WASAMBAZAJI BORA VILAINISHI VYA ORXY KWENDA DUBAI

 


Na Mwandishi Wetu

WASHINDI wawili wa Shindano la Wauzaji na Wasambazaji wa vilainishi vya Oryx wamejishindia safari ya kwenda Dubai ambapo wamekabidhiwa tiketi zao leo jijini Dar es Salaam.

Akizungumza wakati wa kukabidhi tiketi kwa washindi wawili wa shindano hilo Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta amesema Kampuni ya Oryx Services and Specialties Ltd iliendesha shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx.

Amesema shindano hilo lilianza Januari na kumalizika Desemba 2023 na kwamba leo Mei 31, 2024 wametangaza washindi wa shindano hilo ambao ni Mbise Oil Shop iliyopo Arusha (Oryx Shop) na Lwimba Investment Company Ltd iliyopo Dar es salaam (Msambazaji).

Amesema kuwa zawadi wa shindano hilo ni Safari ya kwenda Dubai ambapo leo washindi wao wamekabidhiwa tiketi zao tayari kwa safari huku akifafanua gharama zote za safari hiyo ya siku nne Dubai zimelipiwa na kampuni ya Oryx Services and Specialities Limited. Kila mshindi amepata tiketi mbili kwa ajili ya safari ya Dubai.

"Tunatarajia kutangaza mashindano yafuatayo hivi karibuni ambayo yatakuwa ya kusisimua zaidi kuliko shindano lililopita.Ni matumaini yetu wauzaji wetu wote watashiriki tena vyema kama mwaka uliopita.

"Oryx Energies ni kampuni kubwa na ya muda mrefu ya kimataifa inayotoa huduma za nishati barani Afrika. Oryx Energies huagiza, kuchakata, huhifadhi na kusambaza bidhaa za mafuta ya magari, machine na mitambo (Dizeli, Petroli, Vilainishi) na gesi za kupikia (LPG) zitumikazo katika sekta mbalimbali za uchumi.

"Ni msambazaji namba moja wa bidhaa za mafuta na vilainishi katika sekta ya uchimbaji madini (migodi). Pia Oryx Energies inaongoza kusambaza vilainishi katika sekta zingine za kiuchumi kama usafirishaji wa nchi kavu (pikipiki, magari, treni) na majini, viwandani, ujenzi na kilimo.

Pia Oryx Energies huzalisha na kusambaza vilainishi mbalimbali kuanzia vya magari, mitambo ya migodini na viwandani, uzalishaji wa umeme nk ambavyo vimeidhinishwa na Watengenezaji wakubwa wa Vifaa Halisi (Original Equipment Manufacturers) na vinakidhi au kuzidi viwango vya kimataifa.

Ameongeza katika kuhakikisha bidhaa na huduma zinapatikana kwa watumiaji kote nchini, Oryx Energies inaendelea kuboresha njia zake za usambazaji kwa kupitia Maduka ya Kipekee ya Kampuni (CODOs), Wasambazaji na vituo vya mafuta vya Oryx.

Akizungumza kwa niaba ya washindi , Vaileth Cilwimba kutoka Lwimba Investment Company Ltd jijini Dar es salaam (Msambazaji) amesema ushindani ulikuwa mkubwa lakini anashukuru kituo chao kuibuka washindi kutokana na juhudi wanayofanya katika kukuza bidhaa za Oryx pamoja na kutafuta masoko.

"Tunashukuru kwa kushinda na kupata tiketi kwa ajili ya kwenda Dubai ambapo tumelipiwa kila kitu kwa maana ya gharama zote, kwetu hii inatufanya tuongezee bidii zaidi kwa kuuza zaidi bidhaa bora za Oryx zikiwemo za Vilainishi vya magari,bodaboda na bajaji."

Awali Arthur Awet ambaye ni B2C Key Account Manager Kampuni ya Oryx Services and Specialties Ltd amesema Oryx Services and Specialties LTD iliendesha shindano ya CODO na wasambazaji wao 50 ya kutafuta mtendaji bora wa mauzo katika bidhaa zao zote za vilainishi.

"Leo ni siku ya makabidhiano ya tikiti kwa washindi, ambapo kila duka iliyoshinda imejishindia tiketi mbili ya Kwenda na kurudi Dubai ambayo gharama zote za safari zimelipwa. Safari ya washindi hawa itakua baada ya mwezi wa Ramadhan."
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akiwa kwenye picha ya pamoja na washindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx ambapo washindi hao wamezawadiwa tiketi ya kwenda Dubai. Hafla hiyo imefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akimkabidhi mfano wa zawadi ya tiketi ya Safari ya kwenda Dubai Mwakilishi wa Kampuni ya Mbise Oil Shop iliyopo Arusha (Oryx Shop)(Msambazaji) ambaye ni mshindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx. Zozi la ugawaji wa tiketi hizo limefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Oryx Energies Tanzania Kalpesh Mehta akimkabidhi mfano wa zawadi ya tiketi ya Safari ya kwenda Dubai Vaileth Cilwimba kutoka Lwimba Investment Company Ltd jijini Dar es salaam (Msambazaji) ambaye ni mshindi wa shindano la wauzaji (mawakala) bora wa vilainishi vya Oryx Energies kati ya Maduka ya Oryx na wasambazaji wa Vilainishi vya Oryx. Zozi la ugawaji wa tiketi hizo limefanyika leo Mei 31,2024 Jijini Dar es Salaam.
Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages