KAIMU BALOZI WA ZIMBABWE NCHINI AZUNGUMZA NA WABUNGE WA BUNGE LA TANZANIA WANAOWAKILISHA BUNGE LA AFRIKA LEO MJINI DODOMA

Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akisalimiana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana jana katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana jana katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akizungumza na Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, walioongozwa na Mwenyekiti wa Wabunge hao, Mhe. Asha Juma (katikati) walipokutana jana katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma. Wa pili kulia ni Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulie na kulia ni Mbunge wa Momba, Mhe. David Silinde
Kaimu Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania, Mhe. Martin Tavenyika (kushoto) akiagana na Mwenyekiti wa Wabunge wa Bunge la Tanzania wanaowakilisha Bunge la Afrika, Mhe. Asha Juma (kulia) walipokutana jana katika Ofisi ya Bunge Mjini Dodoma.
Share:

Zoezi la kuwasikiliza wakinamama Waliotelekezwa lafanikisha Watoto 2008 kupata uhakika wa Matunzo kutoka kwa Baba zao.


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda ametoa tathimini  ya Zoezi la kuwasikiliza wakina Mama  waliotelekezwa na kufikaofisini  kwake kwa lengo la kupata msaada wa kisheria lililokuwa likifanyika ofisi za mkoa huo na kumalizika leo ambapo lilifanyika takribani siku 15, mfululizo.

Akizungumza na waandishi wa Habari Makonda amesema zoezi hilo Idadi  ya kina Mama wamejitokeza ni  17,000 ambapo waliandikisha ni 7,000  ikiwa ni pamoja na wakina Baba 200 ambao walifika kutoa malalamiko yao, ambapo wataoto 2008 wamepata uhakika wa kupata fedha za matunzo kutoka kwa baba zao.

Amesema tatizo hilo ni kubwa katika jamii Jambo lililopelekea watoto kuwa omba omba, wanawake wanaotoa mimba na watupa vichanga pamoja na wanaotenda uhalifu wa kuiba pamoja na kuwa panya road, kutokana na kukosa matunzo kutoka kwa wazazi wao.

Amesema katika zoezi hilo wameweza kufanikiwa kusikiliza mashauri 7184, na kuwapatanisha  watoto 2008 waliopata uhakika wa matunzo kutoka kwa baba zao.

 "Tumesajili mafaili 7,184 ambayo tumeyasikiliza na kuyafanyia kazi ambapo familia 2008 wamepata uhakika wa kupata matunzo kutoka kwa baba zao, idadi hii ni kubwa sana kwani wamepata kuwafahamu baba zao na wengine kupata amani ya kuendelea kusoma wakipata huduma stahiki" Amesema Makonda.


Aidha amesema watoto ambao hawana uhakika wa wazazi wao watapatiwa bima za afya kwa ajili matibababu ambapo watoto 2,971 wamesajiliwa kupata huduma hiyo.

Ameainisha makundi matatu ya wakina Baba walioko katika mkoa huo na walipata taarifa ya wito,na kukaidi kufika tayari majina yao yamekabidhiwa kwa kamanda wa Polisi Lazaro Mambosasa ili kuchukuliwa hatua za kisheria,  na kundi la pili ni wale waioko nje ya mkoa huo,ambapo wametumiwa barua kupitia wakuu wa mikoa yao, pamoja na kundi la mwisho ambalo wakina Baba walioko nje ya nchi wametumiwa barua kupitia Waziri  wa ofisi ya Rais Tamisemi Suleiman Jaffo pamoja na mabalozi wao.

Ameongeza kuwa watoto wawili ambao ni wa wachina wameahidiwa kupata huduma za matunzo kutoka kampuni moja iliyopo hapa nchini ambayo inashulika na Ukandarasi ambayo ni ya wachina.

Aidha amewashukuru wanasheria, waandishi wa habari, na watu wote walioshiriki kikamilifu katika Zoezi hilo na kuwataka kuendelea na moyo huo ili kufanikisha maendeleo ya nchi ikiwa ni pamoja na kuanza kuboresha katika ngazi ya Familia.
Share:

Benki ya Barclays Tanzania yasaidia kambi ya upasuaji wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi na kutoa kadi za bima ya afya (NHIF) 200 kwa watoto hao.


Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy (wa tatu kushoto,) akikabidhi vifaa vya kusaidia upasuaji wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa (wa pili kushoto), katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wengine ni watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.
Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji Mikopo Isiyolipwa wa Benki ya Barclays Tanzania, Khatibu Mohammedy(kulia), akikabidhi kadi ya bima ya afya (NHIF) kwa mmoja wa watoto wenye tatizo la vichwa vikubwa na mgongo wazi, Joy Jacob  katika hafla ambayo Barclays pia ilitoa msaada wa kadi za Bima ya Afya (NHIF), kwa watoto 200 pamoja na kuwezesha kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi. Hafa hiyo ilifanyika katika Taasisi ya MOI, Dar es Salaam jana. Wa pili kushoto (mstari wa nyuma) ni kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tiba wa Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dk.Nicephorus Rutabansibwa, watumishi wa MOI na wa kutoka Barclays.
Madaktari wa upasuaji wa MOI wakifanya upasuaji mwa mmoja wa watoto wanaosumbuliwa na tatizo la kichwa kikubwa katika kambi ya upasuaji iliyodhaminiwa na Barclays katika hospitali hiyo jana. Baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo wakiongozwa na Mkuu wa Kitengo cha Ukusanyaji wa Mikopo Isiyolipwa wa Barclays Khatibu Mohammedy (nyuma katikati), wakishuhudia.
Baadhi ya watoto 200 waliopewa msaada wa kadi za bima ya afya (NHIF) na benki ya Barclays Tanzania wakionyesha kadi zao katika hafla hiyo katika hafla ambayo benki hiyo pia ilidhamini kambi ya siku moja ya upasuaji wa watoto 30 wenye matatizo ya vichwa vikubwa na mgongo wazi.
Share:

Kampuni ya Uber imesaini mkataba na Msanii Idris Sultan kuwa Balozi wake nchini Tanzania mwaka 2018


Kampuni ya Uber imemtangaza msanii Idris Sultan kuwa balozi wake mpya nchini Tanzania mwaka 2018. Idris anakuwa msanii wa kwanza nchini Tanzania kuwa balozi wa Uber, programu ya usafiri yenye umaarufu mkubwa, nchini Tanzania.
 
Msanii huyu wa uchekeshaji, muigizaji wa tamthlia, na mtangazaji wa vipindi vya redio ametangazwa rasmi katika hafla ya kukata na shoka iliyokwenda kwa jina la #IdrisnaUber iliyohudhuriwa na wageni wachache na wanahabari wa humu inchini. Shughuli hiyo imefanyika katika mgahawa wa kifahari wa Akemi jijini Dar es Salaam.
 
Tangu mwanzoni mwa zoezi hili, tulifanya juhudi kubwa kuhakikisha kwamba tunampata balozi mwenye ufuasi mkubwa na atakayeiletea Uber ufanisi nchini Tanzania,amenukuliwa Bi.Elizabeth Njeri, Meneja wa Masoko wa Uber Kanda ya Afrika Mashariki. Idris Sultan ni mcheshi na ni msanii ambaye hafanyi mambo yake kwa mazoea, pia anaheshimika katika tasnia ya uchekeshaji,tamthlia, na utangazaji wa vipindi vya redio. Tuna imani kwamba Idris atailetea Uber tija kubwa kwa sababu ni mzalendo kweli kweli - yeye ni kielelezo cha Utanzania na anawasiliana na mashabiki wake kupitia mitandao ya jamii kila wakati. Hizi ndizo sifa tunazosistiza tunapotaka kuwa na mkataba na mabalozi wa kampuni yetu kwa sababu zinasaidia sana katika kuonesha kwamba tunajali maslahi ya wasafiri na madereva wanaotumia mfumo wetu nchini Tanzania.
 
Akizungumza kwenye hafla hiyo Bw Alfred Msemo; Meneja Msimamizi wa Uber nchini Tanzania, alisema; “Kampuni ya Uber inajituma kutumia uwezo wake kupitia oparesheni zake kimataifa ili kuwa karibu na wateja wake humu nchini. Mchango wa Idris Sultan katika muziki wa Tanzania unaendana na dhamira yetu ya kujenga kampuni ya kimataifa inayogusa maisha ya madereva na wasafiri wanaotumia mfumo wetu hapa nchini. Tutaendelea kuwahudumia wasafiri wetu sambamba na kutoa fursa za ajira kwa madereva wanaotumia mfumo wetu.
 
Idris alifurahi sana alipotangazwa kuwa Balozi wa Uber nchini Tanzania; “Nimefurahi sana na ni heshima kubwa kwangu kupata fursa hii adimu ya kushirikiana na Uber,kwa sababu mimi nishabiki mkubwa wa mapinduzi yaliyoletwa katika sekta ya usafiri kupitia kwa mfumo wake kote duniani. Nimefurahi kuona jinsi Uber imepata umaarufu jijini Dar es Salaam, binafsi mara nyingi mimi hutumia usafiri wa uberX nikiwa na marafiki zangu kwenye mitoko yetu ya jioni na sasa wamaleta huduma nyingine ya bajaji; uberPOA ambayo nina hamu sana kuitumia - utaniona hivi karibuni. Uber inaendelea kubadilisha maisha ya maelfu ya madereva jijini Dar es Salaam sambamba na kuwapa wasafiri uhuru wa kuchagua usafiri wanaotaka. Nimefurahi sana kuwa sehemu ya kampuni ambayo inajituma kuleta mabadiliko chanya katika maisha yetu.
 
Baadaye kwenye hafla hiyo, Idris alipanda jukwaani na kuwatumbuiza mashabiki, wanahabari,na wafanyakazi wa Uber kwa kionjo cha kazi yake ya uchekeshaji. Msanii huyo na mshindi wa zamani wa shindano la Big Brother Africa alivunja mbavu za umati huo kwa vichekesho vyake. 
 
Tangazo hili linakuja siku chache tangu Uber ilipo tangaza kushirikiana na Tigo kwenye mpango ambao wateja wa Tigo wanapata bando za bure wanapotumia programu ya Uber. Ushirikiano huu wa kipekee nchini Tanzania umekuwa na manufaa makubwa kwa wasafiri na madereva wanaotumia Uber na umechochea wasafiri na madereva zaidi kujiandikisha kutumia program ya Uber nchini Tanzania.
Share:

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu akutana na uongozi wa juu wa NBC jijini Dar

Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kulia), wakati alipotembelea ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  Wa pili kushoto ni Mkurugenzi wa Wateja BInafsi wa nbc, Filbert Mponzi. 
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kushoto), akimsikiliza  Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Filbert Mponzi wakati alipotembelea ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.  
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Anthony Mtaka (kulia), akimsikiliza  Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi (kushoto), wakati Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa benki hiyo, Filbert Mponzi akiangalia  wakati alipotembelea ofisi za makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam hivi karibuni.
Share:

Airtel Tanzania yaongoza katika mitandao ya kijamii

Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda akiongea baada ya Airtel kuibuka kinara katika kutoa hudumia kupitia mitandao ya kijamii, akishuhudia Mkurugenzi wa Mawasiliano Airtel Tanzania, Bi Singano Mallya
Airtel Tanzania imetajwa kuwa moja ya makampuni bora ambayo yanajibu vizuri maswali ya mashabiki na wateja wake katika robo mwaka ya kwanza ya mwaka 2018.
Ripoti hii imetolewa na kampuni ya Socialbakers ambayo ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii. 
Kwa mujibu wa Socialbakers, tathmini ya robo hii ya mwaka ilifanyika kuanzia Januari 1, 2018 hadi Machi 31, 2018 na kuifanya Airtel Tanzania iibuke kidedea.
Kampuni hiyo ya Social bakers imekabidhi cheti kama ishara ya ushindi huu na kuonesha kuwa Airtel iliweza kujibu vizuri maswali ya mashabiki wake na wateja kupitia mtandao wa Face book kwa asilimia 98 na hivi kuyapiku makampuni mengine yote ya simu Tanzania. 
Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania, Bwn Isack Nchunda alisema wanajivunia kupata utambulizi huo na inaonesha jinsi gani wamekuwa wakijituma kuhakikisha wateja wao wanapata majibu ya maswali yao kwa wakati kupitia mitandao ya kijamii hususani Face book. 
“Tunayo faraja kuweza kutambuliwa kwa namna hii na sisi tunalo jukumu la kuendelea kuhakikisha wateja na mashabiki wetu wanapata majibu wanayohitaji kwa wakati na mitandao ya kijamii imeturahisishia kazi hii hususani kupitia Face book tumeweza kujibu maswali kwa haraka na kwa wateja wengi zaidi kwa wakati mmoja,” alisema. 
Mitandao ya kijamii kama Face book inatakiwa kutangazwa zaidi ili itumike kwa wingi kwani itapunguza usumbufu wa wateja kusubiri majibu kwa muda mrefu kama ilivyokuwa hapo awali ambapo walilazimika kupiga simu Airtel. “Kwa kupitia mitandao ya kijamii majibu yanatolewa hapo hapo na hili ndilo limetufanya tutambuliwe kwani tumeweza kutumia njia hii kwa ufanisi mkubwa na tathmini ya Socialbakers imeonesha kuwa katika robo ya kwanza ya mwaka huu tulijibu maswali kwa asilimia 98 na hivi kuibuka kidedea,” aliongeza Ndunda
Kwa mujibu wa Socialbakers, utambulizi huu unatokana na namna kampuni imeweza kujibu maswali ya watu kwa muda wa mwezi mitatu. Ili utambuliwe, lazima kampuniipokee maswali 50 kutoka kwa mashabiki katika robo husika na maswali hayo yaweze kujibiwa kwa zaidi ya asilimia 65. 
Socialbakers ni moja ya makampuni yanayoongoza duniani katika kutoa tathmini kuhusu namna makampuni mbalimbali yanawajibika katika kujibu maswali ya wateja wao katika mitandao ya kijamii hususani Face book, Twitter, Google+, LinkedIn na YouTube ili kusaidia makampuni kujua mafanikio ya kampeni mbalimbali kupitia mitandao hii.
Share:

DC MJEMA AONJA ADHA YA MAFURIKO AKIKAGUA MIUNDOMBINU ILALA

 
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Sophia Mjema akisaidiwa kuvuka kwenye daraja la muda alipokuwa akikagua leo daraja la Mto Msimbazi linalounganisha Ulongoni B na Gongo la Mboto, Dar es Salaam, ambalo ni moja ya madaraja yaliyobomoka kutokana athari za mvua za masika zinazoendelea kunyesha. Mjema alifanya ziara ya kukagua miundombinu ya barabara iliyoathiriwa na mvua katika wilaya hiyo. 
Mkuu wa Wilaya Mjema, akizungumza na wakazi wa Ulongoni baada ya kuwafuata upande wa pili kwa kutumia daraja hilo hatari.
 Mjema akiondoka baada ya kukagua daraja hilo la Ulongoni B.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema (kulia) akishauriana na Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Edward Mpogolo pamoja na Mkurugenzi wa Manisapaa ya wilaya hiyo, Msongela Palela alipofika kukagua daraja la Banguo Pugu Mnadani eneo ambalo mto umeacha kupita darajani na kumega eneo la barabara hali iliyosababisha kukata mawasiliano ya usafiri katika eneo hilo.
Wakiangalia jinsi mto Msimbazi ulivyoacha mkondo wake wa kawaida na kumega ardhi maeneo ya makazi ya watu pamoja na kuharibu barabara.
 Baadhi ya nyumba eneo la Bangua ambazo zimo hatarini kubomolewa na mafuriko.
 Nyumba iliyozungukwa na mto kila upande.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa na mtoto nyumba anayoishi na wazazi wake. Mtoto huyo alisema kuwa hajaenda shule kutokana na eneo hilo kutokuwa na eneo la kuvuka ng'ambo ya pili iliko shule yao.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema akioneshwa mkondo wa maji ambao umezibwa baada ya baadhi ya wakazi wa Majohe, kuuziba kwa kujenga nyumba kwenye mkondo huo kitendo ambacho kimesababisha maji kuingia kwenye majumba ya watu.
Mjema akiangalia baadhi yanyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
Diwani wa Kata ya Majohe, Waziri Mweneviale akimuonesha Mjema baadhi ya nyumba ambazo zimejengwa kwa kuziba mkondo wa maji eneo la Majohe, Dar es Salaam. Mjema ameamuru nyumba hizo zivunjwe kupisha mkondo huo.
 Mjema akikagua moja kati ya nyumba zilizojengwa kwenye mkondo wa maji.
Msingi wa nyumba ukiendelea kujengwa kwenye mkondo wa maji licha ya uongozi wa serikali ya Kata ya Majohe kuwakataza kujenga katika eneo hilo.
Wananchi wa Gongo la Mboto wakiangalia jinsi Mto Msimbazi ulivyosababisha maporomoko baada ya kufurika kufuatia mvua kubwa za masika zinazoendelea kunyesha sasa.
Daraja linalounganisaha Gongo la Mboto na Ulongoni A, limezungushiwa utepe ili watu wasipite baadaya kuathiriwa na mafuriko.
 Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja
 la Ulongoni A.

Nyumba iliyopo kando ya mto Msimbazi Ulongoni A, ikiezuliwa mabati  baada ya kuona imo hatarini kuathiriwa na mto huo.
Mkuu wa Wilaya ya Ilala akipita kwenye mfereji wa maji alipokwenda kukagua daraja  la Ulongoni A.
Mjema akisafiri kwa baada ya kumaliza kugua athari za mvua katika daraja la Ulongoni A
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (331) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (129) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages