Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akibadilishana hati za mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay, makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo biashara nchini. NBC pia ilipokea mfano wa hundi ya Dola 1,000,000 kutoka PASS zitakazotumika kama dhamana katika mikopo ya kilimo itakayotolewa na benki hiyo. Hafla ilifanyika jijini Arusha leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akisaini hati za makubaliano ya ushirikiano wa miaka mitano na Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay, makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo biashara nchini. NBC pia ilipokea mfano wa hundi ya Dola 1,000,000 kutoka PASS zitakazotumika kama dhamana katika mikopo ya kilimo itakayotolewa na benki hiyo. Hafla ilifanyika jijini Arusha leo. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto), akipokea mfano wa hundi wa Dola 1,000,000 kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay makabaliano yatakayoiwezesha NBC kusaidia mnyororo wa thamani wa sekta ya kilimo biashara nchini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Biashara wa NBC, Elvis Ndunguru na Ofisa Mtendaji Mkuu wa PASS, Anna Shenalingigwa.
Mkurugenzi Mtendaji wa Asasi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi akizungumza katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (wa pili kushoto, walioketi) na Mkurugemzi Mtendaji wa PASS, Nicomed Bohay (kushoto kwake), wakipozi kwa picha ya kumbukumbu pamoja na watumishi wa taasisi hizo mbili mara baada ya kumalizika kwa tuki hiyo mjini Arusha leo.
SEKTA ya kilimo na
ufugaji nchini kupitia Taasisi ya Kusaidia Sekta Binafsi ya
Kilimo (PASS) na Benki ya NBC Tanzania wameingia katika ushirikiano wa
kuwawezesha wakulima nchini kupata mikopo ili kuongeza mnyororo wa thamani
katika sekta hiyo.
Akiongea kwenye utiaji wa saini
makubaliano ya ushirikiano huo wa miaka mitano, kati ya PASS na NBC
jijini Arusha leo, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi amesema kuwa
ushirikiano huo utawezesha benki hiyo kutekeleza mipangokazi yao ya kuongeza
mnyororo wa thamani katika kilimo biashara.
Ameeleza kuwa
ushirikiano huo kati ya taasisi hizo mbili utawezesha wakulima wafugaji nchini
kupata mafunzo bora yenye tija ya kuongeza mapato au mavuno, uandaaji wa
maandiko ya kibiashara na uwekezaji kwenye kilimo,kupata huduma za kilimo kwa
makundi,kujengewa uwezo wa kuendesha biashara kwa faida na dhamana ya mikopo
hadi asilimia 60%.
Amesema kuwa hayo yote
yanalenga kumwezesha mkulima na mfugaji kutoka pale alipo na kuendelea kukua
ili aweze kutoa mchango wake katika kujenga uchumi imara wa nchi yetu na huduma
hizi zinapatikana katika matawi yoteya NBC nchi nzima.
“Niwaombe wadau wa
kilimo na mifugo nchini kuchangamkia fursa hii kwa kutembelea katika matawi
yetu na makubaliano haya kati yetu na PASS ni kwa kipindi cha miaka mitano
kuanzia sasa na yatakuwa bora na yenye manufaa makubwa kwa wadau wa sekta ya
kilimo kwa siku za usoni”alisisitiza Sabi.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Asasi ya kusaidia Sekta Binafsi ya Kilimo (PASS), Nicomed Bohay ameeleza
kuwa taasisi hiyo imekuwa ikisaidia wateja katika kuandaa miradi bora ya
uwekezaji ambayo inaweza kupatia faida kubwa na kuwezesha upatikanaji wa huduma
za fedha kwa ajili ya ufadhili wa miradi kupitia udhamini wa mikopo kwa
kushirikiana na benki za kibiashara.
Amesema kuwa wameshaingia makubaliano
na benki za kibiashara 16 nchini na makubaliano hayo na benki ya NBC taasisi
yao imetoa dola za kimarekani million 1 kwa ajili ya udhamini wa mikopo ambayo
itatolewa kwa wakulima na wafugaji kupitia benki ya NBC.
“PASS imeendelea kuwa shirika la mfano,
jumla ya wajasiriamali wa kilimo 929,172 wamefaidika na mikopo iliyodhaminiwa
na PASS inayofikia shilingi bilioni 712 kati ya mwaka 2000 na 2018,” alisema.
Pamoja na hayo Mkurugenzi wa PASS
aliongeza kuwa, mwaka 2019 ni mwaka wa pili wa mpango mkakati wao wa miaka
mitano (2018-20220 wakilenga kuutengeneza ajira 700,000 kupitia sekta ya kilimo
wakitarajia familia zipatazo 235,253 kunufuaika kupitia mikopo yenye thamani ya
shilingi bilioni 210.6.