Mkurugenzi mshauri wa USAID afanya ziara kukagua miradi ya USAID Afya Yangu na Kizazi Hodari Kanda ya Kusini

MSHAURI Mkuu wa kiufundi wa watoto yatima na walioko katika mazingira magumu kutoka USAID Sarah Dastur akiwa kwenye picha na baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi ya JJ Mungai iliyopo Manispaa ya Iringa baada ya kuwatembelea walengwa wanaonufaika na miradi ya USAID Afya yangu na Kizazi Hodari, Kanda ya Kusini mwishoni mwa wiki.

Iringa Jumatatu Agosti 5 2024, MSHAURI Mkuu wa kiufundi wa watoto yatima na walioko katika mazingira magumu kutoka USAID Sarah Dastur amefanya ziara ya siku moja ndani ya Mkoa wa Iringa kwa lengo la kuwatembelea walengwa wanaonufaika na miradi ya USAID Afya yangu na Kizazi Hodari, Kanda ya Kusini. Miradi hiyo miwili inatekelezwa na Deloitte Consulting Limited kupitia shirika la Msaada Kutoka Kwa Watu Wa Marekani.

Miradi hiyo inalenga kushughulikia utoaji wa huduma ya afya kwa wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI, kifua kikuu, uzazi wa mpango pamoja na mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia Nchini Tanzania.

Sarah Dastur alitembelea shule ya Msingi ya JJ Mungai kuona miradi inavyowasaidia wanafunzi hao hasa katika mapambano ya ukatili wa kijinsia dhidi yao, aliwatembea walengwa wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI eneo Isakalilo, pia alitembelea hospital ya Tosamaganga moja ya hospital zinazotoa huduma ya dawa kwa ya kufubaza virusi vya UKIMWI (ARV).

Moja ya wanaufaika wa mradi wa USAID Afya yangu ambaye ameomba kutotajwa jina lake wala kuchukuliwa picha ameshukuru mradi huo kuwa Mkombozi na Msaada Mkubwa kwa watanzania wengi hasa wale wenye uwezo wa chini kwa kuwarudushia tabasamu.

Aidha alitoa ombi kwa niaba ya wenzake uongezwe usiri kwa vituo/ club ambazo wanakutana vijana wanaoishi na maambukizi ya UKIMWI kwa lengo la kubadilishana mawazo kwani vingi vipo katikati ya muingiliano wa watu jambo ambalo linaondoa ufalagha wao akieleza linachochea hali ya unyanyapaa kwa watu wenye Elimu hasi.
Dkt Stella Mtera ambaye ni Msimamizi wa kitengo cha CTC hospitali ya Tosamaganga iliyopo manispaa ya Iringa akimsikiliza MSHAURI Mkuu wa kiufundi wa watoto yatima na walioko katika mazingira magumu kutoka USAID Sarah Dastur wakati alipotembelea walengwa wanaonufaika na miradi ya USAID Afya yangu na Kizazi Hodari, Kanda ya Kusini mwishoni mwa wiki.
Share:

Benki ya DCB yaunga mkono jitihada za serikali ujenzi wa Reli ya SGR

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, akihutubia mkoani humo jana, katika hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa huo kabla hawajaondoka Kwa treni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na Benki ya Biashara ya DCB kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na utalii kupitia Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.

Katika kuunga mkono juhudi zilizofanywa na serikali inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan za ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR pamoja na kukuza utalii kupitia Royal Tour, Benki ya Biashara ya DCB imedhamini safari ya walimu zaidi ya 1000 kutumia treni ya SGR kutoka Dar es Salaam hadi Morogoro na kisha Mikumi ili kukuza utalii wa ndani na kujifunza mambo yatakayowasaidia wanafunzi wao wawapo madarasani.

Akizungumza katika hafla ya kuwaaga walimu hao kutoka Jiji la Dar es Salaam, katika Stesheni ya SGR, jijini humo jana, Mkurugenzi Mtendaji wa DCB, Bw. Sabasaba Moshingi alisema taasisi yao imeshirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo kuwapa nafasi walimu hao kutembelea mbuga za wanyama ya Mikumi ili kujionea vivutio vya utalii vitakavyowasaidia kuwafundisha wanafunzi wa mashuleni.

Alisema DCB inamilikiwa na Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam ambalo ndiko wanakotoka walimu hao hivyo akawashauri kutumia huduma zilizoboreshwa za benki hiyo kama vile kuweka amana, bima mbalimbali na mikopo yenye masharti nafuu ili kuboresha maisha yao na kuacha kuangukia katika taasisi zinazotoa mikopo inayowaumiza na yenye masharti magumu.

Naye Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, Bw. Ramadhan Mganga alisema DCB ndio mkombozi halisi wa watanzania kwani wanazo huduma na bidhaa tofauti zinazokidhi mahitaji ya kibenki ya watanzania hivyo kutoa hamasa kwa walimu hao na kwa watanzania kwa ujumla kuchangamkia huduma hizo.

Aidha alisema ili kufanikisha safari hiyo wamedhamini mabasi 30 yatakayowasafirisha walimu hao kutoka Morogoro kwenda Mikumi ikiwa pia ni kutambua mchango wa walimu hao katika maendeleo ya benki yao.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Bw. Albert Chalamila aliipongeza DCB Kwa kufanikisha safari hiyo ya walimu akisema ofisi yake itaendelea kuandaa safari kwa makundi mengine ikiwa ni sehemu ya mkakati wa muda mrefu wa kuitangaza treni ya SGR.

Ziara hii sio tu itaongeza maarifa kwa walimu kupitia ziara ya Mikumi, bali pia itaongeza chachu ya kampeni inayoendelea ya Royal Tour,”alisema.

Benki ya Biashara ya DCB ilianzishwa mwaka 2002 ikitokana na wito wa Rais wa awamu ya tatu, Hayati, William Benjamin Mkapa, kufuatia kilio cha mitaji cha wananchi wenye kipato cha chini na cha kati wa Jiji la Dar es Salaam kukosa mikopo katika benki nyingi za kibiashara kwa kutokidhi vigezo vilivyokuwa vikiweka na benki hizo.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, Bw. Ramadhan Mganga akizungumza kuhusu udhamini wa benki hiyo Kwa ziara ya walimu 1000 wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa ziara yao kwenda Mikumi kwa kutumia treni ya SGR kutokea mkoani humo jana. Benki ya imedhamini mabasi 30 Ili kusafirisha walimu hao kutoka Morogoro kuelekea Mikumi Ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na utalii kupitia Royal Tour.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila (katikati), akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshi mkoani humo jana, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa huo kabla hawajaondoka katika stesheni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na DCB kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB, Bw. Sabasaba Moshingi (kulia), akisalimiana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam, Dk. Toba Nguvila, mkoani humo jana, wakati wa hafla ya kuwaaga walimu zaidi ya 1000 wa Mkoa wa Dar es Salaam, kabla hawajaondoka kwa treni ya SGR kuelekea Morogoro na baadae Mikumi katika ziara yao ilidhaminiwa na Benki ya Biashara ya DCB ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour. Kutoka Morogoro, DCB ilitoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi Mikumi.
Baadhi ya walimu kutoka jijini Dar es Salaam wakiwasili kwa treni ya SGR mjini Morogoro jana, wakiwa safarini kuelekea katika mbuga za wanyama ya Mikumi. Benki ya Biashara ya DCB ili kusaidia mkakati wa kuitangaza SGR na Royal Tour imedhamini safari hiyo Kwa kutoa mabasi 30 kusafirisha walimu hao hadi mbugani huko kutoka Morogoro.
Share:

TCB YAINGIA MKATABA WA MAKUBALIANO NA ZEEA KUWEZESHA MIKOPO VIKUNDI MAALUM

Benki  ya Biashara Tanzania (TCB)  imesaini mkataba wa makubaliano (MOU) na Wakala wa serikali wa uwezeshaji wananchi kiuchumi zanzibar ( ZEEA) Makubaliano haya ya kimkakati yanalenga kuanzisha mpango maalum wa mikopo utakaonufaisha makundi maalum wakiwemo wanawake na vijana wanaojihusisha na shughuli za kiuchumi visiwani Zanzibar. Mpango huu unakusudia kuchochea ukuaji wa biashara, ongezeko la ajira, na maendeleo ya kiuchumi katika ukanda huu wa Afrika Mashariki.

Akishuhudia kusainiwa kwa hati hizo jijini Dar es salaam Katibu mkuu ofisi ya Raisi kazi uchumi na Uwekezaji zanzibar Mariam amesema tayari shilingi bilioni 2 zimeshakusanywa na halmashauri visiwani humo ili kuanza uwezeshaji akiitaka benki ya TCB kuhakikisha inafanya tathmini ya mikopo wanayotoa kwa makundi hayo ili ziweze kurejeshwa kwa wakati na wengine waweze kukopa .


Ameeleza kuwa mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali,kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao. Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha uchumi wa ndani, kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupambana na ukosefu wa ajira na kuleta maendeleo na kuwa Kupata fursa ya mikopo ni muhimu kwa maendeleo na ukuaji wa biashara ndogondogo na za kati

Kwa upande wake Afisa mtendaji mkuu wa TCB ADAM MIHAYO amesema Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla na kwamba Mkataba huu wa makubaliano unathibitisha dhamira ya Benki ya TCB kuwezesha uchumi jumuishi na maendeleo ya kiuchumi kwa ujumla.

Amesema  mkataba huo utawezesha  kutoa mikopo nafuu kwa makundikiasi cha shilingi milioni 30 kwa kikundi, huku wakipewa muda miezi 24 sawa na miaka miwili Kwa kutoa mikopo nafuu kwa makundi hayo, TCB na ZEEA watawasaidia wajasiriamali kupanua biashara zao, kutengeneza fursa mpya za ajira, na hivyo kupunguza uhaba wa ajira.

Mpango huu pia utazisaidia biashara kujiendesha, kukabiliana na mfumuko wa bei, pamoja na kuwekeza katika vitendea kazi, na kuzipa ustahimilivu,Tuna furaha kushirikiana na ZEEA kuwainua wajasiriamali wanawake, vijana na makundi mengine maalum yaliyomo visiwani Zanzibar,” alisema Adam Mihayo,Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya TCB. 

Kwa upande wake mkurugenzi Mtendaji wa ZEEA Juma Burhan Mohamed amesema wanalenga kuipatia benki ya TCb kiasi cha shilingi bilioni 1.8 ili waanze utoaji wa mikopo hiyo  na kwamba Mpango huu unaendana na lengo  la kuwezesha maendeleo ya kiuchumi kwa kujenga uchumi jumuishi Kwa
kuyawezesha makundi maalum, wanaziinua biashara binafsi, pamoja na kuimarisha mfumo mzima wa uchumi na kutengeneza mazingira imara ya
kiuchumi.” alisema
Mbali na kuchangia maendeleo ya kiuchumi, makubaliano haya pia yanakusudia kuimarisha uchumi wa buluu visiwani Zanzibar. Kupitia mikopo hii itakayoinua biashara ndani katika sekta hii, TCB na ZEEA wanapigia chapuo eneo hili nyeti la shughuli za kiuchumi lenye uwezo wa kuchangia maendeleo kwa kiasi kikubwa.

Mchango wa Benki ya TCB katika kuunga mkono jitihada za Serikali katik na kupokea maombi ya mkopo yanayofikia wastani wa Mpango huu wa mikopo umekusudiwa kutia chachu juhudi za kijasiriamali, kuwapa wajasiriamali uthubutu wa kuanzisha na kupanua biashara zao Malengo ya uwezeshaji huu ni kuwa chanzo cha mabadiliko mengine kama kuimarisha biashara na uchumi.

Share:

UINGEREZA KUENDELEA KUFADHILI MIRADI YA UKIMWI NCHINI

Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wenye umri mdogo wa Kampeni ya kupanda mlima kilimanjaro ya GGM Kili Challenge, Regina Enos Baraka (kulia), mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda na kushuka mlima huo, mjini Moshi, Kilimanjaro, hivi karibuni. Kampeni hiyo ya kila mwaka ina lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki. Regina anaishi katika Kituo cha Moyo wa Huruma cha Geita kilichoanzishwa kwa msaada kutoka Mfuko wa Kili Challenge.

Balozi wa Uingereza nchini, Mhe. David Concar amesema nchi yake itaendelea kuunga mkono juhudi zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika kupambana na ugonjwa wa Ukimwi Ili kutimiza malengo ya Kimataifa ya muda wa kati na mrefu ili kuona hakuna maambukizi mapya, unyanyapaa na vifo vinavyohusiana na VVU .

Balozi Concar aliyasema hayo wakati wa mapokezi ya wapanda mlima Kilimanjaro 71 walikuwa wakishiriki Kampeni ya kila mwaka ya GGM Kili Challenge mjini Moshi, Kilimanjaro, inayoandaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kupambana na Ukimwi (TACAIDS)

Njia kuu ambayo Uingereza inafanya ni kuwa mmoja wachangiaji wakubwa wa Mfuko wa Kimataifa wa kupambana na UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria, kwa miaka mitatu kutoka 2024 hadi 2026, Uingereza itatoa pauni bilioni 1 kwa mfuko huo, ambao kwa jumla utatoa dola milioni 602 kwa Tanzania."

Nitoe pongezi kwa AngloGold Ashanti na Bodi ya Wadhamini ya Geita Gold Mining Limited Kilimanjaro Challenge dhidi ya HIV/AIDS pamoja na TACAIDS kwa kuifanya Kili Challenge kuwa tukio la kila mwaka la kupendeza likileta ujumbe wa nguvu kwa wanaoishi na VVU”, alisema.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mwakilishi ukutoka Geita Gold Mining, Mhandisi Nzuamkende alisema kampeni hiyo inayofanyika Kwa mwaka wa 22, inalenga kukusanya fedha kuchangia jitihada za Serikali ya Tanzania kufikia malengo ya sifuri tatu (Maambukizi mapya Sifuri, Unyanyapaa Sifuri na vifo vinavyohusiana na UKIMWI Sifuri).

Tunapokusanyika hapa ili kusherehekea mafanikio yenu, ninatoa shukrani zangu za dhati kwa kila mmoja wenu kwa kukabiliana na hofu zenu, na kushinda mojawapo ya milima mirefu zaidi na yenye changamoto duniani."

Juhudi zenu, kwenye miteremko ya Mlima Kilimanjaro na kwenye njia tambarare za baiskeli, hazijadhihirisha tu nguvu ya uamuzi na umoja lakini pia zimeleta athari kubwa katika dhamira yetu ya pamoja ya kupambana na VVU na UKIMWI, mmetuonyesha kwamba hakuna changamoto isiyoweza kuzuilika tunapokutana kwa sababu moja na kwa hilo, nawapongeza nyote”, alisema.

Aidha aliwashukuru wafadhili na washiriki wote kutokana na michango yao inayoendelea kufanikisha Kampeni hiyo hadi kuufanya Mfuko wa Kili Challenge Against HIV/AIDS Trust kuwa mfuko wa kimataifa, unaohusisha wapanda mlima na waendesha baiskeli kutoka mabara yote na zaidi ya nchi 20.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TACAIDS, Dk. Jerome Kamwela alisema Tanzania inafanya vizuri kueleka malengo ya kimataifa ya muda mrefu na wa kati ambayo ni kufikia 95 tatu kufikia mwaka 2025 ambazo kama tawimu za karibuni zinavyoonesha kuwa kuna watu milioni 1.7 wanaishi na VVU, hivyo 95 ya kwanza ni kuona watu hao wanatambuliwa na kujua hali zao ambapo sasa imefika asilimia 83, huku 95 ya pili ni wale wanaoishi na VVU watumie dawa za kufubaza makali ya ukimwi (ARV) ambapo Tanzania imevuka lengo kwa kufikisha asilimia 98 na 95 ya tatu wale wanaotumia ARV asilimia 95 wawe wamefubaza virusi, utafiti wa mwisho unaonyesha maambukizi mapya yakipungua.

Nao baadhi ya washiriki wenye umri mdogo waliopanda Mlima Kilimanjaro, Regina Baraka na Baraka Erasto, kutoka kituo cha Moyo wa Huruma cha mkoani Geita, kilichoanzishwa kupitia mfuko wa Kili Challenge walielezwa kufurahishwa kwa uzoefu walioupata Kwa mara ya kwanza wakipanda mlimani hivyo kutoa hamasa Kwa vijana wadogo wenye umri kama wao kujitokeza kushiriki katika Kampeni hiyo Ili kuweza kuleta mabadiliko kwa wenye VVU.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akikabidhi cheti kwa mmoja wa washiriki wenye umri mdogo wa Kampeni ya kupanda mlima kilimanjaro ya GGM Kili Challenge, Baraka Erasto (kulia), mara baada ya kumaliza zoezi la kupanda na kushuka mlima huo, mjini Moshi, Kilimanjaro, hivi karibuni. Kampeni hiyo ya kila mwaka ina lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki. anaishi katika Kituo cha Moyo wa Huruma cha Geita kilichoanzishwa kwa msaada kutoka Mfuko wa Kili Challenge.
Balozi wa Uingereza nchini Tanzania, Mhe. David Concar, akihutubia katika hafla ya kuwapokea wapanda mlima Kilimanjaro waliokuwa wakishiriki kampeni ya kila mwaka ya GGM Kili Challenge yenye lengo la kusaidia miradi inayojikita katika kutokomeza VVU na Ukimwi. Kampeni hiyo imendaliwa na Kampuni ya Dhahabu ya Geita Gold Mining kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) ambapo jumla ya wapanda mlima 48 na waendesha baisketi 23 walishiriki zoezi hilo lilioanza Julai 19 kufikia tamati yake mjini humo hivi karibuni.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages