Benki ya Absa Tanzania yafanya uwekezaji mkubwa katika huduma za kidigitali

Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Ndabu Lilian Swere (wa pili kushoto) akionyesha jina la mshindi wa droo ya kwanza ya kampeni ya Tumia na Ushinde 'Spend & Win' ambapo mkazi wa Dar es Salaam Bw, Rashid Nassoro Said aliibuka kidedea kwa kujishindia gari jipya aina ya Subaru Forester 2024 lenye thamani ya zaidi ya shs milioni 40. Kampeni hiyo inayochezeshwa kila mwezi kwa kwa muda wa miezi mitatu, inahamasisha matumizi ya kadi na hduma za kidigitali katika kufanya miamala mbalimbali ya kibenki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.

Benki ya Absa Tanzania imesema imefanya uwekezaji mkubwa katika huduma zake za kibenki kwa njia za kidigitali ili kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha huduma za kibenki zinawafikia watanzania wengi na kwa gharama nafuu.

Hayo yalisemwa na Mkuu wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa benki hiyo, Bi. Ndabu Lilian Swere wakati wa droo ya kwanza ya Kampeni ianyoendelea ya ‘Tumia Ushinde’ (Spend & Win), ambayo lengo lake kubwa ni kuhamasisha wateja wa benki hiyo na watanzania kufanya miamala mbalimbali ya kibenki kwa kutumia kadi ama huduma za kibenki kwa njia za kidigitali.

Kampeni hii ya miezi mitatu ina lengo la kuwazawadia gari wateja wetu wanaofanya miamala ya kibenki kwa kutumia kadi za ATM ama huduma za kidigitali kwa kutumia mifumo yetu inayowawezesha wateja kupata huduma kiuharaka na kiurahisi hivyo kutimiza malengo yao."

Sisi kama Absa Benki Tanzania tumeimarisha huduma zetu za kidigitali ili kwenda sambamba na jitihada zinazofanywa na serikali kusaidia kufikisha huduma za kibenki kwa wale ambao hawajafikiwa na huduma hizi huku wakiendelea kutumia mifumo ya kibenki ya kiasili."

Mifumo ya kidigitali ya benki yetu ni ya haraka na tumeimarisha kwa kiwango cha kimataifa mifumo ya usalama hivyo tunapenda kuwatoa hofu wateja wetu wote kuendelea kufanya miamala kwa kutumia mifumo yetu ya kidigitali bila hofu yoyote”, alisema Bi. Ndabu.

Naye Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga alisema kampeni hiyo inaenda sambamba na lengo kuu la kuwepo kwa benki hiyo ambalo ni kuiwezesha Afrika na Tanzania ya Kesho, hatua moja baada ya nyingine ikiwezeshwa na chapa mpya ya benki hiyo isemayo ‘Stori yako ni ya thamani’.

Tunapotoa zawadi hii kwa wateja wetu na huku tukiboresha huduma zetu kwa njia za kidigitali tunaamini kuwa tunasaidia kuandika stori mbalimbali za washindi na wateja wetu, lakini pia tunaisaidia serikali yetu kuandika stori yake ya kuona huduma za kibenki zinawafikia watanzania wengi kila kona ya nchi yetu”, alisema Bw. Luhanga.

Kampeni ya Spend & Win itadumu kwa muda wa miezi mitatu na ikishuhudia kila mwezi mshindi mmoja akiibuka na gari jipya aina ya Subaru Forester lenye thamani za zaidi sh shs milioni 40, ambapo mshindi hutakiwa kufanya miamala kila wakati kwa kutumia kadi ama huduma za kibenki kwa njia ya mtandao. Katika hafla ya jana, mkazi wa Dar es Salaam, Rashidi Nassoro Saidi aliibuka kidedea na kujishindia moja ya zawadi hiyo ya gari.
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Aron Luhanga (kulia) akizungumzai jijini Dar es Salaam jana wakati wa droo ya kwanza ya kampeni ya Tumia na Ushinde 'Spend & Win' ambapo mkazi wa Dar es Salaam Bw, Rashid Nassoro Said aliibuka kidedea kwa kujishindia gari jipya aina ya Subaru Forester 2024 lenye thamani ya zaidi ya shs milioni 40. Kampeni hiyo inayochezeshwa kila mwezi kwa kwa muda wa miezi mitatu, inahamasisha matumizi ya kadi na huduma za kidigitali katika kufanya miamala mbalimbali ya kibenki. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Share:

Wafanyabiashara waipongeza serikali kushughulikia changamoto za kikodi

    

Mkuu wa Kitengo cha Shughuli za Kibenki wa Benki ya Absa Tanzania, Alred Urasa (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT), uliodhaminiwa na benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. SABFT moja ya malengo yake makuu ni kuwaunganisha wawekezaji kutoka nchini huko na wawekezaji wa Tanzania wenye ni ya kuwekeza nchini Afrika Kusini kunufaika na fursa zinazopatikana katika pande zote mbili.

Na mwandishi wetu, Dar es Salaam

WAFANYABIASHARA wanachama wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT), wametoa pongezi za serikali za nchi zote mbili kwa kushughulikia changamoto ya kero za kikodi zilizokuwa zikiwakabili kwa muda mrefu.

Akizungumza jijini Dar es Salaam jana wakati wa mkutano wa wafanyabiashara hao, uliofanyika kwa udhamini wa Benki ya Absa kwa kushirikiana na Shirika la Ndege la Afrika Kusini (SAA), Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Bw. Manish Thakrar alisema changamoyo ya kodi kutozwa mara mbili imekuwa kilio cha muda mrefu kwao lakini kutoka juhudi zinazoendelea kufanywa kwa ushirikiano wa serikali za Tanzania na Afrika Kusini, chemba za biashara na wadau wengine ni imani yao hadi kufikia mwisho wa mwaka huu kero hizo zitakuwa zimeondolewa kabisa.

Alisema Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT) lilianzishwa miaka 24 iliyopita kwa lengo kubwa la kuwaunganisha wawekezaji kutoka nchini huko na wawekezaji wa Tanzania wenye ni ya kuwekeza nchini Afrika Kusini hivyo kunufaika na fursa zinazopatikana katika pande zote mbili.

Kipindi kutoka mwaka 1997 kupitia mpango wa ubinafsishaji, kimsingi kumekuwa na ongezeko kubwa la uwekezaji wa wafanyabiashara kutoka Afrika Kusini katika miradi mikubwa katika sekta za mawasiliano, uzalishaji, vinywaji na vyakula, hivyo kutoa fursa za ajira kwa watanzania pia kunufaisha wafanyabiashara wa ndani.

Natoa shukurani za kipekee kwa Benki ya Absa Tanzania kwa udhamini mkubwa katika tukio hili, lakini pia tunaipongeza benki hii kwa jinsi inavyoweka juhudi katika kutoa huduma na bidhaa pamoja na masuluhisho mbalimbali katika kusaidia mahitaji ya kifedha kwa wafanyabiasha wa Afrika Kusini na wa Tanzania”, alisema Bw. Thakrar.

Akizungumza wakati wa mkutano huo, Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Rwegalulira akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Bw. Obedi Laiser alisema, wamejipanga vizuri katika kuhudumia wateja wao kutoka nje ya Tanzania kwa ubunifu zaidi ikiwa na masuluhisho tofauti ya huduma za kibenki kwa wateja wadogo, wa kati na wakubwa.

Majukwaa kama haya yana faida sana kwani sisi benki tunakuja kama kiunganishi ili tuweze kuwasaidia katika biashara zao zinazohitaji huduma za kifedha kama vile mikopo, fedha za kigeni, pamoja na ushauri wa namna bora ya kufanya biashara nchini Tanzania kulingana na taratibu na miongozo ya serikali.

Absa inafanya biashara sambamba na lengo kuu la kuanzishwa kwake ambalo ni Kuiwezesha Afrika na Tanzania ya Kesho Pamoja, hatua moja baada ya nyingine, huku tukiongozwa na ahadi mpya ya chapa ya benki yetu isemayo ‘Story yako ina thamani’ hivyo kwa kutoa huduma bora za kibenki kwa wafanyabiashara hawa, tunaamini tunasaidia kuandika story za mafanikio za wateja wetu kwa manufaa yao na maslahi mapana ya Tanzania na Afrika Kusini”, alisema Bi. Irene.

Jukwaa na Wafanyabiashara wa Afrika Kusini kwa sasa lina jumla ya wanachama 100 kutoka katika sekta mbalimbali kama vile mabenki, madini, mawasiliano, viwanda vya uzalishaji, maduka makubwa na nyinginezo.
Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Rwegalulira, akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT), uliodhaminiwa na benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. SABFT moja ya malengo yake makuu ni kuwaunganisha wawekezaji kutoka nchini huko na wawekezaji wa Tanzania wenye ni ya kuwekeza nchini Afrika Kusini kunufaika na fursa zinazopatikana katika pande zote mbili.
Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Rwegalulira (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT), uliodhaminiwa na benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. SABFT moja ya malengo yake makuu ni kuwaunganisha wawekezaji kutoka nchini huko na wawekezaji wa Tanzania wenye ni ya kuwekeza nchini Afrika Kusini kunufaika na fursa zinazopatikana katika pande zote mbili.
Mkurugenzi wa Masoko ya Fedha za Kigeni wa Benki ya Absa Tanzania, Bi. Irene Rwegalulira (kushoto), akizungumza wakati wa mkutano wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT), uliodhaminiwa na benki hiyo, jijini Dar es Salaam jana. SABFT moja ya malengo yake makuu ni kuwaunganisha wawekezaji kutoka nchini huko na wawekezaji wa Tanzania wenye ni ya kuwekeza nchini Afrika Kusini kunufaika na fursa zinazopatikana katika pande zote mbili.
Baadhi wa wafanyabiashara na wajumbe wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT), wakihudhuria mkutano wa jukwaa hilo uliodhaminiwa na Benki ya Absa Tanzania, jijini Dar es Salaam jana. SABFT moja ya malengo yake makuu ni kuwaunganisha wawekezaji kutoka nchini huko na wawekezaji wa Tanzania wenye ni ya kuwekeza nchini Afrika Kusini kunufaika na fursa zinazopatikana katika pande zote mbili.
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wafanyabiashara wa Afrika Kusini nchini Tanzania (SABFT), Bw. Manish Thakrar (katikati), pamoja na baadhi ya viongozi wa jukwaa hili, wakikata keki kufurahia mafanikio ya jukwaa hilo, wakati wa mkutano wao, uliodhaminiwa na Benki ya Absa Tanzania jijini Dar es Salaam jana. SABFT moja ya malengo yake makuu ni kuwaunganisha wawekezaji kutoka nchini huko na wawekezaji wa Tanzania wenye ni ya kuwekeza nchini Afrika Kusini kunufaika na fursa zinazopatikana katika pande zote mbili.
Share:

Rais wa Zanzibar aipongeza Benki ya Absa Tanzania kuboresha afya ya mama na mtoto

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (wa pili kulia), akikabidhi cheti cha shukurani kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser kwa kutambua mchango wa benki hiyo katika kuwezesha kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha’ iliyoanzishwa na Shirika la Amref Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Zanzibar. Ilikuwa ni katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha iliyofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana. Wengine kutoka kushoto ni, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui, Mwenyekiti wa Bodi ya Amref, Bw. Anthony Chamungwana na Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dk. Florence Temu.

Na mwandishi wetu, Zanzibar

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, ameipongeza Benki ya Absa Tanzania kwa mchango wake wa shs milioni 150 kuchangia kampeni ya ‘Uzazi ni Salama’ yenye lengo la kuboresha afya ya mama na mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua.

Mheshimiwa Rais Mwinyi alitoa pongezi hizo katika hafla ya tatu ya shukurani na uchangishaji fedha wa kampeni hiyo, iliyoandaliwa na Shirika la Amref Tanzania, Wizara ya Afya Zanzibar, kwa udhamini mkuu wa Benki ya Absa Tanzania na kufanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana.

Leo tumekusanyika hapa kwa lengo la kuunga mkono juhudi za kuokoa maisha kupitia kampeni hii, iliyoanzishwa mwaka 2020 ikiwa na lengo la kukusanya fedha kiasi cha shs Bilioni 1."

Aidha nimefahamishwa, mwezi juni mwaka huu, Amref, wizara yetu ya afya pamoja na Benki ya Absa Tanzania wakiungwa mkono na wadau kadhaa walitoa vifaa tiba vyenye thamani ya shs milioni 262.6 kwa ajili ya vituo vya afya 28 katika mikoa mitano ya Zanzibar, niwashukuru Amref Tanzania, wadhamini wakuu Benki ya Absa Tanzania na wadau wote kwa kujitolea kuunga mkono jitihada ya serikali ya Zanzibar katika kuboresha huduma za afya”, alisema Rais Mwinyi.

Pamoja na hayo alisema ni jambo la kutia moyo kuona Zanzibar ikiwa kwenye njia sahihi ya kufikia malengo endelevu (SDG) 2030 ya kupunguza vifo vya wajawazito hadi chini ya vifo 70 kwa vizazi hai 100, vifo vya watoto wachanga hadi kufikia 12 kwa kila vizazi 1000 na vifo vya watoto chini ya miaka mitano hadi 25 kwa kila vizazi hai 1000 kufikia 2030.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bwana Obedi Laiser alisema wametoa msaada kuunga mkono juhudi zinazofanywa za serikali za mbili za, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuwekeza katika sekta ya afya hususan katika kupunguza vifo vya akina mama na watoto.

Benki ya Absa Tanzania tunaenda sawa na lengo la taasisi yetu lisemalo ‘Kuiwezesha Afrika na Tanzania ya kesho kwa pamoja, hatua moja baada ya nyingine’ hapa tukihakikisha jamii yetu inapata huduma za afya stahiki."

Lakini pia msaada huu unaenda sambamba na ahadi yetu ya chapa tuliyoizindua hivi karibuni isemayo ‘Stori yako ina thamani’, hivyo kwa kuunga mkono juhudi hizi, tunaamini tunazisaidia serikali zetu katika kuandika stori zake zile zinazohakikisha watanzania wote wanapata huduma bora za afya”, alisema Bw. Laiser.

Awali akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dk. Florence Temu alimshukuru Rais Dk. Mwinyi kwa kukubali, kujitoa na kuunga mkono kampeni ya Uzazi ni Maisha tokea ilipoanzishwa mwaka 2020.

Niwashukuru pia wadhamini wakuu, Benki ya Absa pamoja na wafadhili wetu wengine waliokuwa nasi tokea mwanzo kufanikisha malengo ya kampeni hii yenye kauli mbiu ya ‘Changia Vifaa Tiba kwa Uzazi Salama’ ambapo kati ya malengo yetu ya kukusanya kiasi cha shs Bilioni 1, hadi sasa tumeshapokea ahadi zenye thamani ya shs 989,831,145, Zaidi ya asilimia 98.9 ya malengo yetu tukipokea kiasi cha shs 740,457,422 sawa na asilimia 75”, alisema Dk. Florence.

Hafla hiyo pia ilihudhuriwa na Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassoro Mazrui, Naibu Waziri, Mhe. Hassan Khamis Hafidh, Katibu Mkuu, Dk. Mngereza Mzee Miraji, mabalozi na wawakilishi wa mashirika ya kimataifa na kitaifa ya maendeleo, watendaji na watumishi wa serikali na mashirika ya umma.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati) na wengine kutoka kushoto; Mwenyekiti wa Bodi ya Amref Tanzania, Bw. Anthony Temu, Waziri wa Afya Zanzibar, Mhe. Nassor Mazrui, Mkurugenzi Mkazi wa Amref Tanzania, Dk. Florence Temu na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, wakifanya dua katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha wa kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha’ iliyofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi, akihutubia katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha ya kampeni ya Uzazi ni Maisha iliyofanyika katika Ikulu ya Zanzibar, jana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Absa Tanzania, Bw. Obedi Laiser, akizungumza kuhusu udhamini na malengo ya benki hiyo katika kuiwezesha kampeni ya ‘Uzazi ni Maisha’ iliyoanzishwa ma Shirika la Amref Tanzania pamoja na Wizara ya Afya Zanzibar, katika hafla ya shukurani na uchangishaji fedha kwa ajili ya kampeni hiyo katika Ikulu ya Zanzibar, jana. Kampeni hiyo ina lengo la kuboresha afya ya mama na mtoto wakati wa ujauzito na kujifungua.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ya Zanzibar, Mhe. Dk. Hussein Ali Mwinyi (katikati),akipozi kwa picha ya kumbukubu na baadhi ya wafanyakazi wa benki ya Absa Tanzania, pamoja na viongozi wengine, mara ya baada ya hafla ya shukurani na uchangishaji fedha ya kampeni ya 'Uzazi ni Salama' iiyofanyika Ikulu ya Zanzibar, jana.
Share:

Tanzania Breweries Plc (TBL) na WWF Wakabidhi Mradi wa Maji Kijiji Cha Minazi mirefu, Ruvu Stesheni

   Katika hatua muhimu ya kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji kwa jamii za wenyeji na mazingira, Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) na WWF Tanzania wamekabidhi rasmi miundombinu ya mfumo wa maji unaotumia nishati ya jua, ikijumuisha kisima, sehemu ya kunyweshea mifugo, na kituo cha maji kwa matumizi ya nyumbani katika Wilaya ya Kibaha.

Katika tukio hilo hilo, washirika hao wawili pia walizindua mradi wa majaribio wa miradi ya urejeshaji wa mazingira chini ya mpango wa "Bankable Nature Solutions" (BNbS) ili kuimarisha usalama wa maji wa muda mrefu na ulinzi wa mazingira.

Hafla ya makabidhiano iliyofanyika Kijiji cha Minazimikinda, Wilaya ya Kibaha, ilihudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Mheshimiwa Nickson Simon John, ambaye alisifu ushirikiano kati ya TBL na WWF. Alisisitiza umuhimu wa ushirikiano katika kukabiliana na changamoto za maji nchini, hususan katika maeneo yanayokua kwa kasi kama Pwani na Dar es Salaam.

"Maji ni rasilimali muhimu kwa ukuaji wa jamii zetu na uchumi. Ushirikiano huu unaonesha nguvu ya kufanya kazi kwa pamoja katika kutatua uhaba wa maji. Juhudi za TBL na WWF Tanzania za kuboresha usalama wa maji, hasa katika Dar es Salaam na maeneo jirani, ni za kupongezwa na ni hatua muhimu kuelekea kuhakikisha upatikanaji endelevu wa maji safi kwa wote," alisema Mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Nickson Simon John.

Mfumo mpya wa maji unaotumia nishati ya jua utatoa maji safi na ya kuaminika kwa jamii zinazozunguka, ukiwasaidia kaya na mifugo katika eneo hilo. Miundombinu hii inashughulikia changamoto za uhaba wa maji kwa sasa na kutumia teknolojia rafiki wa mazingira ili kuhakikisha matumizi endelevu kwa muda mrefu.
Mradi huu ni sehemu ya dhamira kubwa ya TBL kwa uendelevu, inayooana na mkakati wake wa kuleta athari chanya kwa jamii inazozihudumia huku ikiunga mkono uhifadhi wa rasilimali za asili za Tanzania. Ushirikiano na WWF Tanzania chini ya mpango wa BNbS unalenga kuhakikisha kuwa mifumo ya asili inabaki salama wakati changamoto za maji zinashughulikiwa.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa TBL Michelle Kilpin, alisisitiza umuhimu wa mradi huo: "Kwa TBL, uendelevu ni msingi wa shughuli zetu. Mfumo huu wa maji unaotumia nishati ya jua, pamoja na uzinduzi wa mradi wa majaribio wa Bankable Nature Solutions, ni hatua muhimu kuelekea kuhakikisha kwamba watu na mazingira wote wananufaika na juhudi zetu. Kwa kushirikiana kwa karibu na WWF Tanzania, tunahakikisha upatikanaji wa maji kwa jamii hii na kulinda mifumo muhimu ya ikolojia ambayo ni muhimu kwa mustakabali wetu."
Mbinu ya Bankable Nature Solutions (BNbS) inatumia rasilimali za asili kwa njia endelevu, ikigeuza juhudi za uhifadhi wa mazingira kuwa miradi inayoweza kujiendesha kifedha na kuleta manufaa kwa uchumi na jamii. Kupitia mpango huu, TBL na WWF Tanzania wanalenga kuunda mfano wa kurudiwa unaoweza kutekelezwa nchi nzima ili kukabiliana na uhaba wa maji na kuimarisha uhifadhi wa mazingira.

Mkurugenzi wa Nchi wa WWF Tanzania, Dkt. Amani Ngusaru, alielezea umuhimu wa kulinda vyanzo vya maji. “Ulinzi wa vyanzo muhimu vya maji ni muhimu kwa kudumisha maisha ya binadamu na usawa wa mazingira. Kupitia mbinu za ubunifu kama Bankable Nature Solutions, tunaweza kuunda suluhisho la muda mrefu kwa ajili ya watu na mazingira.”

"Ushirikiano wetu na TBL unaonesha jinsi biashara na mashirika ya uhifadhi wa mazingira yanavyoweza kushirikiana kufanikisha matokeo ya kudumu. Kwa uzinduzi wa mradi wa majaribio wa BNbS hapa Kibaha, tunaweka msingi wa suluhisho za muda mrefu na endelevu ambazo zinalinda rasilimali zetu za asili huku zikihakikisha jamii zinapata huduma muhimu kama maji." alisema Dkt. Ngusaru

Tukio hilo lilihudhuriwa na viongozi wa eneo hilo, wanajamii, na wadau muhimu ambao walipongeza mpango huo kwa kuwa na mtazamo wa mbali na manufaa ya muda mrefu kwa jamii. Kisima cha maji cha nishati ya jua, sehemu ya kunyweshea mifugo, na kituo cha maji kwa matumizi ya nyumbani vinatarajiwa kunufaisha moja kwa moja mamia ya kaya na mifugo yao.

Ushirikiano kati ya TBL na WWF Tanzania haukabiliani tu na upungufu wa maji, bali pia unaimarisha ulinzi wa vyanzo vya maji, muhimu kwa kuhifadhi bioanuwai na kudumisha huduma za mazingira kwa vizazi vijavyo.
Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Blog Archive

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages