Mwanamke ni kiungo katika uhifadhi wa mazingira

Catherine Kahuka (kushoto) na Gloria Wangeleja (kulia), wawakilishi kutoka taasisi ya PLPDF kupitia Shirika la Uhifadhi Mazingira Daniani (WWF), ofisi ya Tanzania wakipanda mtiti.

Na Asha Mwakyonde

SHIRIKA la Uhifadhi wa Mazingira  Duniani (WWF), ofisi ya Dar es Salaam Tanzania kwa kushirikiana na Taasisi ya Vodacom Tanzania imepanda miti mia moja na kuwatembelea akina mama waliojifungua katika Hospitali ya Taifa Muhimbili - Mloganzila  ikiwa ni kuelekea maadhimisho ya siku ya Wanawake Duniani ambayo hufanyika Machi 8, kila mwaka.

Upandaji miti huo ulienda sambamba na uchangiaji damu na utoaji zawadi kwa watoto waliozaliwa hospitalini hapo  ikiwa ni kujumuika pamoja na akina mama hao katika siku hiyo ya wanawake duniani.

Akizungumza jijini Dar es Salaam hospitalini hapo mara baada ya kufanya shughuli hizo Meneja Mawasiliano wa WWF, Joan Tanisa amesema kuwa shirika la uhifadhi mazingira kupanda  miti ni moja kati ya kazi zao za msingi.

Joan amesema mazingira yakiwa mazuri mama mwenye mzigo wa mkubwa wa kuilea familia yake  anaweza kupata nafuu na kwamba miti inapopandwa na kustawi vizuri  kutakuwa na upatikanaji wa maji ya kutosha  na mama huyo hatapata shida ya kutembea umbali mrefu kutafuta maji.

Amesema kuwa mwanamke ni kiungo katika suala la uhifadhi wa mazingira kwani shughuli nyingi anazozifanya zinahusiana na mazingira na kwamba ana nafasi ya kubwa ya kuelimisha familia yake juu ya uhifadhi huo.

"Kwa wanawake wenzetu wa vijijini wabaolima, wanaokwenda kutafuta kuni na ndio wanaohudumia familia hivyo ndio mwalimu wa kwanza wa kuweza kutoa elimu ya uhifadhi mazingira,"amesema Joan.

Ameongeza  kuwa wamepanda miti maeneo mbalimbali  hapa nchini hivyo wameona wafanye kitu gani ambacho kitangusa  mwanamke moja kwa moja katika yale ambayo anayafanya  kila siku.

Naye Meneja Ruzuku na Mawasiliano wa Taasisi ya Vodacom Sandra Oswadi amesema taasisi hiyo ni ya kujitolea kwa jamii  na kwamba wamejumuika na akina mama hao waliojifungua  kwa kupanda miti na kutoa zawadi kwa watoto.

"Siku hii tumekuja kupanda miti ambayo imetokana na mkakati wetu wa miaka mitatu wa kutunza mazingira. Kwa mwaka wa kwanza tumedhamiria kupanda miti 70,000 ambao unaishia mwishoni mwa mwezi huu,"amessema.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Uunguzi na Ukunga kutoka hospitali ya Nuhimbili - Mloganzila Redemptha Matindi  ametoa shukrani kwa WWF na taasisi ya Vodacom  kwa kupanda miti na kuungana na wanawake waliojifungua na kulazwa hospitalini hapo.
Share:

UMOJA WA WANAWAKE KITUNDA WAFANYA ZIARA KUTEMBELEA WENYE UHITAJI MAALUM

Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Taasisi ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), Anna Haule pamoja na Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda akikabidhi msaada wa taulo za wasichana kwa wasichana waliopo katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Baadhi ya Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakikabidhi msaada wa godoro, unga na sukari kwa Mmoja wa wakazi wa kata hiyo mwenye mazingira magumu kuelekea maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yatakayofanyika tarehe 8 machi. Umoja huo umefanya hafla ya kuwatembelea watu wenye uhitaji mbalimbali pamoja na kutembelea kituo cha watoto yatima cha Camp Caleb kilichopo mtaa wa Kipera kata ya Kitunda.  Matembezi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaan jana.

Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiongozana kwa pamoja wakiwa na misaada yao kueleka kwa watu wenye uhitaji katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani. Ni miongoni wa mwa mila na desturi za umoja huo kusaidia wenye uhitaji maalum. Matembezi hayo yamefanyika jijini Dar es Salaan jana.

Baadhi ya Wanawake wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakisalimiana na Mmoja wa wakazi wa Kitunda, Bibi Tausi Ramadhani baada ya kuwasili mahali alipohifadhiwa kwaajili ya kumkabidhi msaada katika kuadhimisha siku ya wanawake duniani.
Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakikabidhi msaada wao kwa Bibi Tausi Ramadhani katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yanafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.

Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakikabidhi msaada wao kwa Mwakilishi wa Bibi anayeishi katika mazingira Magumu Bibi Salum katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yanafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Mwanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda akizungumza jambo na watoto yatima pamoja na wanaishi katika mazingira magumu baada ya kuwasili katika kituo cha Kulea watoto hao cha Camp Caleb kilichopo katika mtaa wa Kipera kata ya Kitunda kwa ajili ya kutoa msaada katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Baadhi ya Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiimba nyimbo za kukataa unyanyasaji wa kijinsia baada ya kuwasili katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb kilichopo katika mtaa wa Kipera kata ya Kitunda kwa ajili ya kukabidhi msaada katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani.
Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka akigawa biskuti kwa watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda wakiwa katika picha ya pamoja na watoto wanaolelewa katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.
Afisa Maendeleo kata ya Kitunda, Sosina Soka (wa pili kushoto), Mkurugenzi wa Taasis ya Uwezeshaji Wajasiriamali ya Open Mind and Thoughts Organization (OMTO), pamoja na Wanachama wa Umoja wa Wanawake wa Kata ya Kitunda msaada wa chandarua kwa watoto waliopo katika kituo cha Kulea watoto yatima pamoja na wanaoishi katika mazingira magumu cha Camp Caleb katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani ambayo kwa kata ya Kitunda yatafanyika tarehe 7 machi katika viwanja vya shule ya msingi Kerezange.

HABARI KATIKA PICHA













Heri ya Maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani
Share:

BENKI YA NIC YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA CCBRT

Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank, Margret Karume (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi akiongea na waandishi wa habari kutoa shukrani zake kwa Benki ya NIC mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa NIC Benki, Bi Nasikiwa Berya akiongea kabla kukabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank, Margret Karume (kushoto) akisikiliza taarifa mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT (hayupo pichani).

Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Benki ya NIC imeadhimisha siku hiyo muhimu kwa wanawake kwa kutembelea na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula hospitali ya CCBRT.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake huazimishhwa kila mwaka kusherehekea mafanikio waliyopata wanawake katika nyanja mbali mbali kama vile kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kisiasa.

Maadhimisho haya pia yanasaidia kupaza sauti juu ya suala la usawa wa kijinsia. Yakiwa na kauli mbiu ‘Usawa kwa Wote’, kauli hiyo inahimiza kuwa usawa siyo jambo la wanawake bali ni jambo la kibiashara. Usawa wa kijinsia ni muhimu kwa uchumi na kwa maendeleo ya jamii. Usawa wa kijinsia siyo jambo la mjadala wa siku moja ambao utaisha katika siku ya wanawake duniani bali ni suala endelevu.

Ili kusaidia jamii ambayo inatuzunguka, tumeamua kutumia siku hii kuimarisha uhusiano wet na hospitali ya CCBR. Benki yetu leo imeamua kuja hapa na kutoa misaada mbali mbali itakayowasidia wanawake wanopata matibau ya fistula hospitalini hapa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Margaret Karume.

Akizunguma wakati wa kutoa misaada hiyo, mkurugenzi wa benki hiyo alisema benki yake ni moja kati ya taasisi zinazojali suala la usawa i kwenye mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ajira na kuongeza kuwa pia benki hiyo inathmini jamii inayozizunguka na huzisadia katika nyanja za elimu, afya na mazingira.

“Tunafurahi kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani pamoja wanawake hapa CCBRT. Kusaidia jamii inayotuzunguka na wanawake ni moja kati ya vipaumbele vya benki yetu.

Unapomsaidia mwanamke, humsaidii peke yake bali unasaidia jamii nzima nan chi kwa ujumla,” alisema Usawa wa kijinsia unahitaji uwezeshaji kwa wote ukilenga kutatua changamoto ya kutokuwa na maamuzi sawa na pia kumpa kila mtu nguvu na uhuru wa kuamua maisha yake.

Aliongeza kuwa watu wote wakiwa wamewezeshwa, familia zinanufaika na manufaa haya yanakwenda mpaka kwa vizazi vijavyo na familia kwa ujumla.

Benki ya NIC itaendelea kusaidia jamii katika namna mbali mbali ambazo zitamnufaisha mtu mmoja mmoja na jamii yote kwa ujumla wake,” alisema.
Share:

Coral Paints yatangaza mafanikio ikitimiza miaka 30

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati), akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo mbele ya waandishi wa habari na wageni wengine waalikwa. Katika hafla hiyo. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii Diamond Platnumza kuwa Balozi mpya wa Coral Paints.
Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz akiimba wimbo, maalum kuhamasisha matumizi ya rangi ya kampuni hiyo wakati Kampuni ya Insignia Ltd ikimtangaza kuwa balozi sambamba na maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (kushoto), na Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz (kushoto kwake), wakishangilia katika hafla ambayo kampuni hiyo ilitangaza kuadhimisha miaka 30 tokea kuanzishwa kwake nchini na pia kumtangaza Diamond kama balozi wao. Wengine ni wawakilishi kutoka Coral Paint na Wasafi Media. Hafla hiyo ilifayika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati), akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo mbele ya waandishi wa habari. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii Diamond Platnumz kuwa Balozi mpya wa Coral Paints.

Na Mwandishi Wetu,

KAMPUNI ya rangi ya Coral Paints imeadhimisha miaka 30 tangu ilipoasisiwa huku ikijivunia ushirika wake katika kukuza uchumi wa wananchi na taifa zima kwa kuwainua mamia ya wajasiliamali nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Kishan Dhebar, alisema wengi miongoni mwa wajasirimali hao kwa sasa ni mawakala wakubwa wa Coral Paints ndani na nje ya nchi.

“Wapo ambao tulianza nao miaka 30 iliyopita na tumekuwa tukitumia takriban Sh. 100 milioni kila mwaka kwa ajili ya kuwainua wajasiriamali wa Tanzania. Hadi sasa tuna takriban mawakala 1,500 ndani na nje ya nchi,” alisema Dhebar.

Dhebar alisema Coral Paints katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Moshi ambako ndiko kampuni hiyo ilikozaliwa mwaka 1990, ikiasisiwa na Watanzania kabla ya kupanuka na kuwa kinara katika soko la rangi, ikichagizwa na kauli mbiu ya ‘Kupamba na Kusherehekea’.

Akizungumzia mafanikio ya kampuni kwa miaka yake 30, mmoja wa wafanyakazi, Amani Mosha, alisema iikuwa ni miaka ya kujivunia kutokana na ubora wa bidhaa wanazozalisha na kuziingiza sokoni.

“Bidhaa zeu ni bora na zenye mng’ao unaodumu kwa muda mrefu na kukidhi matakwa ya wateja ikionyesha thamani halisi ya nyumba au garii,” alisema Mosha.

Awali Dhebar alimtambulisha msanii maarufu nchini, Diamond Platinum kuwa Balozi wa Chapa ya Coral Paints, akisema kwa kuwa wao huzalisha bidhaa bora, ndio maana wamemchagua mtu bora kushirikiana nao.

Diamond, kwa upande wake aliahidi kutoiangusha kampuni hiyo na kwamba atatumia kipaji chake kusambaza ‘simulizi ya kila ukuta’ kama ilivyo kauli mbiu mpya ya Coral Paints.

“Nitaanza kwanza kwa kuipamba Tandale. Nyumba ambazo hazijapakwa rangi tutaipaka rangi za Coral ili baadate tusherehekee,” alisema Diamond.
Share:

Benki ya Absa Tanzania yadhamini Kili Marathon 2020 kwa mafanikio

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (katikati), pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakishiriki mbio za Kilomita 21 za Kilimanjaro marathon pamoja na wakimbiaji wengine. Absa ilikuwa mmoja wa wadhamini ikigharamia kituo cha kutoa maji ya kunywa na viburudisho kwa wakimbiaji. Mashindano hayo yalifanyika mjini Moshi, Kilimanjaro leo.  
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (kushoto), akimpongeza mmoja wa wakimbiaji wao aliyeshiriki mbio za kilomita 42 wakati wa mashindano ya Kilimanjaro marathon 2020 pamoja na wakimbiaji wengine mjini Moshi, Kilimanjaro leo. Absa ilikuwa mmoja wa wadhamini ikigharamia kituo cha kutoa maji ya kunywa na viburudisho kwa wakimbiaji. Mashindano hayo yalifanyika Moshi, Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (kushoto), pamoja na wakimbiaji wengine wakionyesha medali zao walizopewa baada ya kushiriki mshindamo ya Kilimanjaro Marathon 2020 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro leo. Absa ilikuwa mmoja wa wadhamini ikigharamia kituo cha kutoa maji ya kunywa na viburudisho kwa wakimbiaji pamoja na kupeleka wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Baadhi ya wakimbiaji wa Benki ya Absa Tanzania pamoja na wakimbiaji wengine, wakitimua mbio wakati wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 mjini Moshi Kilimanjaro leo. Absa ilidhamini mashindano hayo kwa kutoa kituo cha maji na viburudisho kwa wakimbiaji pamoja na kupeleka wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Mkimbiaji akipewa maji ili kupoza kiu katika kituo cha maji kilichowekwa kwa ufadhili wa Benki ya Absa Tanzania wakati wa mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon mjini Moshi, Kilimanjaro leo.  
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghirwa (kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro. Anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Wakimbiaji wa Benki ya Absa Tanzania, wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Mjini Moshi, Kimanjaro juzi. Absa ilidhamini mashindano hayo kwa kutoa kituo cha maji na viburudisho kwa wakimbiaji pamoja na kupeleka wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Share:

Nabii Suguye atoa Njia za Kufanya Maombi yako Kujibiwa na Mungu


Na Mwandishi wetu,

Nabii Suguye wa Kanisa la Huduma ya Upatanisho (WRM) lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es salaam, jumapili ya leo amewafundisha maelfu ya waumini waliohudhuria Ibada ya leo kanisani hapo iliyokuwa maalumu kwaajili ya Unabii wa mtu mmoja mmoja na Maombi ya Mapatano juu ya Masharti ya kupelekea maombi yako kujibiwa na Mungu.

“Watu wa Mungu tumekuwa watu wa kuutafuta uso wa Mungu juu ya maitaji yetu lakini wengi wetu majibu yamekuwa hayapatikani na kuanza kujiuliza kama kweli Mungu yupo lakini siri ni kuwa wamefeli kufata kanuni za Mungu za Maombi”

“Ukitaka maombi yako yajibiwe yakupasa uwe na Imani ya Kiungu; Kuna Imani ya kibinadamu lakini pia kuna imani ya Kiungu.”

Alisema Nabii Suguye na kunukuu maandiko kutoka katika kitabu cha Warumi 4:17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.”

“Imani ya Mungu ni kuyaleta mambo yasiyokuwepo kana kwamba yamekwisha kuwepo. Kama unaona umaskini imani ya Mungu inaona Utajiri, kama unaona haiwezekani Imani ya Mungu inaona kuwezekana.”

Nakuongeza kwa kunukuu neno kutoka kwenye waraka wa Waebrania 11:3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.”

“Wengi wetu tunafeli kwakua tunashindwa kuifanyia mazoezi imani. Imani sio tu ya mdomoni kwa kusema namjua Mungu, imani inatakiwa itendewe kazi maandiko yanasema imani pasipo matendo imekufa ndani yake.”

Nabii Suguye aliendelea kusema “Ili maombi yako yajibiwe usiache KUOMBA. Neno linasema msijisumbue kwa lolote Bali kwa kusali na kuomba. Katika kuomba unatakiwa kutamka mambo ambayo unayataka bila kumwekea Mungu mipaka wala mashaka kwakua mashaka huzuia Maombi kufanikiwa.”

“Unapoomba usiombe kwa kumuwekea mipaka Bwana ya kukubariki na kukufanyia muujiza. Wengi tumekua hatujibiwi kwakua tunamwekea Bwana mipaka tunapokua tunaomba. Unapopokea majibu ya Daktari na Ukaanza kuomba usizitazame taarifa za daktari unapofanya maombi amini kuwa Mungu anauwezo wa kufanya zaidi ya wanachokiwaza wanadamu.” Alisema Nabii.

“Mashaka ni hatari katika maisha ya mwamini, Mungu anataka tuwe majasiri tuliojaa imani tunaojua wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea. Usikubali Mashaka ipoteze Baraka zako, simama na Mungu wakati wote mashaka isipate nafasi kwako.” Aliongeza Nabii Suguye.

Nabii Suguye aliendelea kusema kuwa “Unatakiwa kuamini kuwa Mungu yupo na humjibu kila amtafutaye, ndio Mungu huangalia imani yako hivyo unapoomba, kuwa na Imani ya kupokea.
Share:

Wafanyakazi wa DCB washiriki Kilimanjaro Marathon mjini Moshi



Wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB, wakishiriki mbio za Kilomita 21 pamoja na wakimbiaji wengine katika Mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Mjini Moshi, Kimanjaro leo.
Wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB, wakipasha viungo kabla ya kuanza mbio za Kilomita 21 za mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi, Kimanjaro, leo.
Baadhi ya wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB, wakitimua mbio wakati wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 mjini Moshi Kilimanjaro, leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (Katikati), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB wakishiriki mbio za kujifurahisha za kilomita 5 wakati wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi, Kimanjaro leo.
Wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB, wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Mjini Moshi, Kimanjaro leo.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (331) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (129) MICHEZO (41) SIASA (3)

Pages