Jinsi TEHAMA inaweza kupunguza uzalishaji wa kaboni na kuifikishaAfrika katika uchumi wa kijani.

 Smarter%2BEnergy%2Bfor%2Ba%2BBetter%2BLife

(Johannesburg, 21 Aprili 2021) Kampuni ya teknolojia ya kimataifa, Huawei inaamini kuwa teknolojia ya habari na mawasiliano au TEHAMA, ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni kwa asilimia 20 katika muongo mmoja ujao.

William Xu, ni Mkurugenzi wa Bodi na Rais wa Taasisi ya Utafiti wa Mikakati wa Huawei, hivi karibuni alisema uendelevu wa nishati ni changamoto kubwa ambayo itazikabili nchi zote kwa muongo mmoja ujao.

“Matumizi ya nishati ulimwenguni yanaongezeka kwa kiwango cha asilimia 1.7 kila mwaka. Hivi sasa asilimia 85 ya nishati hutokana mabaki ya mimea na wanyama wa kihistoria yaani ”fossils”. Uendelevu wa nishati hii ni changamoto kubwa inayotukabili sisi sote. Kwa kuwezesha sekta mbalimbali, teknolojia ya TEHAMA ina uwezo wa kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni kwa asilimia 20 katika muongo mmoja ujao." Xu alisema.

Aliongeza kuwa wakati nchi nyingi zimejikita kupunguza uzalishaji wa kaboni, mahitaji ya nishati mbadala yameongezeka, na hapa ndipo TEHAMA inapotoa fursa mpya katika uzalishaji, uhifadhi na matumizi ya umeme.

"Kwa matumizi ya nishati, lazima tupendekeze mifumo jumuishi ya nishati kwa majumbani na viwandani na kuunda jamii, vyuo na miji isiyozalisha kaboni.” alisema Xu.

Hivi karibuni, Huawei ilitangaza kuwa itazingatia ubunifu na teknolojia mpya kusaidia viwanda kupunguza matumizi yao ya nishati ili kupunguza uzalishaji wa kaboni ulimwenguni.

Barani Afrika pia, nchi nyingi zinazidi kuhamia katika matumizi ya nishati mbadala ili kusonga mbele katika nishati endelevu kwa siku zijazo.

Pamoja na algorithm yake ya muunganisho wa gridi inayoendeshwa na utashi wa kutengenezwa (Artificial Intelligence), Huawei imetoa zaidi ya mifano ya gridi 200 ya umeme kwa nchi zaidi ya 30. Hii imesaidia mitambo ya umeme kuunganishwa na gridi kwa uimara huku ikipelekea kuwepo na chanzo bora cha umeme wa jua.

Katika umeme wa jua pekee, Afrika imepata maendeleo makubwa katika miaka ya hivi karibuni. Zaidi ya gridi 6,200 ambazo hujumuisha gridi kubwa kabisa, za biashara na viwanda pamoja na zile ndogo zimethibitishwa kuwepo barani humo.

Kwa kuongezea, mataifa mengine tisa ya Kiafrika, mbali na Afrika Kusini na Misri, yapo njiani kujiunga na 'Gigawatt Club', lebo isiyo rasmi kwa kundi la nchi zilizo na uwezo wa kuzalisha gigawatt moja ya umeme kutokana na jua.

Huang Su, Mkurugenzi wa Huawei katika Biashara ya Umeme Dijitali Kusini mwa Africa, alisema kwamba karibu nusu ya idadi ya watu wasio na uwezo wa kupata umeme duniani wanaishi kusini mwa jangwa la Sahara.

 

"Kwa hivyo kuna haja kubwa na ya dharura ya kuharakisha ukuaji wa nishati mbadala kote katika eneo hilo ili kuhakikisha nishati ya kutosha, nafuu na ya kuaminika kwa Waafrika wote na kwa nchi kupata faida ya uchumi wa kijani." anasema.

Huawei imetumia zaidi ya miaka 30 ya utaalam na uzoefu katika teknolojia ya kidijitali ili kufanya uzalishaji wa umeme wa jua na matumizi kuwa bora zaidi na ya kuaminika kwa gharama ndogo.

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages