ADAM MIHAYO MKURUGENZI MPYA TANZANIA COMMERCIAL BANK
MKAZI WA KINONDONI MANYANYA AJISHINDIA PIKIPIKI KUPITIA DROO YA Y9 MICROFINANCE
SERIKALI YAZINDUA MPANGO WA TAIFA WA KUDHIBITI UKIMWI, MAGONJWA YA NGONO NA HOMA YA INI
WASHINDI WA DROO YA SABA Y9 MICROFINANCE WAPATIKANA
WASHINDI WA DROO YA 6 Y9 MICROFINANCE WAPATIKANA
Meneja masoko wa taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi. Sophia Mang’enya (katikati) akizungumza na mshindi wa pikipiki droo ya sita kwa njia ya simu Baraka Barazae mkazi wa Dar es Salaam ambaye amejishindia pikipiki na Robert Keraryo mkazi wa Butiama ambaye amejishindia simu janja. Hafla ya kuchezesha droo hiyo imefanyika leo jijini Dar es salaam, Wengine pichani kutoka kushoto ni Afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Bi. Pendo Mfulu.
Washindi wa Droo ya sita ya Y9 Microfinance wapatikana mshindi wa pikipiki ni Baraka Barazae mkazi wa Kinyerezi jijini Dar es Salaam na mshindi wa simu Robert Keraryo Mkazi wa Butiama mkoani Kagera.
Akizungumza wakati wa kuchezesha droo hiyo Meneja Masoko ya taasisi ya kifedha Y9 microfinance Bi Sophia Mang'enya ameeleza kuwa huu ni muendelezo wa Y9 microfinance kuchezesha droo kila wiki na kupata washindi wawili.
Alisema "Matamanio makubwa ya Y9 microfinance ni kuhakikisha kuwa kila mtanzania anapata huduma za kifedha popote alipo, hilo ndio lengo kuu la kuanzishwa kwa Y9 microfinance".
Aligusia kuwepo kwa wimbi kubwa matapeli wa mtandaoni na amewasihi wateja wa Y9 microfinance kuwa makini na wizi huo wa mitandaoni, amewasihi watanzania kuitumia Tehama kwa maendeleo sio kutumia Tehama kufanya uhalifu.
Alieleza namna ya kushiriki ni rahisi hakikisha umepakua app ya Y9 microfinance kisha kujisajili na kuanza kukopa na moja kwa moja utaingia kwenye droo hii baada ya marejesho.
Kwa upande wake afisa kutoka bodi ya michezo ya kubahatisha nchini Pendo Mfulu ameeleza "kama bodi ya michezo ya kubahatisha nchini tumeridhishwa na namna ya uchezeshwaji wa droo hii na upatikanaji wa washindi.
Over 1,300 Empowered Women Food Vendors in Tanga Region Celebrate the Success of the Mwanamke Shujaa Campaign, Courtesy of Coca-Cola Kwanza Ltd, in Collaboration with Oryx Gas and ISW
TANZANIA COMMERCIAL BANK PLC YAZINDUA TAWI JIPYA MPWAPWA DODOMA
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw. Jema Msuya (wa tatu kushoto) akikata keki wakati wa maadhimisho ya wiki ya hudima kwa mteja. Hafla hiyo iliyofanyika katika tawi jipya la benki hiyo lililozinduliwa hivi karibuni Mpwapwa mkoani Dodoma. Wengine pichani ni Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo Edmund Mndolwa, Meneja wa Tawi hilo pamoja na wateja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw. Jema Msuya akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa tawi jipya la benki hiyo lililozinduliwa hivi karibuni Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Kaimu kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdallah Shaib.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw. Jema Msuya pamoja na maafisa wengine wa benki hiyo wakifurahia mara baada ya kuzindua tawi jipya la benki hiyo lililozinduliwa hivi karibuni Mpwapwa mkoani Dodoma ambapo mgeni rasmi katika uzinduzi huo alikuwa Kaimu kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Abdallah Shaib.
ZAIDI YA MAWAKALA 1300 WA TANZANIA COMMERCIAL BENKI PLC WAPATIWA MAFUNZO YA UTOAJI HUDUMA BORA.
Tanzania Commercial Bank imetoa semina kwa mawakala wake zaidi ya 1300 wanaotoa huduma za kifedha maeneo mbalimbali ya jiji la Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuboresha huduma na ufanisi kwa wateja wa TCB wanaojipatia huduma za kibenki kwa mawakala hao.
Akizungumza katika semina hiyo,Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Bw, Jema Msuya alisema semina hizo ni mwendelezo wa mafunzo kwa mawakala waTCB nchi nzima ili kuboresha huduma, kukuza biashara zao na kuleta ufanisi kuboresha katika kumuhudumia mteja.
Alisema TCB Hadi sasa tumekuwa na mwakalazaidi zaidi ya 5600 ambao hutoa huduma nchi nzima huku ikiwa na matawi 82 na mashine za ATM zaidi ya 400 lengo likiwa kusogeza huduma kwa wateja wake.
Jema alisema huduma ya TCB Wakala iliyoanzishwa ili kusaidia na kuondoa kero mbalimbali kwa wateja wa TCB ikiwemo foleni katika matawi mbalimbali ya benki hiyo huku ikitoa ajira kwa mawakala zaidi ya elfu 5600 ambao nao wameajiri vijana mbalimbali ambao wanajipatia kipato.
Mafunzo haya yanaenda sambamba na kuwapongeza mawakala waliofanya vizuri kwa mwaka huu katika kazi zao, ili kuleta chachu kwa wengine kufanya vizuri zaidi.
kwa upande wake mmoja ya mawakala Raqeeb Hamidu ameishukuru TCB kwakuandaa semina hizi marakwamara kwasababu wanazidi kunufaika nakuongeza uwezo wakuwahudumia wateja kwa uadilifu mkubwa na wepesi.
Tanzania commercial bank imekuwa Benki ya kwanza kwakutujali sisi mawakala na wateja wake maana hizi semina zinakwenda kumsaidia wakala wa zamani lakini pia wakala wapya
Tanzania Commercial Bank yaungana na Standard Chartered Bank katika utoaji wa huduma za kibenki.
Benki ya Standard Chartered Tanzania iliandaa hafla ya kiamsha kinywa kwa wateja wake wa Biashara katika Hoteli ya Hyatt Regency ikiwa pamoja na Benki ya Biashara Tanzania lengo ikiwa ni kuhamasisha huduma inayowawezesha wateja wa SCB kutumia mtandao wa TCB kuweka na kutoa pesa kwenye Matawi yake 82 pamoja na Wakala 5,600 wa TCB kote nchini.
Ushirikiano huu unalenga kutoa urahisi, wakati halisi na mazingira salama kwa wateja wa Standared Chartered Bank kutekeleza huduma zao za benki.
Katika Hafla hiyo ilihudhuriwa na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TCB, Bw. Jema Msuya pamoja na wawakilishi waandamizi kutoka benki hiyo, Rayson Foya, pamoja na Kaimukurugenzi wa Standared Chartered ambae pia ni Mkuu wa Kitengo cha Miamala Efeh Amoah pamoja na maafisa wengine kutoka SCB.
Bharti Enterprises Founder commends President Samia Suluhu Hassan for advancing digital adoption in Tanzania
TANZANIA COMMERCIAL BANK YAANDAA CHAKULA CHA JIONI KWA AJILI YA WATEJA WAKE MAADHIMISHO WIKI YA HUDUMA KWA MTEJA
Baadhi ya maofisa wa Tanzania Commercial Bank pamoja na wateja wa benki hiyo wakiwa katika hafla ya chakula cha jioni kilichoandaliwa na benki hiyo ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Tanzania Commercial Bank ambaye ni Mkurugenzi wa Tehama Bw. Jema Msuya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na maafisa wa benki hiyo wakati wa chakula jioni kilichoandaliwa na benki hiyo kwa ajili ya wateja wake ikiwa ni maadhimisho ya wiki ya huduma kwa mteja.