Wanafunzi wa Sekondari ya Sullivan wawakumbuka wenye mahitaji
TPB YAPATA FAIDA YA BILIONI 21
BENKI ya TPB imepata faida ya Shilingi bilioni 21 kabla ya kodi kwa mwaka 2020. Kiasi hicho ambacho kimepatikani kabla ya kodi, kinatajwa na uongozi wa benki kuwa ni kikubwa ukizingatia changamoto mbalimbali zilizojitokeza mwaka jana, hasa janga la Corona lililoathiri dunia nzima.
Akizungumza kwenye mkutano wa mwaka wa wanahisa jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Bodi wa benki hiyo, Dkt. Edmund B. Mndolwa alisema benki hiyo inaendelea kufanya vizuri kwa kupata faida hiyo kabla ya kodi.
Utendaji kazi uliotukuka, ufanisi na umakini wa menejimeti ya benki huku wakisimamiwa kwa karibu na Bodi tumeweza kupata faida kubwa ambalo ni jambo la kujivunia sana kwa kufanya kazi kubwa kwa tija,’’ alisema Dkt. Mndolwa.
Alisema kwamba pamoja na kwamba benki hiyo ina mtaji mdogo, ikilinganishwa na benki nyingine, imeendelea kufanya vizuri katika nyanja zote kwa miaka takriban kumi.
Dkt. Mndolwa alisema kwamba benki hiyo itaendelea kujipanga na kupanua shughuli zake za kibenki nchini na kuweka mikakati madhubuti ya kukabiliana na changamoto za kiuchumi kwa sasa katika sekta ya fedha nchini.
Benki ya TPB ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Namba 11 ya mwaka 1991, kama ilivyofanyiwa mabadiliko mwaka 1992. Mwaka 2016 jina la Benki lilibadilishwa na kuwa Benki ya TPB badala ya Benki ya Posta Tanzania.
Katika kuendelea kuelezea matukio makubwa Kwa mwaka 2020, Dkt. Mndolwa alisema serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
iliziunganisha Benki ya TPB na Benki ya Biashara ya TIB.
Lengo likiwa kuunda benki kubwa ya serikali itakayo boresha huduma, kupanua wigo wa mtandao na kutengeneza faida kubwa.
Benki ya TPB itaendelea kuboresha huduma zake na kubuni huduma mpya zinazokidhi matarajio ya wateja na kuwafikia wateja wengi zaidi wa kipato cha chini. Miongoni mwa huduma kama hizo ni SONGESHA na M-KOBA ambazo zinatolewa na Benki ya TPB kwa kushirikiana na Kampuni ya simu ya Vodacom.
Mwenyekiti wa Bodi, Dkt. Edmund Mndolwa akimalizia taarifa yake amesema Benki ya TPB inafanya vizuri katika soko la mabenki na hivyo kutoa wito kwa wateja kuendelea kuiunga mkono Benki yao. Mwelekeo ni mzuri na ndiyo maana benki imeendelea kukua na hadi kufikisha thamani ya Mali za Shilingi trioni moja mwisho mwa mwaka 2020 ikishika nafasi ya Saba kati ya benki zaidi ya 50 kote nchini.
Benki ya Akiba yashiriki katika zoezi la kutoa na kuchangia damu
BENKI YA NBC YASOGEA KARIBU ZAIDI KWA WAFANYABIASHARA WANAOCHIPUKIA
Benki ya Taifa ya Biashara leo imezindua kampeni yake ya Twende Sawa na NBC yenye lengo la kuwafuata na kuwapa elimu wafanyabiashara wanaochipukia katika maeneo yao ya kazi na biashara. Kampeni hiyo imezinduliwa leo katika hafla fupi iliyofanyika Makao Makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na wadau mbali mbali wakiwemo wafanyakazi na baadhi ya wateja wa benki hiyo.
SULLIVAN PROVOST YAJA NA SIKU YA KUTOA ZAWADI KWA WAHITAJI
Urusi Na Tanzania Kuanzisha Miradi Ya Mazingira
Rais wa Jumuiya ya Urafiki wa Tanzania na Urusi Yuri Korobov (kushoto), akiteta jambo na Rais wa Jumuiya ya Wanadiaspora wa Kiafrika nchini Urusi Dk. Prof Zunebe Kinfu Tafesse wakati walipokutana kujadili namna watakavyoungana na Tanzania kuunda miradi ya pamoja ya mazingira mazungumzo hayo yalifanyika nchini Urusi hivi karibuni.
Na Mwandishi Wetu
JUMUIYA ya Urafiki ya Urusi ambayo iliundwa nchini Urusi na watu maarufu na wajasiriamali, inaungana na Tanzania kuanzisha na kukuza miradi ya mazingira na kufikia kiwango cha kimataifa.
Mkuu wa Shirika, mwanachama wa Jumuiya ya Kijiografia ya Urusi, Yuri Korobov anasema “Kwanza, tumejipanga kufanya kazi katika miradi ya mazingira. Hii ni kati ya Urusi na Tanzania, tatizo la ukataji miti hovyo ni baya. Kuna baadhi ya watu wamekuwa wakikata misitu ya asili iliyoenea kwenye maeneo mbalimbali.
“Tanzania inakabiliwa na matatizo kadhaa ya mazingira, hiyo imekuwa ikiathiri maendeleo ya mazingira kwa kiasi kikubwa.
“Tatizo kubwa linaloikabili Tanzania ni uharibifu wa ardhi, uchafuzi wa mazingira, kukosa maji safi katika baadhi ya maeneo ya mjini na vijijini na upoteaji wa wanyamapori,”.
Jumuiya ya Urafiki ya Urusi inajipanga kufanya kazi na mashirika kama Baraza la Kitaifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) ambalo lina jukumu la kuishauri serikali juu ya mambo yote yanayohusiana na mazingira.
Korobov alisema pia wataangalia changamoto zingine ambazo zimekuwa kikwazo katika kuathiri mazingira Tanzania.
Kuangalia migodi iliyotelekezwa, ambayo haihifadhiwi vizuri baada ya kuchimba madini, ikitoa gesi hatari za kemikali ambazo husababisha uharibifu wa udongo.
Ukataji miti kwa wingi
“Shida zote hapo juu zinaweza kupunguzwa kwa gharama ya teknolojia zilizopo nchini Urusi. Ndio sababu tumepanga kufanya mafunzo ya pamoja na kubadilishana wataalamu - wanamazingira, wahandisi, wakemia na wanaojitolea,” alisema Korobov.
Jumuiya ya Urafiki ya Urusi na Tanzania zinatarajiwa kutia saini makubaliano yao ya kwanza na Jumuiya ya Urafiki ya Tanzania mwishoni mwa Juni 2021. Kama sehemu ya makubaliano, vyama vitaunda baraza la biashara, ambalo litajumuisha watumishi wa umma na wajasiriamali.
“Kwa pamoja tutafanya kazi na kutekeleza uelewa wa jinsi miradi inapaswa kutekelezwa kila mahali, hata katika miradi ya kibiashara, ambayo tutashiriki kama washauri na kutoa msaada wa habari, kuna mwelekeo wa mazingira,” alisema Korobov.
Aliongeza, shirika limepanga kutekeleza miradi mingine kadhaa, ambapo miongoni mwao ni uundaji wa jukwaa la ushirikiano wa kiuchumi kati ya biashara ya Tanzania na Urusi, kufanyika kwa jukwaa la uchumi lenye kaulimbiu ya kuvutia uwekezaji wa pande zote, utayarishaji wa mipango ya elimu kwa wanafunzi na vijana wa Urusi na Tanzania, ushirikiano katika maendeleo ya sekta ya kilimo ya nchi zote mbili, na pia utekelezaji wa mipango salama ya utalii, ubadilishaji wa kitamaduni.
Jumuiya ya Urafiki na Tanzania ilianzishwa nchini Urusi Aprili 2021 na kikundi cha watu maarufu na wajasiriamali kukuza miradi ya mazingira katika kiwango cha kimataifa.
Mwaka 2019, Sochi iliandaa mkutano wa kwanza wa uchumi wa Urusi na Afrika, ambao ulisababisha tamko lenye malengo ya maendeleo zaidi ya ushirikiano wa Urusi na Afrika katika nyanja za siasa, usalama, uchumi, sayansi, teknolojia na tamaduni.
Mkutano wa pili wa Urusi na Afrika umepangwa kufanyika mwaka 2022.
Tunatarajia urafiki wenye matunda kati ya Urusi na Tanzania kuelekea nchi rafiki ya mazingira na ushirikiano utakaoendelea.