BENKI YA NIC YAADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI KATIKA HOSPITALI YA CCBRT

Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank, Margret Karume (kushoto) akimkabidhi vifaa mbalimbali Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi akiongea na waandishi wa habari kutoa shukrani zake kwa Benki ya NIC mara baada ya kupokea vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.
Meneja Chapa na Mawasiliano wa NIC Benki, Bi Nasikiwa Berya akiongea kabla kukabidhi vifaa mbalimbali kwa ajili ya wagonjwa wa Fistula waliolazwa kwenye hospitali hiyo ikiwa ni sehemu ya kusherehekea kwa pamoja maadhimisho ya wiki ya wanawake Duniani. Hafla hiyo imefanyika Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa NIC Bank, Margret Karume (kushoto) akisikiliza taarifa mbali mbali kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT (hayupo pichani).

Na Mwandishi Wetu

Ikiwa ni sehemu ya kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Wanawake Duniani, Benki ya NIC imeadhimisha siku hiyo muhimu kwa wanawake kwa kutembelea na kutoa misaada mbali mbali kwa wanawake wanaotibiwa ugonjwa wa Fistula hospitali ya CCBRT.

Siku ya Kimataifa ya Wanawake huazimishhwa kila mwaka kusherehekea mafanikio waliyopata wanawake katika nyanja mbali mbali kama vile kijamii, kiuchumi, kitamaduni na kisiasa.

Maadhimisho haya pia yanasaidia kupaza sauti juu ya suala la usawa wa kijinsia. Yakiwa na kauli mbiu ‘Usawa kwa Wote’, kauli hiyo inahimiza kuwa usawa siyo jambo la wanawake bali ni jambo la kibiashara. Usawa wa kijinsia ni muhimu kwa uchumi na kwa maendeleo ya jamii. Usawa wa kijinsia siyo jambo la mjadala wa siku moja ambao utaisha katika siku ya wanawake duniani bali ni suala endelevu.

Ili kusaidia jamii ambayo inatuzunguka, tumeamua kutumia siku hii kuimarisha uhusiano wet na hospitali ya CCBR. Benki yetu leo imeamua kuja hapa na kutoa misaada mbali mbali itakayowasidia wanawake wanopata matibau ya fistula hospitalini hapa,” alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Margaret Karume.

Akizunguma wakati wa kutoa misaada hiyo, mkurugenzi wa benki hiyo alisema benki yake ni moja kati ya taasisi zinazojali suala la usawa i kwenye mambo mbali mbali ikiwa ni pamoja na ajira na kuongeza kuwa pia benki hiyo inathmini jamii inayozizunguka na huzisadia katika nyanja za elimu, afya na mazingira.

“Tunafurahi kushiriki maadhimisho ya siku ya wanawake duniani pamoja wanawake hapa CCBRT. Kusaidia jamii inayotuzunguka na wanawake ni moja kati ya vipaumbele vya benki yetu.

Unapomsaidia mwanamke, humsaidii peke yake bali unasaidia jamii nzima nan chi kwa ujumla,” alisema Usawa wa kijinsia unahitaji uwezeshaji kwa wote ukilenga kutatua changamoto ya kutokuwa na maamuzi sawa na pia kumpa kila mtu nguvu na uhuru wa kuamua maisha yake.

Aliongeza kuwa watu wote wakiwa wamewezeshwa, familia zinanufaika na manufaa haya yanakwenda mpaka kwa vizazi vijavyo na familia kwa ujumla.

Benki ya NIC itaendelea kusaidia jamii katika namna mbali mbali ambazo zitamnufaisha mtu mmoja mmoja na jamii yote kwa ujumla wake,” alisema.
Share:

Coral Paints yatangaza mafanikio ikitimiza miaka 30

Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati), akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo mbele ya waandishi wa habari na wageni wengine waalikwa. Katika hafla hiyo. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii Diamond Platnumza kuwa Balozi mpya wa Coral Paints.
Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz akiimba wimbo, maalum kuhamasisha matumizi ya rangi ya kampuni hiyo wakati Kampuni ya Insignia Ltd ikimtangaza kuwa balozi sambamba na maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (kushoto), na Balozi Mpya wa Rangi za Coral, Msanii wa kizazi kipya Diamond Platnumz (kushoto kwake), wakishangilia katika hafla ambayo kampuni hiyo ilitangaza kuadhimisha miaka 30 tokea kuanzishwa kwake nchini na pia kumtangaza Diamond kama balozi wao. Wengine ni wawakilishi kutoka Coral Paint na Wasafi Media. Hafla hiyo ilifayika jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Insignia Ltd ambao ni watengenezaji wa Rangi za Coral & Galaxy Paint, Kisan Dhebar (katikati), akizungumzia maadhimisho ya Miaka 30 ya kampuni hiyo jijini Dar es Salaam leo mbele ya waandishi wa habari. Katika hafla hiyo kampuni hiyo ilimtangaza msanii Diamond Platnumz kuwa Balozi mpya wa Coral Paints.

Na Mwandishi Wetu,

KAMPUNI ya rangi ya Coral Paints imeadhimisha miaka 30 tangu ilipoasisiwa huku ikijivunia ushirika wake katika kukuza uchumi wa wananchi na taifa zima kwa kuwainua mamia ya wajasiliamali nchini.

Akizungumza wakati wa hafla ya maadhimisho hayo jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo, Kishan Dhebar, alisema wengi miongoni mwa wajasirimali hao kwa sasa ni mawakala wakubwa wa Coral Paints ndani na nje ya nchi.

“Wapo ambao tulianza nao miaka 30 iliyopita na tumekuwa tukitumia takriban Sh. 100 milioni kila mwaka kwa ajili ya kuwainua wajasiriamali wa Tanzania. Hadi sasa tuna takriban mawakala 1,500 ndani na nje ya nchi,” alisema Dhebar.

Dhebar alisema Coral Paints katika miji ya Dar es Salaam, Mwanza, Dodoma na Moshi ambako ndiko kampuni hiyo ilikozaliwa mwaka 1990, ikiasisiwa na Watanzania kabla ya kupanuka na kuwa kinara katika soko la rangi, ikichagizwa na kauli mbiu ya ‘Kupamba na Kusherehekea’.

Akizungumzia mafanikio ya kampuni kwa miaka yake 30, mmoja wa wafanyakazi, Amani Mosha, alisema iikuwa ni miaka ya kujivunia kutokana na ubora wa bidhaa wanazozalisha na kuziingiza sokoni.

“Bidhaa zeu ni bora na zenye mng’ao unaodumu kwa muda mrefu na kukidhi matakwa ya wateja ikionyesha thamani halisi ya nyumba au garii,” alisema Mosha.

Awali Dhebar alimtambulisha msanii maarufu nchini, Diamond Platinum kuwa Balozi wa Chapa ya Coral Paints, akisema kwa kuwa wao huzalisha bidhaa bora, ndio maana wamemchagua mtu bora kushirikiana nao.

Diamond, kwa upande wake aliahidi kutoiangusha kampuni hiyo na kwamba atatumia kipaji chake kusambaza ‘simulizi ya kila ukuta’ kama ilivyo kauli mbiu mpya ya Coral Paints.

“Nitaanza kwanza kwa kuipamba Tandale. Nyumba ambazo hazijapakwa rangi tutaipaka rangi za Coral ili baadate tusherehekee,” alisema Diamond.
Share:

Benki ya Absa Tanzania yadhamini Kili Marathon 2020 kwa mafanikio

Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (katikati), pamoja na wafanyakazi wa benki hiyo wakishiriki mbio za Kilomita 21 za Kilimanjaro marathon pamoja na wakimbiaji wengine. Absa ilikuwa mmoja wa wadhamini ikigharamia kituo cha kutoa maji ya kunywa na viburudisho kwa wakimbiaji. Mashindano hayo yalifanyika mjini Moshi, Kilimanjaro leo.  
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (kushoto), akimpongeza mmoja wa wakimbiaji wao aliyeshiriki mbio za kilomita 42 wakati wa mashindano ya Kilimanjaro marathon 2020 pamoja na wakimbiaji wengine mjini Moshi, Kilimanjaro leo. Absa ilikuwa mmoja wa wadhamini ikigharamia kituo cha kutoa maji ya kunywa na viburudisho kwa wakimbiaji. Mashindano hayo yalifanyika Moshi, Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga (kushoto), pamoja na wakimbiaji wengine wakionyesha medali zao walizopewa baada ya kushiriki mshindamo ya Kilimanjaro Marathon 2020 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi, mkoani Kilimanjaro leo. Absa ilikuwa mmoja wa wadhamini ikigharamia kituo cha kutoa maji ya kunywa na viburudisho kwa wakimbiaji pamoja na kupeleka wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Baadhi ya wakimbiaji wa Benki ya Absa Tanzania pamoja na wakimbiaji wengine, wakitimua mbio wakati wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 mjini Moshi Kilimanjaro leo. Absa ilidhamini mashindano hayo kwa kutoa kituo cha maji na viburudisho kwa wakimbiaji pamoja na kupeleka wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Mkimbiaji akipewa maji ili kupoza kiu katika kituo cha maji kilichowekwa kwa ufadhili wa Benki ya Absa Tanzania wakati wa mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon mjini Moshi, Kilimanjaro leo.  
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghirwa (kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Aron Luhanga kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kufanikisha mashindano ya mwaka huu ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika leo katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Moshi Mkoani Kilimanjaro. Anayeshuhudia ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe.
Wakimbiaji wa Benki ya Absa Tanzania, wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Mjini Moshi, Kimanjaro juzi. Absa ilidhamini mashindano hayo kwa kutoa kituo cha maji na viburudisho kwa wakimbiaji pamoja na kupeleka wafanyakazi wake kushiriki mbio hizo.
Share:

Nabii Suguye atoa Njia za Kufanya Maombi yako Kujibiwa na Mungu


Na Mwandishi wetu,

Nabii Suguye wa Kanisa la Huduma ya Upatanisho (WRM) lililopo Kivule, Matembele ya Pili, Ukonga, jijini Dar es salaam, jumapili ya leo amewafundisha maelfu ya waumini waliohudhuria Ibada ya leo kanisani hapo iliyokuwa maalumu kwaajili ya Unabii wa mtu mmoja mmoja na Maombi ya Mapatano juu ya Masharti ya kupelekea maombi yako kujibiwa na Mungu.

“Watu wa Mungu tumekuwa watu wa kuutafuta uso wa Mungu juu ya maitaji yetu lakini wengi wetu majibu yamekuwa hayapatikani na kuanza kujiuliza kama kweli Mungu yupo lakini siri ni kuwa wamefeli kufata kanuni za Mungu za Maombi”

“Ukitaka maombi yako yajibiwe yakupasa uwe na Imani ya Kiungu; Kuna Imani ya kibinadamu lakini pia kuna imani ya Kiungu.”

Alisema Nabii Suguye na kunukuu maandiko kutoka katika kitabu cha Warumi 4:17 (kama ilivyoandikwa, Nimekuweka kuwa baba wa mataifa mengi); mbele zake yeye aliyemwamini, yaani Mungu, mwenye kuwahuisha wafu, ayatajaye yale yasiyokuwako kana kwamba yamekuwako.”

“Imani ya Mungu ni kuyaleta mambo yasiyokuwepo kana kwamba yamekwisha kuwepo. Kama unaona umaskini imani ya Mungu inaona Utajiri, kama unaona haiwezekani Imani ya Mungu inaona kuwezekana.”

Nakuongeza kwa kunukuu neno kutoka kwenye waraka wa Waebrania 11:3 Kwa imani twafahamu ya kuwa ulimwengu uliumbwa kwa neno la Mungu, hata vitu vinavyoonekana havikufanywa kwa vitu vilivyo dhahiri.”

“Wengi wetu tunafeli kwakua tunashindwa kuifanyia mazoezi imani. Imani sio tu ya mdomoni kwa kusema namjua Mungu, imani inatakiwa itendewe kazi maandiko yanasema imani pasipo matendo imekufa ndani yake.”

Nabii Suguye aliendelea kusema “Ili maombi yako yajibiwe usiache KUOMBA. Neno linasema msijisumbue kwa lolote Bali kwa kusali na kuomba. Katika kuomba unatakiwa kutamka mambo ambayo unayataka bila kumwekea Mungu mipaka wala mashaka kwakua mashaka huzuia Maombi kufanikiwa.”

“Unapoomba usiombe kwa kumuwekea mipaka Bwana ya kukubariki na kukufanyia muujiza. Wengi tumekua hatujibiwi kwakua tunamwekea Bwana mipaka tunapokua tunaomba. Unapopokea majibu ya Daktari na Ukaanza kuomba usizitazame taarifa za daktari unapofanya maombi amini kuwa Mungu anauwezo wa kufanya zaidi ya wanachokiwaza wanadamu.” Alisema Nabii.

“Mashaka ni hatari katika maisha ya mwamini, Mungu anataka tuwe majasiri tuliojaa imani tunaojua wapi tumetoka, wapi tulipo na wapi tunaelekea. Usikubali Mashaka ipoteze Baraka zako, simama na Mungu wakati wote mashaka isipate nafasi kwako.” Aliongeza Nabii Suguye.

Nabii Suguye aliendelea kusema kuwa “Unatakiwa kuamini kuwa Mungu yupo na humjibu kila amtafutaye, ndio Mungu huangalia imani yako hivyo unapoomba, kuwa na Imani ya kupokea.
Share:

Wafanyakazi wa DCB washiriki Kilimanjaro Marathon mjini Moshi



Wafanyakazi wa Benki ya Biashara ya DCB, wakishiriki mbio za Kilomita 21 pamoja na wakimbiaji wengine katika Mashindano ya Kilimanjaro Marathon yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Mjini Moshi, Kimanjaro leo.
Wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB, wakipasha viungo kabla ya kuanza mbio za Kilomita 21 za mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi, Kimanjaro, leo.
Baadhi ya wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB, wakitimua mbio wakati wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 mjini Moshi Kilimanjaro, leo.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Harrison Mwakyembe (Katikati), Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Dk. Anna Mghwira (wa pili kushoto) pamoja na baadhi ya wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB wakishiriki mbio za kujifurahisha za kilomita 5 wakati wa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 yaliyofanyika katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika Mjini Moshi, Kimanjaro leo.
Wakimbiaji wa Benki ya Biashara ya DCB, wakipiga picha ya kumbukumbu mara baada ya kumalizika kwa mashindano ya Kilimanjaro Marathon 2020 katika Uwanja wa Chuo cha Ushirika, Mjini Moshi, Kimanjaro leo.
Share:

NBC yadhamini Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezeji katika Sekta ya Madini

Wakala wa Mauzo katika Kitengo cha Hazina na Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya NBC, Emmanuel Charles Gasirabo akihojiwa na vyombo vya habari wakati wa mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo.
Waziri Mkuu, Mheshimiwa Kassim Majaliwa (kushoto), akitembelea mabanda ya maonyesho ya wadau wa sekta ya madini wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo. Anayemuongoza katikati ni Waziri wa Madini, Doto Biteko.
Kamishna wa Tume ya Madini, Prof. Abdulkarim Mruma, akishikana mikono na Meneja Mahusiano wa Taasisi za Umma wa Benki ya NBC, Azza Mnzava (wa pili kushoto), mara baada ya kamishna huyo kutembelea banda la NBC wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo. Wengine kushoto ni Wakala wa Mauzo katika Kitengo cha Hazina na Masoko ya Fedha za Kigeni, Emmanuel Gasirabo (kushoto), na Meneja Mahusiano Kitengo cha Wateja Rejerejea Maalumu, Daniel Kaila.
Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo, akisalimiana Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mine, Simon Shayo baada ya kutembelea banda la NBC wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano huo. Kulia ni Ofisa Mahusiano wa NBC kitengo cha Wateja Maalumu, Daniel Kaila.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia), akizungumza na Makamu wa Rais wa Kampuni ya Geita Gold Mine, Simon Shayo baada ya kutembelea banda la NBC wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini uliomalizika juzi katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. NBC ilidhamini mkutano. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Meneja Mahusiano wa Taasisi za Umma wa NBC, Azza Mnzava na Wakala wa Mauzo katika Kitengo cha Hazina na Masoko ya Fedha za Kigeni, Emannuel Gasirabo.
Share:

WATEJA WA NBC WAENDELEA KUIBUKA KIDEDEA KUPITIA NBC MALENGO

Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (wa pili kushoto), akizungumza wakati wa droo ya mwezi Januari ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo ambapo jumla ya washindi watano walijishindia pikipiki mpya kila mmoja. Wanaoangalia kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli Masudi, Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye, Meneja Kampeni ya Malengo, Mtenya Chewa na mmoja wa washindi wa bodaboda wa droo ya Disemba, Rosemary Kibodya.
Meneja wa Kampeni ya Malengo wa Benki ya NBC, Mtenya Cheya ( wa pili kulia), akiziungumza kwa simu na mmoja wa washindi wa droo ya kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo aliyejishindia bodaboda. Juma ya washindi watano walishinda zawadi hiyo. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Wengine kutoka kushoto ni Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha, Masuli Masudi, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye na mshindi wa bodaboda wa mwezi Disemba.
Meneja Masoko wa Benki ya NBC, Alina Maria Kimaryo (kulia), akikabidhi zawadi ya bodaboda kwa Bi. Rosemary Kibodya, mmoja wa washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo. Makabidhiano hayo yalifanyika pamoja na droo ya mwezi Januari ambapo jumla ya washindi watano waliojishindia bodaboda walipatikana. Wengine kutoka kushoto ni Meneja Tawi la Corporate, Mariam Kombo na Meneja wa Bidhaa za Kuwekeza, Dorothea Mabonye.
Meneja wa Tawi la NBC Corporate, Mariam Kombo akikabidhi kadi ya pikipiki kwa Rosemary Kibodya, mmoja wa washindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana wa kampeni ya Ibuka Kidedea na NBC Malengo. Makabidhiano hayo yalifanyika pamoja na droo ya mwezi Januari ambapo jumla ya washindi watano waliojishindia bodaboda walipatikana.

Dar es Salaam Februari 19, 2020. BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC), moja ya benki kongwe nchini imeendelea kuboresha maisha ya wateja wake kwa kuendelea kutoa zawadi mbalimbali kupitia kampeni yake inayoendelea ya akaunti ya Malengo iitwayo 'Ibuka Kidedea na NBC Malengo'.

Akizungumza wakati wa droo ya Mwezi Januari katika droo za kila mwezi za kampeni ya Ibuka Kidedea jijni Dar es Salaam leo, Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo alisema kampeni hiyo imeendelea kufanya vizuri tokea ilipozinduliwa Oktoba mwaka jana, ikishuhudia wateja wa zamani wakiweka amana katika akaunti zao za Malengo huku wateja wapya wakijiunga na NBC Malengo ili kujishindia zawadi na kunufaika na manufaa lukuki yanayopatikana sambamba na akaunti hiyo.

“Tunaposema ‘Ibuka Kidedea' ni kweli tunamaanisha, Kwani mjuavyo hadi sasa jumla ya washindi 10 wamejishindia zawadi za bodaboda huku washindi nane wameshinda safari za mapumziko kwenda sychelles na Serengeti.

“NBC Ibuka Kidedea imekuja kusaidia watanzania kutimiza malengo yao. Watanzania wana malengo mbalimbali kila mmoja ana malengo yake, natoa wito kwa wateja wetu na wasio wateja kujiunga na NBC Malengo ili kutimiza malengo yenu kwa urahisi na uhakika”, alisema Bi. Maria.

Bi Maria aliongeza kuwaNBC inajali maisha ya wateja wake na watanzania kwa ujumla na ndio sababu kila mara imekuwa ikiingiza bidhaa na huduma zinazoendana na kukidhi mahitaji halisi ya watanzania.

“NBC ni benki ya kizalendo, tunajua fika mahitaji halisi ya watanzania, tunajua mahitaji ya wateja wetu, akaunti ya Malengo ya NBC ni moja ya fursa iliyoletwa na NBC ili kumuwezesha mteja wetu kujiwekea akiba kidogo kidogo ili kutimiza malengo yake.

“NBC tunataka wateja wetu na watanzania wawe na utamaduni wa kujiwekea akiba hata Kama ni kidogo kidogo kwani mswahili wanasema 'bandu bandu humaliza gogo”, alisema.

Pamoja na hayo meneja huyo anasema wale wote wanaojiunga na NBC Malengo sio tu kupata nafasi ya kuibuka kidedea lakini pia wanashuhudia akaunti zao zikipata faida nono  kila mwezi hivyo kuwasaidia kutimiza malengo yao.

“NBC hatuishii kwenye Malengo tu, tunaposema 'NBC Daima Karibu Nawe' tunamaanisha kuwa NBC ipo karibu na kila mmoja anayehitaji huduma za kibenki, iwe ni akaunti za vikundi, wanawake, mikopo ya aina mbalimbali, huduma za kibenki kwa wajasiriamali, wafanyakazi, katika sekta za kilimo na madini, kila mahali NBC tupo”, aliongeza Bi Maria.

Katika droo ya leo waahindi watano waliibuka kidedea na kujishindia pikipiki mpya aina ya Yamaha kila mmoja huku zawadi kubwa ikipangwa kuwa pikipiki ya miguu mitatu aina ya Toyo itakayotolewa katika droo kubwa inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao.

Mbali na droo hiyo pia mshindi wa droo ya mwezi Disemba mwaka jana Bi. Rosemary Kibodya wa Dar es Salaam alikabidhiwa pikipiki yake katika tukio lililoshuhudiwa pia na wakaguzi kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (275) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (119) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages