ACB BANK YAJIKITA KULETA MAPINDUZI YA KUTOA HUDUMA BORA KWA WATEJA WAKE

   

Na Mwandishi wetu

Akiba Commercial Bank Plc( ACB) imesema itahakikisha inaendelea kujikita kuleta mapinduzi ya utoaji huduma bora za kibenki hapa nchini kwa kuboresha huduma zake ikiwemo kuweka fedha na kutoa fedha pia kutoa mikopo ya muda mfupi na mrefu kwa .

Akizungumaza Jijini Dar es salaam na Waandishi wa habari Mkurugenzi Mtendaji wa Akiba Commercial Bank Plc, Silvest Arumasi wakati katika banda la benki hiyo katoka maonyesho ya ya 47 ya Sabasaba ndani ya amesema kuwa benki ya Akiba imeboresha huduma zake ambazo zitakuwa chachu ya kukidhi matarajio ya wateja waliopo pamoja na wateja watarajiwa katika kujipatia huduma.

Hata hivyo amebainisha kuwa Maboresho makubwa yamefanywa kwa huduma za wateja binafsi,(Personal banking) ambayo inawalenga Waajiriwa wa sekta za Umma na sekta binafsi ambapo mteja anaweza kupata mikopo ya aina mbalimbali kuendana na mahitaji yake mathalani huduma za mikopo ya kujenga na kuboresha makazi, pia mikopo ya muda mfupi (Salary advance) kwa ajili ya kutatua dharura za kifedha kwa muda mfupi.


" Benki imezidi kuboresha huduma za mikopo kwa wateja wakubwa ,w (Corporate customers) wakati,na wadogo kuendana na mahitaji ya soko na tunatoa huduma za bima kwa wajasiriamali pamoja na vikundi mbalimbali ikiwemo mikopo ya bima –IPF (Insurance Premium Financing)" amesema Mkurugenzi

Sambamba na hayo Mkurugenzi amebainisha kuwa benki imeboresha huduma zake kwa kupitia Mawakala wake (Akiba Wakala) na simu ya mkononi (Akiba Mobile) pia imeboresha mifumo ya utumaji pesa kwenda nje ya nchi.

Aidha wito umetolewa kwa wafanyabiashara kuchangamkia fursa hiyo na amewashukuru kuchagua benki ACB hiyo kutumia huduma zake ikiwemo wafanyakazi ,Wajasriamali hivyo amewasisitiza waendelee kupata huduma bora kwani ni benki sahihi na bora inayolenga kutimiza malengo ya Wateja wake.
Share:

DKT MPANGO AISHUKURU TANZANIA COMMERCIAL BANK

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi wa shule ya msingi Muyama mara baada ya gafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasani ofisi mbili za walimu na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (wapili kulia), akikata utepe kuashiria kupokea Madarasa, Samani mbalimbali na Ofisi za Walimu yaliokarabatiwa na Tanzania Commercial Bank (TCB) katika Shule ya Msingi Muyama iliopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma ikiwa ni utaratibu wa Benki hiyo kurudisha kwa kutoa msaada kwa jamii (CSR).

Hafla hiyo imefanyika katika shule hiyo hivi karibuni wengine pichani ni kutoka (kushoto), Afisa Mtendaji Mkuu wa Tanzania Commercial Bank, Sabasaba Moshingi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Prof Joyce Ndalichako na viongozi wengine wa serikalini pamoja na Maafisa wa Benki

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Philip Mpango, ameishukuru Tanzania Commercial Bank kwa kutoa msaada wa ukarabati wa Vyumba Vitatu vya Madarasa, Ofisi Mbili za Walimu madawati 50 pamoja na printer na vitu mbalimbali vya ofisini katika Shule ya Msingi Muyama iliopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma

Akipokea msaada huo aliushukuru ongozi mzima wa Benki ya TCB kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la Elimu Mkoa wa Kigoma na maeneo mengine hapa nchini.

Makamu wa Rais Philip Mpango alipokea msaada huo alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi mkoani humo na kutaka taasisi nyengine kuiga mfano mzuri unaofanywa na Tanzania commercial bank

Ameeleza kuwa Benk ya TCB imeonesha ukomavu wake hasa kwenye swala la elimu ya kifedha maana bila elimu hakuna chochote kwenye maendeleo ya nchi yetu.

Dkt Mpango ameongeza kuwa hata yeye amesoma katika shule hiyo ambayo leo Tanzania commercial bank wametoa msaada wa vitu hivi kwaajili ya kukuza elimu na maeneo mengine alisema mpango.

Nae Afisa Mtendaji Mkuu wa TCB, Bw Sabasaba Moshingi alitoa shukrani za dhati kwa Mhe Mpango kwa kuweza kufika kwenye hafla fupi ya makabidhiano na kuhaidi kuwa benki itaendelea kusaidia jamii katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu. Vile vile alitoa rai kwa wananchi wa Buhigwe na maeneo ya karibu kuweza kujiunga na huduma mbalimbali zinazotolewa na benki.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na maafisa kutoka benki ya TCB mara baada ya hafla ya kupokea vyumba vitatu vya madarasa na ofisi mbili za walimu na Samani mbalimbali za maofisini yaliokabidhiwa na Tanzania commercial Bank (TCB), katika Shule ya Msingi Muyama iliyopo Wilaya ya Buhigwe mkoani Kigoma.

Share:

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

LILIAN-FAVOUR MAKAWA

Popular Posts

Labels

Recent Posts

Label Cloud

BIASHARA (255) BURUDANI (4) KIMATAIFA (10) KITAIFA (114) MICHEZO (38) SIASA (3)

Pages