Benki ya NBC yawafunda Wanawake Kuhusu Ubora wa Bidhaa ya Mikopo

 PIC%2B1.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TABWA) Bi Noreen Mawala (kushoto), akikabidhi zawadi kwa niamba ya wanawake wajasiliamali nchini kwenda kwa Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo (Kulia) na Meneja Bidhaa na Huduma za Kibenki kutoka Benki ya hiyo Bw Jonathan Bitababaje (katikati) ikiwa ni ishara ya kutambua mchango wa benki hiyo katika kuwasaidia na kuwawezesha wanawake wajasiliamali nchini. Makabidhiano hayo yalifanyika jana wakati wa kufunga Maonesho ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC, yaliyofanyika jijini Dar es Salaam.PIC%2B2.Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo akizungumza WANAWAKE WAFANYA BIASHARA  na washiriki wa maonesho hayo waliohudhulia mafunzo ya ujasiliamali yaliyodhaminiwa na benki ya NBC kwa kushirikiana na TABWA pamoja na wadau wengine ili kuwatia shime wanawake katika ujasiliamaliPIC%2B9.

Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo (kushoto), akikabidhi cheti cha ushiriki wa mafunzo hayo kwa mmoja kati ya washiriki  waliohudhuria semina hiyo.


Dar es Salaam: Machi 8, 2021: Wanawake wajasiliamali na wafanyabiashara nchini wameshauriwa kuongeza jitiahada zao zaidi katika kuboresha zaidi mawazo ya biashara sambamba na kuongeza ubora za wa bidhaa zao ili kuongeza ushawishi kwa taasisi za kifedha nchini ziweze kuwakopesha kwa urahisi.


Akizungumza wakati wa kufunga Maonesho ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania yaliyofanyika jijini Dar es Salaam kwa siku nne, Meneja Mahusiano wa Benki ya NBC, Bi Consolatha Shayo alisema taasisi za kifedha zinashawishika zaidi kutoa mikopo kwa kuzingatia ubora wa wazo la biashara na sio jina au jinsia ya mkopaji.


Alisema hiyo ndio sababu benki hiyo imekuwa mstari wa mbele kuhakikisha inaendelea kuwaongezea ujuzi wajasiliamali hao ili kuboresha mawazo na bidhaa zao ili kuwajengea uwezo utakaowezesha kufanya biashara zao kwa weledi na kutengeneza faida itayowawezesha kurejesha mikopo yao.


“Ndio maana kupitia wataalamu ambao tunawatumia kutoa elimu kwa wajasiliamali kupitia maonesho kama haya, tumekuwa tukifundisha na kusisitiza sana juu ya umuhimu wa kujenga zaidi majina ya bidhaa zao kuliko majina yao binafsi kwa kuwa taasisi za kifedha zinatazama zaidi biashara zao na sio jinsia wala majina yao binafsi,’’ alisema  Consolatha.


Pamoja na kudhamini maonesho hayo, benki hiyo pia iliandaa programu kadhaa za mafunzo kwa wajasiliamali ikiwemo kliniki ya biashara kwa kushirikisha taasisi na mamlaka mbalimbali ikiwemo Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (Brela) na Shirika la Viwango Tanzania (TBS).


Zaidi benki hiyo ilitumia fursa hiyo kutangaza huduma zake mahususi kwa ajili ya wanawake na wajasiliamali zikiwemo akaunti za NBC Kua Nasi na akaunti mpya ya Johari.


“NBC Kua Nasi ni akaunti maalum kabisa kwa wote wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo kama vile mama na baba lishe, wenye maduka ya reja reja, wasindikaji wa vyakula na mazao, bodaboda, wazabuni wa taasisi mbalimbali wakati akaunti ya Johari ni mahususi kwa ajili ya wanawake na inawezesha kuweka akiba kidogo kidogo kwa kianzio cha shilingi 10,000 tu. Akaunti zote hizi hazina makato ya mwezi,’’ alisema.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi ya Wafanyabiashara wanawake Tanzania (TABWA) Bi Noreen Mawala ambae taasisi yake ndio iliratibu maonesho hayo pamoja na kuipongeza benki ya NBC pamoja na wadau wengine kwa kufanikisha maonesho hayo, alisema taasisi hiyo kwasasa inaandaa safari ya mafunzo na maonesho ya biashara katika nchi za Oman na Comoro ili kutoa fursa kwa wafanyabiashara hao kutangaza biashara zao katika mataifa hayo.


“Baada ya mafanikio kupitia maonesho haya yaliyokwenda sambamba na maadhimisho ya siku ya mwanamke Duniani  tunatarajia kuwa na safari za maonesho ya biashara zetu katika nchi za Oman na Comoro ili kufungua milango zaidi ya kutangaza biashara zetu nje nchi,’’ alisema.

Share:

BENKI YA NBC YADHAMINI MAONESHO YA WAFANYA BIASHARA WANAWAKE TANZANIA

Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (kushoto), akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa wafanya biashara wanawake yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC yenye kauli mbiu MWANAMKE MILIKI KIWANDA KWA UCHUMI ENDELEVU, maonesho yaliyozinduliwa na waziri huyo katika viwanja vya mlimani city jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho.
Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanya biashara wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki hiyo ambapo katika uzinguzi huo mgeni rasmi alikuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo halfla ya uzinduzi huo umefanyika katika viwanja vya mlimani city jijini Dar es Saalam.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi (Uwekezaji) Kitila Mkumbo (katikati) akipokea zawadi ya kifungashio kilichotengenezwa na wajasiliamali wakitanzania wakati wa hafla ya uzinduzi wa maonesho ya wafanya bishara wanawakeTanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya NBC kutoka kwa Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla (kushoto) ni Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho
Baadhi ya wanawake waliohudhulia hafla ya uzinduzi huo wakifurahia jambo kutoka kwa mgeni rasmi.
Picha ya pamoja waziri pamoja na wadhamini wa maonesho hayo.

Serikali imewataka wanawake kuchangamkia fursa zinazotolewa katika mikoa wanayoishi ili kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili hasa kwenye swala zima la mitaji.

Hayo yameelezwa leo jijini Dar es Salaam na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (uwekezaji), Profesa Kitila Mkumbo ambae pia ni Mbunge wa Jimbo la Ubumgo wakati alipoalikwa kuwa Mgeni rasmi na kuzindua maonyesho ya biashara za wanawake Tanzania yaliyodhaminiwa na Benki ya Taifa ya bishara NBC,kwa lengo mahususi la kuwainua wanawake kiuchumi yanayofanyika Mlimani City kwa siku tatu mfurulizo.

Waziri Mkumbo amesema Serikali kwa kutambua umuhimu na mchango wa maendeleo kwa wanawake kwa Taifa, letu na Serikali inayoongozwa na jemedali wetu Rais John Pombe Magufuli wameanzisha dirisha maalumu la mikopo kwa halmashauri zote nchini kwa ajili ya kuwainua wanawake na vijana.

"Tunatambua jitihada zenu na malengo yenu lakini Serikali tunatoa wito kwa wanawake wote nchini kuchangamkia fursa zinazotolewa kupitia mikoa yao ziweze kuwasaidia kwenye changamoto zinazowakabili,” amesema Waziri Mkumbo.

Waziri huyo pia ameishukuru Benki ya Taifa ya Biashara NBC ambayo ndio mdhamini mkuu wa maonesho hayo kwa uzalendo walioufanya kutambua kuwa hakuna maendeleo bila wanawake na kulibeba hili ili wanawake waweze na vijana waweze kwenda sawa na spidi ya uchumi wa kati na kuzitaka Taasisi nyengine kuiga mfano huo kwani utaleta matokeo nyanya katika sekta ya uwekezaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Chama cha Wafanyabiashara Tanzania (Tabwa), Noreen Mawalla aliiomba Serikali kuwasaidia majengo ya wazi ili wanawake wafanyie biashara zao katika mazingira mazuri na salama yatakayowawezesha kulipa kodi kwa wakati.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Wajasiliamali wa Benki ya Taifa ya Biashara NBC Mussa Mwinyidaho katika uzinduzi huo leo, amemwambia Waziri kuwa lengo kuu la udha mini wa benki hiyo kwa maoneso ya wanawake wafanya biashara tanzania ni kuwawezesha wajasiliamari wadogo na wa kati ambao ndiyo walengwa wakuu wa maonesho haya.

NBC ni Benki inayo wajali wateja wake na watanzania wote kwa ujumla hivyo ili waweze kuwa wafanyabiashara bora nilazima wapate elimu ya kifedha hivyo tunawakaribisha NBC waje wapate elimu pia kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki hiyo alisema mwinyidaho.
Share:

AKIBA COMMERCIAL BANK YAPATA MBIA WA KIMKAKATI (STRATEGIC INVESTOR) AMBAYE NI NATIONAL BANK OF MALAWI YA NCHINI MALAWI

01
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Akiba Commercial Bank, Juliana Swai (kulia), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya kutangaza kuwa Benki hiyo imepata mbia wa kimkakati ambaye ni National Bank of Malawi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Dora Saria.
02
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Akiba Commercial Bank Juliana Swai (kulia), pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Dora Saria wakinyanyua mikono yao kwa pamoja kuashiria mafanikio kwa benki hiyo mara baada ya kumtangaza mbia wao mpya, National Bank of Malawi.

Akiba Commercial Bank (ACB) imepata mbia wa kimkakati (Strategic Investor) ambaye ni National Bank of Malawi (NBM) ya nchini Malawi iliyoingia makubaliano yakuwekeza katika ACB ili kuongeza mtaji wake.

Hii ni mikakati mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya Akiba Commercial Bank ambayo itapelekea kuleta mabadiliko makubwa na yenye tija hasa katika sekta ya kifedha kwa benki hiyo.

Akizungumza na wanahabari makao makuu ya benki hiyo Dar es salaam,  Kaimu Mkurugenzi wa Akiba Commercial Bank Bi. Juliana Swai amesema kupitia mbia huyu Benki hiyo sasa imeweza kuimarisha mtaji wake na kukidhi vigezo vya Benki Kuu hususani swala zima la mtaji wa uendeshaji wa Benki ya Biashara baada ya mbia wake National Bank of Malawi NBM kuwekeza kiasi cha shilingi billion 17 za kitanzania.

Bi swai amesema lengo kuu la mkakati huu ni kuimarisha mtaji wa Benki lakini pia benki imekuwa ikiangalia mahitaji ya soko lake na kuona kuwa kuna haja ya kupata mwekezaji au mbia wa kimkakati kwa ajili ya kuifanya benki iwe imara zaidi na kuweza kuboresha huduma zake na kuanzisha huduma nyingi zaidi ambazo zinahitajika kwenye soko la Tanzania

“Kupitia Ubia huu naomba niwaahidi wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla mabadiliko makubwa na chanya katika huduma zetu na mifumo yetu ya utoaji huduma yanakuja.

Tunaamini kuwa tutaweza kuwahudumia wateja wetu kwa weledi zaidi kupitia utalaamu na uzoefu wa taasisi hizi mbili makini kwenye sekta ya fedha” amesema Bi Juliana Swai.

Ameongeza kuwa benki hiyo inatambua mahusiano mazuri na undugu kati ya nchi hizi mbili ambazo pia zina mahusiano makubwa ya kibiashara na faida mojawapo ya wazi ni kuwepo kwa mazingira wezeshi ya kufanya biashara kati ya nchi hizi mbili kupitia huduma za kifedha ambazo zitapatikana kwa urahisi zaidi.

Bi Juliana amesema aidha uwekezaji huu utasaidia pia kuwepo kwa mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara kwa nchi ambazo zipo kusini mwa bara la Afrika wakiwepo wanachama wa SADC

Malawi ni moja ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika zinazotumia bandari ya Dar es Salaam kama lango kuu la kibishara hii itarahisisha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi wanaotumia bandari ya Dar es Salaam .

NBM ilianzishwa mwaka 1971 baada ya muungano wa Barclays Bank DCO na Benki ya Standard ya Afrika Kusini, ni moja ya benki kubwa nchini Malawi inayotoa huduma za benki ikiwemo rejareja yaani (Personal and Retail banking), wateja wakubwa (Corporate banking), huduma za kibenki za uwekezaji na udalali katika soko la hisa na mitaji.

Sasa Akiba Commercial Benki imekuwa mhimili imara katika sekta ya fedha na imefungua ukurasa mpya kibiashara. Nawakaribisha Watanzania wote wafike Akiba Commercial Bank ili waweze kufaidika na fursa mbalimbali kwa maendeleo ya maisha yao na biasharazao

Akiba Commercial bank ni Benki ya biashara ambayo tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1997 imekuwa ikitoa huduma zake kwa wateja wengi wakiwani wajasiriamali wadogo, wakati na wajuu;yaani Micro, Small and Medium entrepreneurs (MSMEs)

Benki imeweza kuwafikia zaidi ya Watanzania 200,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, na Dodoma. Watanzania hawa wameweza kufaidika na huduma za mikopo mbalimbali ya kijasiriamali,pamoja na kuweka amana zao benki kwenye akaunti kulingana na matakwa yao. Aina za akaunti ni kuanzia zawatoto wadogo, vijana,watu wazima, na za biashara na makampuni. Aidha, huduma za benki kupitia simu za mikononi yaani Akiba Mobile zimeleta unafuu na urahisi zaidi katika kuwafikia wateja wetu popote pale walipo.

 

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages