BENKI YA NBC YATINGA KIBITI YAWAPA SOMO WAJASIRIAMALI WANAWAKE

  nbc%2B1

Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu (watatukushoto) akipokea msaada wa madawati  viti pamoja na meza 500 kwa ajili ya shule za wilaya hiyo kutoka kwa Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa Benki ya NBC Bw Elibariki Masuke(wa pili kulia) msaada huo ukilenga kuboresha sekta ya elimu  Wengine pichani ni Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe (kushoto),Mkurugenzi wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki ya NBC Bi Neema Singo (wa pili kushoto) pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi CCM Wilaya ya Kibiti Bw Abduljabir Marombwa hafla hiyo imefanyika hivi karibuni wilayani kibiti.nbc%2B3

Mkurugenzi wa Wateja wa wadogo wa benki ya NBC Bw Elibariki Masuke akizungumza na wajasiriamali wanawake wilayani Kibiti wakati wa mafunzo ya kibiashara na ujasiriamali kwa  wanawake wajasiriamali 150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza mitaji yao na benki hiyo.
NBC%2B5
M
eneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya NBC Bw Jonathan Bitababaje akitoa mafunzo kwa wajasiriamali hao.

Kibiti, Pwani:  April 17, 2021: Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) imetoa msaada wa madawati 250, viti viti pamoja na meza 250 wilayani Kibiti mkoni Pwani ikiwa ni sehemu ya Mpango wa kipekee wa uwajibikaji wa Jamii (CSR) ambao unaplenga kuchangia utoaji wa elimu bora nchini.

 

Zaidi, benki hiyo pia imetoa mafunzo ya kibiashara na ujasiriamali kwa  wanawake wajasiriamali 150 wilayani humo ili kuwajengea uwezo wa kuemdesha biashara zao kwa ufanisi huku wakizingatia nidhamu ya fedha kabla hawajapatiwa mikopokwa ajili ya kukuza mitaji yao.

 

Madawati hayo yalikabidhiwa na Mkurugenzi wa Idara ya wateja wadogo wa benki hiyo Bw Elibariki Masuke wakati wa hafla fupi ya makabidhiano iliyofanyika kwenye ofisi ya Mkuu wa Wilaya Hiyo Bw Gullamhussein Kifu . Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Mbunge wa jimbo la Kibiti Bw Twaha Mpembenwe pamoja na maafisa wengine wa wilaya hiyo akiwemo  Mkurugenzi Mtendaji.

 

Bwana Masuke alisema kuwa benki hiyo imejitolea kusaidia katika kuboresha ustawi wa jamii kupitia misaada ya kijamii ikiwemo elimu na kwamba wameguswa sana na suala la changamoto ya madawatikwenye baadhi ya maeneo hapa nchini sababu iliyosababisha wao kuchukua hatua hiyo ili kuboresha  zaidi sekta hiyomuhimu.

 

"Ni furaha kwetu kuwa sehemu ya kutatua changamoto kwenye sekta muhimu kama hii. Kupitia ushirikiano na ushawishi tunaoupata kutoka kwa Mbunge wa Kibiti na ofisi ya Mkuu wa wilaya tunaahidi kuendelea kushirikiana na jamii ya wana Kibiti huku pia tukifikiria namna kufungua tawi letu wilayani  Kibiti kufuatia fursa mbalimbali tunazoziona ikiwemo kilimo na mradi wa kituo cha kupozea umeme wa Mradi wa Bwawa la Mwalimu Nyerere,’’ alisema.

 

Alishauri pia wanafunzi na walimu watakaonufaika na msaada huo kutunza madawati na meza hizo ili viweze kutumika kwa muda mrefu na hivyo kusaidia walengwa wengi zaidi.

 

Kuhusu mafunzo kwa wajasiriamali wanawake  Bwana Masuke alisema kuwa miongoni mwa sababu zinazokwamisha utoaji wa mikopo kwa wajasiriamali wengi ni pamoja na wao kuendesha biashara zao bila kuzingatia misingi ya kifedha ikiwemo kutunza kumbukumbu za mahesabu ikiwemo mapato na matumizi.

 

Kwa mujibu wa Bw Masuke ni kutokana na uwepo wa changamoto hiyo ndio sababu benki hiyo imekuwa ikishirikiana na taasisi nyingine ikiwemo TanTrade, SIDO, VETA na washauri binafsi kuelimisha wajasiriamali kuhusu namna bora ya kusimamia na kuendesha biashara zao ili kuwajengea uwezo kabla ya kuwapatia mikopo.

 

"Tumekuwa tukishirikiana na washirika wengine kutoa mafunzo kwa wajasiriamali na wafanyabiashara kwenye maeneo kama usimamizi wa hesabu, utunzaji wa vitabu na uongozi, ili tuwaweke vizuri kwa ufikiaji rahisi wa mikopo", Masuke alisema.

 

Akizungumza mara tu baada ya kupokea msaada huo Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Bw Gullamhussein Kifu pamoja na kuishukuru benki ya NBC kwa kutoa msaada kwa wakati haswa unaohitajika, aliiomba benki hiyo ifungue tawi lake wilayani humo mapema iwezeknavyo ili iweze kuwasaidia wakulima na wafanyabiashara husani wadogo.

 

"Msaada huu utasaidia kupunguza changamoto ya uhaba wa madawati katika baadhi ya shule zetu…tunashukuru sana NBC tunaomba muendelee kusaidia kwenye maeneo mengine pia ikiwemo sekta ya afya ." Alisema.

 

Akizungumzia mafunzo kwa wajasiriamali wanawake wilayani humo Bw Kifu alitoa wito kwa washiriki kuhakikisha wanayatumia vyema kwa kuwa yanalenga kuwasaidia katika upatikanaji wa mikopo sambamba na kuendesha biashara zao kwa ufanisi na kwa faida

 

“Kibiti ni wilaya  changa inayohitaji watu wake ili kuendelea. Kabla hatujapokea wawekezaji kutoka nje ni lazima tuanze sisi wenyewe humu ndani. Kupitia mafunzo haya tunakwenda kupata wajasiriamali na wafanyabaishara wenye weledi wa kutosha kutambua fursa zilizopo na kuzitumia,’’ alisema.


Kwa upande wake Mbunge wa jimbo hilo Bw Twaha Mpembenwe aliiomba benki hiyo iendelee kuwekeza zaidi wilayani humo kwa kufungua tawi lake sambamba na kuwasaidia wajasiriamali na wakulima hususani wa zao la ufuta pamoja na vijana ambao kwasasa wanakibiliwa na changamoto ya huduma za kifedhaikiwemo mikopo na elimu ya biashara na kilimo cha kisasa.

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages