WAKAZI WA MBINGA WAIPOKEA KWA BASHASHA TANZANIA COMMERCIAL BANK YAZIDUA TAWI JIPYA

 .com/img/a/Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jenerali Wilbert Ibuge (katikati) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililofunguliwa katika barabara ya mkibili mjini Mbinga mkoani Ruvuma ikiwa ni tawi la tatu la benki hiyo katika mkoa huo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB), Sabasaba Moshingi pamoja na Meneja wa Tawi la Tanzania Commercial bank mbinga Egno Ngole .

.com/img/a/
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jenerali Wilbert Ibuge (wapili kulia), akisaidi katika kitabu cha wageni alipotembelea na kuzidua tawi jipya la Tanzania Commercial Bank lililofunguliwa katika barabara ya mkibili mjini Mbinga mkoani Ruvuma ikiwa ni tawi la tatu la benki hiyo katika mkoa huo (kulia) ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank Sabasaba Moshingi, Meneja wa Tawi hilo Egno Ngole pamoja na maofisa wengine wa Tanzania Commercial Bank.
.com/img/a/
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brig. Jenerali Wilbert Ibuge (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na  kushoto kwake ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank (TCB) Sabasaba Moshingi, Meneja wa Tawi hilo Egno Ngole pamoja na maofisa wengine wa Tanzania Commercial Bank.


Tanzania Commercial Bank (TCB) imeendelea kuongeza jitihada kuwafikia Watanzania katika kila kona ya nchi  kwa madhumuni ya kujenga jamii yenye uchumi wa kati, na kuunga mkono juhudi  na malengo ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha kila Mtanzania anafikiwa na huduma za kibenki.

Benki hiyo iimetimiza azma hiyo kupitia huduma zake mbalimbali katika kuigusa jamii kwa kufungua tawi Mji wa Mbinga, Mkoani Ruvuma katika hafla fupi iliyohudhuriwa na wadau mbalimbali.


Tawi hilo la Mbinga linakuwa tawi la tatu kuzinduliwa mwaka huu na kuifanya benki hiyo sasas kuwa na mtandano wenye jumla ya matawi 82 Tanzania Bara na Visiwani ili kuleta manufaa  kwa wajasiriamali na wananchi wa mkoa huo.


Pamoja na kusogeza  huduma za kibenki kwa wananchi, Tanzania Commercial Bank pia inategemewa kufungua na kuendeleza fursa mbalimbali za kibiashara kwa lengo la kuinua uchumi katika mkoa huo.


Akiongea katika hafla ya uzinduzi wa Tawi hilo Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bnk, Sabasaba Moshingi,  alisema wateja wa benki hiyo wapo katika mikono salama na kuwaomba wananchi  waitumie benki hiyo kwani imekuwa ikifanya mambo mengi yanayolenga jamii.


Moshingi alisema kuwa uzinduzi wa tawi la Tanzania Commercial Bank wilayani Mbinga ni moja ya mikakati ya benki hiyo ya kupanua na kusogeza huduma za kibenki karibu zaidi kwa wananchi hasa katika maeneo yanayokua kwa kasi na ambayo yenye maendeleo ya kiuchumi.


“TCB inaamini kufungua matawi  katika maeneo yenye muwamko wa kiuchumi utakaoongeza  ukuwaji wa shughuli za kifedha  kwa wananchi na kuinua kipato cha wajasiriamali, “ alisema Moshingi.“ Mchakato wa Tanzania Commercial Bank unaenda sambamba na malengo ya serikali yetu ya kusogeza huduma bora kwa wananchi wote”


Tawi la Mbinga  ni mwendelezo wa ufunguzi wa matawi ya benki hiyo mwaka 2002, tulianza na uzinduzi wa matawi ya Kigamboni, Dar es Salaam na Mpanda,  likiwa ni mkakati wa Tanzania Commercial Bank wa kuchangamkia fursa ya kukua kwa shughuli za kibiashara  na za kiuchumi wilayani humo.


 Akizungumza na wadau mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa tawi la Mbinga, Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Brig. Jenerali Wilbert Ibuge ,aliipongeza Tanzania Commercial Bank kwa kuona fursa kubwa wilayani humo zinazotokana na shughuli mbalimbali za kimaendeleo zinazofanywa na wananchi wa mkoa wa Ruvuma.


Aliwaomba  wananchi wa mkoa huo kuchangamkia fursa zinazotolewa na Tanzania Commercial Bank kwa kufungua akaunti nakujipatia mikopo kwa mashari nafuu.  “ Benki hii ni yakwetu tuitumie kwa faida maana imekuwa benki ya kwanza kujali wananchi wa Ruvuma,  hili ni tawi la tatu katika mkoa wetu kufunguliwa na benki hii,” alisema Brig. Jenerali Ibuge.


Tanzania Commercial Bank Plc ni taasisi ya fedha iliyoundwa kisheria kutoka iliyokuwa Benki ya Posta Tanzania (Tanzania Postal Bank), ikitoa bidhaa na huduma ili kukidhi mahitaji ya benki ya kibinafsi na ya kibiashara ya wateja.

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages