Benki ya Absa Tanzania Yakamilisha Kampeni ya Kusisimua ya "Spend & Win" kwa Droo ya Mwisho na Hafla ya Kukabidhi Gari

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), akihutubia hadhira wakati wa droo ya tatu ya Kampeni ya "Spend and Win" na hafla ya kukabidhi Subaru Forester kwa mshindi wa pili, Bi. Alyshah Bharwani (wa tatu kushoto), katika hafla jijini Dar es Salaam leo. Wa pili kushoto ni Meneja wa Masoko wa Absa, Beda Buswalo. Mteja wa benki hiyo, Bi. Amalia Lui Shio, alitangazwa mshindi wa tatu.
Mshindi wa pili wa Kampeni ya "Spend and Win" ya Benki ya Absa Tanzania, Bi. Alyshah Bharwani (wa tatu kushoto), akionesha funguo za Subaru Forester mara baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Lilian Swere (kushoto), katika hafla jijini Dar es Salaam leo. Tukio hilo pia lilihusisha droo ya tatu ya kampeni, ambapo mteja wa benki hiyo, Bi. Amalia Lui Shio, alitangazwa mshindi. Kulia ni Bw. Jamil Kanji, mmoja wa wanafamilia wa Alyshah.

Benki ya Absa Tanzania imehitimisha rasmi Kampeni yake ya "Spend & Win" kwa mafanikio makubwa, kupitia droo ya tatu na ya mwisho iliyofanyika leo, ambayo imeashiria mwisho wa miezi mitatu ya msisimko, ubunifu, na zawadi kwa wateja.

Hafla hiyo ilipambwa na kutangazwa kwa mshindi wa tatu na wa mwisho, Bi. Amalia Lui Shio, ambaye atapokea zawadi yake—Subaru Forester ya mwaka 2014, Januari 2025.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Ndabu Swere, Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Wateja Binafsi katika Benki ya Absa Tanzania, alimtangaza mshindi na kuwapongeza washindi wote watatu waliotangazwa katika kampeni hiyo.

'“Tunayo furaha kumtangaza Bi. Amalia Lui Shio kama mshindi wa droo ya tatu na ya mwisho ya Kampeni ya ‘Spend & Win,” alisema Bi. Swere. “Stori yako ni muhimu, na kupitia kampeni hii, tumepata fursa ya kuwawezesha wateja wetu kubadilisha maisha yao. Bi. Amalia Lui Shio atapokea rasmi gari lake mwezi ujao, na tunasubiri kwa shauku kusherehekea tukio hili la kusisimua pamoja naye.

Wakati wa hafla hiyo, Bi. Ndabu pia alikabidhi funguo za Subaru Forester ya mwaka 2014 kwa mshindi wa pili, Bi. Alyshah Aminmohamed Bharwani, ambaye alitoa shukrani za dhati kwa Benki ya Absa kwa zawadi hiyo ya kubadilisha maisha.

Ninawashukuru sana Benki ya Absa kwa kampeni hii. Kushinda gari hili ni jambo kubwa sana kwangu na familia yangu, na nimefurahi sana kuwa sehemu ya safari hii,” alisema Bi. Bharwani.

Kampeni ya "Spend & Win" ambayo ilizinduliwa tarehe 10 Septemba 2024, iliwapa wateja wa Benki ya Absa Tanzania fursa ya kushinda moja kati ya magari matatu ya Subaru Forester kwa kufanya miamala kwa kutumia kadi zao za Absa au majukwaa ya kidijitali. Wateja walikidhi vigezo vya kuingia kwenye droo kwa kufanya angalau miamala 20 ya kadi yenye jumla ya TZS milioni 5 au zaidi kwa mwezi, huku miamala ya kidijitali ikiongeza nafasi zao za kushinda.

Akiongelea mafanikio ya kampeni hiyo, Bi. Ndabu aliwashukuru wateja wote waliopata nafasi ya kushiriki na kusisitiza dhamira ya benki hiyo ya kutoa suluhisho za kibunifu na uzoefu mzuri kwa wateja wake.

Kwa niaba ya Benki ya Absa Tanzania, napenda kuwashukuru wateja wetu wote walioshiriki kampeni hii na kuwapongeza washindi wetu watatu: Bw. Rashid Nassoro Said, Bi. Alyshah Aminmohamed Bharwani, na Bi. Amalia Lui Shio,” alisema Bi. Ndabu. “Katika Absa, tumejizatiti kuwawezesha wateja wetu na jamii, na kampeni kama hii ni mojawapo ya njia tunazotumia kuonyesha shukrani zetu huku tukitimiza dhamira yetu ya ‘Kuiwezesha Kesho Afrika ya kesho, Pamoja, Hatua moja baada ya nyingine."

Tunapohitimisha kampeni hii, nataka kuwahakikishia wateja wetu kuwa huu sio mwisho. Absa itaendelea kuanzisha kampeni na fursa za kusisimua za kuwazawadia na kuwaunga mkono wateja wetu wanapofanikisha malengo yao.

Hitimisho la Kampeni ya "Spend & Win" linaimarisha nafasi ya Benki ya Absa Tanzania kama benki ya kidijitali inayoongoza na mshirika wa kuaminika katika safari za kifedha za wateja wake.
Share:

Benki ya Absa Tanzania Yashinda Tuzo 11 za Heshima Mwaka 2024

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akizungumza na waandishi wakati akitangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia Tuzo mbalimbali 11 ilizopata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.

• Kutambuliwa kwake kunadhihirisha, Ufanisi katika Ubunifu wa Kifedha, Uongozi na kujali Wateja.

Benki ya Absa Tanzania inajivunia kutangaza mafanikio yake makubwa ya kushinda tuzo 11 za heshima mwaka 2024. Tuzo hizi zinatambua mchango mkubwa wa benki katika uwezeshaji wa kifedha, uvumbuzi, utawala bora, na huduma kwa wateja.

Tuzo muhimu ambazo benki imeshinda mwaka huu ni pamoja na:

• Chapa ya Benki Inayokua Haraka Zaidi 2024, iliyotolewa na World Brand Magazine.

• Benki ya Wateja rejareja na Wateja Wadogo na wa Kati inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 zilizotolewa na World Economic Magazine Awards.

• Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha Tanzania, iliyotolewa na Tanzania Women Industrial Awards.

• MD/CEO Bora wa Mwaka, iliyotolewa na Top 100 Executive List Awards.

• Hatifungani Bora ya Mwaka, iliyotolewa na Soko la Hisa la Dar es Salaam.

• Muwasilishaji Bora wa Ripoti ya Taarifa za Fedha 2023, iliyotolewa na Bodi ya Taifa ya Wahasibu na Wakaguzi wa Hesabu (NBAA)

• Mwajiri Bora anayeinukia na Mwajiri Bora katika Usimamizi na Maendeleo ya Vipaji, zilizotolewa na Chama cha Waajiri Tanzania (ATE).

• Benki inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu za Mikopo Tanzania, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

• Benki inayopendwa zaidi na kufikika zaidi Kusini mwa Afrika, iliyotolewa na Consumer Choice Awards Afrika 2024.

Utendaji bora wa Benki ya Absa Tanzania mwaka 2024 umeoneshwa kupitia matokeo yake mazuri ya kifedha kwa nusu ya kwanza ya mwaka. Mapato ya jumla yaliongezeka kwa 25% kufikia TZS bilioni 105, huku faida kabla ya kodi ikipanda kwa 65% kufikia TZS bilioni 54. Amana za wateja ziliongezeka kwa 21%, zikionesha uimara wa benki hiyo na uwezo wake wa kutoa ukuaji endelevu.

Tuzo ya Chapa ya Benki Inayokua haraka zaidi inaadhimisha maendeleo makubwa ya Benki ya Absa Tanzania tangu ilipoanzishwa mwaka 2020. Ndani ya miaka minne tu, Absa imepata kiwango sawa cha imani na kutambuliwa kama benki za ndani na kimataifa zenye karibu karne moja ya historia nchini Tanzania. Tuzo hii inaonyesha ahadi ya chapa ya Absa: 'Stori yako ina Thamani', inadhihirisha kujitolea kwa benki hiyo katika kuthamini Stori za kipekee za wateja wake, kuunda suluhisho za kibunifu, na kuiwezesha jamii.

Tuzo ya Benki inayofanya vizuri zaidi katika kuwawezesha wanawake kupata huduma za kifedha inaonyesha dhamira ya Absa katika kukuza ujumuishi wa kifedha. Kupitia bidhaa kama Akaunti ya Absa She Business, benki hiyo imewawezesha wanawake wajasiriamali kupata huduma za kibenki bila gharama, msaada wa ushauri, na programu za kujenga uwezo.

Katika sekta ya SME, suluhisho maalum za Absa na ushirikiano wa kimkakati zimesaidia benki kushinda tuzo ya Benki inayotoa huduma Kwa wateja wadogo na wa Kati (SME) inayokua haraka zaidi Tanzania 2024.

Tuzo ya Benki ya Wateja Rejareja inayokua haraka zaidi Tanzania 2024 inaonyesha msisitizo wa benki hiyo katika mabadiliko ya kidijitali na urahisi wa wateja, ikiwa ni pamoja na upanuzi wa huduma za uwakala na suluhisho za kibunifu kama jukwaa la malipo la Mobi Tap.

Kutambuliwa kwa Mkurugenzi Mtendaji kama MD/CEO wa Mwaka na tuzo ya Ripoti Bora za Kifedha 2023 kunathibitisha kujitolea kwa Absa kwa utawala bora, uwazi, na uongozi wa mfano wa kuigwa.

Tuzo kutoka Consumer Choice Awards, kama Benki Inayotoa Huduma Rafiki na Utulivu wa Mikopo Tanzania, zinaonyesha dhamira ya Absa ya kuwapa wateja nafasi ya kwanza katika shughuli zake.

Akizungumza wakati wa mkutano na waandishi wa habari, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, alisema: "Tuzo hizi ni ushahidi wa nguvu ya ushirikiano wetu na wateja na wadau wetu. Tunaheshimika kutambuliwa katika nyanja nyingi, na tutaendelea kujitolea kuimarisha Afrika ya Kesho kupitia suluhisho za kibenki zenye ubunifu, ujumuishi, na athari chanya.

Benki ya Absa Tanzania inapoendelea na safari yake ya ukuaji na mabadiliko, inabaki imara katika dhamira yake ya kutoa huduma bora na kuwawezesha jamii. Tuzo hizi ni kielelezo cha kujitolea kwa benki hiyo kwa uvumbuzi, uwazi, na kuridhisha wateja wake.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (kushoto), akionesha Moja ya tuzo waliyoshinda wakati akizungumza na waandishi wa habari kutangaza mafanikio ya benki kwa Mwaka 2024 kupitia tuzo mbalimbali 11 walizipata. Pamoja naye ni Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa benki hiyo, Bw. Aron Luhanga.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), pamoja na baadhi ya maofisa wa ngazi za juu wa benki hiyo, wakionesha kwa waandishi wa habari, tuzo mbalimbali 11 ambazo benki hiyo imeshinda kwa mwaka 2024, alipokutana nao, jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Benki ya Absa Tanzania yang'ara tuzo za Chaguo la Walaji

       

Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania kwa Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Sengati Giattas, wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji Mhe. Stanslaus Nyongo (wa tatu kushoto) akikabidhi tuzo ya Benki Bora inayopendwa Zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa pili kushoto) akionesha tuzo ya Benki Bora inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika wakati wa hafla ya kila mwaka ya utoaji wa Tuzo za Chaguo la Walaji, iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser na Mkurugenzi wa Sheria na Udhibiti wa Sera na Kanuni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Sengati Giattas (katikati), wakionesha tuzo za Benki Bora kwa kutoa Huduma Bora rafiki za Mikopo nchini Tanzania na Benki Bora inayopendwa zaidi na inayofikika zaidi Kusini mwa Afrika, mara baada ya kukabidhiwa, wakati wa hafla ya kila mwaka ya Tuzo za Chaguo la Walaji, jijini Dar es Salaam jana. Wengine ni wakuu wa vitengo mbalimbali wa benki hiyo.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages