Sanlam yachangia TZS 172,500,000 kuunga mkono mapambano dhidi ya ugonjwa wa COVID-19 nchini

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu (wa pili kushoto), akipokea mfano wa hundi ya shs 172,500,000 zilizotolewa na Kampuni ya Bima ya Sanlam Life Insurance na Sanlam General Insurance kusaidia juhudi za serikali katika kupambama wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu unaosababishwa na virusi vya Corona (covid-19). Hafla ya makabidhiano ilifanyika ofisini kwa Waziri Mkuu, jijini Dar es Salaam hivi karibuni. Kutoka kushoto ni;  Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Sanlam Life, Charles Mbaga, Mwenyekiti wa Bodi wa Sanlam, Balozi Dk. Matern Lumbanga, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Kanda ya Afrika Mashariki, Julius Magabe na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam Genral Tanzania, Gift Noko.

Na Mwandishi Wetu.

WAKATI maambukizi ya virusi vya Corona Tanzania yakiongezeka, Sanlam Life Insurance na Sanlam General Insurance ambayo ni makampuni tanzu ya Sanlam Group yanayoongoza kwa kutoa huduma za bima nchini, yameungana na Watanzania wengine kuchangia Shilingi 172,500,000 katika juhudi za kuupiga vita ugonjwa wa COVID-19.

Fedha hizo zimekabidhiwa rasmi kwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa ambaye pia ni Mwenyekiti wa Taifa wa Kamati ya kukabiliana na maambukizi ya COVID-19 ambapo Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amepokea msaada huo kwa niaba ya Waziri Mkuu.

Fedha zilizotolewa zinalenga kusaidia upatikanaji wa vifaa kinga na vifaa tiba husika kwa wahudumu wa afya, wagonjwa na jamii kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi mchango huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Sanlam – Kanda ya Afrika Mashariki, Bwana Julius Magabe amesema kampuni ya Sanlam imeguswa na janga hili la kidunia na kuona ni busara kuunga mkono juhudi za serikali katika mapambano haya na kutoa mchango huu.

“Makampuni ya bima ya Sanlam nchini yakiwa sehemu ya jamii, yanatambua kuwa ni wajibu muhimu kama taasisi kuwa sehemu ya jitihada hizi za kuhakikisha usalama wa afya ya jamii ambayo inatuzunguka,” amesema Bwana Magabe.

Bwana Magabe alieleza zaidi kuwa kama Sanlam Group na kampuni zake zilizopo Tanzania (Sanlam Life Insurance na Sanlam General Insurance), wanaimani kuwa elimu kwa jamii kuhusiana na janga hili la COVID-19 inatakiwa kuendelea kutiliwa mkazo, na kwamba michango ya wadau mbalimbali wa maendeleo itakuwa na msaada mkubwa kwenye hili, kusaidia watu kubadili tabia kama inavyoelekezwa na wataalamu wa afya, ili jamii ya Watanzania ibaki salama.

Kwa niaba ya Waziri Mkuu, Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu ameushukuru uongozi wa Sanlam kwa kuunga mkono juhudi za serikali katika wakati huu muhimu.

“Msaada huu umekuja katika wakati muafaka kwetu na hivyo, pamoja na shukurani, tunatoa wito kwa kampuni, taasisi na wafanyabiashara binafsi kuendelea kuisaidia serikali kwa hali na mali katika mapambano haya. Tunaahidi hatutawaangusha,” amesema Ummy.

Pamoja na kuchangia mapambano dhidi ya COVID-19, makampuni ya Sanlam yamechukua hatua stahiki pahala pa kazi kuhakikisha usalama wa wateja na wafanyakazi unalindwa.
Share:

Nabii SUGUYE atia SAINI leso za WAUMINI

Nabii Nicolaus Suguye akisaini moja ya Kitambaa cha muumini wa Kanisa hilo

Na Mwandishi wetu,

KATIKA jambo lililowashangaza wengi, ndani ya Kanisa la WRM lillopo Kivule Matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es Salaam, Kiongozi na Msimamizi Mkuu wa huduma hiyo, Nabii Nicolaus Suguye ameendesha Ibada ya kutia saini vitambaa vya maelfu ya waumini wa kanisa hilo.

Neno saini limetoholewa kutoka katika neno la kiingereza ‘sign’ ili lifanane na muundo wa Kiswahili na liwe ni neno kamili la Kiswahili na kutumika kama kitenzi na wakati mwengine kama nomino.

Nabii Suguye akionesha dhamiri ya dhati kuhakikisha kila aliyehudhuria Ibada hiyo anamsainia kitambaa chake.

Saini (kitenzi) ni kutoa idhini ili kitendo Fulani kitendeke au kipatikane. Matumizi yaliyozoeleka na kukubaliwa na wengi ni kutoa idhini au kuthibitisha kupatikana kwa kitu au jambo Fulani na mara nyinine ni kwa kuandika jina lako.

Tunatumia neno hili tunapotaka kuweka saini mahali fulani. Ni sahihi kusema kuweka saini na wala siyo kutia saini. Kutia lina maana ya kufanya kitu kiwemo ndani ya kitu kwa mfano nitilie chai badala ya kusema niwekee chai. Kuweka kitu maana yake ni kukitua kitu kama vile kuweka kitabu mezani au kuweka silaha chini.

Msururu wa Waumini ukisubiria kusainiwa Leso zao na Nabii Suguye

Neno sahihi (nomino) lina maana ya kuthibitisha au kuidhinisha kwa jambo kutendeka au kupatikana.

Awali nabii Suguye aliwafundisha maelfu ya waumini wa kanisa hilo umuhimu wa kuthibitishwa na Mungu, “Unapothibitishwa ni rahisi kwako kuomba lolote kwa Yule aliyekuthibitisha na akalifanya”

Mkiniomba neno lo lote kwa jina langu, nitalifanya.” Nabii alinukuu kutoka kwenye maandiko ya Biblia Injili ya Yohana 14:14

“Ninaposaini Leso ya kila mtu aliye hudhulia mahali hapa hii ni Saini ya USHINDI, ninapoisaini mahali hapa imesainiwa mbinguni na kupitishwa kuwa MSHINDI” alisema Nabii Suguye.

Nabii Suguye akiwahubiria maelfu ya waumini waliohudhuria Ibada hiyo

Akifundisha katika Ibada hiyo alisema kupitia tendo hilo la Imani iwe ni fahari kwao kujua kuwa, kuna umuhimu wa kujitakasa na kuwa katika mstari ule Neno la Mungu linatufundisha ili tupate kuthibitishwa nakuwa na hakika ya kupokea yale yote tuyaombayo kwa Mungu.

“Basi imani ni kuwa na hakika ya mambo yatarajiwayo, ni bayana ya mambo yasiyoonekana.” Waebrania 11:1



“Kupitia saini hii nakutabiria ukafanikiwe katika kila kitu utakachokwenda kukifanya kwaajili ya Utukufu wa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo.” Alisema Nabii Suguye wakati wa Ibada hiyo.
Share:

Washindi wa Ongeza Mshahara Wako na Absa Tanzania wapatikana

Mkuu wa Bidhaa kwa Wateja Rejareja wa Benki ya Absa Tanzania, Heristraton Genesis (wa pili kushoto), akichukua tiketi, ili kumpata mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya akaunti ya mshahara ya benki hiyo iliyopewa jina la ‘Ongeza Mshahara wako’ jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Ili kushinda mteja mpya hutakiwa kufungua akaunti ya mshahara ama kwa mteja wa zamani kupitisha mshahara wake benki katika mwezi ulio ndani ya kipindi cha promosheni ili kujishindia kiasi cha fedha hadi asilimia 100 ya mshahara uliowekwa. Wengine kutoka kushoto ni, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Rasuli Masudi, Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Absa, John Beja na Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Beda Biswalo.
Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Benki ya Absa Tanzania, John Beda (wa pili kulia), akisoma jina la mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya akaunti ya mshahara ya benki hiyo iliyopewa jina la ‘Ongeza Mshahara wako’ jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Ili kushinda mteja mpya hutakiwa kufungua akaunti ya mshahara ama kwa mteja wa zamani kupitisha mshahara wake benki katika mwezi ulio ndani ya kipindi cha promosheni ili kujishindia kiasi cha fedha hadi asilimia 100 ya mshahara uliowekwa. Wengine kutoka kushoto ni, Mkuu wa Bidhaa kwa Wateja Rejareja, Heristraton Genesis, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Rasuli Masudi, na Meneja Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Beda Biswalo.
Mkuu wa Bidhaa kwa Wateja Rejareja wa Benki ya Absa Tanzania, Heristraton Genesis (wa pili kushoto), akisoma jina la moja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya akaunti ya mshahara ya benki hiyo iliyopewa jina la ‘Ongeza Mshahara wako’ jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Ili kushinda mteja mpya hutakiwa kufungua akaunti ya mshahara ama kwa mteja wa zamani kupitisha mshahara wake benki katika mwezi ulio ndani ya kipindi cha promosheni ili kujishindia kiasi cha fedha hadi asilimia 100 ya mshahara uliowekwa. Wengine kutoka kushoto ni, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Rasuli Masudi, Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Absa, John Beja na Meneja Msoko na Mawasiliano wa beni hiyo, Beda Biswalo.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Beda Biswalo (kulia), akichanganya tiketi  ili kumpata mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya akaunti ya mshahara ya benki hiyo iliyopewa jina la ‘Ongeza Mshahara wako’ jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Ili kushinda mteja mpya hutakiwa kufungua akaunti ya mshahara ama kwa mteja wa zamani kupitisha mshahara wake benki katika mwezi ulio ndani ya kipindi cha promosheni ili kujishindia kiasi cha fedha hadi asilimia 100 ya mshahara uliowekwa. Wengine kutoka kushoto ni, Mkuu wa Bidhaa kwa Wateja Rejareja, Heristraton Genesis, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Rasuli Masudi, Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Absa, John Beja.
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Beda Biswalo (wa pili kulia), akisoma jina la mmoja wa washindi wa droo ya kwanza ya promosheni ya akaunti ya mshahara ya benki hiyo iliyopewa jina la ‘Ongeza Mshahara wako’ jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Ili kushinda mteja mpya hutakiwa kufungua akaunti ya mshahara ama kwa mteja wa zamani kupitisha mshahara wake benki katika mwezi ulio ndani ya kipindi cha promosheni ili kujishindia kiasi cha fedha hadi asilimia 100 ya mshahara uliowekwa. Wengine kutoka kushoto ni, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Rasuli Masudi, Mkuu wa Bidhaa kwa Wateja Rejareja, Heristraton Genesis na Mkuu wa Mtandao wa Matawi wa Absa, John Beja.
Share:

Wafanyakazi wanawake wa Jubilee Insurance na Jubilee Life insurance waadhimisha Siku ya Wanawake kwa kutoa misaada Hospitali ya Mwananyamala

Muuguzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Rose Musa (wa tatu kushoto), akipokea msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike vilivyotolewa na wafanyakazi wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance na Jubilee Life Insurance kwa kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya matukio kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana. 
Wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Bima ya Jubilee na Jubilee Life pamoja na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala wakionyesha ishara maalumu ya kauli mbiu ya Siku ya Wanawake Duniani 2020 isemayo ‘Wanawake katika Mshikamano Tutaendelea Mapambano’ wapolitembelea hospitalini hapo kutoa msaada  wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Ofisa Rasilimali Watu wa Kampuni ya Jubilee Insurance, Grace Tupa (kushoto), na mwenzake kutoka Jubilee Life Insurance, Doreen Offen Martin (kulia), wakikabidhi msaada wa shuka na vitu vingine kwa mmoja wa wazazi aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Tatu Hashim wakati wafanyakazi wanawake wa kampuni hiyo wakitembelea hospitalini hapo kutoa msaada  wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi hiyo hospitali hapo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Ofisa Utumishi na Utawala wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala, Mansour Anchi (kushoto), akizungumza wakati wafanyakazi wanawake wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance na Jubilee Life Insurance wapolitembelea hospitalini hapo kutoa msaada  wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi ya wazazi ya hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Meneja Mawasiliano wa Kampuni ya Bima ya Jubilee Insurance, Angela Tungaraza (kushoto), na Ofisa Mawasiliano wa kampuni hiyo, Baraka Mosha (kulia), wakikabidhi msaada wa shuka na vitu vingine kwa mmoja wa wazazi aliyejifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwananyamala, Tatu Hashim wakati wafanyakazi wa kampuni hiyo wakitembelea hospitalini hapo kutoa msaada wa vitu mbalimbali vikiwemo sabuni, mashuka na mataulo ya kike kusaidia wanawake waliolazwa katika wodi hiyo hospitali hapo ikiwa ni sehemu ya matukio yao kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani. Hafla hiyo ilifanyika hospitalini hapo, Mwananyamala, Dar es Salaam jana.
Share:

SCANIA IKO TAYARI KULETA MABASI YANAYOTUMIA GESI YA ASILI NCHINI TANZANIA

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd, Lars Eklund, akizungumza wakakati wa  kampuni hiyo kutangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus RapidTransit) hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu ya Scania iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd, Lars Eklund, akizungumza wakakati wa  kampuni hiyo kutangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus RapidTransit) hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi kuu ya Scsnia iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam. Mwengine pichani ni Meneja Masoko wa Scania, Eliavera Timoth. Hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu ya Scania iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya  Scania Tanzania Ltd, Eliavera Timoth (kulia), akizungumza wakakati wa  kampuni hiyo kutangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus RapidTransit) hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi kuu ya Scsnia iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd, Lars Eklund hafla hiyo ilifanyika katika ofisi kuu ya Scania iliyoko vingunguti jijini Dar es Salaam.

Na Mwandishi wetu;

Kampuni ya magari ya Scania Tanzania Ltd yatangaza kuleta mabasi yatumiayo gesi asilia ambayo ni bora kwa soko la Tanzania hasa kwa usafiri wa umma (Bus Rapid Transit). Bidhaa hii ni sehemu ya juhudi ya kampuni kuhakikisha inaongoza katika kuboresha sekta ya usafirishaji nchini. Kampuni ya Scania inaamini kuwa ni wakati sahihi kwa Tanzania kuingiza katika mfumo huu na mingine kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu kimazingira na kiuchumi.

Tanzania ina akiba kubwa ya gesi asilia na inahitaji maelfu ya mabasi ya jiji kwa mfumo wa BRT ambayo kampuni ya Scania inaweza kuleta. Kampuni ya Scania imekuwa imefanikiwa kuleta magari ya mfumo wa gesi kwa muda mrefu sehemu mbalimbali duniani kama Amerika Kusini, Ulaya na Australia.

Moja ya faida ya mabasi yanayoendeshwa na mfumo wa gesi asilia (Compressed Natural Gas) ni kwamba mfumo wake wa injini utasaidia kupunguza hewa chafu (Carbon dioxide) kwa asilimia 20 ambapo CO2 inatajwa kuwa ndio chanzo cha joto kali duniani, itapunguza gharama za uendeshaji, gharama kwa abairia na itasaidia serikali kuongeza mapato kupitia uuzaji wa gesi asilia.

Akizungumza na wanahabari katika ofisi kuu iliyoko Vingunguti kando na barabara ya Julius Nyerere jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Mtendaji wa Scania Tanzania, Lars Eklund amesema Tanzania inaelekea kuwa nchi ya viwanda, hivyo ufanisi unahitajika na kwamba mazingira yasisahaulike.

“Tunaamini ya kwamba Tanzania inahitaji kuwa na teknolojia mpya ili iendane na kasi ya nchi zilizoendelea. Tanzania ni tajiri sana kwa gesi asilia na ni muhimu kutumia nishati hii ya ndani kwa faida ya nchi, nchi itapata faida sana kwani itapunguza kiasi cha mafuta yanayoagizwa nje” na badala yake inaweza kuuza gesi ya ndani kwa waendeshaji wa ndani. Hakuna njia bora na ni ghari sana kujaribu kubadili injini ya dizel kuwa injini ya gesi. Alisema Bwana Lars Eklund.

Kumekuwa na taaria kupitia vyombo vya habari kutaka kubadili mfumo wa sasa wa magari ya BRT kutoka injini ya dizel kwenda injini ya gesi, suala hili halina tija kiufundi na kiuchumi kwa sababu injini ya dizeli imeundwa kufanya kazi katika mzunguko wa dizeli wakati injini za gesi na petrol zinaendeshwa kulingana na kanuni ya Otto na ujazo wa kuziba cheche. Kwa hiyo ni muhimu sana kuwepo kwa mipango bora ya upanuzi wa miundo mbinu ya gesi asili ambapo itasaida wauzaji na waendeshaji kuthubutu kuwekeza katika bidhaa sahihi za gesi asilia zitakazotumiwa barabarani haraka iwezekanavyo. Alisema Bwana Lars Eklund.

Kama sehemu ya kukuza huduma zake nchini, kampuni ya Scania Tanzania inatafuta kushirikiana na taasisi mbalimbali za elimu kufadhili wanafunzi wanaochukua elimu kuhusu matumizi ya gesi asilia (Compressed Natural Gas). Hii itasaidia kuongezeka kwa idadi ya mafundi na wataalamu katika uwanja huo hivyo kuongezeka kwa msaada kwa watumiaji wa mabasi yenye mfumo wa gesi nchini. Mpango huu sio tu sehemu ya kujitolea kuboresha huduma lakini pia ni njia ya kurudisha fadhila kwa jamii zetu zinazotuzunguka. Alisema Bwana Eliavera Timoth, Meneja Masoko Scania Tanzania.

KUHUSU SCANIA TANZANIA LIMITED
Kampuni ya Scania Tanzania inafanya kazi kama kampuni ndogo ya Scana CV AB yenye makao makuu yake nchini Sweden. Kampuni ya Scania Tanzania inajihusisha na uingizaji na usambazaji wa bidhaa za Scania nchini. Kampuni hii ina ofisi sehemu mbalimbali nchini ambapo makao makuu yake ni Dar es Salaam, huku ofisi nyingine ni Mwanza, Arusha na Mbeya.
Share:

Absa workplace gender equality initiative receives accolades

Minister of State in Prime Minister’s Office (Investment), Hon Angela Kairuki (left), is ushered in by Absa Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed at Hyatt Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam last Friday where she officiated at the Absa women empowerment forum together with the launch of ABT’s Red Skirts program, designed to inspire, empower and develop women leaders at Absa. The events were part of ABT women activities to celebrate the 2020 International Women Day. Looking on is Absa Tanzania Legal and Compliance Director, Irene Sengati Giattas.
Minister of State in Prime Minister’s Office (Investment), Hon Angela Kairuki (left), cuts a ribbon to symbolize the launch of Absa Bank Tanzania Red Skirts program, designed to inspire, empower and develop women leaders at ABT. The launch, part of Absa women’s activities to celebrate the 2020 International Women Day, was accompanied by the bank’s women empowerment forum in Dar es Salaam last Friday. From right are ABT Managing Director, Abdi Mohamed and the bank’s Legal and Compliance Director, Irene Sengati Giattas.
Minister of State in Prime Minister’s Office (Investment), Hon Angela Kairuki (centre), listens to Absa Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed at a function where the minister launched the ABT Red Skirts program, designed to inspire, empower and develop women leaders at the bank. The launch, which was part of Absa women’s activities to celebrate the 2020 International Women Day, was matched with the bank’s women empowerment forum in Dar es Salaam last Friday. Left is the bank’s Legal and Compliance Director, Irene Sengati Giattas.
One of Absa Bank Tanzania three winners of top 50 Women in Management Award, Sabiha Gulam receives award from Minister of State in Prime Minister’s Office (Investment), Hon. Angela Kairuki, at a function where the minister launched the ABT Red Skirts program, designed to inspire, empower and develop women leaders at the bank. The launch, which was part of Absa women’s activities to celebrate the 2020 International Women Day, was synchronized with the bank’s women empowerment forum in Dar es Salaam last Friday. Centre is ABT Managing Director, Abdi Mohamed and the bank’s Legal and Compliance Director, Irene Sengati Giattas.
A panelist during the Absa Bank Tanzania women empowerment forum, Brenda Msangi Kinemo (second left), who is CCBRT CEO, drives a point home at a function where ABT launched The Red Skirts program, designed to inspire, empower & develop women leaders at the bank. Looking on from left are; NLC Tanzania Chief Executive, Catherine Kimaryo, Lindam Group Managing Director, Zuhura Sinare Muro, CEO Roundtable Executive Director, Santina Benson and Grassroots Business Fund Africa Regional Director, Lilian Mramba.
Minister of State in Prime Minister’s Office (Investment), Hon Angela Kairuki (second left), takes a look at some handmade items by women at the function.  Left is Absa Bank Tanzania Legal and Compliance Director, Irene Sengati Giattas, and the banks MD, Abdi Mohamed.
A cross-section of attendees at the Absa Bank Tanzania women empowerment forum in Dar es Salaam last Friday.
ABT Red Skirts champions pose for a memento photo with the forum’s panelists, together with the bank’s top executives during a function at the Hyatt Kilimanjaro Hotel in Dar es Salaam last Friday.

By Our Reporter

The Minister for State Prime Minister’s Office (Investment), Hon Angela Kairuki, has commended initiative by Absa Bank Tanzania to address gender gap at workplace in the country, during a women Empowerment Forum organized by the bank in Dar es Salaam on International Women Day.

“I would like to use this opportunity to urge other banks and companies to borrow a leaf from this initiative so that we are able to address the gender gap, especially in the corporate world in our country, in Africa and the world at large, “said the minister.

The forum went hand in hand with launch of The Red Skirts, a programme designed to inspire, empower & develop women leaders at Absa Bank Tanzania,

The minister said: “It is important to note the fact that we need more women in boardrooms is not just mere advocacy rhetoric. It is so because despite commendable progress made during the past 25 years since the Beijing Conference, women are still lacking in top executive positions.”

Speaking at the event, Absa Bank Managing Director Abdi Mohamed took the opportunity to highlight the universality of the issue or gender equality. “The equality campaign is bringing together people of every gender, race, religion and country to drive actions that will create gender equality in the world.”

Elaborating on the status of women at Absa, he noted: “We have four Tanzanian women director in the bank. In 2006 that number was zero.

The MD further noted that of the bank’s total workforce of 485, female are 233 or 48 per cent, and that of the bank’s 15 branch managers, 8 are female.

“We meet every year to review our progress, we do not meet to celebrate perfection, but tp reflect on progress,” added Mr. Mohamed.
Share:

Absa Bank Tanzania sponsors celebrated local golfer

Absa Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed hands over a box contains some golf sports gears and travelling documents to Tanzania renowned golf player, Victor Mbunda (left), on his mission as Tanzania’s flag-bearer in the coming Kenya Open Golf Championship to be staged at Karen Country Club in Nairobi, Kenya on date to be disclosed soon. Mbunda participation is full sponsored by Absa Tanzania. Right is ABT Head of Marketing and Corporate Relations, Aron Luhanga and others from second left are veteran golfers, Martin Warioba and Marian Mugo. A brief occasion was held in Dar es Salaaam during the weekend.

By Staff Reporter

ABSA Bank Tanzania said it has fully sponsored local golf celebrity, Victor Mbunda,  on his mission as Tanzania’s flag-bearer in the coming Kenya Open Championship.

Speaking in Dar es Salaam yesterday, Absa Bank Tanzania Managing Director, Abdi Mohamed, said the bank was happy with Mbunda’s ambition, giving rise to the decision to support him.

“We always aim to bring possibilities into life and, knowing that Mbunda is the current number one golfer in Tanzania, it is our willingness to be part of his success story by facilitating him into this tournament,” said Mohamed.

He said the bank was always proud to be associated with sports so as to inspire Tanzanian youth, as Mbunda does, into showing they were capable to brush shoulders with world-class sportsmen.

Kenya Open is an annual golf tournament founded in 1967. It has been an event on Europe-based Challenge Tour schedule since 1991, before being affix onto the European Tour in 2019.

The tourney’s past champions include Seve Ballesteros, Ian Woosnam, Ken Brown, Christy O’Connor Jr and Trevor Immelman.

“Mbunda is a symbol of ambitions. We, Absa Bank Tanzania respect the ambitions of our customers as well as those of our nation at large. As a way of putting in action the noble aim of our ‘Africanacity’ maxim, we feel obliged to give Mbunda support, and we believe he won’t let us down,” said Mohamed.

Earlier, Absa Tanzania Head of Marketing and Corporate Relations Aron Luhanga, said Mbunda would be fully sponsored.

“We provide a return ticket to Nairobi, allowances as well as golf gears,” he said.

Luhanga urged Tanzanians to play down the misguided notion that golf was reserved for the affluent, saying it was like any other sports and was open to people from all walks of life, whether driven by the urge to keep fit or are out to make money.

Mbunda, flanked by veteran golfers Martin Warioba and Marian Mugo, thanked Absa Bank Tanzania for giving him a helping hand, and promised not to let them down.

“I am willing to be brand ambassador for Absa Bank Tanzania in the tourney as well as in other future golf   contests. You have showed the way,” he said.

The four-day regional classic is scheduled to take off at the Karen Country Club in Nairobi, Kenya on date to be disclosed soon.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (331) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (129) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages