Benki ya NBC yaendelea kuipiga jeki sekta ya Madini

Waziri wa Nishati, Dkt. Medard Kalemani (kushoto) akimsikiliza  Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Geita, Martin Nkanda wakati wa maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Katikati ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira. NBC ni mmoja ya wadhamini wa maonesho hayo.
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantine Kanyasu (kushoto) akisalimiana na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Geita, Martin Nkanda katika Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini. Katikati ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (kushoto), akisalimiana na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Geita, Martin Nkanda wakati akiwasili katika hafla ya Ufunguzi wa Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yaliyofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita hivi karibuni. Wapili kulia ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira. NBC inadhamini maonyesho hayo.

Waziri Mkuu, Kassim Majakiwa (kushoto), akisalimiana na Meneja wa NBC Kanda ya Ziwa, Japhet Mazumira, akipokwenda kufungua rasmi maonesho hayo.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Gabriel Robert (kulia) akisalimiana na Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira wakati akitembelea banda la benki hiyo katika  Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Katikati ni Meneja Uendeshaji Tawi, Thadei Tibalinda.

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kulia), akisalimiana na Ofisa Huduma kwa Wateja, Aggrey Kanani wakati akitembelea banda la Benki hiyo wakati wa Maonesho ya pili ya Teknolojia na Uwekezaji kwenye Sekta ya Madini yanayofanyika katika Viwanja vya CCM Kalangalala mjini Geita. Katikati ni Meneja wa NBC kanda ya ziwa, Japhet Mazumira.
Share:

Benki ya NBC yasaini makubaliano na Jeshi la Polisi ya ulinzi katika matawi yake nchini

Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberat Sabas (wa pili kushoto) na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas wakibalishana hati za makubaliano ya ulinzi wa askari wa jeshi hilo katika matawi yote NBC nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Jana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Gustavus Babile, Mkuu wa kitengo cha Sheria wa NBC, Doxa Mbapila na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Alelio Lowassa.
Kamishna wa Operesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Liberat Sabas (kushoto) na Ofisa Fedha Mkuu wa Benki ya NBC, Waziri Barnabas wakisaini hati za makubaliano ya ulinzi wa askari wa jeshi hilo katika matawi yote ya NBC nchini. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam Jana. Wanaoshuhudia kutoka kushoto ni, Mkuu wa Kitengo cha Sheria, Kamishna Mwandamizi wa Polisi, Gustavus Babile, Mkuu wa kitengo cha Sheria wa NBC, Doxa Mbapila na Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa NBC, Alelio Lowassa.
Share:

Benki Ya DCB Yazidi Kung’ara


Benki ya Biashara ya DCB imetangaza kumaliza kampeni ya bidhaa yake ya akaunti ya muda maalumu inayojulikana kama ‘DCB Lamba Kwanza’ kwa mafanikio makubwa huku ikivuka malengo yake iliyojiwekea ya shilingi Bilion 15 na kuongeza amana kwa shilingi Bilioni 18.5 ambayo ni zaidi ya asilimia 123.

Kampeni ya DCB Lamba Kwanza iliyozinduliwa Mei 29 mwaka huu na kudumu kwa muda wa miezi mitatu huku ikiwa na lengo la kukusanya amana za kiasi cha shilingi Bilioni 15, iliwawezesha wateja wa benki hiyo  kuwekeza na kupata riba ya hadi asilimia 14 ya amana wanayowekeza  ambapo mteja alianza kupokea riba yake ya mwezi  papo hapo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko alisema ‘tunatoa shukurani zetu za dhati kwa wateja wetu kwa kuweza kuipokea bidhaa hii na kuweza kunufaika nayo kwani wamenufaika sana, kila mwezi umekua mwezi wa faida. Mteja anafurahia riba yake inayolipwa mwanzo wa mwezi kila mwezi, malipo ya riba ni rafiki mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu (3) mpaka miaka miwili (2). Ni jambo la fahari kuona Benki ya kitanzania inatoa fursa kwa Watanzania na kuwawezesha kuboresha maisha na uchumi’.

Alisema DCB Lamba Kwanza imepokewa kwa mikono miwili na wateja wetu na kufanikiwa kuvuka malengo kwa kukusanya amana ya zaidi ya shs bilioni 18.5 ambapo awali Benki ilikusudia kuuza kiasi cha shs bilioni 15.

 “Kwa namna ya kipekee ningependa kwanza kabisa kuwashukuru wateja wetu kwa kuendelea kutuunga mkono kwa kila bidhaa tunayoiingiza sokoni na kutuwezesha kuvuka malengo hii inaonyesha ni jinsi gani DCB inavyo aminika kwenye soko.

“Benki ya DCB tupo imara na tumejidhatiti katika kubuni na kuingiza bidhaa zitakazokidhi kiu ya mahitaji ya huduma za kifedha kwa wateja wetu,”

Kwa sasa benki imeendelea kufanya maboresho katika baadhi ya huduma zake ikiwa ni pamoja na kupunguza riba na kuongeza muda wa marejesho hadi miaka 15 kwa mikopo ya ujenzi na ununuaji wa nyumba za makazi kwa wateja wetu wote hususan wafanyabiashara na waajiriwa. Hii imefanya benki yetu kuongoza kutoa mikopo mingi zaidi ya ujenzi wa nyumba na ununuaji wa nyumba Tanzania. (kwa takwimu za Tanzania Mortage Refinance-taasisi iliyo chini ya benki kuu). Tunatoa wito kwa wajasiriamali wote na wafanyakazi wenye lengo la kununua au kujenga nyumba kuwahi fursa hii.

Vilevile benki inatoa huduma za kidigitali kupitia DCB DIGITAL inayomuwezesha mteja kufungua akaunti kupitia simu yake ya mkononi, DCB sokoni inayomsaidia mkulima,wenye viwanda vya kilimo  pamoja na wafanya biashara wa kilimo kwenye mnyororo wa thamani. Vile vile tuna akaunti na huduma nyingi zinazotoa fursa kwa watanzania kuweka akiba lakini pia kupata faida ya fedha zao.

Kampeni hii ni muendelezo wa mafanikio yanayofanywa na Benki ya DCB kwani Benki hii imeendelea kupata faida, na kufikia kipindi cha nusu ya kwanza ya  mwaka huu imeweza kupata faida ya sh. bilioni 1.2 ikiwakilisha ongezeko la asilimia 118% kutoka faida ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2018. Utendaji wa benki umeimarika,huku ufanisi katika nyanja zote muhimu ukiongezeka kwa kiwango cha kuridhisha ukichagizwa na kukua kwa biashara na ukusanyaji wa mikopo chechefu. Vile vile benki imeendelea kuvunja rekodi  katika malengo kama  ilivyotokea  hivi karibuni ilipotangaza kuvuka malengo katika zoezi la uuzwaji wa hisa zake kwa  kuuza hisa milioni 36.6, ikiwa ni zaidi ya malengo ya awali  ya kuuza hisa milioni 33.9 na  kufanikiwa kukusanya sh. Bilioni 9.7 sawa na asilimia 108.99 ya matarajio ya awali ya kukusanya shilingi Bilioni 8.9.

“Tunafurahi kuwaambia kuwa lengo letu limetimia, kampeni imeisha lakini bidhaa ya DCB Lamba Kwanza itaendelea, hivyo wale wateja ambao bado hawajafungua akaunti hii bado ipo na wanaweza kuwahi katika matawi yetu kuanza kuwekeza na ‘KULAMBA’ riba.

Ikumbukwe Kuwa

Benki ya Biashara ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama Benki ya Jumuiya ya Wananchi “community bank” na Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kufuatia kilio cha wakazi wengi wa Jiji kutokuwa na njia rahisi ya kupata mitaji midogo midogo ya biashara.

Benki ya DCB imekuwa ni benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa mwaka 2008, na imeweza kukuza mtandao wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la Dodoma, na inatarajia kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.

Uboreshaji huduma na mahusiano ya wateja umekuwa ndio kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na za muda mrefu hasa kutoka kwa wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali yaliyoendelea kuwekeza na benki ya DCB. 

Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 195,611 Agasti 2019 na hivyo kuchangia ongezeko kubwa la miamala ya kibenki. 

Benki ya DCB imefungua mtandao wa mawakala na huduma za kijiditali hadi kufikia 1000 nchi nzima. 

Share:

NBC zindua mkopo wa bima

Waziri wa Ujenzi, na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwele (kushoto), akizungumza na MKurugenzi wa Biashara wa Benki ya NBC, Elvis Ndunguru (wa tatu kushoto), mara baada ya mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori  Tanzania (TATOA), ambako benki hiyo ilizindua rasmi huduma yake mpya ya mkopo wa bima.  Wanaoangalia ni baadhi ya maofisa wa benki hiyo.

BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua mkopo wa bima ikiwalenga zaidi wafanyabiashara walio katika sekta ya uchukuzi.

Akizungumza na washiriki wa mkutano mkuu wa mwaka wa Chama cha Wamiliki wa Malori Tanzania (TATOA) jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru alisema mkopo huo unapatikana kwa kuanzia kiasi cha shilingi milioni 1 mpaka milioni 300.

Alisema mkopo wa bima wa NBC ni kwa ajili ya bima za biashara zote zikiwemo biashara za magari, bidhaa zilizo safarini, majanga ya moto, ujambazi, hatari zote za barabarani na ajali kwa wafanyakazi.

“Mtu yoyote mwenye mahitaji ya bima akiwa na rasilimali zozote kama vile nyumba ana sifa ya kupata mkopo huu bila kuwa na dhamana yoyote.

“Utalipia miezi miwili ya bima yako NBC na sisi tutalipia miezi 10 inayobaki kwa wakala wa kwa niaba yako, nawe utailipa benki kila mwezi kidogo kidogo. Mkopo huu una riba ndogo kabisa kuliko mikopo yote inayotolewa na benki”, aliongeza Bwana Ndunguru.

Pamoja na hayo mkurugenzi huyo alisema, uamuzi wa kuanzisha huduma inayowalenga wafanyabiashara imetokana na kasi ya utendaji wa serikali ya awamu ya tano katika kuondoa kero zikizokuwa zikiizorotesha sekta ya uchukuzi.

“NBC imeongeza kutoa mikopo zaidi katika sekta ya usafirishaji, mkopo wa bima kutoka NBC unakuwezesha kuendelea kuikinga biashara yako dhidi ya hasara au matatizo mengine yoyote hata kama huna fedha taslimu za kulipia bima”, alisema.

Awali akifungua mkutano huo, Waziri wa Ujenzi,  Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Isack Kamwele alipongea NBC katika juhudi inazofanya katika kuinua  sekta ya biashara ndogo na za Kati.

Akitoa mfano Waziri Kamwele alisema ni hivi karibu Benki ya NBC ilisaini makubaliano na Shirika la Posta Tanzania ambapo benki itaweka ofisi katika kila palipo na tawi la Shirika hilo popote nchini.
Share:

NBC yaendelea kusaidia ujenzi wa shule na ofisi za walimu nchini

Meneja wa Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (wa nne kushoto), akishikana mikono na Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan wakati akimkabidhi msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika shuleni hapo Visiwani Zanzibar jana.
Meneja wa Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (wa nne kulia) akikabidhi msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 8 kwa Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi vilivyotolewa na NBC ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika shuleni hapo, Zanzibar jana.
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (katikati, mwenye suti nyeusi) akikabidhi baadhi ya vifaa vya ujenzi vikiwemo mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 8 kwa baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Maandalizi ya Kisimkazi vilivyotolewa na NBC mjini Zanzibar jana. Wa nne kushoto ni Mkuu wa Mkoa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan.
Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan (wa pili kushoto), akizungumza kabla hajapokea msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kutoka benki ya NBC kwa ajili ya kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi katika hafla iliyofanyika visiwani Zanzibar jana. Wa nne kulia ni Meneja wa NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso.
Meneja wa Tawi la Benki ya NBC Zanzibar, Ramadhani Lesso (wa pili kulia) akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa mabati 140 pamoja na vifaa vingine vya kuezekea vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 8 kwa ajili ya kuezekea madarasa manne pamoja na ofisi mbili za walimu za shule ya Maandalizi Kizimkazi vilivyotolewa na benki hiyo visiwani Zanzibar jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja, Hassan Khatibu Hassan.
Share:

Benki ya NBC yasaidia ujenzi wa kituo cha polisi Lindi

Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda (katikati aliyevaa suti), akikabidhi msaada wa mabati 135 pamoja na  mifuko 30 ya simenti vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga kusaidia  ujenzi wa kituo cha polisi cha Rondo Mnara ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika tawi la NBC mkoani Lindi.
Meneja wa Benki ya NBC Mkoa wa Lindi, Iovin Mapunda (katikati aliyevaa suti), akikabidhi msaada wa mabati 135 pamoja na  mifuko 30 ya simenti vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga kusaidia  ujenzi wa kituo cha polisi cha Rondo Mnara ikiwa ni sehemu ya shughuli za kusaidia jamii za benki hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika tawi la NBC mkoani Lindi.
Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Shaibu Ndemanga, akishikana mikono na Meneja wa Tawi la NBC Mkoa wa Lindi, Iovin  (kulia) wakati akipokea  msaada wa mabati 135 pamoja na  mifuko ya simenti 30 yenye thamani ya shilingi milioni 4 vilivyotolewa na NBC kusaidia ujenzi wa kituo cha polisi cha Rondo Mnara ikiwa ni sehemu ya shughuli za kuisaidia jamii za beni hiyo zinazoendelea kufanyika sehemu mbalimbali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika katika Tawi la NBC mkoani Lindi. Kushoto ni  Mwakilishi wa Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Lindi, Inspekta Benard Simpemba.
Share:

Benki ya NBC yaendelea kusogeza huduma karibu na wateja

Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega (kushoto), akishikana mikono na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya huku Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya akiangalia katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Arusha hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro (wa pili kushoto), akibadilishana mawazo na Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Linley Kapya wakati wa hafla ya chakula cha usiku iliyoandaliwa na benki ya NBC jijini Arusha juzi. Kutoka kushoto ni Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya, Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa Benki ya NBC, Linley Kapya (wa pili kushoto) akishikana mikono  na Katibu Tawala Mkoa wa Arusha, Richard Kwitega katika hafla iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake jijini Arusha hivi karibuni. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Gabriel Daqarro na Meneja wa Tawi la NBC Arusha, Mirage Msuya.
Mkurugenzi wa Wateja Wakubwa wa Benki ya NBC, Linley Kapya (katikati) akizungumza na baadhi ya wateja katika hafla waliyowaandalia jijini Arusha hivi karibuni kwa lengo la kufahamiana na kupata mrejesho wa huduma wanazopewa na benki hiyo.
Share:

BENKI YA KCB TANZANIA YADHAMINI LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA 2019/20

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (kushoto), akikabidhi hundi ya shilingi milioni 500 kwa Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia, kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. Wanaoshuhudia, (watatu kulia) Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, (Mkuu wa Idara ya Masoko wa Benki hiyo Bi. Christine Manyeye na Mwanasheria Mkuu waBenki ya KCB, Bi. Anthonia Kilama hafla ya makabidhiano hayo imefanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario (wa tatu kushoto), Pamoja na Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia, wakionyesha hundi ya shilingi milioni 500 iliyotolewa na benki hiyo kwa ajili ya udhamini wa Ligi kuu Tanzania Bara. Benki ya KCB imeendeleza udhamini wa ligi hiyo kwa msimu wa 2019/20 ikiwa msimu wa tatu mfululizo. (watatu kulia) ni Mwenyekiti wa Bodi Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga,  wengine ni viongozi kutoka TFF na KCB.

Benki ya KCB Tanzania imengia mkataba na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ili kuwa mdhamini mwenza wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara  kwa msimu wa 2019/2020. Mkataba huo wenye thamani ya shilingi  za Kitanzania 420,000,000 kabla ya kodi, ulitiwa saini leo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB, Nd. Cosmas Kimario na Rais wa TFF Nd. Wallace Karia katika Hoteli ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.

Benki ya KCB Tanzania ilidhamini ligi hiyo kwa mara ya kwanza msimu wa 2017/18 kwa thamani ya shilingi za Kitanzania 325,000,000 na kuongeza udhamini kwa msimu wa 2018/19 kufikia shilingi za Kitanzania 420,000,000. Mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa udhamini wa misimu iliyopita ndiyo yameivutia Benki ya KCB Tanzania kuendeleza udhamini huo kwa kiasi cha shilingi za Kitanzania 420,000,000 kupelekea jumla ya udhamini ndani misimu mitatu kuwa shilingi za Kitanzania 1.165bn.

Hafla ya kutia saini makubaliano hayo imehudhuriwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Benki ya KCB Tanzania, Nd. John Ulanga, Katibu Mkuu TFF, Nd. Kidao Wilfred, Mwenyekiti wa bodi ya Ligi Kuu, Nd. Steven Mnguto na Mkurugenzi wa Bodi ya Ligi, Nd. Boniface Wambura, Pamoja na Wakurugenzi wa Bodi na wafanyakazi Benki ya KCB Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kusainiwa mkataba huo, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya KCB Tanzania, Nd. Cosmas Kimario alisema kwamba pamoja na dhamira ya benki hiyo kurudisha kwa jamii, udhamini huo pia ni fursa kubwa kwa Benki ya KCB kuwekeza kwenye sekta yenye kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa kukuza ajira na vipaji vya vijana wa Kitanzania.

Zaidi ya kutengeneza ajira kwenye soka, Benki hiyo imewekeza kwenye programu ya KCB 2jiajiri ambayo hadi sasa imetoa mafunzo ya uweledi wa biashara kwa wanawake 256 na vijana 100 kuanzia mwezi Oktoba. “Matarajio ya benki yetu ni kuona Watanzania wengi zaidi wanapata ajira kupitia sekta mbali mbali tunazozigusa.” Alisema Nd. Kimario.

“Sisi Benki ya KCB, mbali na biashara tunatimiza  wajibu wetu katika jamii inayotuzunguka kwa kuiunga mkono serikali yetu kupinga umasikini nchini. Hivyo pia tunasaidia jamii hitaji kupitia sekta za: elimu, afya, mazingira, wajasiriamali, watoto waishio katika mazingira magumu.” Aliongeza Nd. Kimario.

Rais wa TFF, Nd. Wallace Karia aliishukuru Benki ya KCB Tanzania kwa kuidhamini Ligi kuu Tanzania Bara jambo ambalo alisema litasaidia kufanikisha msimu huu wa ligi kuu 2019/20. Pia alizitaka taasisi zingine na watu binafsi kuiga mfano huo kuweza kutoa michango ya hali na mali ili kukuza maendeleo ya soka kwa timu za ligi kuu.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages