NBC yadhamini Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma

Naibu Waziri  wa Wizara ya Viwanda,  Biashara na Uwekezaji Mhandisi Stella Manyaya (kulia), akisalimiana na Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Maonyesho hayo yalifanyika katika viwanja vya Majimaji mjini Songea mkoani Ruvuma.
 
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda,  Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akisaini kwenze kitabu cha wageni alipotembelea banda la Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambayo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Maonesho hayo yalifanyika katika Viwanja vya Majimaji mjini Songea MKoani Ruvuma mwishoni  mwa wiki. Wengine kushoto kwa waziri ni Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale, Ofisa Mauzo, Jennifer Peter, pamoja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC, Hilaria Mhagama.
Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na Ofisa Huduma kwa Wateja wa Benki ya NBC, Hilaria Mhagama alipotembelea banda la Benki ya NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini.  Wa pili kushoto ni  Meneja wa Benki ya NBC Tawi la Songea Simon Ntwale, na Ofisa Mauzo wa benki hiyo, Jennifer Peter.

Naibu Waziri wa Wizara ya Viwanda, Biashara  na Uwekezaji, Mhandisi Stella Manyaya (kushoto), akishikana mikono na Ofisa Mauzo wa Benki ya NBC  Tawi la Songea, Jennifer Peter  alipotembelea banda la NBC wakati wa Maonesho ya Viwanda na Kongamano la Uwekezaji Ruvuma ambapo NBC ilikuwa ni mmoja wa wadhamini. Wa pili kushoto  ni  Meneja wa NBC Tawi la Songea, Simon Ntwale pamoja na Ofisa Huduma kwa Wateja wa NBC Songea, Hilaria Mhagama.

Naibu Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Mhandisi Stella Manyanya amesema Maonesho ya Viwanda na kongamano la uwekezaji Ruvuma litaleta fursa nyingi za kibiashara na uchumi mkoani humo imeelezwa mjini Songea mwishoni mwa wiki.

Alisema Mkoa wa Ruvuma umejaliwa kuwa na fursa nyingi sana na kwa muda mrefu hawakuwa wakifanya tukio kama hilo lakini sasa kupitia kongamano hilo litawafungua  kuwafahamisha watu mbalimbali kuwa nini kinapatikana mkoa huo wa Ruvuma.

Alisema changamoto zinazowakabili wawekezaji wadogo ni pamoja na upatikanaji wa mitaji  lakini kwa sasa mkoa wa Ruvuma umepata mkombozi hususani Benki ya NBC ambayo inatoa mikopo mikubwa na midogo kwa masharti nafuu sana kinachotakiwa ni uaminifu.

 "Nawakaribisha sana wawekezaji na wadau wote ambao wana nia thabiti ya  kuja kuwekeza Ruvuma kwani mkoa huu umekuwa na nishati ya umeme ya kuridhisha inayoweza kukidhi mahitaji," alisema.

Kwa upande wake Meneja wa Tawi la NBC Songea,Simon Ntwale amesema kuwa maonesho hayo yamekuwa fursa nzuri kwa Benki ya  NBC kwa sababu wameweza kukutana na wadau mbalimbali watakaoweza kufungua fursa mbalimbali za kibiashara.aziri Mkuu na Mkuu wa Mkoa huo amesema kuwa Ruvuma itakuwa na  wawekezaji mbalimbali.

Alisema NBC imepata faida ya kuingia mkataba na taasisi ya PASS ambapo wanakwenda kuwawezesha wakulima kupata mikopo ya kilimo ambapo mkopaji anaweza kupata pembejeo za kilimo.

Ntwale pia amewatoa shaka wakulima wakubwa na wadogo pamoja na wachakataji na wawekezaji wadogo kujitokeza kwa wingi ili kupata mkopo endapo kampuni ya PASS  itakuwa imeadhinisha kwa mteja husika kupata mkopo huo.

 "Wawekezaji na wakulima wadogo msiogope kuitumia Benki ya NBC kwani ni benki yenu ambayo ipo tayari  kuwasaidia ili mtimize malengo yenu kwani wengi wamenufaika na mikopo hiyo hadi sasa wanafanya biashaza za mazao yao hadi nje ya nchi," alisema.
Share:

Uzinduzi wa reli ya Tanga- Moshi utaongeza kipato kwa mikoa ya kaskazini


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Martin Shigela (kulia), akimsikiliza Meneja Kiwanda cha Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wa pili kushoto) katika hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor na Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Agnes Hokororo.
Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Diana Malambugi akishikana mikono na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Massanja Kadogosa (kulia) wakati wa hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor, Meneja Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema na Meneja Mauzo Taifa wa kampuni hiyo, Leslie Massawe.

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Massanja Kadogosa (kulia) akishikana mikono na Meneja Mauzo Taifa wa kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Leslie Massawe wakati wa hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.Wengine kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano na Mawasiliano ya Nje wa Tanga Cement, Bi. Mtanga Noor, Meneja Kiwanda cha Tanga Cement, Mhandisi Ben Lema, Meneja Rasilimali watu wa Kampuni ya Tanga Cement, Diana Malambugi na Meneja Biashara wa Kampuni hiyo, Peet Brits.

Meneja Kiwanda cha Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema akizungumza wakati wa hafla ya ufunguzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki. Kulia ni Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo.

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa (katikati) akipunga mkono kwa baadhi ya wakazi na mashuhuda wengine waliofika katika uzinduzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wakazi wa Moshi na wananchi wengine wakiangalia treni la kwanza la mizigo lililobeba saruji ya Tanga Cement baada ya kuwasili katika  stesheni ya Moshi wakati wa uzinduzi wa safari za treni hiyo litakalofanya safari zake katika reli ya Dar- Tanga- Kilimanjaro. Uzinduzi huo ulifanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya Tanga (TCPLC) pamoja na washuhudiaji wengine wakihudhuria uzinduzi wa safari za treni za mizigo katika reli ya Dar - Tanga - Kilimanjaro uliofanyika mjini Moshi, Kilimanjaro mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Uzinduzi wa reli ya Tanga - Moshi utaongeza kipato kwa mikoa ya kaskazini

Na Mwandishi wetu, Moshi

Uzinduzi wa huduma za reli kati ya Tanga na Moshi utaongeza kipato kwa mikoa miwili hiyo, kuchagiza kukua kwa sekta  ya ujenzi majumba  na zaidi kuifanya Tanga ijitwalie hadhi yake ya zamani enzi za  kilele cha zao la katani katika soko la dunia, ambapo Tanga ulikuwa  ni mji maarufu, amesema Mkurugenzi Mtendaji wa Tanga Cement  Reinhardt Swart akiongea kuhusu uzuduzi huo.

Kampuni ya Tanga Cement ilikuwa ni mteja wa kwanza wa huduma hizo mpya ambazo zilisita miaka 12 iliyopita, ambapo treni hiyo iliwasili katika stesheni ya treni ya moshi mjini ikikokota mabehewa yaliyosheheni jumla ya tani 800 kwa mpigo, mzigo ambao ni swan a ule ambao ungesafirishwa na malori 30.

“Ninaamini usafirishaji kwa urahisi wa  bidhaa kati ya vituo hivyo viwili utaongeza kiwango cha watu kuzalisha kipato kwa mikoa yote miwili. Sisi tunahitaji watu wengi zaidi wajipatie pesa mifukoniu mwao ambayo itawasaidia kujenga nyumba bors ambazo bila shaka zinahitaji aruji, hivyo tutaongeza mauzo yetu, kuonheza kipato cha wanahisa wetu kupitia gawio, serikali ya Tanzania itavuna kodi ambayo itasaidia  katika maendeleo ya nchi,” alisema mkurugenzi huo.

Aliongeza kuwa Tanga ni eneo muhimu la kiuchumi  na ina miundombinu yote muhimu ambayo ni bandari, barabara na reli. Wahusika wakivisimamia hii miundombinu vyema na kuitumia ipasavyo, alisema ana uhakika kuwa ‘ baada  ya mika michache, tanga itakuwa zaidi ya ilivyokuwa enzi zake za kilele cha katani, kitu kilichofanya Tanga uwe ni mji maarufu  nchini Tanzania na Afrika Mashariki.

Kampuni ya Tanga Cement ni kati ya wateja wakubwa wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRC) na mwaka 2016 illisaini mkataba wa iliyokuwa TRL kuwezesha usafirishaji wa saruji kutoka Tanga Cement kuwaendea wateja wa kampuni hiyo waliopo mikoa ya Mwanza na Kigoma.  

Mkataba huo wa makubaliano ulitiwa saini ili kuwezesha usafirishaji wa zaidi ya tani 35,000 za saruji kwa mwezi. Kampuni ya Tanga cement ilitengewa vichwa vitano vya treni na kichwa cha treni cha kupangia mabehewa ili kuwezesha usafirishaji watani 20,000 kwa mwezi kutoka Ponge hadi kigoma, na tani 15,000 kwenda mwanza.

“Hii ilikuwa ni hatua muhimu ya mafanikio katika kupatia ufumbuzi usafirishaji wa saruji. Tumejenga uhusiano mzuri sana na TRC ambapo tunakutana mara kwa mara  kuhakikisha kuwa kila jambo linakwenda sawia hasa kuhusiana na utekelezaji wa mkataba huo  wa makubaliano na tunatoa mapendekezo yanapohitajika na kushauri marekebisho ya hapa na pale, aliongeza Ndugu Swart.

Kukua kwa ujenzi wa mjumba mbao mkurugezi huyo wa Tanga cement  anautabiri siyo ndoto ya alinacha, kwa kuwa wadau wanakubaliana kuwa  matumizi ya reli katika kusafirisha saruji kutapunguza gharama za usafirishaji wa bidhaa hiyo muhimu kwa ujenzi, na hivyo kusababisha bei ya saruji kushuka.

Akiongea katika uzinduzi huo, Mgeni Rasmi Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alisema kuwa wachambuzi wa kimataifa wanakadiria kuwa kutumia reli badala ya barabara kunapunguza gharama za usafirishaji kwa  kiwango cha asilimia 30-40.

Kwa mujibu wa wadau wa sekta ya usafirishaji, kusafirisha tani moja ya saruji kutoka Tanga hadi Moshi kwa barabara kunagharimu Tsh 40,000, wakati reli inakadiriwa kugharimu Tsh 28,000. Tanga Cement yenyewe inatarajia kusafirisha jumla ya tani 1,600 kwa wiki na 80,000 kwa mwaka kutoka kiwandani Tanga hadi Moshi.

Waziri Mkuu Majaliwa Alisema “Usafiri wa reli ni kichocheo kikubwa cha ukuaji wa uchumi nchini, kwa kutumia reli, inawezekana kusafirisha  bidhaa nyingi kwa wakati moja. Nina hamu ya kuona kuwa watu wanatumia fursa hii ya huduma ya reli kuagiza bidhaa, na bila shaka bei ya bidhaa itapungua”

Akiongea katika hafla hiyo ya uzinduzi, Mwenyekiti wa Bodi wa TRC Prof. Kondoro, naye alichangia swala la reli kupunguza gharama, na akasema kuwa kuziduliwa kwa huduma za reli kati ya Tanga na Moshi ni sehemu ya mkakati wa serikali na TRC kuhakikisha kuwa gharama za usafirishaji wa bidhaa zinapungua, kama njia ya kusaidia kufikia uchumi wa kati unaotegemea viwanda.

Alisema Prof. Kondoro “Uzinduzi huu ni  sehemu ya mkakati madhubuti wa kuona kwamba tunasafirisha bidhaa kwa gharama nafuu, na kwa kuwa kutumia reli kunapunguza gharama za usafirishaji, hii itasababisha bei za bidhaa kushuka sokoni.  

Kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa TRC Masanja Kadoigosa, kwa mara ya mwisho treni ya mizigo kwenda Moshi kutokea Tanga, umbai wa km 438, ilikuwa mwaka 1993, huku treni ya abiria ikisitisha safari zake  mwaka 1994.

Ujenzi upya wa reli  ya  Tanga – Moshi ulianza mwaka 2017 na kukamilika mwaka 2019, na ulijumuisha wafanyakazi 525, wahandisi 12, vibarua 466 na wafanyakazi maalum 47, huku mitambo zaidi ya 43 ya aina mbalimbali ikitumika, alisema Kadogosa.




Mtandao wa reli Tanzania umetambaa juu ya jumla ya maili 2707, ukipita juu ya madaraja  zaidi ya 3,000 na vituo 126, alisema mkurugenzi huyo wa TRC ndugu Kadogosa.
Share:

BENKI YA NBC YATOA SHILINGI BILIONI 2.1 KUKOPESHA WASTAAFU

Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Venance Mashiba (wa pili kulia), na Mkurugenzi Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa (kulia kwake), wakikata keki kusherehekea uzinduzi rasmi tawi jipya la Benki ya NBC Tegeta katika jengo la Kibo Complex, nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam hivi karibuni. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Kitengo cha Makampuni, Linley Kapya, Mnadhimu Mkuu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Joyce Mbago, Meneja wa Tawi la Tegeta, Edward Chibombo na Mkurugenzi wa Fedha, Waziri Barnabas.
Meneja wa Kanda ya Mashariki wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC), Venance Mashiba (wa nne kushoto), na Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa (kushoto kwake), wakikata utepe kuzindua rasmi tawi jipya la Benki ya NBC Tegeta nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam. Wengine kutoka kushoto ni, Mkurugenzi wa Kitengo cha Makampuni, Linley Kapya, Mnadhimu Mkuu Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu wa benki hiyo, Joyce Mbago, Mkurugenzi wa Fedha, Waziri Barnabas na Meneja wa Tawi la Tegeta, Edward Chibombo.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Gaudence Shawa, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Tawi jipya la benki hiyo la Tegeta katika jengo la Kibo Complex jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Wateja Binafsi wa NBC, Gaudence Shawa (katikati waliokaa) Mkurugenzi wa Kitengo cha Makampuni, Linley Kapya (kulia kwake) na Mkurugenzi wa Fedha, Waziri Barnabas (kushoto kwake), wakiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi katika tawi hilo na baadhi ya maofisa wa NBC katika hafla hiyo.
Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) nchini imetoa mikopo yenye jumla ya kiasi cha shilingi Billioni 2.1 kwa wastaafu tokea ilipozindua huduma ya mikopo ya wastaafu Juni mwaka jana.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo, Theobald Sabi, Mkurugenzi wa Wateja Binafsi, Bw Gaudence Shawa katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Tawi jipya la Benki hiyo la Tegeta Kibo Commercial Complex alisema kwamba benki hiyo imewatambua wastaafu kama kundi muhimu la kiuchumi.

“NBC tumewatambua wastaafu wanaopokea pensheni kama kundi la kiuchumi ambalo lina uwezo wa kuchangia katika uchumi wa taifa letu kwa kuwezeshwa kifedha,” 

“Kikwazo kikubwa, kwa siku za huko nyuma, ilikuwa kutokuwepo kwa bima ya mikopo kwa watu waliovuka umri wa miaka 60, sasa ipo bima inayowakinga wastaafu waliovuka umri huo hapa nchini,” aliongeza alipozungumza na wageni waalikwa jana kwenye hafla ya uzindi.

Alifafanua kwamba kwa kutambua umuhimu wa wafanyabiashara wadogo na wakati, mnamo mwaka 2016, uongozi wa benki hiyo uliunda kurugenzi maalum ya kuhudumia wateja hao na hadi mwezi machi mwaka huu benki hiyo imeshatoa jumla Tsh 155 billioni kama mikopo kwa wafanyabiashara 3,000 nchini.

Aliongeza kwamba benki hiyo kwa kushirikiana na Shirika la Fedha la Kimataifa (IFC) ambayo Benki tanzu ya Benki ya Dunia imefanya mapitio ya kina ya utaratibu mzima wa utoaji wa mikopo katika kundi hilo ili waweze kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa viwanda nchini.

Bw Shawa alifafanua kwamba kupitia hotuba ya mkurugenzi mtendaji alisema benki hiyo imewawezesha wateja binafsi takribani 27,000 kwa mikopo isiyokuwa na dhamana yenye thamani Tsh 337,000 kati ya hao 53% ni watumishi wa serikali na 47% ni kutoka sekta binafsi.

“Azma ya benki hii ni kuwakuza wafanyabishara wadogo hadi wafikie hatua ya kuchangia katika uchumi wa Tanzania na katika kutimiza lengo hilo benki hii imezindua klabu za biashara zijulikanazo kama ‘Business Clubs” katika mikoa mbali mbali nchini,” alisema.

Alisema kwamba dhumuni la kuanzisha Klabu hizo ni kuwajengea uwezo wafanyabiashara hao kwa mafunzo maalum ya kuendesha biashara zao kwa njia ya kisasa na kuongeza uzalishaji, faida na tija ya uendeshaji.

Bw Shawa aliongeza kwamba mafunzo hayo yanaratibiwa na benki hiyo kwa kushirikiana na taasisi kadhaa kama vile Mamlaka ya Biashra Tanzania, Kituo cha Uwekezaji (TIC), Shirika la Kuendeleza Viwanda Vidogo (SIDO), Chama cha wenye Viwanda na Kilimo Tanzania (TCCIA) na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

Pamoja na mambo mengine hadi kufikia disemba mwaka jana benki hiyo ilikuwa imetoa mafunzo hayo kwa takribani wafanyabiashara 7,000 na lengo ni kuwafikia zaidi ya 1,000.

Aliongeza kwamba benki hiyo ni mojawapo wa benki hapa nchini iliyojiunga na mfumo wa Kukusanya Fedha za Umma (GePG) mwaka jana na hadi kufikia disemba 2018, ilikuwa imekusanya maduhuli ya serikali Tsh 201 billioni ikionyesha ukusanyaji wa wastani Tsh 16 billioni kwa mwezi.

Benki hiyo ni moja ya taasisis za fedha kongwe nchini iliyoanzishwa kwa sheria namba 1 ya 1967 iliyopitishwa na bunge la Tanzania kwa lengo la kupeleka huduma za kibenki kwa watanzania na hivyo kwa kuwawezesha wananchi kiuchumi.
Share:

TIMU ZILIZOFUZU KWENDA NUSU FAINALI KOMBE LA PROPHET SUGUYE ZATAMBIANA

Beki wa Msongola Joging FC Mark Mome, akimdhibiti Mshambuliaji wa Fair Play FC wakati wa mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule ambapo katika mchezo huo Fair Play iliibuka na ushindi wa 7-6 kwa mikwajui ya penati mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mlinda mlango wa Msongola Joging Fc akijaribu kuufuata mpira amb ao ulimshinda nguvu nakwenda chini wakati wamchezo wao dhidi ya Fair Play FC wakati wa mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule ambapo katika mchezo huo Fair Play iliibuka na ushindi wa 7-6 kwa mikwaju ya penati mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Wachezaji wa timu hizo wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule ambapo katika mchezo huo Fair Play iliibuka na ushindi wa 7-6 kwa mikwaju ya penati mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Nahodha na Mshambuliaji wa timu ya Kivule Forest FC Jovin Baroteli, mwenyejezi nyeupe akijaribu kuwatoka Mabeki wa Biashara FC wakati wa mchezo wao katika ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya Shule ya Msingi Misitu Kivule, nje kidogo ya jiji la Dar es Salaam ambapo mchezo huo umemalizika kwa timu ya Kivule Forest kuibuka na ushindi wa 3-1 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mlinda mlango wa Biashara FC akikamata mpira uliopigwa na mshambuliaji wa Kivule Forest, Jovin Baloteli, wakati wa mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule ambapo ambapo mchezo huo umemalizika kwa timu ya Kivule Forest kuibuka na ushindi wa 3-1 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Wachezaji wa timu hizo wakiwania mpira wakati wa mchezo huo.
Share:

LIGI YA PROPHET SUGUYE YAFIKIA HATUA YA ROBO FAINALI UKIPIGWA NJE


Beki wa machimbo FC Ekson Kavali, (katikati), akijaribu kumtoka Mshambuliaji wa Magereza FC, Frank William (kushoto), wakati wa mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule, ambapo katika mchezo huo Magereza iliibuka na ushindi wa 1-0 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mlinda mlango wa Machimbo FC, Dotto Doto,  akikamata mpira wakati wamchezo wao dhidi ya Magereza FC katika mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule, ambapo mchezo huo umemalizaka  Magereza ikiibuka na ushindi wa 1-0 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Wachezaji wa timu hizo wakiwania mpira wakati wa mchezo wa ligi ya Prophet Suguye Cup inayoendelea katika viwanja vya shule ya Msingi Misitu Kivule ambapo katika mchezo huo Magereza iliibuka na ushindi wa 1-0 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Wachezaji wa Magereza FC wakishanvilia baada yakupata goli lao la kwanza amabalo ndio lilikuwa la ushindi katika mchezo huo.
Share:

BENKI YA BIASHARA YA DCB YAJIKITA KWENYE VIWANDA NA KILIMO YAJA NA BIDHAA MAHUSUSI IJULIKANAYO DCB SOKONI KUWAWEZESHA WATANZANIA KIUCHUMI

Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, James Ngaluko (kulia) na Mkurugenzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni, Callington Kayuni (kushoto) wakiangalia mchele baada ya kutoka katika mashine wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichojengwa kwa mkopo kutoka DCB. Uzinduzi huo ulifanyika pamoja na uzinduzi wa huduma ya DCB Sokoni, kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani  Songwe mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, James Ngaluko, akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni uliofanyika pamoja na uzinduzi wa bidhaa  ya DCB Sokoni kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani  Songwe mwishoni mwa wiki. Kiwanda hicho kimejengwa kwa mkopo kutoka DCB. Kushoto ni kurugenzi wa kiwanda hicho, Callington Kayuni na kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Mikopo Midogo wa DCB, Haika Machaku na Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo, Rahma Ngassa.
Kaimu Mkurugenzi Wilaya ya Mbozi, Richard Mwailanga (kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni kilichojengwa kwa mkopo kutoka Benki ya DCB. Uzinduzi huo uliofanyika pamoja na bidhaa ya DCB Sokoni, kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani  Songwe mwishoni mwa wiki. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa kiwanda, Kallington Kayuni na Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James Ngaluko.
Mkurugenzi wa kiwanda cha kukoboa mpunga cha Kayuni, Callington Kayuni akionyesha Mchele baada ya kutoka katika mashine kwa Mkurugenzi wa Biashara wa Benki ya DCB, James Ngaluko (kulia) na kwa wahudhuriaji wegine, wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichojengwa kwa mkopo kutoka DCB. Uzinduzi huo ulifanyika pamoja na uzinduzi wa bidhaa ya DCB Sokoni, kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani  Songwe mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Biashara DCB, Rahma Ngassa (kutoka kushoto waliosimama), Mkurugenzi wa Mikopo Midogo, Haika Machaku na Mkurugenzi wa Biashara wa DCB, James Ngaluko wakiangalia mchele baada ya kutoka katika mashine yan kukoboa wakati wa uzinduzi wa kiwanda hicho kilichojengwa kwa mkopo kutoka DCB. Uzinduzi huo ulifanyika pamoja na uzinduzi wa bidhaa ya DCB Sokoni,  kiwandani hapo Mlowo, Mbozi mkoani  Songwe mwishoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Mikopo Midogo wa DCB, Haika Machaku (kushoto), akisalimiana na mmoja wa wakazi wa Wilaya ya Mbozi waliohudhuria uzinduzi wa kiwanda hicho uliofanyika paoja na uzinduzi wa bidhaa ya DCB Sokoni ya benki hiyo.

KATIKA kuhakikisha azma ya serikali ya awamu ya tano ya kuwa na uchumi wa kati unaotegemea viwanda ifikapo Mwaka 2025 inatimia, Benki ya Biashara ya DCB imeingia na mpango kabambe wa kuviwezesha viwanda vya kilimo kwa kuja na bidhaa maalum ya DCB SOKONI ambayo inatoa suluhisho la kudumu kwa wakulima na wenye viwanda huku ikilenga kuwawezesha wakulima na wafanyabiashara kiuchumi.

Bidhaa hii mpya itamuwezesha mfanyabiashara mwenye azma ya kufungua viwanda vya kilimo kupata mikopo ya kuanzisha viwanda vya kilimo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa bidhaa hiyo ukiofanyika pamoja na uzinduzi wa kiwanda kipya cha kukoboa mpunga cha mteja wao Bwana Callington kayuni, kilichopo katika kijiji cha Mlowo Mbozi Mkoa wa Songwe juzi, Mkurugenzi wa Biashara wa benki hiyo, James Ngaluko alisema ‘tunayo furaha kubwa leo kushiriki kwenye uzinduzi huu muhimu na wa tija wa kiwanda hichi kikubwa na cha kisasa cha kukobolea mpunga kilichojengwa kwa uwezeshwaji mkubwa wa Benki ya biashara ya DCB, tunaamini kiwanda hichi kitakuwa mkombozi wa kweli kwa wakulima wanaofanya shughuli zao za kilimo katika kijiji hichi na vijiji vilivyopo karibu na hapa.

Mkurugenzi huyo alisema kuwa kwa kuleta bidhaa hii mahususi ya DCB Sokoni, itawawezesha wafanyabiasha na wakulima sasa kufanya mapinduzi ya kweli kiuchumi kwa kutegemea kilimo pamoja na minyororo ya thamani kwani kupitia DCB  tunakuongezea thamani ya mazao ya mkulima.

Alizitaja njia ambayo bidhaa ya DCB Sokoni itamuwezesha mteja kuwa ni pamoja na Kujenga kiwanda, kununua na kusafirisha mazao kutoka shambani, kuuza mazao ghafi au Kuchakata mazao na kuyaongezea thamani, usambazaji kwenda sokoni kwa wateja, ulinzi kutokana na bima ya maisha, kiwanda, pamoja na  mazao ghalani katika kipindi chote cha mkopo, ununuaji wa nyumba ya makazi (Mortgage loan) utakaomwezesha kulipa taratibu kwa kipindi kirefu, ununuaji wa pembejeo kwa wafanyabiashara wa pembejeo na zana za kilimo, ubadilishaji wa fedha za kigeni zitokanazo na mauzo ya mazao na uwekezaji wa fedha kwa faida nzuri kupitia huduma ya DCB Lamba Kwanza.

“Natoa wito kwa wateja  na wasio wateja kujiunga na DCB sokoni kwani tunatoa mikopo ya bei nafuu sana ambapo mkulima, mfanya biashara hawezi kushindwa kulipa na pia tunatoa thamani kwa mazao yako ili mteja aweze kushindana kwenye soko na bidhaa zake zinufaike na mnyororo wa thamani”, aliongeza Bwana Ngaluko.
Pamoja na hayo alisema uwezeshwaji wa viwanda vya kilimo kama ilivyo katika kiwanda hichi cha mteja wetu cha kukoboa mpunga, utachangia kwa kiasi kikubwa kasi ya uwekezaji kwa watanzania. Vilevile uwezeshaji huu utasaidia pia kuongeza kiasi cha mazao ya biashara yanayouzwa nje ya nchi, mazao ya biashara kama pamba, kahawa, korosho na mengineyo, hivyo kutuletea fedha za kigeni na kuinua pato la Taifa.

“Ni matumaini yetu wakulima na wafanyabiashara wa mkoa wa Songwe na maeneo jirani wataleta mazao yao katika kiwanda hiki hivyo kuweza kupata chakula na biashara itakayowaongezea kipato na kuinua maisha yao.

“Benki inaunga mkono juhudi za serikali katika kuiwezesha sekta ya kilimo kifedha, sekta hii inakabiliwa na changamoto nyingi, baadhi ikiwa ni ukulima unaotegemea mvua za msimu na changamoto za upatikanaji wa masoko, kupitia DCB Sokoni ni imani yetu tutaweza kuleta ufumbuzi wa baadhi ya  changamoto hizo,” alisema mkurugenzi huyo.

Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi na Mmiliki wa kiwanda hicho, Callington Kayuni aliishukuru Benki ya DCB kwa uwezeshaji wa kifedha alioupata uliowezesha ujenzi wa kiwanda hicho kutoka hatua ya awali mpaka mwisho kiwanda chenye uwezo wa kukoboa hadi magunia 350 kwa siku.

“Nilipeleka michanganuo ya kuomba msaada wa kifedha katika Taasisi nyingi za Fedha, naishukuru DCB kwasababu walilipokea andiko langu kwa mikono miwili na matokeo yake ndio haya ambayo kila mmoja wenu anashuhudia kwa macho yake uwekezaji huu tulioufanya hapa Karacha, wilayani Mbozi,” alisema.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alitaja changamoto ya masoko kuwa ni moja ya mambo yayozorotesha ufanisi wa kiwanda kwani wakulima wanaoleta mpunga kukobolewa kiwandani hapo hutegemea kupata soko hapo hapo la mchele hivyo wapo mbioni kuomba mkopo wa kifedha kutoka DCB utakaowezesha suala hilo.

Naye Richard Mwailanga aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa Wilaya ya Mbozi katika hafla hiyo alisema serikali katika wilaya ya Mbozi inaunga mkono juhudi za Taasisi za Fedha Kama DCB katika uwezeshaji wa viwanda kwani viwanda hivyo vinasaidia kuongeza mapato na pia kukuza uchumi kwa wakazi wa eneo hilo.

Pamoja na hayo aliongeza uanzishwaji wa viwanda kama hivyo utapunguza changamoto iliyopo sasa ya wakulima kuuza mazao yao yakiwa hayajatayarishwa jambo linalofanywa mazao yao kuuzwa kwa bei ya chini.

“Wakulima wengi wa Mbozi wangependa pia kuchukua mikopo kama alivyofanya Bwana Kayuni baadhi wanaogopa kutokana na hofu ya urejeshaji wa mikopo na riba, natoa wito kwa taasisi za fedha kuweka utaratibu rafiki katika eneo hilo hususani katika mikopo inayowahusu wakulima na kilimo,”. Aliongeza
Share:

TLED yawawezesha Wajasiriamali wadogo kushiriki maonyesho ya SABASABA

Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael (katikati),  akipata maelezo kutoka kwa mmoja mjasiliamali mdogo na wawanufaika wa mradi huo Anchila Petro (kulia), wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam. (Kushoto)  ni Mjasiliamali na mnufaika wa  wa TLED Sitta Tumma.
Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael (kulia), akionesha moja ya Bidhaa iliyoandaliwa na Mashine waliotoa msaada kwa Mnufaika na mjasiliamali Selena Chibando wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaamwengine ni wajasilia mali na wanufaika wa TLED.
Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael akizungumza wakati wa maonyesho hayo.
Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Jemima Michael (katikati), akiuliza  jambo  kwa Mjasiliamali mdogo na mnufaika wa mradi huo Mariamu Juma, (kushoto) wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam kulia ni mjasilia mali na mnufaika wa TLED.

The Tanzania Local Enterprise Development (TLED) ni mradi wa ni uliandaliwa kwa miaka mitano (April 2015 – Machi 2020) unaofadhiliwa na Global Affairs Canada (GAC).

Akizungumza na waandishi wa habari, Afisa Mawasiliano wa Mradi wa TLED Bi Jemima Michael, anasema TLED ni mradi maalumu kwa Wajasiriamali wa biashara ndogo ndogo na wakati, katika kukabiliana na vikwazo vya biashara vinavyowakabili hasa upatikanaji na ukuaji wa masoko katika sekta ya biashara ya kilimo, kwa kuzingatia changamoto za ziada zinazowakabili wanawake wajasiriamali.

Bi Jemima ameongeza kuwa TLED nia yake kuu ni kutoa rasilimali muhimu za biashara kwa wajasiriamali wa ndani ili kuongeza ajira endelevu kwa wanawake na wanaume katika sekta ya biashara ndogo na ya kati, na kuboresha utoaji wa ajira kutokana na maendeleo na huduma za kifedha kwa wajasiriamali katika mikoa sita nchini.

Mikoa iliyofaidika na mradi wa TLED ni Shinyanga, Mwanza, Lindi, Mtwara, Iringa na Njombe huku malengo mahususi ni kuhakikisha mnufaikaji wa mradi huo anapatiwa elimu na ushauri kutoka kwa timu ya washauri wakuu (wanaojitolea) na wafanyakazi wa mradi.

Aidha Bi Jemima aliongeza kuwa TLED huakikisha wanufaikaji wa mradi huu wanaunganishwa na soko la biashara zao, upatikanaji wa teknolojia na upatikanaji wa fedha kwaajili ya kuendeshea biashara hizo.

Awali Afisa huyo alielezea malengo ya mradi huo ni kuwafikia wajasiriamali 1760 mpaka ukomo wa mradi huo, ambapo kwasasa mradi huo umeweza kuwafikia watu 1361 sawa na 77% ya walengwa wote wa mradi.

Kupitia maonesho haya ya Sabasaba tumeyatumia kuwapa fursa wajasiliamali kujifunza kwa kuona wenzao wanafanya nini na kuzitangaza biashara zao kimataifa kupitia jukwaa hili la maonesho ya sabasaba, aliongeza Bi Jemima Michael.


Bi Careen Charles, mjasiriamali wa kutengeneza mikoba asili kutokea shinyanga ameushukuru mradi wa TLED kwa kumpa fursa ya kushiriki katika maonesho ya sabasaba, na kumsaidia kupata soko la biashara zake la uhakika.
Share:

Benki ya NBC yangara maonesho ya Sabasaba, yatwaa tuzo ya mshindi wa kwanza taasisi za kifedha

Makamu wa Rais,Samia Suluhu Hassan (kushoto) akilakiwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi kabla hajatembelea banda ya benki hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe. 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, akikabidhi kikombe cha mshindi wa kwanza katika Kitengo cha Taasisi za Fedha kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC, Theobald Sabi, wakati wa ufunguzi rasmi wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba,Dar es Salaam jana. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za fedha.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (katikati) akisalimiana na baadhi ya watendaji wa NBC wakati alipotembelea banda ya benki hiyo katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia kwa Makamu wa Rais ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Thaobald Sabi. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za Fedha. 
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa tatu kulia) akisikiliza maelezo ya bidhaa zinazotengenezwa na mmoja wa wajasiriamali wakati akitembelea banda la Benki  ya NBC katika maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam katika Viwanja vya Sabasaba yaliyofunguliwa rasmi jijini Dar es Salaam Jana. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Theobald Sabi na kulia kwake ni Waziri wa Viwanda na BIashara, Innocent Bashungwa. NBC ilitwaa tuzo ya mshindi wa kwanza ya Muoneshaji Bora katika kundi la Taasisi za Fedha.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan (wa pili kulia), akisikiliza maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazoonyeshwa na mmoja wa wajasiriamali katikabanda la Benki ya NBC, wakati wa maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam kwenye Viwanja vya Mwalimu J.K Nyerere, Sabasaba, Dar es Salaam Jana. NBC iliibuka na ushindi wa kwanza wa Muoneshaji Bora katika kundi  la Taasisi za Fedha. Kulia kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi na anayeangalia kwa karibu ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Innocent Bashungwa.


BENKI ya NBC imeibuka kidedea kwa mwaka wa pili mfululizo katika maonesho ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanayoendelea katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar  es Salaam kwa kutwaa ushindi wa kwanza katika Kundi la Taasisi za  Fedha.

NBC inashiriki maonesho ya mwaka huu ikiongeza udhamini wake kwa kudhamini kliniki ya biashara ambapo watu wanaenda na kupata mafunzo, maelekezo na majibu toka kwa watalaamu waliobobea kutoka taasisi zinazohusika kwenye maswala ya biashara.

Akizungumza viwanjani hapo, jijini Dar es Salaam, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo akisema NBC inasaidia usindikaji wa mazao ya kilimo kwa maendeleo endelevu ya viwanda na wamewapa nafasi wajasiriamali ambao wananufaika na huduma za kibenki za NBC kuja kuuza bidhaa zao  na wapo kwenye banda la wajasiriamali la NBC hapo Sabasaba. 

"Tuna tawi na ATM, hivyo tunatoa huduma zote za kibenki. Tunafubgua Fasta Akaunti ambapo mteja anakuja na kitambulisho kimoja tu na anafunguliwa akaunti na kuanza kuitimia papo hapo na kuondoka na kadi yake ya ATM," Alina.  

Mbali na hilo pia wale watakaoingia katika banda la NBC wataweza kuunganishwa  kwenye huduma za NBC Kiganjani yaani Mobile Banking na Online Banking ambapo wateja wanaweza kulipa bili, kuweka na kutuma pesa moja kwa moja kutoka na kwenda kwenye akaunti zao za NBC.

Aidha  meneja huyo aliongeza kuwa huduma kama za kubadili fedha za kigeni, bima kwa ajili ya elimu na huduma nyingine za kibenki zinapatikana mahali hapo hivyo akatoa wito kwa watu wote wanaotembelea maonesho hayo kufika katika banda la NBC.
Share:

ROBO FAINALI YANUKIA LIGI YA PROPHET SUGUYE CUP


Kiungo na mshambuliaji wa Stone town FC, Mpoki  Jeremia, akijaribu kumtoka beki wa Relini FC, wakati wa mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye  Cup inayoendelea katika viwanja vya  Shule ya Msingi Kivule Jijini  Dar es Salaam ambapo Relini FC iliichapa Stone Town mabao 7-1 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Mshambuliaji wa  Relini FC , Edga Ramsei akimtoka mchezaji wa Stone Town Mlisho Simbe Jeremia, akijaribu kumtoka beki wa Relini FC, wakati wa mchezo wa Ligi ya Prophet Suguye  Cup inayoendelea katika viwanja vya  Shule ya Msingi Kivule Jijini  Dar es Salaam ambapo Relini FC iliichapa Stone Town mabao 7-1 mchezo huo umepigwa leo viwanjani hapo.
Manahodha wa timu hizo wakishikana mikono kabla ya kuanza mchezo wanaoshuhudia ni waamuzi wa mchezo huo
Wachezaji wa timu hizo wakishikana mikono na waamuzi  kabla ya kuanza kwa mchezo huo.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages