Airtel Tanzania Yawapa Walimu Mafunzo ya Ujuzi wa Kidijitali Kupitia Mpango wa SmartWASOMI

Mkurugenzi wa Machapisho na Utafiti kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Bw. Kwangu Zabron Masalu (Katikati), akizungumza jijini Dar es Salaam jana, wakati wa warsha iliyoandaliwa kwa walimu wa IT, iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na UNICEF na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data. Kushoto ni Bw. Audax Tibuhinda kutoka Unicef na kulia Bw. Jackson Mmbando, Meneja Mahusiano wa Airtel Tanzania.

Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na UNICEF na Wizara ya Elimu, imeandaa warsha ya mafunzo kwa walimu wa IT chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, mradi wa kisasa wa ujifunzaji wa kidijitali unaolenga kuboresha upatikanaji wa elimu bora kupitia teknolojia.

Warsha hiyo imewakutanisha walimu 60 kutoka shule za msingi na sekondari ambazo tayari zimeunganishwa na mpango wa Airtel SmartWASOMI. Mpango huu ulizinduliwa mwezi Mei 2024 na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ikiwa ni ushirikiano kati ya Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, UNICEF na Serikali ya Tanzania. Zaidi ya shule 400 kote nchini zimeunganishwa na jukwaa hili, likiwa na huduma ya bure ya mtandao (zero-rated) kwa majukwaa ya mitaala ya Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) na Shule Direct, hivyo kuwapa maelfu ya wanafunzi na walimu fursa ya kupata rasilimali za ujifunzaji wa kidijitali bila gharama za data.

Akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni wa Airtel Tanzania, Bi. Beatrice Singano, alisisitiza umuhimu wa walimu katika mafanikio ya mpango huo.

Walimu ndio msingi wa mfumo wetu wa elimu, lengo la warsha hii ya mafunzo ni kuongeza uwezo wa walimu katika kufundisha kwa njia ya kidijitali na kuboresha matokeo ya elimu kwa wanafunzi wa shule za sekondari. Tunawekeza kikamilifu katika kuboresha elimu kupitia kuwaandaa walimu kutoa elimu bora inayojumuisha matumizi ya teknolojia,” alifafanua.

Bi. Singano aliongeza kuwa Airtel SmartWASOMI imeondoa kikwazo kikubwa cha ujifunzaji wa kidijitali kwa kutoa huduma ya kuingia kwenye maudhui ya elimu bila gharama ya data kupitia mtandao wa Airtel, hivyo kuwapa wanafunzi na walimu njia rahisi na ya uhakika ya kufikia vifaa vya kujifunzia vilivyokubaliwa na serikali.

Katika mafunzo ya leo, walimu walipata uzoefu wa moja kwa moja wa kutumia zana za ujifunzaji wa kidijitali kupitia jukwaa la Airtel SmartWASOMI, ikiwa ni pamoja na kufikia maudhui ya mitaala, rasilimali shirikishi, na mbinu za kuingiza zana hizi kwenye ufundishaji wa kila siku darasani. Hii itasaidia walimu kurahisisha upangaji wa masomo, kuboresha ufundishaji kwa kutumia maudhui ya kidijitali, kutoa kazi shirikishi, na kufuatilia maendeleo ya wanafunzi kwa ufanisi zaidi, hivyo kuongeza ushirikiano na ubora wa ufundishaji darasani,” alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi wa Machapisho na Utafiti kutoka Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Bw. Kwangu Zabron Masalu, akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa taasisi hiyo, Dk. Aneth Komba, alisema kuwa mafunzo hayo ni sehemu ya utekelezaji wa juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan, ambaye amesisitiza sana matumizi ya teknolojia ya mawasiliano. Matokeo yake, masomo ya teknolojia sasa yanafundishwa kuanzia elimu ya awali hadi ngazi ya chuo kikuu.

Lengo ni kuhakikisha kuwa fursa hii inaleta mapinduzi katika mfumo wa elimu wa Tanzania, tukizingatia kuwa elimu yetu kwa sasa inalenga zaidi kuzalisha wahitimu wenye ujuzi na umahiri katika kila ngazi,” alisema Bw. Masalu.

Walimu walioshiriki warsha hiyo waliupokea mpango huo kwa furaha kubwa, kwa wengi, ilikuwa mara yao ya kwanza kushiriki kwenye jukwaa kubwa la kidijitali linalolenga shule za sekondari nchini Tanzania.

Bi. Neema Avumba, mwalimu kutoka Shule ya Msingi TEGETA A, jijini Dar es Salaam alisema: “Ningependa kutoa shukrani zangu kwa Airtel Tanzania, UNICEF na serikali kwa kuandaa mafunzo haya leo, kabla ya warsha hii, wengi wetu hatukujua uwezo wa zana za kidijitali, sasa najihisi nimewezeshwa kuleta mbinu mpya darasani, tayari naona jinsi zitakavyowavutia na kuwashirikisha wanafunzi kwa njia ambayo hatukuweza hapo awali.

Kwa upande wake, Bw. Nassoro Shamsi, mwalimu kutoka Shule ya Msingi Mji Mwema, Kigamboni, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam, aliongeza kwa kusema: “SmartWASOMI imefungua fursa mpya. Sasa tunapata maudhui ya mtaala yaliyowezeshwa na nyenzo za kufundishia bila gharama za data kwa kutumia mtandao wa Airtel. Nimefurahi sana kuanza kutumia ipasavyo jukwaa hili baada ya mafunzo haya.

Mbali na mafunzo ya kiteknolojia, warsha hiyo pia iliwawezesha walimu kushirikiana, kuuliza maswali na kubadilishana uzoefu. Lengo si kuongeza ujuzi tu, bali pia kuunda mtandao wa mabalozi wa ujifunzaji wa kidijitali kote nchini.

Mpango wa Airtel Tanzania ni kufikia zaidi ya shule 1,000 ifikapo mwisho wa mwaka 2025, kwa kuendelea kuwekeza katika miundombinu ya kidijitali, ushirikiano madhubuti na jamii pamoja na msaada kutoka kwa wadau muhimu. Juhudi hizi zinaendana na ajenda ya kitaifa ya kukuza upatikanaji jumuishi wa elimu bora ya kidijitali na kuchangia malengo mapana ya kukabiliana na upungufu wa walimu wenye sifa, kuongeza uelewa wa kidijitali kwa wanafunzi, na kuhakikisha usawa katika upatikanaji wa rasilimali za elimu katika mikoa yote.
Ofisa Vifaa vya Intaneti wa Mradi wa SmartWASOMI, Bw. Harrison Isdory (kulia), akitoa mafunzo kuhusu matumizi ya baadhi ya vifaa hivyo katika wakati wa warsha iliyoandaliwa kwa walimu wa IT, iliyoandaliwa na Airtel Tanzania kupitia Airtel Africa Foundation, kwa kushirikiana na UNICEF na Wizara ya Elimu, chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI, unaolenga kuboresha elimu ya kidigitali kwa kuwawezesha walimu na wanafunzi kupata maudhui ya kielimu kupitia maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu Tanzania na Shule Direct bila gharama ya vifurushi vya data. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Airtel Money na TCDC Waingia Ubia Kuboresha Sekta ya Kilimo Kidijitali

      

Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba (wa pili kushoto), akisaini makubaliano (MoU) na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege, ili kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Waliosimama wakishuhudia kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Sheria wa Airtel Tanzania, Bw. David Lema(kushoto), na Mwanasheria wa TCDC, Bw. Harry Mbogoro. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.

Airtel Money Tanzania imesaini makubaliano ya kuingia katika ushirikiano wa kimkakati na Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC) kwa lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini.

Akizungumza wakati wa kutangaza ushirikiano huo, Mkurugenzi wa Airtel Money Tanzania, Bw. Andrew Rugamba alisema: “Kwa mujibu wa Shirika la Chakula na Kilimo (FAO), kilimo kinachangia takribani asilimia 30 ya Pato la Taifa na kuajiri zaidi ya asilimia 75 ya Watanzania. Hata hivyo, bado wakulima wengi wadogo hawajafikiwa na huduma rasmi za kifedha. Kupitia ushirikiano huu, Airtel Money itatoa suluhisho la malipo ya kidijitali kwa wakulima na vyama vya ushirika, kuwezesha ununuzi wa pembejeo, upatikanaji wa simu janja za bei nafuu, pamoja na kujenga historia ya matumizi ya kifedha. Pia tutatoa elimu ya fedha na huduma kwa wateja kupitia mtandao wetu mpana wa mawakala.

Ushirikiano huu unafikiwa kutokana na mafanikio ya majaribio yaliyofanyika na Airtel kwa kushirikiana na Vyama vya Ushirika vya Masoko ya Mazao (AMCOS), mkoani Morogoro, ambapo Airtel Money lengo lake ni kurahisisha malipo ya pembejeo kidijitali. Matokeo ya awali yalionesha mafanikio makubwa kwa kuongeza uwazi, ufanisi, na upatikanaji wa huduma kwa wakulima wadogo, huku yakipunguza changamoto za kifedha zilizokuwa kikwazo kwa maendeleo yao.

Bw. Rugamba aliongeza: “Kupitia ushirikiano huu, tunaweza kupanua huduma hizi na kuwafikia maelfu ya wakulima nchini kote. Tunajibu moja kwa moja wito wa Waziri wa Kilimo, Mhe. Hussein Bashe, alioutoa Desemba 2023, akiitaka sekta binafsi kushirikiana kwa karibu na wakulima wadogo ambao wengi wao hulima chini ya ekari 2.5, na wanahitaji msaada wa kubadilika kibiashara.

Kwa upande wake, Kamishna na Mtendaji Mkuu wa TCDC, Dkt. Benson Ndiege, alisema: “Makubaliano haya yanaashiria hatua muhimu katika kuimarisha maendeleo ya sekta ya ushirika na kilimo nchini. Kwa kushirikiana na Airtel Money, tunatoa fursa kwa wakulima wetu kustawi na kuendelea kuchangia kikamilifu katika uchumi wa taifa.

Ushirikiano huu pia utawezesha ushiriki wa Airtel Money katika majukwaa mbalimbali ya kitaifa ya kilimo kama vile Maonesho ya Nane Nane, Siku ya Kimataifa ya Ushirika (ICUD), na matukio mengine muhimu yanayoandaliwa na TCDC, hivyo kusaidia kupanua zaidi wigo wa ujumuishwaji wa kifedha vijijini.

Kwa kuweka malipo ya wakulima kwenye mfumo wa kidijitali, na kutoa elimu na nyenzo za kifedha, ushirikiano huu kati ya Airtel Money na TCDC unatarajiwa kubadilisha maisha ya wakulima wa vijijini, kuongeza tija ya kilimo, na kuchochea mabadiliko ya kweli katika mustakabali wa sekta ya kilimo nchini Tanzania.
Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba (wa pili kushoto), akibadilishana hati za makubaliano (MoU) na Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege, katika hafla ya utiaji saini makubaliano hayo yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Wengine ni Mkurugenzi wa Sheria wa Airtel Tanzania, Bw. David Lema (kushoto), na Mwanasheria wa TCDC, Bw. Harry Mbogoro. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege (kulia), akizungumza katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano kati ya tume hiyo na Kampuni ya Airtel Tanzania yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Kushoto ni Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.
Mrajis na Mtendaji Mkuu wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Dk. Benson Ndiege (aliyeketi kulia), Mkurugenzi wa Airtel Money, Bw. Andrew Rugamba (aliyeketi Katikati), wakipiga picha ya kumbukumbu katika hafla ya utiaji saini hati za makubaliano kati ya tume hiyo na Kampuni ya Airtel Tanzania yenye lengo la kuboresha sekta ya kilimo kupitia huduma za mawasiliano na huduma fedha kidijitali. Ushirikiano huu unalenga kuwawezesha wakulima kupata huduma salama na za haraka za malipo, kuongeza ujumuishwaji wa kifedha na kupanua upatikanaji wa pembejeo kwa gharama nafuu, hususan katika maeneo ya vijijini. Hafla hiyo ilifanyika mjini Dodoma jana.
Share:

Airtel UNICEF waunganisha shule 30 Mkoani Dodoma na intaneti ya BURE

Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Dodoma, Bi. Grace Samweli, (Kulia) akipokea moja ya vifaa vya intaneti kutoka kwa Meneja wa Kanda wa Biashara wa Airtel Tanzania, Salum Ngururu, wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa zaidi ya 30 kwa ajili ya shule za sekondari iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Msaada wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Airtel SmartWASOMI ili kurahisisha upatikanaji wa nyenzo za kufundishia na kusomea kidijitali bila gharama yoyote kwa shule zote za sekondari nchini.

Kampuni ya Airtel Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kupitia mradi wake wa kijamii wa Airtel SmartWASOMI, imekabidhi na kufunga vifaa vya intaneti ya kasi kwa shule 30 za sekondari mkoani Dodoma. Vifaa hivi vitawawezesha walimu na wanafunzi kupata huduma ya intaneti bure, ili kujisomea bure kupitia maktaba mtandaoni ya Taasisi ya Elimu Tanzania na majukwaa ya elimu.

Akizungumza katika hafla ya makabidhiano iliyofanyika katika Shule ya Sekondari Mtemi Mazengo, Mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki, Meneja wa Kanda ya Airtel Tanzania Dodoma, Bw. Salum Ngururu alisema, SmartWASOMI siyo tu mtandao, bali ni mfumo wa kidijitali unaoleta vifaa, maudhui ya kielimu yanayolingana na mtaala, na jukwaa la usomaji na ufundishaji wa kisasa

Mpango huu unaunga mkono jitihada za Serikali kupitia Wizara ya Mawasiliano katika kutumia teknolojia ya mawasiliano (TEHAMA) kwenye sekta ya elimu,” alisema meneja huyo.

Naye Bi. Grace Samwel akizungumza wa niaba ya Afisa Elimu wa Mkoa wa Dodoma,aliishukuru Airtel na kusema, “Shule zetu sasa zinaweza kusoma kidijitali kwenye maktaba mtandao ya Taasisi ya Elimu (TET) au kupata maudhui kutoka maktaba mtandao ya Shule Direct bila bila gharama ya bando, tunawashukuru Airtel kwa kuwezesha elimu ya kidijitali kufika hadi kwa wanafunzi wetu bila gharama yoyote.

Pia Airtel imeeleza kuwa mradi wa Airtel SmartWASOMI tayari umeshatekelezwa katika mikoa ya Zanzibar, Kilimanjaro, Arusha, Tabora, Mbeya na sasa Dodoma, ikiwa ni sehemu ya mpango mpana wa kuunganisha shule 3,000 nchini kwa kushirikiana na Serikali na UNICEF.

Kwa upande wake, Mwalimu Florian Kashasila alisema; “Vifaa vya intaneti ya kasi ya Airtel tulivyopatiwa leo vitasaidia sana walimu na wanafunzi kupata nyenzo za kufundishia na kujifunzia, ambazo awali hazikupatikana kirahisi shuleni.

Airtel Tanzania imesisitiza dhamira yake ya kuendelea kuwa sehemu ya mabadiliko ya elimu nchini kwa kuhakikisha shule haziachwi nyuma katika safari ya ujumuishaji wa kidijitali.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Dodoma, Bi. Grace Samweli, (kushoto) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Fufu Sekondari, Mohammed Hassan, vifaa vya intaneti vya Airtel Tanzania wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa zaidi ya 30 kwa ajili ya shule za sekondari iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Msaada wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Airtel SmartWASOMI ili kurahisisha upatikanaji wa nyenzo za kufundishia na kusomea kidijitali bila gharama yoyote kwa shule zote za sekondari nchini.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Dodoma, Bi. Grace Samweli, (kushoto) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Mwanakianga, Bi. Theresia Mdemu, vifaa vya intaneti vya Airtel Tanzania wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa zaidi ya 30 kwa ajili ya shule za sekondari iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Msaada wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Airtel SmartWASOMI ili kurahisisha upatikanaji wa nyenzo za kufundishia na kusomea kidijitali bila gharama yoyote kwa shule zote za sekondari nchini.
Afisa wa Kitengo cha Ufundi wa Airtel Tanzania, Bw. Harrison Isdory (aliyesimama), akitoa maelezo kwa wakuu wa shule za sekondari mkoani Dodoma kuhusu mradi wa Airtel SmartWASOMI na jinsi vifaa vya intaneti vya Airtel Tanzania vitakavyoboresha ufundishaji na usomaji kwa njia ya kidijitali katika shule za sekondari mkoani humo. Kushoto ni Meneja wa Kanda wa Biashara wa Dodoma wa Airtel Tanzania, Bw. Salum Ngururu, na upande wa kulia ni, Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari wa Mkoa wa Dodoma, Bi. Grace Samweli.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Dodoma, Bi. Grace Samweli, (kushoto) akimkabidhi Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Pandambili, Bw. Mengi Lekuchela, vifaa vya intaneti vya Airtel Tanzania wakati wa hafla ya makabidhiano ya vifaa zaidi ya 30 kwa ajili ya shule za sekondari iliyofanyika mkoani Dodoma mwishoni mwa wiki. Msaada wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Airtel SmartWASOMI ili kurahisisha upatikanaji wa nyenzo za kufundishia na kusomea kidijitali bila gharama yoyote kwa shule zote za sekondari nchini.
Mwakilishi wa Afisa Elimu Sekondari Mkoa wa Dodoma, Bi. Grace Samweli (Kulia), Meneja Biashara wa Kanda wa Airtel Tanzania, Salum Ngururu (kushoto) na Afisa wa Kitengo cha Ufundi wa Airtel Tanzania, Bw. Harrison Isdory (Katikati) wakiwa kwenye picha ya pamoja na wakuu wa shule za sekondari jijini Dodoma, mara baada ya makabidhiano ya vifaa vya Intaneti chini ya mpango wa Airtel SmartWASOMI. Msaada wa vifaa hivyo ni sehemu ya utekelezaji wa mradi wa Airtel SmartWASOMI ili kurahisisha upatikanaji wa nyenzo za kufundishia na kusomea kidijitali bila gharama yoyote kwa shule zote za sekondari nchini.
Share:

AKIBA COMMERCIAL BANK PLC YAANDAA JUKWAA LA WATEJA MKOANI MBEYA ZAIDI YA WATEJA 150 WASHIRIKI.

   Tanzania – 18 Juni 2025 – Akiba Commercial Bank Plc (ACB) iliandaa mkutano Maalum wa Wateja jijini Mbeya lililowakutanisha zaidi ya wateja 150 kutoka sekta mbalimbali, kwa lengo la kuimarisha mahusiano na kuwataarifu wateja kuhusu maendeleo ya Benki pamoja na fursa mbali mbali za kuwainua wateja kiuchumi.

Jukwaa hili lililenga kutoa taarifa kuhusu maendeleo ya hivi karibuni ya benki, hususan katika huduma za kidijitali na maboresho ya uzoefu wa wateja. Aidha, lilitumika kama jukwaa la kutoa elimu ya kifedha kwa wateja ili kuwasaidia kufanya maamuzi sahihi ya kifedha. Wateja walishiriki kikamilifu kwa kutoa maoni, mrejesho na mapendekezo kuhusu huduma za benki.


Benki ilitumia fursa hiyo kusikiliza, kujifunza na pia kutoa shukrani kwa wateja wake kwa uaminifu na ushirikiano wao wa muda mrefu. Akizungumza katika tukio hilo, Bi. Wezi Mwazani, Afisa Mkuu wa Biashara wa Benki ya Akiba, alitoa pongezi kwa mwitikio mkubwa na kusema: "Mwonekano wa ushiriki huu mkubwa unatupa faraja kuwa wateja wetu wanatuamini na wamechagua Akiba kama Benki yao pendwa. Hatuchukulii jambo hili kuwa la kawaida, na tunaendelea kujitolea kuwahudumia kwa ubora siku zote.


" Bw. Ntupa, Kiongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa Soko la Mbeya, alipongeza juhudi za Benki kwa kuandaa jukwaa lenye maana kubwa, hasa kwa kuweka kipaumbele kwenye elimu ya kifedha. "Majukwaa kama haya ni muhimu kwa maendeleo ya biashara, yanatoa maarifa kwa wateja wetu na kuimarisha uhusiano wa kuaminiana kati ya benki na jamii ya wafanyabiashara," alisema Bw. Mtupa. Akihitimisha tukio hilo,
Afisa Biashara Mkuu wa Akiba Commercial Bank Plc Bi. Wezi Mwazani akifungua mkutano wa wateja ulioandaliwa na benki hiyo mkoani mbeya.

Bw. Humphrey Nyandidi, Meneja wa Tawi la Mbeya, alishukuru wateja kwa ushirikiano wao na kuahidi kuendelea kuwahudumia kwa bidii na kujituma. "Tunathamini sana uaminifu wenu, na tunaahidi kuendelea kuwahudumia kwa ari na moyo wa dhati ili kutimiza matarajio yenu na hata kuvuka kiwango hicho," alisema. Jukwaa hili la wateja ni sehemu ya mkakati mpana wa Benki ya Akiba wa kuimarisha mahusiano na wateja wake kupitia majukwaa ya majadiliano na mirejesho kutoka kwa wateja. Benki inaendelea kujikita katika kutoa huduma shirikishi za kifedha pamoja na elimu ya fedha.

Share:

AKIBA COMMERCIAL PLC YASHIRIKIANA NA TIA KUPANDA MITI 1,500 KATIKA KAMPENI YA UTUNZAJI WA MAZINGIRA

Dar es Salaam, 13 Juni 2025: Akiba Commercial Plc imeonyesha dhamira yake endelevu ya kutunza mazingira kupitia zoezi la kupanda miti kwa ushirikiano na Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) katika kampasi ya Kurasini, Dar es Salaam. Miti 1,500 imepandwa kama sehemu ya mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) unaolenga kukuza utunzaji wa mazingira na kuimarisha ustawi wa jamii. Zoezi hilo liliongoza na Afisa Biashara Mkuu wa Benki hiyo Bi. Wezi Mwazani (Picha ya kwanza) kwa kushirikiana na wafanya kazi wengine pamoja na wanafunzi wa TIA.

Akizungumza kwa niaba ya benki katika tukio hilo, Bwana Emmanuel Mseti, Meneja Mwandamizi wa Kitengo cha Wateja Binafsi, alitoa shukrani za dhati kwa uongozi, wafanyakazi na wanafunzi wa TIA kwa mapokezi na ushirikiano mzuri uliowezesha mafanikio ya shughuli hiyo ya kimazingira. Alibainisha kuwa zoezi hili si ishara tu bali ni kitendo kinachoonyesha imani ya Benki kwamba kulinda mazingira ni jukumu la pamoja.
Shughuli hii ni mfano halisi wa imani yetu kuwa kulinda mazingira ni jukumu la kila mmoja wetu. Jukumu letu halikomi tu kwenye kupanda miti peke yake bali, tunaendelea kuhimiza huduma rafiki kwa mazingira kupitia huduma zetu za kidijitali kama ACB Mobile, Internet Banking na Akiba Wakala, ambazo si tu huongeza urahisi na ufanisi, bali pia hupunguza matumizi ya karatasi na kuunga mkono utunzaji wa mazingira,” alisema Bwana Mseti.
Benki pia ilibainisha juhudi zake nyingine za utunzaji wa mazingira ikiwemo jukumu endelevu la kutunza na kuboresha Viunga vya Independence Square jijini Dodoma. Katika tukio hilo, Bwana Mseti aliwahimiza wanafunzi wa TIA kuchukua jukumu la kulinda miti iliyopandwa na kuhakikisha inakua vizuri kwa faida ya vizazi vijavyo.

Pia aliwahakikishia kuwa Benki itaendelea kushirikiana na TIA katika kampeni za mazingira katika kampasi zake nyingine pindi itakapohitajika.

Kwa mtazamo wa Uwajibikaji kwa Jamii, Akiba Commercial inaamini kuwa kwao kurudisha kwa jamii si chaguo bali ni wajibu.

Kupitia sekta za afya, elimu, uwezeshaji wa kiuchumi, na utunzaji wa mazingira, Benki imejitolea katika maendeleo jumuishi na endelevu yanayonufaisha jamii inayoihudumia.

Ili kupata taarifa zaidi kuhusu ushiriki wetu katika maswala ya kijamii na huduma za kibenki kwa ujumla, tafadhali skani QR yetu hapa chini.
Share:

UWT TANGA YAKUNWA NA UCHAPAKAZI WA MBUNGE UMMY MWALIMU

Na - Mwandishi Wetu, TANGA

Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) imempongeza Mbunge wa Jimbo la Tanga Mjini, Ummy Mwalimu, kwa uchapakazi na uwajibikaji wake wa kuwaletea wananchi maendeleo na namna anavyoilea Jumuiya hiyo muhimu kwa uhai wa Chama.

Pongezi hizo zimetolewa na Mwenyekiti wa Jumuiya hiyo wilaya ya Tanga, Bi. Moza Seif, katika Baraza lake la Kikanuni lililokaa Juni 12, 2025 katika Ukumbi wa CCM wilaya ya Tanga ambapo pamoja na mambo mengine, Baraza hilo lilikuwa na ajenda ya kusoma Utekelezaji wa Ilani kwa Madiwani wa Viti Maalum wa Jiji la Tanga.

Bi. Moza amempongeza Mbunge Ummy Mwalimu ambaye amekuwa bega kwa bega na Jumuiya hiyo katika kusukuma gurudumu la maendeleo ndani ya Jiji la Tanga. Katika kuunga mkono juhudi za maendeleo zinazofanywa na Mbunge huyo, uongozi wa UWT Tanga ulimpatia Mbunge Ummy Mwalimu Zawadi mbalimbali za Pongezi ambazo zilipokelewa na Bi. Mwanahawa Mwalimu kwa niaba ya Mbunge.

Sambamba na hilo, Madiwani wa Viti Maalum wa Jiji la Tanga walisoma Utekelezaji wa Ilani ambapo kazi nyingi na miradi mingi ya maendeleo imefanyika katika kipindi cha uongozi wao. Aidha, wanachama wameaswa kuwa wamoja kuelekea Uchaguzi Mkuu Mwezi Oktoba, 2025 kwa kuepuka fitna, majungu na makundi.

Katika hatua nyingine, Baraza hilo lilihudhuriwa viongozi mbalimbali wa Chama wakiwemo Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Tanga, Meja Mstaafu Hamisi Bakari Mkoba ambaye alikuwa Mgeni Rasmi pamoja na Katibu wa CCM wilaya ya Tanga, Jamal Khimji.
Share:

Mkurugenzi wa Benki ya DCB, Sabasaba Moshingi aongoza wafanyakazi wa benki hiyo kujitolea damu wakiadhimisha Siku ya Wachangia damu Duniani

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Aga Khan, Bw. Sisawo Konteh (Kulia) akishikana mikono na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw.Sabasaba Moshingi, wakati yeye na baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo walipofika hospitalini hapo kujitolea damu kuadhimisha Siku ya Wachangiaji Damu Duniani, jijini Dar es Salaam Leo.

BENKI ya Biashara ya DCB imesema itaendelea kufanya jitihada tofauti katika kusaidia afya za watanzania wenye uhitaji wa kupata damu kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali imeelezwa jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza katika zoezi la kujitolea damu kama sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wachangia Damu Duniani, jijini Dar es Salaam leo, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema yeye pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake wameamua kujitolea damu kwani licha ya benki yao kujishughulisha na utoaji wa huduma za kifedha lakini pia wanabeba jukumu la kuhakikisha watu wanaohitaji damu salama mahospitalini wanazipata bila kuwa na haja ya kusubiria ndugu waje kujitolea.

Leo tupo hapa pamoja na washirika wenzetu hospitali ya Aga Khan kwa lengo la kuchangia damu, tutaendelea kushiriki matukio mengine kama haya na mengineyo yenye lengo la kusaidia kuokoa maisha ya watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu na mahitaji mengine ya kibidamu”, alisema Bw. Moshingi.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkuu wa Kitengo cha Maabara katika Hosptali ya Aga Khan, Dk. Caroline Ngimba alitoa hamasa kwa watanzania wote nchini kuwa na moyo na utamaduni wa kujitolea damu bila kusubiri siku rasmi za kitaifa ama kimataifa bali liwe ni jambo endelevu kwani uhitaji wa damu upo kila siku mahospitalini.

Uzuri ukichangia damu kama afya inaruhusu kila baada ya miezi mitatu unaweza kuchangia tena, tungeomba tabia hii iwe endelevu kwani hakuna kiwanda cha kutengeneza damu, damu inayopewa mwanadamu inatoka kwa mwanadamu”, alisema Dk. Caroline.

Naye mtaalamu wa utoaji damu kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Peter Chami alitoa shukurani kwa Benki ya DCB, huku akizitaka taasisi nyingine kuiga mfano wa benki hiyo ili kuokoa maisha ya watanzania wenye shida ya damu kwani mahitaji ya damu ni makubwa sana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw.Sabasaba Moshingi, akifanyiwa uchunguzi wa afya yake kabla hajajitolea damu katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam leo, alipongoza baadhi ya wafanyakazi wa benki hiyo kujitolea damu, kuadhimisha Siku ya Wachangiaji Damu Duniani. Picha nyingine zikionesha matukio mbalimbali katika hafla hiyo.
Mkurugenzi wa Mikopo wa Benki ya DCB, Bw. Deogratius Thadei, akijitolea damu katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Wachangiaji Damu Duniani, katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam leo, ambako yeye pamoja na baadhi ya wafanyakazi wenzake walishiriki. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Maabara, Dk. Caroline Ngimba na kulia ni Mtaalamu wa mishipa Kutoka Mpango wa Taifa wa Damu Salama, Bw. Peter Chami.
Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya DCB, waliojitolea damu pamoja na baadhi ya wafanyakazi wengine wa benki hiyo wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wachangia damu Duniani katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam, leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya DCB, wakishiriki zoezi la uchangiaji damu Ili kusaidia wenye uhitaji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wachangia damu Duniani, jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya DCB, wakijitolea damu kusaidia wenye uhitaji ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Wachangia damu Duniani, jijini Dar es Salaam leo.
Share:

Benki ya Absa Tanzania Yathibitisha Uwazi na Dhamira ya Ukuaji Katika Mkutano na Gavana wa BoT

Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (katikati), akizungumza na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kutoka kushoto), wakati wa ziara yao katika ofisi ya gavana jijini Dar es Salaam jana. Ujumbe huo ulifanya mazungumzo ya kina na gavana, ukimpa taarifa kuhusu masuala muhimu yakiwemo utendaji wa kifedha wa benki hiyo, sera za faragha na ulinzi wa taarifa, mipango ya ukuaji na upanuzi, maendeleo ya udhibiti, na maeneo mengine muhimu ya kipaumbele kama Utawala wa Mazingira, Jamii na Uongozi (ESG) pamoja na huduma za kijamii, ikionesha dhamira thabiti ya taasisi hiyo ya kifedha kwa uwazi, ulinganifu wa udhibiti na ukuaji endelevu. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria na Udhibiti wa Benki ya Absa, Bw. Alistides Kashasira na Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Bw. Oscar Mwamfwagasi. Kulia ni baadhi ya maafisa kutoka Benki Kuu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kutoka kushoto), akizungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), wakimtembelea gavana ofisi kwake, jijini Dar es Salaam jana. Ujumbe huo ulifanya mazungumzo ya kina na gavana, ukimjulisha kuhusu masuala muhimu yakiwemo utendaji wa kifedha wa benki hiyo, sera za faragha na ulinzi wa taarifa, mipango ya ukuaji na upanuzi, maendeleo ya udhibiti, na maeneo mengine muhimu ya kipaumbele kama Utawala wa Mazingira, Jamii na Uongozi (ESG) pamoja na huduma za kijamii, yakionesha dhamira ya benki hiyo katika uwazi, kuzingatia kanuni na ukuaji endelevu. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Kitengo cha Sheria na Udhibiti wa Absa, Bw. Alistides Kashasira na Afisa Mkuu wa Uendeshaji, Bw. Oscar Mwamfwagasi.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (kulia), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), pamoja na ujumbe wake, mara baada ya kikao kilichofanyika katika ofisi ya gavana jijini Dar es Salaam jana. Ujumbe huo ulifanya mazungumzo ya kina na gavana, ukimpa taarifa juu ya masuala muhimu yakiwemo utendaji wa kifedha wa benki, sera za faragha na ulinzi wa taarifa, mipango ya ukuaji na upanuzi, maendeleo ya udhibiti, pamoja na maeneo mengine muhimu kama Utawala wa Mazingira, Jamii na Uongozi (ESG) na huduma za kijamii, yakionesha dhamira thabiti ya benki hiyo kwa uwazi, ulinganifu wa udhibiti na maendeleo endelevu.
Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bw. Emmanuel Tutuba (wa nne kutoka kushoto), na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kutoka kushoto), wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya maafisa waandamizi kutoka Benki ya Absa na Benki Kuu jijini Dar es Salaam jana, wakati wa ziara ya ujumbe wa Absa katika ofisi ya gavana. Kupitia mazungumzo ya wazi na ushirikiano na benki kuu, Benki ya Absa inaendelea kulinganisha malengo yake na vipaumbele vya kitaifa na kuchangia kikamilifu katika mustakabali wa kifedha wa nchi.
Share:

Akiba Commercial Bank Yakutana na Wateja wa Mwanza: Zaidi yaWateja 250 Wahudhuria Mkutano wa Mahusiano

Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Bw. Silvest Arumasi (katikati), akizungumza na wateja wa Benki hiyo mkoa wa Mwanza wakati wa hafla ya kukuza na kuimarisha mahusiano na wateja hao pamoja na kupokea mrejesho kwa ajili ya kufanya maboresho ya bidhaa pamoja na viwango vya huduma. wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa Biashara Mkuu wa ACB, Bi. Wezi Mwazani pamoja na mwakilishi wa wafanya Biashara wa soko kuu la Mwanza.
Meneja wa Akiba Commercial Bank Tawi la Mwanza Bw.Emmanuel Makula akitambulisha timu yake ya ushindi ya Tawi hilo Wakati wa hafla ya kukuza na kuimarisha mahusiano na wateja wa benki hiyo mkoa wa mwanza.

Benki ya Akiba imeendelea kuonyesha dhamira yake ya kuwa karibu na wateja kwa kuandaa mkutano maalum na wateja wa Mwanza uliofanyika tarehe 22 Mei 2025 katika ukumbi wa Gold Crest Hotel.

Tukio hili lilivutia zaidi ya wateja 250, ikiwa ni ishara ya hamasa kubwa na utayari wa jamii ya Kanda ya Ziwa kunufaika na huduma Benki hiyo.

Katika mkutano huo wa ana kwa ana, wateja walipata nafasi ya kuzungumza moja kwa moja na viongozi waandamizi wa benki, kutoa maoni yao kuhusu huduma, kueleza changamoto wanazokutana nazo katika shughuli za kifedha, pamoja na kujifunza kuhusu huduma na bidhaa mpya za benki.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Akiba, Bw. Silvest Arumasi, alipata nafasi ya kuzungumza na wateja na kueleza kuwa mkutano huu ni sehemu ya mikakati ya Benki katika kuimarisha mawasiliano na wateja wake. Alisema:

Benki ya Akiba inaamini katika kusikiliza wateja wake. Lengo letu ni kuelewa vizuri zaidi mahitaji yao halisi ili tuweze kutoa huduma zinazogusa maisha yao kwa namna chanya, hasa katika mazingira yao ya kila siku.

Bw. Arumasi aliongeza kuwa benki inaendelea kuweka mkazo katika kutoa msaada kwa wafanyabiashara wadogo na wa kati kwa kuwapa jukwaa la kuzungumza moja kwa moja na wataalamu wa kifedha na kupata ushauri wa kibiashara wenye manufaa ya moja kwa moja.

Afisa Mkuu wa Biashara, Bi. Wezi Mwanzani, alieleza kuwa mwitikio mkubwa wa wateja wa Mwanza ni ushahidi wa Imani ya Wakazi wa Mwanza kwa Benki ya Akiba pamoja na uhitaji mahitaji mkubwa wa huduma za kifedha. Alisema

Tunashukuru kwa mwitikio mzuri kutoka kwa wateja wa Mwanza. Kama benki, tutaendelea kutoa huduma bunifu na zinazolenga kumsaidia mteja katika uhalisia wa biashara zake. Mwanza ni sehemu muhimu ya mpango wetu wa kuhakikisha huduma zetu zinawafikia watu wote.

Bi. Wezi alisisitiza kuwa dhamira ya benki ni kuijenga jamii jumuishi kifedha, kwa kuhakikisha watu wote wanapata nafasi sawa ya kutumia huduma za kifedha kama njia ya kujikwamua kiuchumi.

Mbali na majadiliano, tukio hili pia liliambatana na utoaji wa elimu ya kifedha. Wateja walielimishwa kuhusu usimamizi wa fedha binafsi na za biashara, matumizi salama ya huduma za kidijitali kama benki mtandao na miamala kwa njia ya simu, pamoja na mbinu bora za kukuza biashara kwa njia endelevu.
Share:

Startups reimagining farming through digital mechanization.

In the heart of the country, where smallholder farmers have long relied on traditional tools like hoes and ox-plows, a new generation of agricultural startups is sowing the seeds of transformation.


Young entrepreneurs are reimagining farming by introducing affordable mechanization solutions that are bridging the productivity gap and driving food security.


One such trailblazer is Greenbiz Limited, a startup based in Kisongo, Arusha. This is a platform that captures what farmers are already doing, how much they save weekly, how they repay loans, and their farming activities and turns that into a digital credit profile.


Co-founder Daniel Elibariki says that the idea was born from a simple but powerful realization: rural farmers, especially women, were doing everything right; saving weekly, working hard, and forming cooperative groups, yet remained locked out of formal finance because they lacked collateral. 
“We saw these groups, known as Village Community Bank (VICOBA), as a foundation we could build on.
 By digitizing their financial records and aggregating their data, we realized we could build a trust bridge between these farmers and banks. That’s how the journey started out of a desire to make finance fairer and more inclusive for the people who need it most,” he says.


The startup addresses the financing gap for smallholder farmers, particularly the lack of access to credit due to traditional collateral requirements.


Agriculture contributes over 25 percent to Tanzania’s GDP, yet most smallholder farmers still rely on informal lending or personal savings. Without finance, there's no mechanization, no inputs, and no scaling. Given the growing threats from climate change and food insecurity, closing this gap has never been more urgent.


The company uses the profiles to secure collateral-free loans from partner banks and integrates agricultural advisory and sensor technology to help farmers make data-driven decisions and the result is that a farmer wakes up not just hoping for rain, but knowing when to plant, how much to borrow, and where to improve.

 
“We are focused on micro-mechanization, tools and technologies that fit the scale and budget of smallholder farmers. Things like soil sensors, drip irrigation kits, and precision planting tools. These might seem small, but for a farmer using only hand tools, they’re game-changers. We're filling the gap between traditional labor and full-scale mechanization, which is often unaffordable or unsuitable for small farms,” Elibariki says.
Elibariki says that one of the biggest hurdles in their operations has been digital and financial literacy.


“Farmers need to understand not just how to use our platform or devices, but why they matter. That’s why training is central to our model. We host in-person sessions and partner with local leaders and youth to serve as digital champions in each village. Building trust has also been key, most rural communities have been burned by “solutions” that disappeared after a pilot,” he adds.


Grenbiz Limited is among the beneficiaries of KilimoTech Accelerator. The brainchild of Youth Entrepreneurship for the Future of Food and Agriculture (YEFFA), the strategic initiative is supported by Alliance for a Green Revolution in Africa (AGRA) and implemented by Sahara Accelerator and aims to accelerate digital innovations in agricultural mechanization for Tanzania's smallholder farmers.

Emmanuel Senzighe, Kilimotech Accelerator Project Manager, says that The project focuses on enhancing productivity and sustainability in the sunflower, maize, horticulture, and rice value chains by supporting Agritech startups (Agripreneurs) and fostering partnerships among key stakeholders.


The program focuses on scaling Agritech startups (Agripreneurs) by providing tailored support, technical and business diagnostics, and technical mentorship. By connecting young women and men SMEs to mechanization, irrigation, and financial service providers, Kilimotech Accelerator fosters a vibrant ecosystem of innovators, startups, and key stakeholders.


This comprehensive approach aims to enhance the productivity of Tanzania’s agriculture sector by leveraging digital platforms to address key barriers such as high equipment costs, limited system integration, and restricted access to financing.


It further enables the most underserved farmers, particularly youth and smallholders, to leapfrog into modern mechanization by making essential technologies more accessible, affordable, and readily available.

   
“GreenBiz is one of nine innovative solutions currently being accelerated with tailored support to refine their offerings and develop proof-of-concept models that can enable scalable impact. The Accelerator is committed to driving sustainable growth and market readiness for these startups through mentorship, targeted workshops, ecosystem engagement, and strategic collaboration, ultimately aiming to expand youth employment and enhance access to mechanization services,” he adds.
      
As for Elibariki, KilimoTech has been instrumental in the growth of their startup and they see a brighter future on the horizon.


“The mentorship helped us refine our product-market fit, the network connected us with potential partners, and the exposure has opened doors to potential investors and partners we wouldn’t have accessed on our own. It’s been a catalyst for our next phase of growth,” he says. 
He notes that they expect a twofold impact from their operations: increased productivity through timely decision-making and smart investments, and a shift in labor dynamics where technology eases the burden on women and youth.

 
“With access to finance and mechanization tools, farmers can cultivate more land, reduce post-harvest losses, and generate higher incomes. Over time, we hope to see less outmigration of rural youth and more pride in farming as a tech-driven profession,” he says.


According to Elibariki, despite their expectations, their journey has not been devoid of surprises or memorable moments.


“One Maasai woman in our pilot group told us that for the first time in her life, she feels like a "bankable" person. That word “bankable” really stuck with us.


 It’s not just about money. It’s about dignity, confidence, and a sense of being seen and valued by the formal system,” he says.


Still, challenges remain. Agritech is tough because you’re dealing with two notoriously hard sectors, agriculture and finance.

 Getting banks to trust community data and getting farmers to trust tech requires patience and consistency, says Elibariki.


“We’ve faced setbacks in infrastructure, resistance to change, and even skepticism from funders. But the impact we’ve seen makes it all worthwhile,” he adds.


Mechanization has traditionally been the missing link in Africa’s agricultural development. 
According to the UN Food and Agriculture Organization, over 60 percent of sub-Saharan farmers still rely on hand tools. But startups are now stepping into this gap with technology tailored to local realities.


Creating an enabling environment for agri-tech startups means investing not just in individual ventures but in the ecosystem itself. 


Governments, donors, and private sector actors have a role to play in supporting research, building infrastructure (like rural connectivity), and shaping policies that promote innovation.


As the digital revolution sweeps through agriculture, the startups that will succeed are those with both the tools to build and the vision to lead. 


By equipping innovators with the right mix of business savvy and technical depth, we can unlock the full potential of technology to power a more resilient and productive future for farming.
And hopefully, somewhere out there, investors are taking note.
Share:

WATU 12,000 WAHOFIWA KUUGUA UGONJWA WA HIMOFILIA NCHINI

Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (katikati), akika utepe kuashiria uzinduzi wa kliniki ya himofilia, sambamba na maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani katika hafla iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar, jana. Pamoja naye ni wawakilishi kutoka Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Taasisi ya himofilia ya novo nordisk, Wizara za afya kutoka Tanzania na Zanzibar, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Chama cha Himofilia Duniani na wadau wengine.

Na mwandishi wetu, Zanzibar.

TAKWIMU zinaonyesha kati ya watu elfu sita hadi elfu 12, wanahofiwa kuugua ugonjwa wa himofilia nchini huku idadi ya watu waliogundulika kuwa na ugonjwa huo hadi sasa wakiwa ni 451 pekee.

Hayo yalisemwa na Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani iliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani humo jana.

Hafla hiyo iliandaliwa na Chama cha Himofilia Tanzania (HST), kwa uwezeshaji kutoka Taasisi ya himofilia ya novo nordisk na Chama cha Himofilia Duniani kwa ushirikiano kutoka Serikali ya Tanzania na ya Zanzibar, wizara za afya kutoka pande zote mbili, Hospitali ya Taifa Muhimbili na wadau wengine.

Mheshimiwa waziri alisema takwimu za kidunia zinaonesha mtu mmoja kati ya 10 anapatikana na ugonjwa huo, hii ikimanisha kuwa Tanzania yenye watu takribani milioni 61 inaweza kuwa na wagonjwa elfu 6 hadi elfu 12, huku ikielezwa 97% ya watu wenye ugonjwa huu duniani kote hawajagundulika, ambapo kwa upande wa Tanzania waliogundulika mpaka sasa ni 451 tu.

Kama tunavyofahamu himofilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda unaosababishwa na ukosefu wa kiwango cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu hivyo kusababisha damu kuvuja kwa mda mrefu pindi mtu anavyopata jeraha hivyo kuhatarisha maisha yake."

Maisha ya watu wenye matatizo haya yanahitaji uangalizi mkubwa na tahadhari kubwa ili kuzuia uvujaji wa damu, ulemavu na vifo hivyo kuwepo na hitaji la kubaini aina ya himofilia na kupata matibabu ya kuchomwa sindano yenye chembechembe za protini zinazokosekana mwilini ili kusaidia kuzalisha damu”, alisema Waziri Mazrui.

Alisema Mwaka 2020 Hospitali ya Taifa ya Muhimbili ikishirikiana na Taasisi ya himofilia ya Novo Nordisk ilianzisha mradi wa kuongeza kasi ya upatikanaji wa huduma kwa watu wenye magonjwa ya damu lengo kuu ikiwa ni kuunga mkono serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya afya katika kupunguza madhara ya vifo vinavyotokana na magonjwa yasiyo ambukiza ikiwemo himofilia na selimundu.

Pamoja na hayo alisema, lengo kubwa la mradi huu ni kuwezesha upatikanaji wa vipimo vya wagonjwa wa damu, seli mundu, na himofilia katika hospitali za rufaa nchini sambamba na kuanzisha kliniki za magonjwa hayo, kuwezesha mafunzo na upatikanaji wataalamu wa afya waliobobea kwenye hospitali hizo pamoja na upatikanaji wa miundo mbinu sahihi, vipimo na dawa ili wagonjwa wahudumiwe mahali popote nchini bila kulazimika kufika Muhimbili.

Katika maadhimisho haya leo nina furaha kubwa kuwaambia kuwa mradi huu katika kipindi cha uhai wake kuanzia kipindi cha kwanza hadi kipindi cha pili tayari umefanikisha kukamilisha ukarabati wa kliniki za himofilia katika hospitali 13 zikiwemo hospitali za Muhimbili, KCMC, mbeya na Bugando."

Tunawashukuru pia wafadhili wetu kwa msaada wa dawa zenye thamani ya shs milioni 500, kwa kweli mmetusaidia sana na vifaa nyenye gharama kubwa, chini ya uongozi wa maraisi wetu, Samia Suluhu Hassan na Hussein Ali Mwinyi, tunaendelea kufanya kazi usiku na mchana kuhakikisha kila mtanzania anapata matibabu kwa usahihi na kwa wakati, hivyo juhudi zenu hizi zinatufanya twende sambamba na juhudi za viongozi wetu hawa”, aliongeza waziri huyo.

Akizungumzia zaidi kuhusu himofilia, Mwenyekiti wa Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Stella Rwezaura alisema, asilimia 70 ya wagonjwa wa himofilia wanarithi na inabebwa katika kinasaba cha kike, kwani mwanamke ana ‘x’ mbili na mwanaume ana ‘xy’, hivyo endapo mwanamke ana ‘x’ yenye vinasaba vya himofilia, asilimia 50 ya watoto wake wa kiume watakuwa na tatizo hilo hivyo kufanya asilimia 99 ya wagonjwa wa himofilia kuwa wanaume.

Tunaposherehea Siku ya Himofilia Duniani, sambamba na Kauli Mbiu ya Mwaka 2025 isemayo, ‘Wanawake na Wasichana pia wanakumbwa na tatizo la kuvuja damu, licha ya himofilia kuwapata zaidi wanaume, tuwaite wanawake waje kupima, waweze kutambulika mapema hivyo kupata matibabu sahihi."

Lengo la mradi huu ni kuwatambua wagonjwa wengi zaidi na kupata huduma kwani wapo wengi wenye tatizo hili na hii ilitokana na changamoto ya uhaba wa vifaa, mashine na vitendanishi vya kutambua ugonjwa huu, hivyo kwa msaada wa wafadhili, vyama vya wagonjwa pamoja na serikali yetu sikivu ya Tanzania, ikiongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan pamoja Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, wizara yake ya afya na wadau wengine, huduma hizi sasa zinafika karibu kwa wananchi kwa usahihi zaidi”, aliongeza Dk. Stella.

Naye mmoja wa wagonjwa wa Himofilia ambaye pia anauguza watoto wawili wenye ugonjwa huo, Regina Shirima alisema anakabiliwa na changamoto kubwa ya hali duni ya kiuchumi baada ya kutumia muda wake mwingi katika kuhudumia watoto hivyo kutokuwa na muda kabisa wa kujishughulisha na kazi za kujitafutia kipato.

changamoto nyingine ni kwa watoto wenyewe hawapati muda wa kusoma, kucheza na wenzao ama kuwa na furaha kwani muda mwingi wanakuwa wagonjwa, lakini ni ukweli kuwa wanawake ndio wanabeba vinasaba vya himofilia, lawama nyingi zinakuja kwetu kwa kuzaa watoto wenye changamoto hii, hivyo unajikuta familia imekuacha”. Akiongeza kuwa kuna wakati kulikuwa na changamoo ya upatikanaji wa dawa ukizingatia kuwa mgonjwa wa himofilia akikosa dawa tu anaweza uhai wake unakuwa hatarini.

Natoa wito kwa jamii kuwa gonjwa hili la himofilia lipo na mama sio anayesababisha mtoto kuzaliwa na ugonjwa huu, kwani huwezi kupata mtoto bila ya baba”, aliongeza Bi. Regina kwa mshangao.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Lawrence Museru alisema HST imekuwa sauti ya wenye ugonjwa wa himofilia katika kuangalia changamoto wanazopitia katika kutafuta tiba, moja ya changaoto ni utambuzi wa ugonjwa huu katika jamii.

Wagojwa wamekuja kutambulika baada ya kupoteza maisha ama kupata ulemavu wa kudumu kwasababu ugonjwa huo haukutambulika hivyo tunaokoa sauti yao kuona jamii na watoa huduma za afya wanatambua ugonjwa huo na wagonjwa wanapata tiba sahihi."

Tiba sahihi ni ghali sana na serikali haiwezi peke yake, hivyo lazima uwepo ushirikiano kutoka kwa sisi chama ambacho kina wataalamu na wadau wengine ili kuusemea ugonjwa huu, na tunaimani uwepo wako mheshimiwa waziri unafanya ugonjwa huu usemeke katika vyombo vya maaumuzi”, alisema Prof. Museru.

Akimkaribisha Mheshimiwa Waziri, Mkurugenzi wa Tiba na Elimu ya Afya Zanzibar, Dk. Marijani Msafiri alisema katika kipindi cha miaka minne, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar chini ya uongozi wa Dr. Hussein Ali Mwinyi imefanya mapinduzi makubwa katika kuboresha huduma za afya, ikiwa ni pamoja na ujenzi wa hospitali 10 za wilaya na hospitali moja kubwa ya kisasa ya mkoa ya Lumumba.

Ndani ya hospitali hizi sasa tumeimarisha miundombinu na huduma, serikali yetu ya awamu na nane pia imeamua kufanya kazi na sekta binafsi ili kutoa huduma bora kwa wagonjwa wote ikiwa ni pamoja na wagonjwa wa himofilia, zikiwemo huduma za maabara, utoaji wa dawa na uendeshaji wa hospitali”, alisema Dk. Msafiri.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (katikati), akiagana na Mwenyekiti wa Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Stella Rwezaura, mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani iliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar jana. Mstari wa chini ni baadhi ya watoto wanaougua ugonjwa wa himofilia.
Mwenyekiti wa Bodi ya Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Prof. Lawrence Museru (katikati), akiongoza maandamano kuadhimisha Siku ya Himofilia Duniani, Visiwani Zanzibar jana. Maadhimisho hayo yalifanyika pamoja na uzinduzi wa kliniki ya Himofilia katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, visiwani humo.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), akipokea cheti cha shukurani, kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Dk. Stella Rwezaura, mara baada ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani, pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika hafla iliyofanyika kwenye Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar, jana.
Mkazi wa Zanzibar, Baba mwenye watoto wawili wanaougua himofilia, Suleiman Ali Seif, akishiriki matembezi akiwa na watoto wake wenye ugonjwa huo, Murshin Ali (kulia), na Sahir Ali, wakati wa maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani, mjini Zanzibar jana. Maadhimisho hayo yaliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, yaliandaliwa na Chama cha Himofilia Tanzania (HST), kwa uwezeshaji kutoka Taasisi ya himofilia ya novo nordisk na Chama cha Himofilia Duniani. Himofilia ni ugonjwa wa damu kukosa uwezo wa kuganda unaosababishwa na ukosefu wa kiwango cha chembechembe za protini zinazotakiwa kugandisha damu hivyo kusababisha damu kuvuja kwa mda mrefu pindi mtu anavyopata jeraha hivyo kuhatarisha maisha yake.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (kushoto), akisalimiana na Mwenykiti wa Bodi ya Chama cha Himofilia Tanzania, Prof. Lawrence Museru, wakati akipokea maandamano, yaliyokuwa sehemu ya shamrashamra za maadhinisho ya Siku ya Homifilia Duniani, sambamba na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, mjini Zanzibar, jana.
Mmoja wa wadau wa himofilia, akipokea cheti cha shukurani, mara baada ya kukamilika kwa hafla ya maadhimisho Siku ya Homifilia Duniani, sambamba na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, mjini Zanzibar, jana.
Waziri wa Afya wa Zanzibar, Mhe. Nassor Ahmed Mazrui (katikati), akiwa na wawakilishi kutoka Chama cha Himofilia Tanzania (HST), Taasisi ya himofilia ya novo nordisk, Wizara za afya kutoka Tanzania na Zanzibar, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Chama cha Himofilia Duniani na wadau wengine katika hafla ya maadhimisho ya Siku ya Himofilia Duniani iliyofanyika pamoja na uzinduzi wa Kliniki ya Himofilia, katika Hospitali ya Wilaya ya Ijitimai, Visiwani Zanzibar jana.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (271) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (118) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages