Rais wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
Dk. Ali Mohammed Shein (wa pili kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibari hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu,
Rais wa Zanzibar wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein ameipongeza Benki ya NBC kutokana na kasi
yake na juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar.
Akizungumza kwa niaba ya rais wa Zanzibar katika hafla ya futari
iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika mjini Zanzbar hivi karibuni, Mkuu wa
Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema pato la taifa limekuwa
likikuwa mwaka hadi mwaka kutokana na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali
ikiwemo Benki ya NBC.
Aidha Dk.Shein ameihimiza benki hiyo kuendelea na juhudi zake za
kuimarisha mazingira bora na huduma kwa wateja wake ili kwenda sambamba na kasi
ya mabadiliko ya huduma za kifedha yanayotokea siku hadi siku na kukuza
maendeleo bora nchini.
Hata hivyo ameipongeza Benki hiyo kwa kuonesha umuhimu kwa
wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo
ya kufutarisha na kutoa huduma nyengine mbali mbali kwa jamii.
Awali akizungumza katika hafla hiyo ya futari Kaimu Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC, Dk. Kassim
Hussein amesema kukuwa kwa huduma za kifedha Zanzibar pia kunatokana na huduma
bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja
wake.
Amesema mazingira salama yaliopo Zanzibar yanayoimarishwa na
viongozi wakuu wa nchi imewezasha benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma
za kifedha kwa ufanisi na umakini zaidi.
Dk. Kassim amesema licha ya huduma mbali mbali zinazotolewa
na benki hiyo pia imeanzisha huduma za kibenki zinazofuata misingi ya kiislam
ambayo inatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa misingi ya sharia ya kiislamu .
Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutumia benki hiyo katika kufanya
miamala mbali mbali bila kujali misingi ya dini kwani ni salama katika ukuwaji
wa uchumi nchini.
Katika Hafla hiyo ya futari iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein , mawaziri , Jaji mkuu
, Mufti Mkuu wa Zanzibar na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar pamoja na wateja wa benki ya NBC.