AKIBA COMMERCIAL BANK YAPATA MBIA WA KIMKAKATI (STRATEGIC INVESTOR) AMBAYE NI NATIONAL BANK OF MALAWI YA NCHINI MALAWI

01
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Akiba Commercial Bank, Juliana Swai (kulia), akizungumza na wanahabari wakati wa hafla ya kutangaza kuwa Benki hiyo imepata mbia wa kimkakati ambaye ni National Bank of Malawi. Kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Dora Saria.
02
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Akiba Commercial Bank Juliana Swai (kulia), pamoja na Mkuu wa Kitengo cha Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo, Dora Saria wakinyanyua mikono yao kwa pamoja kuashiria mafanikio kwa benki hiyo mara baada ya kumtangaza mbia wao mpya, National Bank of Malawi.

Akiba Commercial Bank (ACB) imepata mbia wa kimkakati (Strategic Investor) ambaye ni National Bank of Malawi (NBM) ya nchini Malawi iliyoingia makubaliano yakuwekeza katika ACB ili kuongeza mtaji wake.

Hii ni mikakati mbalimbali ya kimaendeleo ndani ya Akiba Commercial Bank ambayo itapelekea kuleta mabadiliko makubwa na yenye tija hasa katika sekta ya kifedha kwa benki hiyo.

Akizungumza na wanahabari makao makuu ya benki hiyo Dar es salaam,  Kaimu Mkurugenzi wa Akiba Commercial Bank Bi. Juliana Swai amesema kupitia mbia huyu Benki hiyo sasa imeweza kuimarisha mtaji wake na kukidhi vigezo vya Benki Kuu hususani swala zima la mtaji wa uendeshaji wa Benki ya Biashara baada ya mbia wake National Bank of Malawi NBM kuwekeza kiasi cha shilingi billion 17 za kitanzania.

Bi swai amesema lengo kuu la mkakati huu ni kuimarisha mtaji wa Benki lakini pia benki imekuwa ikiangalia mahitaji ya soko lake na kuona kuwa kuna haja ya kupata mwekezaji au mbia wa kimkakati kwa ajili ya kuifanya benki iwe imara zaidi na kuweza kuboresha huduma zake na kuanzisha huduma nyingi zaidi ambazo zinahitajika kwenye soko la Tanzania

“Kupitia Ubia huu naomba niwaahidi wateja wetu na Watanzania wote kwa ujumla mabadiliko makubwa na chanya katika huduma zetu na mifumo yetu ya utoaji huduma yanakuja.

Tunaamini kuwa tutaweza kuwahudumia wateja wetu kwa weledi zaidi kupitia utalaamu na uzoefu wa taasisi hizi mbili makini kwenye sekta ya fedha” amesema Bi Juliana Swai.

Ameongeza kuwa benki hiyo inatambua mahusiano mazuri na undugu kati ya nchi hizi mbili ambazo pia zina mahusiano makubwa ya kibiashara na faida mojawapo ya wazi ni kuwepo kwa mazingira wezeshi ya kufanya biashara kati ya nchi hizi mbili kupitia huduma za kifedha ambazo zitapatikana kwa urahisi zaidi.

Bi Juliana amesema aidha uwekezaji huu utasaidia pia kuwepo kwa mazingira wezeshi ya ufanyaji biashara kwa nchi ambazo zipo kusini mwa bara la Afrika wakiwepo wanachama wa SADC

Malawi ni moja ya nchi zilizoko kusini mwa Afrika zinazotumia bandari ya Dar es Salaam kama lango kuu la kibishara hii itarahisisha huduma za kifedha kwa wafanyabiashara wa Tanzania na Malawi wanaotumia bandari ya Dar es Salaam .

NBM ilianzishwa mwaka 1971 baada ya muungano wa Barclays Bank DCO na Benki ya Standard ya Afrika Kusini, ni moja ya benki kubwa nchini Malawi inayotoa huduma za benki ikiwemo rejareja yaani (Personal and Retail banking), wateja wakubwa (Corporate banking), huduma za kibenki za uwekezaji na udalali katika soko la hisa na mitaji.

Sasa Akiba Commercial Benki imekuwa mhimili imara katika sekta ya fedha na imefungua ukurasa mpya kibiashara. Nawakaribisha Watanzania wote wafike Akiba Commercial Bank ili waweze kufaidika na fursa mbalimbali kwa maendeleo ya maisha yao na biasharazao

Akiba Commercial bank ni Benki ya biashara ambayo tangu kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1997 imekuwa ikitoa huduma zake kwa wateja wengi wakiwani wajasiriamali wadogo, wakati na wajuu;yaani Micro, Small and Medium entrepreneurs (MSMEs)

Benki imeweza kuwafikia zaidi ya Watanzania 200,000 katika mikoa ya Dar es Salaam, Arusha, Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro, na Dodoma. Watanzania hawa wameweza kufaidika na huduma za mikopo mbalimbali ya kijasiriamali,pamoja na kuweka amana zao benki kwenye akaunti kulingana na matakwa yao. Aina za akaunti ni kuanzia zawatoto wadogo, vijana,watu wazima, na za biashara na makampuni. Aidha, huduma za benki kupitia simu za mikononi yaani Akiba Mobile zimeleta unafuu na urahisi zaidi katika kuwafikia wateja wetu popote pale walipo.

 

Share:

No comments:

Post a Comment

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages