Benki ya Biashara ya DCB yazindua akaunti ya muda maalum ijulikanayo kama ‘DCB Lamba Kwanza’

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya Biashara ya DCB , James Ngaluko (wa tatu kushoto) akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya muda maalum ijulikanayo kwa jina la ‘DCB Lamba Kwanza’ inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 papo hapo mara baada ya kuwekeza. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja wa DCB Tawi la Temeke, Anna Kasyupa, Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa DCB, Rahma Ngassa, Meneja wa Akaunti za Kidigitali, Fredrick Mwakitwange na Meneja wa Tawi la DCB Magomeni, Fortunata Benedict.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara ya DCB, Rahma Ngassa (wa pili kushoto), akizungumza jijini Dar es Salaam leo, wakati wa uzinduzi wa akaunti mpya ya muda maalum ijulikanayo kwa jina la ‘DCB Lamba Kwanza’ inayomuwezesha mteja kupata riba ya hadi asilimia 14 papo hapo mara baada ya kuwekeza. Wengine kutoka kushoto ni; Meneja wa DCB Tawi la Temeke, Anna Kasyupa, Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko, Meneja wa Akaunti za Kidigitali, Fredrick Mwakitwange na Meneja wa Tawi la DCB Magomeni, Fortunata Benedict.

Benki ya biashara ya DCB imezindua bidhaa maalumu kwa ajili ya wateja wa akaunti ya muda maalum (Fixed Deposit) ijulikanayo kama ‘DCB LAMBA KWANZA’.

Bidhaa hii mpya itamuwezesha mteja wa DCB kuwekeza hadi miaka miwili na kupata riba ya hadi asilimia 14% ya amana atakayo wekeza na riba ya mwezi italipwa papo hapo pindi anapofungua akaunti.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hii jijini Dar es Salaam leo Mkurugenzi wa Biashara, James Ngaluko alisema Akaunti hii itamuwezesha mteja wetu kupata riba kila mwezi hivyo kufanya wateja wa DCB kufurahia maisha kwani kila mwezi ni mwezi wa faida.

Riba inalipwa mwanzo wa mwezi kila mwezi, malipo ya riba ni rafiki mteja anaweza kuwekeza kuanzia miezi mitatu (3) mpaka miaka miwili (2). Ni matumaini yetu wateja wetu watachangamkia fursa hii na watafurahia akaunti hii kwani tumeboresha maisha na uchumi’.

Alisema Lengo kubwa la kuanzishwa kwa akaunti hii ni kuwapa fursa wateja wa DCB kuweza kuwekeza kwa faida na manufaa. Wateja na wasio wateja wa DCB wanaweza sasa kufungua akaunti hii ya DCB Lamba Kwanza na kuweza kuwekeza.

‘Tumekuja na jina hili la ‘DCB Lamba Kwanza’ kama lilivo neno lenyewe, mteja wetu ataweza kulamba riba ya mwezi papo hapo pindi atakapofungua akaunti’ aliongeza mkurugenzi wa biashara.

Pamoja na hayo Bwana Ngaluko aliongeza kuwa akaunti ya DCB lamba kwanza HAINA STRESS kwani itamuwezesha mteja kupata kipato kikubwa kila mwezi kwa kipindi kirefu, hivo kuitofautisha na akaunti nyingine kama hizi…..’ukiwa na akaunti ya DCB lamba kwanza kila mwezi ni mwezi wa mshahara’.

Mteja anaweza kufungua akaunti katika tawi lolote la DCB ama kupitia huduma za kidigitali kwa kupiga *150*85# huku mteja akihakikishiwa usalama wa pesa zake wakati huohuo hakuna makato ya akaunti ya kila mwezi na hakuna gharama ya kufungua akaunti.

Ikumbukwe kuwa Benki ya Biashara ya  DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikiwa kama Benki ya Jumuiya ya Wananchi “community bank” na Manispaa za Jiji la Dar es Salaam kufuatia kilio cha wakazi wengi wa Jiji kutokuwa na njia rahisi ya kupata mitaji midogo midogo ya biashara. Benki ya DCB imekuwa ni benki ya kwanza kuorodheshwa kwenye Soko la Hisa mwaka 2008, na imeweza kukuza mtandao wake wa matawi kufikia matawi nane likiwepo tawi la Dodoma, na inatarajia kuongeza matawi mengine mikoani katika miaka ya mbeleni.

Uboreshaji huduma na mahusiano ya wateja umekuwa ndio kigezo kikuu katika kuongeza amana nafuu na za muda mrefu hasa kutoka kwa wanahisa waanzilishi na mashirika mbalimbali yaliyoendelea kuwekeza na benki ya DCB.

Huduma za kidigitali zimekuwa chachu ya kuongeza ufanisi na kupunguza gharama za uendeshaji na gharama za riba. Akaunti hizi zinajumuisha akaunti ya kidijiti (DCB Digital Account), DCB Kibubu Digital Account, DCB FDR Digital account. Akaunti hizi zinamuwezesha mteja kufungua akaunti na kufanya miamala yote ya kibenki, Kutunza pesa na kuwekeza kwa kutumia simu yake ya mkononi.

Idadi ya wateja imeongezeka kutoka 144,475 mwaka 2017 kufikia 175,204 mwaka 2018 na hivyo kuchangia ongezeko kubwa la miamala ya kibenki.

1. Benki ya DCB ndio benki ya kwanza kuorodheshwa katika soko la hisa la Dar es Salaam.

2. Benki ya DCB ndio benki pekee iliyokua kutoka benki ya wananchi/jamii (community bank) na kufanikiwa kuwa benki ya biashara (commercial bank).

3. Benki ya DCB imefanikiwa kukuza mtandao wa matawi yake kufikia manane huku ikifungua tawi Dodoma na inaendelea na mchakato kufungua matawi na vituo vya huduma (service centers) katika mikoa mingine.




4. Benki ya DCB imefungua mtandao wa mawakala na huduma za kijiditali hadi kufikia 1000.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages