia jamii.. Kushoto ni Daktari wa Kampuni hiyo, Dk. Romana Malikusema.
Share:

NBC yazindua Klabu ya Biashara (NBC-B-Club) Mkoani Morogoro

Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto), aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani Morogoro, akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati akizindua rasmi klabu hiyo mkoani humo jana. Kulia ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru.
Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (wa tatu kushoto),  aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani humo jana, akishikana mikono na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein katika uzinduzi wa klabu hiyo Mkoani Morogoro jana. Klabu hiyo imeanzishwa kusaidia mahitaji ya wafanyabiashara wadogo na wa mkoa huo. Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara NBC, Elvis Ndunguru, Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa kati na Wadogo, Evance Luhimbo na Meneja wa Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo.
Mkuu wa Kitengo cha Wafanyabiashra wa Kati na Wadogo wa Benki ya NBC, Evance Luhimbo akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake wafanyabiashara  wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa Uvuvi na Mifugo wa Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzhim (kushoto), aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Morogoro katika uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya Benki ya NBC mkoani humo akikaribishwa na Mjumbe wa Bodi ya NBC, Dk. Kassimu Hussein wakati akiwasili kuzindua rasmi klabu hiyo mkoani humo jana. Katikati ni Meneja wa Tawi la NBC Morogoro, Sophia Mwombelo. Uzinduzi huo  ulitanguliwa na semina ya siku moja   juu ya kuwajengea uwezo wafanyabiasha wadogo na wa kati. 
Ofisa Biashara Mwandamizi Taarifa za Biashara na Takwimu kutoka Mamlaka ya Biashara Tanzania (Tantrade), Magdalena Shirima akitoa elimu kuhusu fursa za masoko ya nje ya nchi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa Biashara wa Asasi ya Kusaidia Uwekezaji kwenye Kilimo (PASS), Irene Benedicto akizungumza katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Ofisa Mkuu Msimamizi wa Kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Julius Mjenga akitoa elimu kuhusu kodi katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.
Baadhi ya wafanyabiashara wakifuatilia mada katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na benki ya NBC kwa wateja wake wafanyuabiashara wadogo na wa kati Mkoani Morogoro jana. Semina hiyo ilifuatiwa na uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya benki hiyo mkoani humo.


Na mwandishi wetu, Morogoro

JUHUDI binafsi za wafanyabiashara kwa kushirikiana na taasisi za kifedha ni moja ya nyenzo muhimu katika kufikia malengo ya mpango mkakati wa serikali ya awamu ya tano katika kutoa kipaumbele katika uchumi wa viwanda.

Hayo yalisemwa na Mjumbe Mjumbe wa Bodi ya NBC,  Dkt. Kassim Hussein katika hafla ya uzinduzi wa Klabu ya Biashara ya NBC, maarufu kama ‘NBC B-Club’ ya Mkoa wa Morogoro ikiwa ni klabu ya 11 kuzinduliwa katika mikoa mbalimbali nchini.

“Kwenye biashara serikali imefanya mageuzi makubwa mfano  katika kuwahamasisha wafanyabiashara kutumia mashine za kielektroniki, kurasimishwa kwa biashara, lakini kunahitaji juhudi kubwa katika kuangalia masuala ya masoko, vifungashio, mitaji na viwango vya  TFDA ili kufanya biashara hizo zikue”, alisema.

Ni kutokana na hayo alisema NBC B-Club itakuwa faida kubwa kwa wafanyabiashara na nguvu ya kuleta maendeleo kwa taasisi na mtu mmoja mmoja, huku benki  NBC ikiongeza mafunzo ya mara kwa mara kwa kuleta wataalam mbalimbali na kutoa punguzo la riba kwa wanachama wa klabu hizo.

Akizungumza zaidi kuhusu klabiu hiyo Mkurugenzi wa Kitengo cha Biashara NBC, Elvis Ndunguru, alisema lengo pia ni kuwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali ili kuweza kubadilishana uzoefu, kupata fursa mbalimbali za masoko ndani na nje ya nchi pamoja na kuwaunganisha na wafanyabiashara wa nje.

Ndunguru alisema ni rahisi kutoa nafasi ya elimu kwa wafanyabiashara hao kupitia klabu zao, kwenye maeneo wanayobaini yanayotakiwa elimu baada ya kupata mrejesho toka kwa wateja wao.

“Klabu za Biashara tumeshazianzisha maeneo mbalimbali Tanzania, lakini lengo hasa ni kuwakutanisha wafanyabiashara mbalimbali ili kuweza kugundua fursa, kuwapa  elimu, kuleta wataalam tofauti, pia kuna fursa za kupeleka wafanyabiashara katika nchi mbalimbali” alisema Ndunguru.

Pia alisema wanatarajia kuongeza nchi nyingine ambazo zinafanya vizuri kibiashara ikiwemo Uturuki, Ujerumani na Marekani, na kwamba wana mpango wa kutengeneza dirisha maalum la wafanyabiashara wanawake wadogo na wakati ili kuwahamasisha zaidi kuingia katika biashara.

Awali akiongea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Afisa Uvuvi na Mifugo Manispaa ya Morogoro, Mohamed Chamzimu, alisema Klabu hiyo itawawezesha wanachama hao kuwa na uelewa wa biashara wa kisasa, na kwamba mafunzo wanayoyapata yataleta tija na kuongeza weledi katika shughuli zao.

Chamzimu aliwataka wafanyabiashara hao kujitokeza na kujiunga kwa wingi katika klabu hiyo kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Kwa upande wao Wafanyabiashara hao akiwemo Bupe Kamugisha wameipongeza benki hiyo kwa huduma bora na masharti nafuu ya kuchukua mikopo, na kusema kwamba imekuwa haina vitendo vya kutaifisha mali za wateja wao pindi wanapopata ugumu kwenye marejesho.

Nae mfanyabiashara Lusako Mwakiluma alisema mafunzo waliyoyapata  toka kwa taasisi mbalimbali zikiwemo Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTRADE), Shirika la Hifadhi za Jamii (NSSF) yatawasaidia kuboresha biashara zao sambamba na kujua utaratibu unaowapasa kufuata ili kuweza kukidhi viwango vinavyotakiwa.

Uzinduzi wa klabu hiyo ni wa 11 baada ya Klabu nyingine 10 kuzinduliwa katika mikoa mingine  ikiwemo  Mwanza ambayo imeonyesha  mafanikio makubwa.



Share:

Deaf paralegals vital for timely delivery of justice to deaf women

Deaf-women and members of deaf-women association (FUWAVITA) in jovial mood as they celebrate an International Week for  the Deaf held in Dar es Salaam recently. (Photo by Correspondent).

Women in Tanzania face numerous problems such as gender-based violence, sexual harassment and other forms of discrimination from family to national level. “But it is worse when it comes to deaf women due to the fact that their rights are denied and have no access to justice,” says a social welfare expert, Ms Heldina Mwingira.
Poverty and illiteracy are the main factors that lead to the deprivation of deaf women’s rights and lack of access to justice. Reports from the local media and government authorities show that about 55 per cent of the country’s deaf women are illiterate, most of them being poor with limited prospects for decent life.
“Lack of sign language interpreters aggravates deaf women’s limited access to legal aid and justice,” notes Ms Mwingira, who works with a deaf women association based in Dar es Salaam. Currently, there are about 28 sign language interpreters in Tanzania who can hardly serve the whole country.
“Deaf women face many problems and lack access to justice at the judiciary, police, at the office of the Director of Public Prosecutions (DPP) and social welfare offices due to communication barriers as both service seekers (deaf women) and service providers in the formal and informal legal systems do not know sign language,” she adds.
To address these problems and help deaf women to solve legal problems, an association of deaf women, Furaha ya Wanawake Wajasiriamali Viziwi Tanzania (FUWAVITA), is taking bold steps to incorporate legal aid service delivery in its core programmes with a view to helping deaf women to access justice. Recently, FUWAVITA celebrated International Week for the Deaf under the theme “The Right to Use Sign Language is a Solution to Delivery of Legal Aid to Deaf Women in Tanzania’’.
 “The choice of the theme was made purposely to send a clear message to the wider Tanzanian community on the importance of sing language if we really want to remove millions of deaf women out of legal problems in Tanzania,” says Bilbosco Muna, an official and sign language interpreter who works with FUWAVITA.
International Week for the Deaf, which took place at Mwananyamala public grounds on September 23-28, 2019, was sponsored by Legal Services Facility (LSF), a nongovernmental and non-profit organisation that provides financial and technical assistance to legal aid prividors in Tanzania.
Generally, the event which attracted over 1,000 people—including ordinary people, deaf women, primary court magistrates, social welfare officers from Dar es Salaam municipal councils—Temeke, Ilala, Kinondoni and Ubungo—sought to expose participants to general education about deafness, particularly the causes of deafness, the degree of deafness, the type of hearing impairment, testing hearing sensitivity and so on.
Specifically the event intended to educate lawyers, social welfare officers, primary court magistrates and deaf women about using sign language. The assumption behind this approach is that smooth or smart communication between service providers (primary court magistrates, lawyers and social welfare officers) and deaf women will make handling of deaf women cases/problems easier and enable them to get their rights.
Besides exposing service providers to the basics of sign language, FUWAVITA plans to do more by initiating special training to deaf paralegals (both men and women) who will go around providing legal aid to deaf women. At the moment, there are over 4,000 paralegals recruited through LSF funding who provide legal aid to communities, but most of these paralegals do not know sign language. 
“In the course of helping deaf women to solve their problems, paralegals need an interpreter, which many deaf women cannot afford…we have many reported incidents of deaf women who have lost cases, dignity, properties, divorced, forced out of their land/plot and denied their rights (in the formal and informal legal systems) due to communication barrier and inability to hire/pay sign language interpreters,” says Anet Gerana Isaya, FUWAVITA Executive Director.
According to the executive director, training of deaf paralegals will go hand in hand with extensive and regular training of Dar es Salaam-based magistrates, social welfare officers and deaf women themselves on proper use of Tanzanian sign language.
This will eliminate unnecessary costs of hiring sign language interpreters and facilitate communication when it comes to handling of deaf women cases as all parties—magistrates, social welfare officers, deaf paralegals and deaf women will be talking the same language, says the FUWAVITA director, adding that “unlike in the past, there will also be confidentiality in handling sensitive cases involving deaf women and in allowing them to express themselves freely.
At the end of the day, cases of deaf women will be dealt fairly in both the formal and informal legal systems and enable them to access justice,” notes Isaya.
Commenting on this social welfare expert Heldina Mwingira says “recruitment of deaf paralegals will enhance timely and efficient delivery of justice to deaf women facing legal and other problems in our country.” According to FUWAVITA, recruitment of deaf paralegals will start with Dar es Salaam wards and then to upcountry regions depending on the progress and success stories registered in the pilot phase.
Share:

NBC Profits Triple



NATIONAL BANK OF COMMERCE

Dar es Salaam, 30thOctober 2019

The National Bank of Commerce (NBC) the country’s oldest bank, with over 50 year of serving the financial sector in Tanzania, has posted impressive profits during the third quarter of the year. According to the third quarter financial statement, that was released on 30th October 2019, NBC has attained impressive growth of 367% on its Profit After Tax (PAT) compared to last year.

“Our impressive performance for the last nine months is mainly attributed to our ongoing cost savings and efficiency drive, increased fee income from transactional activities and improved quality of the loan portfolio,” said Mr. Theobald Sabi NBC Managing Director.

Taking a closer look, at the NBC third quarter financial statement, as at end of September 2019, NBC had Net Loans and Advances to the tune of TZS 987 Billion and Customer Deposits worth TZS 1.717 Trillion.

“Our total net loans and advances increased quarterly by 3.7%, mainly contributed by additional loan bookings from our Corporate, Retail and Business Banking clients, whilst our overall customer deposits increased by 19.3%” added Mr. Theobald Sabi.

“Our continued focus of onboarding quality loans has started to pay off resulting in lower impairment charges for the third quarter of the year. In addition, Non-Performing Loans (NPLs) ratio has continued to decline to 6.9% down from 10.1% as at September 2018” said Mr. Sabi.
The NBC Digital Transformation agenda continued to deliver impressive results, which have contributed to our bottom line. Our Mobile Banking transactions have grown by 50% compared to last year alone. This represents that our customers are effectively utilizing our electronic offerings and thus reducing the time required to conduct transactions in the branches.

Our purpose is to provide convenient services to our customers and clients. We want our customers to be able to bank or transact wherever they are without visiting branches.  We also want our customers to enjoy the different services and products that we have built in our digital platforms,” said Mr. Theobald Sabi

The Online and Mobile Banking proposition have become popular electronic channels widely used by Retail (Individual) and Corporate clients. The online transactions are safe and secure allowing Bulk Payments, Local and International Payments.

“Our Digital Banking Facilities provides individuals, SMEs, Government Agencies, and Corporates with convenient and efficient Cash Collections and Payment solutions,” said Mr. Sabi.

Another fast growing electronic channel is the NBC Agency Banking (NBC Wakala) that now has a membership of over 2,000 agents spread across the country. Customers are now able to access their accounts and make payments with greater convenience through the growing NBC footprint of agents. NBC Wakala agents are now GePG compliant and thus customers can settle their dues to the Government through the NBC Wakala network. NBC is now one of the leading banks in respect of Government Revenue Collections through GePG.

Our electronic channels are Government Electronic Payment Gateway (GePG) compliant, thus allowing our customers the choice to settle government levies and fees through our convenient electronic channels,” said Mr. Sabi.




Share:

Benki ya NBC yadhamini Gofu ya Mabalozi visiwani Zanzibar

Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto), Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kulia), na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri (wa pili kulia), wakimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Eliah John yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kuisapoti sekta ya michezo na utalii nchini. Mashindano hayo  yalifanyika katika viwanja vya gofu vya  Sea Cliff kisiwani Zanzibar jana.
Meneja wa NBC Tawi la Zanzibar, Ramadhani Lesso (kushoto) akipongezana na Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro, huku mchezaji mwenzao Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa akiwangalia  wakati wa mashindano ya kwanza ya gofu ya Mabalozi yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar  jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na Benki ya NBC kama moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kulia) akimkabidhi zawadi mshindi wa pili wa mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi, Issa Mohamed Chaap yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli  za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini. Mashindano hayo  yamefanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar  jana.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro (kushoto) akipokea zawadi ya kushiriki katika Mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri yaliyofanyika katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana. Mashindano hayo yalidhaminiwa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli  za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
Mbunge wa Kenya, Kassim Sawa (kushoto), akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Kitengo cha Wateja Rejareja Maalum wa Benki ya NBC, Ashura Waziri baada ya kushiriki mashindano ya kwanza ya gofu mabalozi yaliyodhaminiwa na NBC katika viwanja vya gofu vya Sea Cliff Kisiwani Zanzibar jana ikiwa ni moja ya shughuli za kusapoti sekta za michezo na utalii nchini.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Damas Ndumbaro akijiandaa kupiga mpira wakati wa Mashindano ya kwanza ya Golf ya Mabalozi yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli  za kuisapoti sekta ya Michezo na Utalii zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Mashindano hayo  yamefanyika katika viwanja vya Sea Cliff kisiwani Zanzibar  jana.
Wacheza gofu wakipozi kwa picha pamoja mgeni rasmi, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushikiano wa Afrika Mashariki pamoja na maofisa wa Benki ya NBC wakati wa mashindano hayo mjini Zanzibar jana. 

BENKI ya NBC imedhamini mashindano ya kwanza ya gofu ya mabalozi visiwani Zanzibar huku ikiahidi kuendelea kusapoti sekta ya michezo na utalii  visiwani humo kutokana na mchango wake  katika maendeleo ya taifa.

Akizungumza wakati wa mashindano hayo katika Viwanja vya Gofu vya Sea Cliff visiwani humo jana,   Mkuu wa  Kitengo cha Wateja maalumu binafsi wa Benki ya NBC, Ashura Waziri alisema licha ya kuwa michezo husaidia afya kitu ambacho ni muhimu katika uzalishaji mali, lakini pia michezo yenyewe inaweza kuongeza ajira na kuinua uchumi wa wanamichezo na kwa taifa.

“Naihakikishia Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar  kwa kupitia Kamisheni ya Utalii  kuwa NBC itaendelea kuisaidia kwenye michezo kama tulivyofanya kwa kudhamini gofu ya mabalozi, tunathamini michezo kwa wafanyakazi wetu pia, tunaihakikishia wizara ya michezo pia tutaendelea kusapoti michezo,” akaongeza.

Naye Meneja wa Tawi la NBC mjini Zanzibar, Ramadhani Lesso alisema NBC imekuwa mdau mkubwa wa maendeleo visiewani humo na ndio sababu ya kuitikia wito wa Wizara ya Habari na Utalii kupitia Kamisheni ya Utalii kushiriki katika mashindano hayo kwani wamekuwa wakishirikia kwa muda mrefu aatika kusapoti utalii visiwani humo.

“Kama mnavyofahamu benki yetu ina ATM zisizopungua 7 hapa Zanzibar na zote zinatoa huduma ya Visa ambayo ni maalumu kwa ajili ya wananchi wote lakini zaidi kwa watalii. Kwahiyo utakuta watalii wanafaidika sana wanapotumia mashine zetu za kutolea pesa na mashine nyingine zilizopo mahotelini.

“Watalii ni muhimu sana kwetu ndio maaana tulipopata mualiko huu kutoka kwa Mkurugenzi wa Kamisheni ya Utalii tuliona ni sehemu muhimu sana kwetu kwa ajili ya kuunga mkono serikali kwa upande wa maendeleo na vilevile ikiwa ni sehemu ya michezo kama ilivyo sera ya michezo,” aliongeza.

Pamoja na hayo meneja huyo akatoa wito kwa serikali na wadau wa michezo kuunga mkono juhudi za kusapoti mchezo wa gofu ufundishwe mashuleni   na sehemu zote ili watanzania wote waweze kuucheza a kuupenda.

Katika mashindano hayo, ambayo mgeni rasmi alikuwa Naibu Waziri wa Mambo na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Damas Ndumbaro, ambaye pia alikuwa mshiriki,   Eliah John aliibuka kidedea kwa kushika nafasi ya kwanza huku  Issa Mohamed Chaap wote wa visiwani humo kushika nafasi ya pili. 

Share:

Benki ya NBC yajipanga kutoa huduma bora msimu mpya wa ununuzi wa korosho Mtwara

Ofisa Huduma Wateja wa Benki ya NBC Tawi la Mtwara, Lulu Mutayoba (katikati), akitoa maelezo kuhusu huduma za kibenki zotolewazo na NBC kwa watu waliotembelea banda lao wakati wa Kongamano la Uwekezaji na Maonyesho ya Biashara Mtwara yaliyofanyika katika Viwanja vya Chuo cha Elimu Mtwara mwishoni mwa wiki. 

Na Mwandishi wetu, Mtwara

WAKATI wakulima wa korosho wakiendelea na msimu mpya wa korosho kwa mwaka 2019/20 Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imesema itaendelea kuwahudumia na kuwahakikishia usalama wa fedha zao huku ikisogeza huduma hizo karibu zaidi badala ya kusafiri umbali mrefu.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Uwekezaji na Maonyesho ya Biashara mkoani Mtwara mwishoni mwa wiki, Meneja wa NBC Mkoa wa Mtwara, Job Nshatsi alisema wameendelea kuwa mstari wa mbele kutuoa huduma za kibenki, ushauri na mafunzo ya kifedha na biashara yanayowezeha wateja wake ikiwemo wakulima na wafanyabiashara wa korosho.

Alisema katika kuhakikisha wakulima wananufaika na huduma zake tayari wameendelea kuongeza mtandao wao wa mawakala katika maeneo mbalimbali ili kuhakikisha wakulima wanapata fedha kwa wakati lakini pia kwa usalama kwa kuepuka kusafiri na fedha umbali mrefu kwenda palipo na tawi la benki hiyo.

“NBC tunatoa huduma za kibenki maalumu kwa ajili ya kukuza na kuendeleza kilimo-biashara (agribusiness) kwa kushirikiana na Taasisi ya Sekta Binafsi ya Kilimo nchioni (PASS), tukiangalia sekta ya kilimo na mnyororo mzima wa thamani katika kilimo, na kwa Mtwara tutaendelea kutoa huduma ili kusaidia kukuza uzalishaji, uongezaji wa thamani na uuzaji wa zao la korosho,”alisema Nshatsi

Aidha alisema NBC kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi (NEEC) wanaendelea kutoa elimu za kifedha kwenye vikundi mbalimbali vya wajasiriamali lengo ikiwa ni kuwawezesha wajasiriamali hao kupata mbinu mbalimbali katika kuendesha biashara zao.

Nshatsi alizidi kueleza kuwa ili kuhakikisha watu wengi wanafikiwa na huduma za kibenki wamerahisisha ufunguaji wa akaunti kupitia akaunti ya NBC Fasta ambapo mteja anahitajika kuwa na kitambulisho kimoja au barua ya mtendaji na kufunguliwa akaunti.

Wakizungumza baadhi ya wananchi waliohudhuria kongamano hilo waliziomba taasisi za kifedha kuendelea kuwapa elimu ya matumizi sahihi ya fedha hasa katika kipindi hiki cha msimu wa mavuno ya korosho.

“Tunapohudhuria makongamano tunatumaini tutapata elimu mbalimbali lakini watu wa benki waendelee kutoa elimu ya matumizi sahihi ya  fedha ili kuwa endelevu hasa kipindi hiki ambacho wakulima wanauza korosho wasaidiwe wajue baada ya kuuza fedha wanazozipata wanatakiwa kuziendeleza kwenye miradi mingine ya maendeleo,”alisema Asha Chimae



Naye mwanachi mwengine Hansi Chilumba alisema “Wananchi wapo tayari kufanya kazi lakini kinachokosekana ni ujuzi na mtaji, ni vizuri benki kuendelea kutuwezesha hata mmoja mmoja ili kutimiza malengo kwa sababu kila mtu anakuwa na malengo yake lakini tunapounda kikundi inakuwa ngumu kwa wote kukubali wazo la mmoja ili kulifanyia kazi.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages