Tanga Cement yajenga wodi ya wazazi Hospitali ya Wilaya ya Handeni

Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema (wa pili kulia), akishikana mikono na Katibu Tawala wa Wilaya ya Handeni,Upendo Magashi, katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya
daraja la kwanza
la hospitali ya wilaya hiyo pamoja na samani zake lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Wengine ni baadhi ya viongozi wa wilaya hiyo. Hafla ya makabdhiano ilifanyika Handeni, Tanga hivi karibuni.
Meneja Uzalishaji wa Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Mhandisi Ben Lema na Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mgaya Twaha (kulia), wakikata utepe kuashiria makabidhiano rasmi ya  jengo la wodi ya
daraja la kwanza​
la hospitali ya Wilaya ya Handeni lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87 na Tanga Cement. Anayeshuhudia ni Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Upendo Magashi. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni, Mgaya Twaha, akizungumza katika hafla ambayo Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC) ilikabidhi jengo la wodi ya
daraja la kwanza
pamoja samani zake la hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni mkoani Tanga. Kushoto ni Meneja Kiwanda wa Tanga Cement, Mhandisi Ben Leman na kulia ni Katibu Tawala wa Handeni, Upendo Magashi.
Ofisa Mawasiliano wa  Kampuni ya Tanga Cement (TCPLC), Helen Maleko (kulia), akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la wodi ya
daraja la kwanza
pamoja samani zake la hospitali ya wilaya hiyo lililojengwa msaada kwa gharama ya shs milioni 87. Hafla ya makabidhiano ilifanyika, Handeni, Tanga mwishoni mwa wiki. Wengine ni viongozi wa wilaya na kutoka TCPLC. 
Baadhi ya wananchi  na wafanyakazi wa Hospitali ya Wilaya ya Handeni waliohudhuria hafla hiyo.
Viongozi wa kiserikali na kisiasa pamoja na maofisa wa Tanga Cement wakipiga picha ya kumbukumbu mbele ya jengo la wodi ya daraja la kwanza la Hospitali ya Wilaya ya Handeni lililojengwa na kampuni hiyolitatumika kwa wagonjwa maalumu na hata kwa viongozi wakipata dharura wilayani humo.
Share:

Tanzia : MSANII SAM WA UKWELI AFARIKI DUNIA


Usiku wa June 6, 2018 Muimbaji Sam wa Ukweli aliyevuma kwa wimbo wa 'Hata kwetu wapo' amefariki dunia baada ya kuzidiwa ghafla akiwa studio, na kupelekwa katika hospitali ya Mwananyamala Jijini Dar es salaam huku Producer wake Steve aliyekuwa akifanya kazi na Msanii huyo na amesema Sam alikuwa akiumwa na walipomuuliza alisema ni UKIMWI wa kulogwa.

Walichoandika Wolper, Snura na Prof.Jay kuhusu kifo caha Sam wa Ukweli 

..>>> “Sam alianza kuzidiwa toka J’mosi, tulipomuuliza anaumwa nini alisema UKIMWI lakini sio UKIMWI wa kawaida bali wa kulogwa” – Steve

Sasa baadhi ya mastaa mbalimbali wameguswa na tukio hilo na kupost kwenye ukura zao za Instagram…>>>“Dah!!!😢😢😢😢nitasema nini sasa mimi 😢😢tangulia tu mdogo wangu harakati ndio zimeishia hapa kweli????😢😢😢😢😢” – SNURA


.…>>>”Poleni Ndugu wafiwa wote na Mashabiki kwa ujumla jamani🙌 R.i.p Sam Tangulia mwaya 🙏” – WOLPER


……>>>Whaaaat? R.I.P SAM WA UKWELI🙏” Prof. Jay

Share:

Rais Shein aipongeza Benki ya NBC

Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein (wa pili kushoto), akiagana na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo kwa wateja wake mjini Zanzibari hivi karibuni.

Na Mwandishi Wetu,
Rais wa Zanzibar  wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Ali Mohammed Shein ameipongeza Benki ya NBC kutokana na kasi yake na juhudi za kukuza uchumi wa Zanzibar.

Akizungumza kwa niaba ya rais wa Zanzibar katika hafla ya futari iliyoandaliwa na benki hiyo iliyofanyika mjini Zanzbar hivi karibuni, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Ayoub Mohammed Mahmoud amesema pato la taifa limekuwa likikuwa mwaka hadi mwaka kutokana na mchango unaotolewa na taasisi mbali mbali ikiwemo Benki ya NBC.
Aidha Dk.Shein ameihimiza benki hiyo kuendelea na juhudi zake za kuimarisha mazingira bora na huduma kwa wateja wake ili kwenda sambamba na kasi ya mabadiliko ya huduma za kifedha yanayotokea siku hadi siku na kukuza maendeleo bora nchini.
Hata hivyo ameipongeza Benki hiyo kwa kuonesha umuhimu kwa wateja wake kwa kurejesha miongoni mwa faida wanazozipata ikiwemo kwa njia hiyo ya kufutarisha na kutoa huduma nyengine mbali mbali kwa jamii.
Awali akizungumza katika hafla hiyo ya futari Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya NBC,  Dk. Kassim Hussein amesema kukuwa kwa huduma za kifedha Zanzibar pia kunatokana na huduma bora zinazotolewa na benki hiyo inayokwenda sambamba na mahitaji ya wateja wake.
Amesema mazingira salama yaliopo Zanzibar yanayoimarishwa na viongozi wakuu wa nchi imewezasha benki hiyo kufanya kazi zake za kutoa huduma za kifedha kwa ufanisi na umakini zaidi.
Dk. Kassim amesema  licha ya huduma mbali mbali zinazotolewa na benki hiyo pia imeanzisha huduma za kibenki zinazofuata misingi ya kiislam ambayo inatoa huduma mbalimbali za kibenki kwa misingi ya sharia ya kiislamu .
Hivyo ametoa wito kwa wananchi kutumia benki hiyo katika kufanya miamala mbali mbali bila kujali misingi ya dini kwani ni salama katika ukuwaji wa uchumi nchini.
Katika Hafla hiyo ya futari iliyoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohammed Shein , mawaziri , Jaji mkuu , Mufti Mkuu wa Zanzibar na viongozi mbali mbali wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na wateja wa benki ya NBC.
Share:

NBC yazindua huduma mikopo ya Wastaafu jijini Dodoma

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (wa pili kulia), Mkuu wa Wilaya ya Kongwa na Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Deo Ndejembi (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi (kushoto), wakishangilia mara baada ya mheshimiwa waziri kuzindua huduma ya mikopo ya wastaafu ya NBC jijini Dodoma hivi karibuni.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya NBC Tanzania, Theobald Sabi akizungumza katika hafla ya uzinduzi rasmi wa huduma ya mikopo ya wastaafu ya NBC jijini Dodoma hivi karibuni.
Mheshimiwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama akihutubia wakati wa uzinduzi huo jijini Dodoma.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (kushoto),  akisalimiana na Mkurugenzi wa Wateja Bnafsi wa NBC, Filbert Mponzi alipokwenda kuzindua mikopo ya wastaafu ya benki hiyo. Wa pili kushoti ni Meneja Mahusiano wa NBC, William Kallaghe, Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi, na Katibu Tawala Mkoa wa Dodoma, Rehema Madenge.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Walemavu, Jenista Mhagama (kushoto), akiagana na Meneja Mahusiano Sekta ya Umma na Taasisi wa NBC, Pascass Mhindi baada ya kuzindua huduma ya mikopo ya wastaafu ya NBC jijini Dodoma juzi. Kulia ni Meneja wa NBC Kanda ya Kati, James Ndimbo.
Mkuu Wa Wilaya ya Kongwa na akimwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Deo Ndejembi, akizungumza katika hafla ya uzinduzi wa Mikopo ya Wastaafu ya NBC, mjini Dodoma hivi karibuni.

Baadhi ya wastaafu waliohudhuria uzinduzi huo wakifuatilia hotuba mbalimbali katika hafla hiyo.
Share:

Airtel na itel wazindua SMARTPHONE mpya ya A32 F na Bando la Airtel BURE miezi sita

Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu  na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu- kulia Nchuda akionyesha simu mpya ya A32 F ya smartphone baada ya kuzindua kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania. Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kati ni  Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Kulia ni Mkuu wa Masoko na Mauzo  na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.
Mkurugenzi wa Masoko Airtel Tanzania Isack Nchuda akisalimiana na Mkuu wa Masoko na Mauzo itel Dar es Salaam Loalla Xu  baada ya kuzindua simu mpya ya A32 F ya smartphone kwa kushirikiana na itel pamoja na Airtel Tanzania.  Simu hiyo inakuja na GB 12, dakika 300, na sms 300 BURE kwa miezi sita kutoka Airtel. Kulia ni na Meneja Uhusiano Itel Erick Mkomoya.


Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Tanzania na kampuni ya kutengeneza simu ya itel kwa pamoja wamezindua simu mpya ya itel A32 F iliyoambatanishwa na offer ya bando ya intaneti yenye kifurushi cha BURE cha GB 12, dakika 300 pamoja na sms 300 kwa muda wa miezi 6 mfululizo.

Ushirikiano wa Airtel na itel unawahakikishia Watanzania uwezo wa kupata simu za kisasa za smartphone zenye ubora wa juu kwa gharama nafuu zaidi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa uzinduzi wa simu hiyo ya kisasa kabisa yenye ofa kabambe, Mkurugenzi wa Masoko wa Airtel Tanzania Isack Nchuda alisema “Tunajivunia ushirikiano wa Airtel  na itel kwa kuzindua simu mpya na ya kisasa ya A32F. Wenzetu wa itel wanalenga kuhudumia  wateja wa kipato cha kati na cha chini kwa bidhaa zenye ubora na unafuuu, Hivyo basi Airtel ikiwa moja ya makampuni yanayotoa huduma za smartphone za kisasa na  uhakika, tukaona tuwafikishie ofa hii kabambe watanzania wote ili kuwawezesha kuendana na ulimwengu wa kidigitali kwa kutumia mtandao wetu ulio bora na ulioenea kote nchini na simu ya itel.
 
Simu ya A32 F itakuwa inapatikana kwenye maduka yote ya Airtel na itel kote nchini ikiwa  na ofa ya kifurushi cha bando ya intaneti ya 12GB chenye muda wa miezi sita ambapo kila mwezi ni 2GB pamoja na nyongeza ya sms 300 na dakika 300 zote kutoka Airtel Tanzania.

Kwa upande wake, Mkuu wa Masoko Mkoa wa Dar es salaam kutoka itel Mobile Mr. Walle XU, alisema kuwa ni furaha kubwa sana kushirikiana na Airtel kuzindua simu mpya ya kisasa ya itel A32 F ambayo ni smartphone ya kwanza kutumia alama za vidole (finger print) yenye AndroidTM  Oreo™ ambayo ni toleo la kisasa na inapatikana kwa bei nafuu kabisa Tanzania nzima. Simu ya A32 F ni nyepesi sana na inatoa suluhisho bora kwa watumiaji wa huduma za kidigitali kwa uhakika na haraka kabisa itapatikana kwa gharama nafuu, alisema Khosla.

Bwana Walle aliongeza kuwa itel A32 F ina usalama na uhakika kwa kuwa inauwezo wa kutambua vidole vya mwenye simu na iweza kuweka programu nane ambazo zinatumika kwa matumizi mbalimbali kama kupiga picha, kupiga video, kupokea simu, stop alarm pamoja kusajili vidole vitano ambavyo kila kidole kinakuwa na kazi yake maalum.

Alisema vifaa vingine ni ukumbwa wake wa inch 5.0 pamoja na kamera ya kisasa ya 5mp kwa nyuma na mbele 2mp na inaweza kupiga picha kwa mazingira yeyote yale. Pia simu hiyo ina memory ya 8GB+1GB ambazo zinaweza kuzidi mpaka 32GB.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (275) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (119) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages