Benki ya Absa Tanzania na ASA Microfinance Yaadhimisha Miaka Minne ya Mafanikio katika Kuwawezesha Wanawake na Kubadilisha Jamii

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (Katikati), akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, wakati akitangaza mafanikio ya ushirikiano wa kibiashara kati ya benki hiyo na taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance kwa kipindi cha miaka minne. Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Absa imeikopesha ASA kiasi cha shs billioni 40 zilizoiwezesha taasisi hiyo kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali zaidi ya 50,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa, Bi. Abigail Lukuvi, Mkurugenzi wa wateja wa Makampuni wa Absa, Nellyana Mmanyi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ASA Microfinance Tanzania, Bw. Muhammad Shah Newaj na Meneja Mahusiano ya Jamii na Utawala wa ASA, Bi. Veneranda Francis.

Benki ya Absa Tanzania, kwa ushirikiano na taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance, inajivunia kuadhimisha mwaka wa nne wa ushirikiano wa kipekee ambao umewezesha zaidi ya wanawake wajasiriamali 50,000 nchini Tanzania kupata mikopo yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 40 za Kitanzania.

Tangu kuanzishwa kwake mwaka 2022, ushirikiano huu wa muda mrefu umeenda zaidi ya kutoa mikopo pekee, kila mwanamke mjasiriamali aliyewezeshwa si tu anabadilisha maisha yake binafsi, bali pia anagusa maisha ya familia yake, wafanyakazi, wasambazaji, na jamii pana inayomzunguka. Utafiti wa maendeleo unaonyesha kwamba kumwezesha mjasiriamali mmoja mwanamke nchini Tanzania kunaweza kuinua maisha ya watu 15 hadi 20 walioko karibu naye, hii inamaanisha kwamba ushirikiano kati ya Benki ya Absa na ASA Microfinance umegusa maisha ya karibu watanzania milioni moja, ukiimarisha familia na kuchochea ukuaji jumuishi wa kiuchumi.

Akizungumza kuhusu mafanikio haya jijini Dar es Salaam leo katika mkutano na waandishi wa habari, Obedi Laiser, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, alisema: “Taasisi nyingi huzingatia uwezeshaji wa wanawake kama mradi wa muda mfupi, kwa Absa, hili ni jukumu lenye kusukumwa na dhamira ya kweli. Kwa kuwawezesha zaidi ya wanawake 50,000 kupata mitaji na kukuza biashara zao, tunaona athari chanya zinazopanuka, zinazobadilisha familia, kuelimisha watoto, kuunda ajira, na kujenga ustahimilivu katika jamii. Hivi ndivyo tunavyoishi kauli mbiu yetu ya Kuiwezesha Afrika ya kesho, pamoja… hatua moja baada ya nyingine, kwa sababu kwetu Absa, Stori yako ina thamani.

Kwa upande wake, Muhammad Shah Newaj, Ofisa Mtendaji kuu wa ASA Microfinance Tanzania, aliongeza:

Ushirikiano wetu na Benki ya Absa Tanzania umeleta mageuzi makubwa. Kupitia msaada wa Absa, ASA imeweza kupanua huduma za mikopo midogo kwa maelfu ya wanawake wajasiriamali ambao wangeachwa nje ya mfumo rasmi wa kifedha. Pamoja, hatufadhili biashara pekee , tunafadhili heshima, matumaini, na fursa zinazoinua vizazi.

Katika kipindi cha miaka minne iliyopita, ushirikiano huu umeunganisha utoaji wa mitaji na mafunzo ya elimu ya kifedha, kuhakikisha kwamba wanawake wajasiriamali hawapati mikopo tu bali pia maarifa ya kuiendesha kwa uendelevu. Mapema mwezi huu, wanawake 50 kutoka Dar es Salaam walishiriki katika programu ya elimu ya kifedha iliyojumuisha mada za upangaji bajetiakibauwekezaji, na utunzaji wa kumbukumbu, hatua muhimu katika kubadilisha mikopo kuwa uwezeshaji endelevu wa kiuchumi.

Mpango huu unaonyesha mkakati wa Uwajibikaji wa Kijamii wa Absa, unaolenga ujumuishaji wa kifedha, ujasiriamali, na maendeleo endelevu. Pia unaendana na ajenda ya kitaifa ya ujumuishaji wa kifedha nchini Tanzania kwa kupanua huduma za mikopo na elimu kwa makundi yasiyohudumiwa ipasavyo, hivyo kuleta mabadiliko ya kudumu ya ustahimilivu wa kiuchumi.

Kupitia ushirikiano huu endelevu, Benki ya Absa Tanzania na ASA Microfinance zinaendelea kuandika simulizi za mabadiliko , simulizi ambazo mwanamke mmoja aliyewezeshwa hubadilisha si maisha yake tu, bali pia maisha ya wengi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), akikabidhi tuzo kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Bw. Muhammad Shah Newaj, kwa kutambua mchango wa taasisi hiyo, katika kuwawezesha wanawake wajasiriamali nchini, kwa kupitia masuluhisho mbalimbali ya kifedha. Ilikuwa ni katika hafla ambayo Absa ilitangaza mafanikio ya ushirikiano wa kibiashara kati ya benki na taasisi hiyo kwa kipindi cha miaka minne. Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Absa imeikopesha ASA kiasi cha shs billioni 40 zilizoiwezesha taasisi hiyo kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali zaidi ya 50,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Wengine kutoka kushoto ni, Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa, Bi. Abigail Lukuvi, Mkurugenzi wa wateja wa Makampuni wa Absa, Bi. Nellyana Mmanyi, na Meneja Mahusiano ya Jamii na Utawala wa ASA Microfinance, Bi. Veneranda Francis.
Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigal Lukuvi (kushoto), akizungumza katika hafla ambayo, Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser (wa tatu kushoto), akitangaza mafanikio ya ushirikiano wa kibiashara kati ya benki hiyo na taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance kwa kipindi cha miaka minne. Kupitia ushirikiano huo, Benki ya Absa imeikopesha ASA kiasi cha shs billioni 40 zilizoiwezesha taasisi hiyo kutoa mikopo kwa wanawake wajasiriamali zaidi ya 50,000 kutoka sehemu mbalimbali nchini Tanzania. Wengine kutoka kushoto kwake ni, Mkurugenzi wa wateja wa Makampuni, Bi. Nellyana Mmanyi, Ofisa Mtendaji Mkuu wa ASA Microfinance Tanzania, Bw. Muhammad Shah na Meneja Mahusiano ya Jamii na Utawala wa ASA, Bi. Veneranda Francis.
Share:

BENKI YA ABSA TANZANIA YAZINDUA KLABU YA MATEMBEZI NA MBIO FUPI IKIHAMASISHA UMUHIMU WA MAZOEZI KWA AFYA YA MWILI NA AKILI

Mkuu wa Kitengo cha Biashara wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Melvin Saprapasen (katikati) na Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha wa Absa Tanzania, Bi.Irene Rwegalulira (kushoto) wakizindua rasmi Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja wao. Hafla hii ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia) akiwatangulia baadhi ya wafanyakazi na wateja wa kitengo cha biashar, wakati wa uzinduzi rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja. Hafla hii ilifanyika jijini Dar es Salaam leo. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania kitengo cha biashara pamoja na wateja wao, wakishiriki matembezi na mbio fupi jijini Dar es Salaam leo katika hafla ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya Absa Tanzania kitengo cha biashara pamoja na wateja, wakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi rasmi wa Klabu ya matembezi na mbio fupi ya benki hiyo itakayoshirikisha wafanyakazi wa kitengo hicho na wateja. Klabu hiyo itaendesha matembezi hayo mara mbili kwa mwezi ikiwa na malengo ya kuimarisha mahusiano kati ya benki na wateja na pia kuhamasisha umuhimu wa mazoezi ya mwili kwa ustawi wa afya ya mwili na akili.
Share:

WASHINDI WA ABSA GIRLCODE HACKATHON 2015 WAPONGEZWA

Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Emanuel Mwinuka (wa nne kushoto) akizungumza na washiriki wa programu iliyopewa jina la 'Absa GirlCode Hackathon 2025' ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana. Kulia kwake ni Mkuu wa Kitengo cha Malipo ya Kibenki ya Absa, Bi. Rose Mwingira.
Mkurugenzi wa Kitengo cha Rasilimali Watu wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Patrick Foya (wa pili kulia) akikabidhi cheti kwa washindi wa kwanza, Kikundi cha Tokiva Sisters wakati wa programu iliyopewa jina la 'Absa GirlCode Hackathon 2025' ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana. Kutoka kulia ni Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki hiyo, Bw. Oscar Mwamfwagasi na Mkurugenzi wa Kitengo cha Teknolojia wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Emanuel Mwinuka.
Mkurugenzi wa Flo Pads, Bi.Flora Njelekela (kulia) akikabidhi cheti kwa washindi wa pili kikundi cha Code Crafters wakati wa programu iliyopewa jina la 'Absa GirlCode Hackathon 2025', ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Oscar Mwamfwagasi (kulia) akikabidhi cheti kwa washindi wa tatu kikundi cha Tech Divas wakati wa programu iliyopewa jina la 'Absa GirlCode Hackathon 2025' ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Meneja Huduma za Jamii wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (katikati), akizungumza na baadhi ya washiriki wa programu ya 'Absa GirlCode Hackathon 2025', ambapo wanafunzi wa vyuo vikuu wa kike walitakiwa kutengeneza Kodi za kidigitali zitakazoleta ufumbuzi utakaosaidia sekta za kibenki pamoja na jamii kwa ujumla. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Share:

BENKI YA ABSA TANZANIA KUENDELEA KUWAWEZESHA WAJASIRIAMALI WENGI ZAIDI NCHINI

Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (kulia), akizungumza na baadhi ya wanawake wajasiriamali, wanachama wa taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, katika semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, Mr. Muhammed Shah Newaj (kulia), akizungumza kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya taasisi hiyo na Benki ya Absa Tanzania, wakati wa semina ya wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Mkufunzi wa masuala ya kifedha, Bw. Edmund Munyagi (kulia), akifundisha kuhusu 'Usimamizi Binafsi wa Fedha' wakati wa semina iliyoandaliwa na Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania na kuwezeshwa na Benki ya Absa Tanzania, ikishirikisha wanawake wajasiriamali wanachama wa taasisi hiyo jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo iliyohusu elimu ya kifedha na usimamizi wa biashara wenye tija ni sehemu ya mikakati ya Benki ya Absa nchini ya kuwawezesha wajasiriamali sambamba na Lengo la benki hiyo la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Mmoja wa wanawake wajasiariamali mwanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, akichangia hoja wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na usimamizi wa biashara wenye tija, iliyoandaliwa na taasisi hiyo ikiwezeshwa na Benki ya Absa Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo haya ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Baadhi ya wanawake wajasiriamali wanachama wa Taasisi ya huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania, wakishagilia wakati Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi akizungumza nao wakati wa semina kuhusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, iliyoandaliwa na Taasisi ya ASA Microfinance Tanzania kwa uwezeshaji wa benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. Semina hiyo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo katika kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la benki hiyo la 'Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine', kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Meneja Huduma za Jamii na Matukio wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Abigail Lukuvi (katikati), baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi inayotoa huduma za kifedha ya ASA Microfinance Tanzania na wanachama wao, wakionesha alama ya ushindi mara baada ya semina iliyoandaliwa na taasisi hiyo kwa uwezeshaji wa benki hiyo ikihusu elimu ya kifedha na jinsi ya kusimamia biashara kwa ufanisi, jijini Dar es Salaam jana. Mafunzo hayo ni sehemu ya mikakati ya benki hiyo ya kuwawezesha wajasiriamali nchini sambamba na Lengo la Benki ya Absa la Kuiwezesha Afrika ya Kesho, Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, kupitia chapa ya benki hiyo inayosema 'Stori yako ni ya thamani'.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Blog Archive

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (287) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (120) MICHEZO (39) SIASA (3)

Pages