Serikali ya Marekani Yashiriki Uzinduzi wa Ndondo Cup 2024, kupitia kampeni za SITETEREKI na FURAHA YANGU na CHANJO NI MAISHA

Mkazi wa Jiji la Dar es Salaam akipata vipimo vya afya wakati wa hafla ya uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup 2024. Serikali ya Marekani, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) nchini Tanzania, imetangaza ushirikiano na mashindano ya Ndondo Cup 2024  kupitia kampeni zake mashuhuri za ‘SITETEREKI’, ‘FURAHA YANGU’ na ‘CHANJO NI MAISHA’ ili kuchochea huduma za VVU na chanjo. Mashindano haya yatafanyika katika mikoa nane nchini Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Pwani na Kagera.

Wizara ya Afya, Ofisi ya Rais – TAMISEMI na Serikali ya Marekani (USAID na PEPFAR) kupitia mradi wa Breakthrough ACTION, wameungana na kamati ya maandalizi ya Ndondo Cup, na wadhamini wengineo ikiwemo CRDB na ASAS, kusogeza huduma za afya hasa huduma za VVU na chanjo. Ushiriki huu kwenye Ndondo Cup 2024, unafanywa kupitia kampeni ya afya ya vijana iitwayo SITETEREKI, kampeni ya wanaume kupambana na VVU iitwayo FURAHA YANGU na Kampeni yab chanjo ya kitaifa iitwayo CHANJO NI MAISHA. Mashindano ya Ndondo Cup 2024 yatafanyika katika mikoa nane ya Tanzania - Dar es Salaam, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Kagera, Dodoma, Mwanza, na Pwani.

Mashindano yalianza rasmi Juni 30, 2024, na mechi ya ufunguzi ya kusisimua kati ya Manzese Warriors na Makuburi FC kwenye Uwanja wa Kinesi, kata ya Sinza. Washiriki walipata huduma kamili za afya, ikiwa pamoja na vipimo vya VVU na matibabu na huduma za chanjo. Mgeni rasmi aliyefurahishwa na mpango huu wa ubunifu, aliipongeza kamati ya maandalizi na wadhamini kwa kujumuisha burudani na huduma za afya.

"Tumejitolea kubuni mbinu zinazotoa matokeo halisi ya kiafya," alisema Evangelina Chihoma kutoka Ofisi ya PEPFAR.

"Tunaamini kwamba michezo inaweza kuongeza nguvu kubwa katika kuleta mabadiliko ya tabia na kuboresha upatikanaji wa huduma, na tunafurahia kushirikiana na Ndondo Cup na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kufanikisha mashindano haya."

Lulu Msangi, Mtaalamu wa Programu kutoka Shirika la maendeleo la Marekani (USAID) aliongezea, "Tunatumia michezo kuhamasisha Watanzania kupata chanjo na kulinda familia zao."

Mpango huu wa ubunifu utatekelezwa kwenye ngazi ya kitaifa na jamii, ukilenga kuwafikia vijana wanaoshiriki shughuli za kimichezo kupata elimu na huduma za afya hasa zinazohusu VVU na chanjo. Kwa kuingiza huduma za afya katika burudani, mpango huu unalenga upokeaji wa huduma za afya miongoni mwa wavulana na wanaume kwa kutumia umaarufu wa soka.
Mashabiki wa mpira wa miguu kutoka maeneo mbali mbali ya jiji la Dar es Salaam wakifuatilia uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup 2024. Serikali ya Marekani, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) nchini Tanzania, imetangaza ushirikiano na mashindano ya Ndondo Cup 2024 kupitia kampeni zake mashuhuri za ‘SITETEREKI’, ‘FURAHA YANGU’ na ‘CHANJO NI MAISHA’ ili kuchochea huduma za VVU na chanjo. Mashindano haya yatafanyika katika mikoa nane nchini Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Pwani na Kagera.
Evangelina Chihoma ambaye ni Mtaalamu wa taarifa za mkakati kutoka PEPFAR akizungumza wakati wa uzinduzi wa michuano ya Ndondo Cup 2024. Serikali ya Marekani, kwa kushirikiana na Wizara ya Afya na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) nchini Tanzania, imetangaza ushirikiano na mashindano ya Ndondo Cup 2024 kupitia kampeni zake mashuhuri za ‘SITETEREKI’, ‘FURAHA YANGU’ na ‘CHANJO NI MAISHA’ ili kuchochea huduma za VVU na chanjo. Mashindano haya yatafanyika katika mikoa nane nchini Tanzania, ikiwemo Dar es Salaam, Dodoma, Mwanza, Mbeya, Iringa, Ruvuma, Pwani na Kagera.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages