TANZANIA COMMERCIAL BANK YATOA MSAADA WA VIFAA VYA USALAMA BARABARANI

 


Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania Commercial Bank TCB Deogratius Kwiyukwa (kushoto), akishikana mikono na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kinondoni Notkey Kilewa, wakati wa hafla yakukabidhi msaada wa vifaa vya kuongezea usalama barabarani pamoja na vibanda kumi vya kupunzikia askari wa kitengo hicho makabidhiano hayo yamefanyika katika kituo kikubwa cha polisi cha Oystebay jijini Dar es Salaam. wengine pichani ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Ubungo Abas Juma pamoja na Mkuu wa Usalama Barabarani kituo cha Urafiki ubungo Amina Saidi.
Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania Commercial Bank TCB Deogratius Kwiyukwa (kulia), akizungumza wakati wa hafla yakukabidhi msaada wa vifaa vya kuongezea usalama barabarani pamoja na vibanda kumi vya kupunzikia askari wa kitengo hicho makabidhiano hayo yamefanyika katika kituo kikubwa cha polisi cha Oystebay wengine pichani ni Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kinondoni Notkey Kilewa,pamoja na Mkuu wa Usalama Barabarani kituo cha Urafiki ubungo Amina Saidi.
Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania Commercial Bank TCB Deogratius Kwiyukwa (kushoto), akisalimiana na Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kinondoni Notkey Kilewa, wakati wa hafla yakukabidhi msaada wa vifaa vya kuongezea usalama barabarani pamoja na vibanda kumi vya kupunzikia askari wa kitengo hicho makabidhiano hayo yamefanyika katika kituo kikubwa cha polisi cha Oystebay jijini Dar es Salaam. wengine pichani ni Meneja wa Tanzania Commercial Bank Tawi la Ubungo Abas Juma pamoja na Mkuu wa Usalama Barabarani kituo cha Urafiki ubungo Amina Saidi.
 
Mkuu wa Kitengo cha Usalama Barabarani Wilaya ya Kinondoni Notkey Kilewa,akizungumza mara baada ya kupokea mdaa wa vifaa vyakuongezea usalama barabarani kutoka Tanzania Commercial Bank. Kulia ni Mkurugenzi wa Masoko na ukuzaji biashara wa Benki ya Biashara ya Tanzania Commercial Bank TCB Deogratius Kwiyukwa pamoja na Mkuu wa Usalama Barabarani kituo cha Urafiki ubungo Amina Saidi.

 Picha ya pamoja





Share:

WAKAZI WA MBINGA WAIPOKEA KWA BASHASHA TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZIDUA TAWI JIPYA

 .com/img/a/Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jenerali Wilbert Ibuge (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililofunguliwa katika barabara ya mkibili mjini Mbinga mkoani Ruvuma ikiwa ni tawi la tatu la benki hiyo katika mkoa huo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Sabasaba Moshingi pamoja na Meneja wa Tawi la Tanzania Commercial bank mbinga Egno Ngole .

.com/img/a/
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jenerali Wilbert Ibuge (wapili kulia), akisaidi katika kitabu cha wageni alipotembelea na kuzidua tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililofunguliwa katika barabara ya mkibili mjini Mbinga mkoani Ruvuma ikiwa ni tawi la tatu la benki hiyo katika mkoa huo (kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, Meneja wa Tawi hilo Egno Ngole pamoja na maofisa wengine wa Tanzania Commercial Bank.
.com/img/a/
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jenerali Wilbert Ibuge (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, Meneja wa Tawi hilo Egno Ngole pamoja na maofisa wengine wa Tanzania Commercial Bank.


Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuongeza jitihada kuwafikia Watanzania katika kila kona ya nchi  kwa madhumuni ya kujenga jamii yenye uchumi wa kati, na kuunga mkono juhudi  na malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma za kibenki.

Benki hiyo iimetimiza azma hiyo kupitia huduma zake mbalimbali katika kuigusa jamii kwa kufungua tawi Mji wa Mbinga, Mkoani Ruvuma katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali.


Tawi hilo la Mbinga linakuwa tawi la tatu kuzinduliwa mwaka huu na kuifanya benki hiyo sasas kuwa na mtandano wenye jumla ya matawi 82 Tanzania Bara na Visiwani ili kuleta manufaa  kwa wajasiriamali na wananchi wa mkoa huo.


Pamoja na kusogeza  huduma za kibenki kwa wananchi, Tanzania Commercial Bank pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kuinua uchumi katika mkoa huo.


Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bnk, Sabasaba Moshingi,  alisema wateja wa benki hiyo wapo katika mikono salama na kuwaomba wananchi  waitumie benki hiyo kwani imekuwa ikifanya mambo mengi yanayolenga jamii.


Moshingi alisema kuwa uzinduzi wa tawi la Tanzania Commercial Bank wilayani Mbinga ni moja ya mikakati ya benki hiyo ya kupanua na kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi kwa wananchi hasa katika maeneo yanayokua kwa kasi na ambayo yenye maendeleo ya kiuchumi.


“TCB inaamini kufungua matawi  katika maeneo yenye muwamko wa kiuchumi utakaoongeza  ukuwaji wa shughuli za kifedha  kwa wananchi na kuinua kipato cha wajasiriamali, “ alisema Moshingi.“ Mchakato wa Tanzania Commercial Bank unaenda sambamba na malengo ya serikali yetu ya kusogeza huduma bora kwa wananchi wote”


Tawi la Mbinga  ni mwendelezo wa ufunguzi wa matawi ya benki hiyo mwaka 2002, tulianza na uzinduzi wa matawi ya Kigamboni, Dar es Salaam na Mpanda,  likiwa ni mkakati wa Tanzania Commercial Bank wa kuchangamkia fursa ya kukua kwa shughuli za kibiashara  na za kiuchumi wilayani humo.


 Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi la Mbinga, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brig. Jenerali Wilbert Ibuge ,aliipongeza Tanzania Commercial Bank kwa kuona fursa kubwa wilayani humo zinazotokana na shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na wananchi wa mkoa wa Ruvuma.


Aliwaomba  wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa zinazotolewa na Tanzania Commercial Bank kwa kufungua akaunti nakujipatia mikopo kwa mashari nafuu.  “ Benki hii ni yakwetu tuitumie kwa faida maana imekuwa benki ya kwanza kujali wananchi wa Ruvuma,  hili ni tawi la tatu katika mkoa wetu kufunguliwa na benki hii,” alisema Brig. Jenerali Ibuge.


Tanzania Commercial Bank Plc ni taasisi ya fedha iliyoundwa kisheria kutoka iliyokuwa Benki ya Posta Tanzania (Tanzania Postal Bank), ikitoa bidhaa na huduma ili kukidhi mahitaji ya benki ya kibinafsi na ya kibiashara ya wateja.

Share:

Wakazi wa Buza Kanisani walalamikia Uchafuzi wa Mazingira wa Sauti

  


Wakazi wa Buza Kanisani, Mtaa wa Amani, wamelamikia mfanyanya biashara kwa kujenga ukumbi wa sherehe katika eneo la makazi (residentional) , jambo linalosabisha uchafuzi mkubwa wa mazingira kwa njia ya sauti kutokana kelele zinatoka katika ukumbi huo.

 

Wanamshutumu mfanyabiashara huyo Bw. Shayo kwa kuvunja sheria za matumizi ya ardhi kwa  ukumbi wa sherehe na bar kubwa  kwenye la eneo ambalo limepimwa na mamlaka za Serikali kwa ajili ya makazi, na sio biashara.

 

"Tunashindwa kulala usiku, watoto wetu wanashindwa kujisomea usiku kwa kelele na ghasia zinasababishwa na ukumbi huu," amesema bw.Mika Moza, mmoja wa wakazi wa eneo hilo.

 

"Serikali imetumia fedha nyingi za walipa kodi kupima maeneo haya ya makazi, iweje leo mtu anabadilisha matumizi ya ardhi kiholela kwa kufanya biashara kama hii yenye athari kubwa kwa mazingira kwa njia ya sauti/ kelele, alafu serikali ya mtaa iko kimya," amesema mkazi mwingine, Kulwa Muga

 

Wakazi wamedai kuwa wamewasilisha malalamiko yao (kwa maandishi) kwa Afisa mipango miji- Manispaa ya Temeke tangu Mwaka 2013, lakini mpaka sasa hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

 

"Mfanyabiashara huyu Bw. Shayo, ni mbabe na kwa sababu ana pesa kiongozi wa serikali ya mtaa, maafisa wa mipango miji -Temeke Manispaa, wote wametiwa mfukoni, hawawezi kuthibiti jambo hili, hali inayosababisha hadha kubwa kwa wakaxi wa eneo hili," Bi. Moza Mrope, amadai mkazi mwingine.

 

Kuthibisha mahusiana wenye mashaka kati mfanyabiashara huyo, wakazi wanasema baada ya kuvunja sheria kwa miaka za ya tisa, hivi karibuni maafisa mipango miji -Temeke manispaa wamemshauri Bw. Shayo, kubadilisha matumizi ya kiwanja hicho No. 686, Kitalu E, kutoka makazi kwenda biashara, jambo ambalo ni "uvunjifu wa sheria za mazingira."

 

"Kumruhudu abadilishe matumizi ya kiwanja -kutoka makazi kwenda biashara, ni kosa kwa sababu maeneo haya yamepimwa kwa ajili makazi, na si biashara...Manispaa wakiruhusu jambo hili watakuwa wamebariki rasmi uchafuzi wa mazingira na uvunjaji wa sheri za mazingira, bila kujali athari za kelele na uchafu huu mkubwa wananchi walio wengi.

 

Alipohojiwa, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Amani, Bw. Omary Katoto amesema "Sio wakazi wote wanalalamika kuhusu jambo hili, ninachofahamu mimi ni kwamba kulikuwa ugomvi kati ya mfanyabiashara huyo na mtu mmoja katika eneo hilo."

 

"Miaka kama mitatu iliyopita walipelekana polisi, walitishiana maisha sijui, lakini niitwa kama Mwenyekiti wa Serikali wa Mtaa, nikawasihi polisi watuachie jambo lile tukalisuhishe kirafiki kama wa mtaa mmoja, walikubali ...tulikaa chini tuongea na pande zote mbili, tukamaliza. Leo hii nashangaa kuone jambo hili nimeibuka tena.".

 

Alipotafutwa, Afisa Ardhi-Temeke Manispaa, Salumu Ali, amesema “Njia rahisi kwa wakazi hao ni kupeleka malalamiko yao kwa maandishi kwa Mkurugenzi wa Manispaa, ili kuweka pingamizi la kuzuia mabadiliko ya matumizi ya Ardhi ambayo Bw. Shayo, amepanga kuyafanya—kutoka Makazi kwenda biashara.”

 

“Kama mamlaka, tutapokea maoni na mapingamizi ya wananchi hao, na kuyafanyia kazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za maswala ya Ardhi. Hilo ndo naona kama suluhisho kwa wakazi hao wanaolalamika.”

Share:

TANZANIA COMMERCIAL BANK YATINGA KIGAMBONI YAFUNGUA TAWI JIPYA LA KISASA

 


MKUU wa Wilaya ya Kigamboni, Fatuma Almasi Nyangassa, ameiomba benki ya Tanzania Commercial Bank (TCB) kupanua wigo wa huduma zake katika wilaya hiyo ili kuwawezesha wajasiliamali kufikiwa huduma za kibenki na hivyo kupata fursa ya kujikwamua kiuchumi.


Nyangassa ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa tawi jipya na la kisasa la benki hiyo , lililopo karibu na Chuo Cha Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere Kigamboni, ambalo ni sehemu ya mkakati wa kutimiza azma ya kitaifa ya kufikisha huduma za kifedha kwa kila mtanzania.


Amesema katika wilaya ya Kigamboni kuna wafanyabiashara na wajasiriamali wengi ambao wanahitaji huduma za kifedha, na akatumia fursa hiyo kuiomba benki ya TCB kuzidi kongeza na kuboresha miundombinu ya huduma zake ili kuwafikia wananchi wengi zaidi.


“ Wilaya yetu ya Kigamboni inazo shughuli nyingi za kiuchumi vikiwemo viwanda mbalimbali, vikubwa na vidogo, hivyo ujio wa benki hii ya TCB utarahisisha upatikanaji wa huduma za kibenki na hivyo kuiunua ufanisi na ukuaji wa shughuli za uchumi,” alisema Fatma Nyangassa.


Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi, Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, alisema benki hiyo kwa sasa ni miongoni mwa benki kumi bora katika utoaji huduma hapa nchini, na kuwataka wafanyabiashara kujitokeza kwa wingi katika tawi hilo kujipatia huduma mbali mbali, ikiwemo mikopo yenye riba nafuu.


Alisema Moshingi; “ Benki ya TCB pia inajali jamii hasa katika sekta za afya na elimu, na imewekeza katika kuhakikisha kuwa inaunga mkono program mbalimbali za sekta hizo muhimu ili kufanikisha azama ya serikali ya Awamu ya Sita kuinua kiwango cha maisha cha watanzania.


Moshingi amesema kuwa tawi la Kigamboni ni tawi la kwanza kwa wilaya hiyo, na kuongeza kuwa benki hiyo ina mtandao mpana nchini, ikiwa na inatoa huduma kupitia matawi mengine 82, na kuahidi kuwa TCB itaendelea kupanua wigo wa huduma zake ili kila mtanzania na mteja wa benki hiyo afikiwe na huduma na bidhaa mbalimbali zinazotolewa.


01
:Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa (kushoto), akifungua pazia la jiwe la msingi kuashiria uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Benki ya Tanzania Commercial Banki Kigamboni Hafla hiyo imefanyika leo katika ofisi za tawi hilo kigamboni jijini Dar es Salaam kulia ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, Tawi la Tanzania Commercial Bank limekuwa ni tawi la kwanza katika Wilaya hiyo.


02
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa (watatukulia) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la Tanzania Commercial Bank Kigamboni. Hafla hiyo imefanyika katika ofisi za tawi hilo lililopo Kigamboni jijini Dar es Salaam kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, kulia ni Meneja wa Tawi la hilo Lameck Bubewa.
03
Meneja wa Tawi wa Benki ya Tanzania Commercial Bank Lameck Bubewa akizungumza wakati wa hafla wa uzinduzi wa tawi la benki hiyo lililofunguliwa leo na Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa ambae ndio alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.
04
Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni Fatma Nyangasa (katikati),akizungumza wakati wa hafla wa uzinduzi wa tawi la benki ya Tanzania Commercial Bank lililofunguliwa katika wilaya hiyo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, pamoja na Mkurugenzi Tehama na Uwendeshaji wa Tanzania Commercial Bank Jema Msuya
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages